Sukuma Stories

Father Zakaria Kashinje is consolidating all the Sukuma proverbs, sayings, riddles, stories and songs in his running list on our Sukuma Legacy Project Website https://sukumalegacy.org.

Father Zakaria Kashinje is consolidating all the Sukuma proverbs, sayings, riddles, stories and songs in his running list on our Sukuma Legacy Project Website https://sukumalegacy.org.

This website promotes the history, culture, Oral Literature — Stories, Proverbs, Sayings, Riddles and Songs — and visual representations of the Sukuma People in Tanzania in East Africa. Presently he is drawing from: Sybertz, Donald and Joseph Healey. Kueneza Injili Kwa Methali: Hekima ya Kisukuma na Lugha Mbalimbali juu ya Chakula — Kitabu cha Kwanza, Peramiho: Benedictine Publications Ndanda — Peramiho, 1984.

The English translation is Proclaiming the Gospel Through Proverbs: The Wisdom of Sukuma and Different Languages on Food – Book I. Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, Kugundua Mbegu za Injili: Hekima ya Kisukuma na Lugha Mbalimbali juu ya Familia na Ndoa — Kitabu cha Pili, Peramiho: Benedictine Publications Ndanda — Peramiho, 1993.

The English translation is Discovering Seeds of the Gospel: The Wisdom of Sukuma and Different Languages on Family and Marriage – Book II.

133. OGWIZUKA JILATU JANTEMI HUWAGUJIBHUCHA.

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Mbuki ya lusumo lwenulu lulilola Ntemi. Ikale yali giki, Untemi ulu ubhuka lugendo lo gubhayelela abhazengi bhakwe, ojaga na bhanhu bhagunshindilila. Abhanhu bhenabho habho bhabhuchaga imiligo yakwe.

Uwei untemi oladadililaga igiki aguzwala ki. Ulu miligo yukija ugubhuchiwa, yali giki, uogwiizuka nuyo alaibhuche.

Ichene igahaiyagwa nukubhanhu abhatogilwe nulu abhabhamanilile gubhidika bhangi miligo, abhoyi nulu gugema ugwikumya, yaya.

 

KISWAHILI: WAKUKUMBUKA VIATU VYA MFALME NDIYE WA KUVIVAA.

Chanzo cha methali hii kinamwangalia Mfalme (mtemi). Hapo zamani Mfalme/Mtemi kama akifunga safari ya kuwatembelea wananchi wake, alienda na watu wakumsindikiza. Watu hao, ndio waliokuwa wakibeba mizigo yake.

Yeye Mfalme alikuwa hajali kwamba atavaa nini. Kama mizigo ikiachwa kubebwa, atakayeikumbuka, ndiye atakayeibeja.

Hali hiyo husemwa pia kwa watu wapendao au waliozoea kuwabebesha wengine mizigo, ambayo wao hawajaribu hata kuigusa.

Luka 11:46Yesu akamjibu, “Nanyi wataalam wa sheria, ole wenu, kwa sababu mnawatwika watu mizigo mizito ambayo hawawezi kubeba, wala ninyi wenyewe hamwinui hata kidole kimoja kuwasaidia.”

jesus-of-nazareth

ENGLISH: THE ONE WHO REMEMBERS THE SHOES OF THE KING IS THE ONE WHO HAS TO WEAR THEM

The source of that proverb looks at the King. A long time ago the King/Emperor was traveling on a journey to visit his people. He went with some people who wanted to impress him. They were the ones carrying his cargo. The King did not care of what he would wear. If the cargo was left, like shoes, then the person who remembered them was the one who had to wear them. The situation is also said to people who are used to burden others with burdens that they did not even try to touch.

“Jesus answered them, ”You experts of the law, woe to you, because you lay down heavy burdens that you cannot bear, and you yourselves have not even one finger to help.” (Luke 11:46).

132. MONGO NA MBULA

Collected by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey  (African Proverbs, Sayings and Stories)

Aho kale umongo ni mbula jigihalalika. Umongo gugigimba na gundalaha umuna Mbula, na gung’wila, “Lolaga umo nalinabhudula. Nokalaga minzi hangi nalizwilila na guhuuma bho nguzu mpaga abhanhu bhaliduuma ugunikila.”

Imbula igashosha, “Idishene, ubho nduhu nene ubhebhe udiginhu.”  Umongo gukashosha, “Yaya unene gwandija kale nabhiza giki, nokala minzi na nguzu hangi bhanhu bhalongeja gunikumilija noi gufumila miaka igana mpaka igana. Iki bhaliza kulinene bhuli lushiku gudaha minzi. Ehe, ubhebhe ulinabhudula ki?”

Giko lulu, imbula igakolwa na gwiyombela munholo yayo, “ung’wunuyu dubhone na nguzu jakwe!”

Imbula igoya ugutula umongo guuma gete. Umongo gugaiwa  ugogwita gupinihala na guhagigisha guliyomba, ugoyi ubhonduhu mbula gudi ginhu.

KISWAHILI: MTO NA MVUA

Hapo zamani siku moja mto na mvua walibishana. Mto ulijivuna na kumdharau mvua na kumwambia, “Tazama nilivyo na uwezo. Nimejaa maji tena ninabubujika na kuporomoka kwa nguvu hata watu wanashindwa kunivuka.”

Mvua akamjibu, “sivyo bila mimi wewe si kitu.” Mto ukajibu “hapa

na mimi tangu zamani nimekuwa hivihivi, nimejaa maji na nguvu tena watu wameendelea kunisifu sana kutoka karne hadi karne. Maana wanakuja kwangu kila siku kuteka maji. Wewe je, una uwezo gani?”

Basi mvua ikakasirika na kujisemea moyoni mwache, “huyu tuone na nguvu zake!” Mvua ikaacha kunyesha mto ukakauka kabisa. Mto ukakosa la kufanya ukasikitika na kuhakikisha ukisema, wenyewe bila mvua si kitu.

summer-river rain

ENGLISH: THE STORY OF THE RIVER AND THE RAIN

In the past, one day, the river and the rain disputed. The river boasted and despised the rain and said to it, “Behold how powerful I am. I am full of water and I am flowing and I prevent people from crossing. ”

The rain answered, “Without me you are nothing.” The river replied, “I have always been there in the past. I have been full of water and power. People have continued to praise me from centuries to centuries. For they come to me every day to fetch water. What can you to do?”

Then the rain became angry and said in its heart, “Let us see who has power!” It stopped raining for years. The river had nothing to do. It dried up. It proved by itself the saying that the river without the rain is nothing.

 

131. NTEMI NG’HWAYA

Collected by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey  (African Proverbs, Sayings and Stories)

Olihoi Ntemi uyo agabhinha bhanhu bhakwe mitihani kugiki gubhapandika abho bhalinikujo (masala). Imitihani yiniyo yaliibhalolile abhang’wi noi bha walwa, (bhalevi) na abhaduti (bhabehi) bha Njemu. Bhuli igele agalinha ng’ombe iyoilinda.

Untemi agabhawila, “Nang’winhaga ng’ombe iyoilinda bhuliigele. Mlinawiyabhi bho gwita umomutogelilwe ahigulwa ya ng’ombe iyo nang’winhaga.”

Iligele lya bhalevi bhali bhanhu mpungati. Bhagayomba, “UNtemi udinhaga ng’ombe. Duyibhulagagi ing’ombe yiniyo kugiki dulye nyama.” Nghana bhagayibhulaga ing’ombe yiniyo na bhagamfunya ung’wana (indama) bhiyiigwa gwandya guyocha indama yiniyo na yufuada gochiwa inyama yose.

Abhalevi bhenabho bhalibhazunya giki, Untemi agulilumba iligele kulwa guilya inyama yose bho nduhu gulilekeela ipande lyose lyose lya nyama yiniyo. Kunamna yiniyi iligele ligwendelea chiza noi. Nghana bhagayilya ing’ombe ngima nu ng’wana oyo. UNtemi oliabhalolile duhu kugiki abhone nani alina  masala.

Abhabehi bha njemu bhali bhatano, bhagayomba, “Dinhiwagwa ng’ombe yiyi nu Ntemi na ilinda nhale noi. Dudizuyibhulaga, duyilekagi mpaga ibyale tamu.”

Abhabehi bha njemu bhenabho bhagizunilija giko. Hanuma yaho, ing’ombe igabyala ndama. Jubhiza lulu ng’ombe ibhili, ninayo ni ndama.

Abhabehi wa njemu bhagayomba, “Dujijinje ing’ombe jiniji bho gujikabhanya na mbuli. Ulu dulajipandike imbuli, dugudula gugabhanha umubhise. Bhagadula ugukabhanya na mbuli inne.

Untemi Ng’hwaya agayomba, “Abhabehi bha njemu bhalina masala kulebha abhalevi bha walwa, ku nguno bhadayibhulagile ing’ombe iyoyalinda. Uguyibhulaga ing’ombe iyo ilinda, ilisawa na gujibhulaga ng’ombe ibhili.”

KISWAHILI: MFALME NG’HWAYA

Kulikuwepo na Mfalme (Mtemi) aliyewapa watu wake mitihani ili kuwapata wale wenye busara. Mitihani hiyo ililengwa kwa walevi na wavuta bangi. Kila kundi alilipatia ng’ombe mwenye mimba.

Mtemi aliwaambia,  “Nimewapa ng’ombe mmoja mwenye mimba kila kundi. Muko huru kufanya mpendavyo kuhusu ng’ombe niliyowakabidhi.”

Kundi la walevi lilikuwa na watu saba. Wakasema,  “Mtemi ametupatia ng’ombe. Tumwue ng’ombe huyo ili tule nyama.” Kweli walimwua yule ng’ombe na kumtoa yule mtoto (ndama). Wakakubaliana kuanza kumchoma yule ndama na ikafuatia kuchomwa nyama yote.

Walevi hao waliamini kwamba, mtemi atakishukuru kikundi, kwa kula nyama yote bila kubakiza sehemu nyingine ya mnyama huyo. Kwa jinsi hii kikundi kitaendelea vizuri zaidi. Kweli walimla ng’ombe mzima na mtoto wake. Mtemi alikuwa amewatazama tu ili aone nani ana akili.

Wavuta bangi walikuwa watano, wakasema, “Tumepewa ng’ombe huyu na Mtemi na ana mimba kubwa sana. Tusimwue, tumwache hadi azae kwanza.” Wavuta bangi hao wakakubaliana hivyo. Baadaye ng’ombe akazaa ndama. Wakawa sasa ng’ombe wawili, mama na ndama.

Wavuta bangi wakasema “Tuwauze ng’ombe hao kwa kubadilishana na mbuzi. Tukisha wapata mbuzi, tutaweza kugawana baina yetu. Walifanikiwa kubadilishana na mbuzi wanne.

Mtemi Ng’hwaya alisema, “Wavuta bangi wana akili kupita walevi wa pombe, kwa sababu hawakumwua ng’ombe mwenye mimba. Kumwua ng’ombe mwenye mimba, ni sawa na kuwaua ng’ombe wawili.”

cow-2

ENGLISH: KING NG’HWAYA

There was a king who used to give his people tests to find those who were wise. These tests were directed to drunkards and marijuana smokers.  He gave to each group a pregnant cow.

Then the king told them, “I have given to each group a pregnant cow. You are free to do whatever you want with the cow that I gave you.”

A group of drunkards had seven people. They said, “The king has given us a cow. Let us kill the cow for us to eat meat.” They actually killed the cow and took the calf out. They agreed to start roasting the calf and then followed the meat of the cow.

The drunkards believed that the king would appreciate the group for eating all the meat without leaving some. In this way, they thought, they would be regarded to be wiser.  So, they ate the whole cow and the calf. The king just watched them to see which group was wise.

Marijuana smokers were five. They said to each other, “We have been given this cow with a big foetus. Let’s not slaughter her, we leave her until the calf is born first.” The marijuana smokers unanimously agreed on that. Later, the cow gave birth to a calf. There were now two cattle, a mother and a calf.

Marijuana smokers, “Let us sell those two cows by exchanging them with goats. Once we have goats, we’ll be able to divide among ourselves. They managed to exchange them with four goats.

Then King Ng’hwaya said, “Marijuana smokers are more intelligent  than drunkards because they did not kill a pregnant cow. They knew that to kill a pregnant cow is the same as killing two cattle.”

130. JIGANO JA NG’WA ZAKARIA

Collected by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey  (African Proverbs, Sayings and Stories)

Alihoi munhu umo nzunya uyo oliobhatijiwa kale, ilina lwakwe Zakaria Shikolo. Olinsuluja. Amiganiko gakwe pye galigalolile kubhusuluja bhokwe duhu.

Nulu lushiku ulomfungo uwei UShikolo adapandile uwasa ubho guja gujusalila. Abhazunya bhiye ahobhashika gumshauri asalile, adabhadililile nulu hadoo. Agabhashokeja, “Unene Nadina wasa imilimo iliminghi, hangi nadizile aha gutangaja nhulu jawiza, (injili) gubheja lina, uwikaji bhuli sabho duhu.”

Nose UShikolo agapandika sabho ninghi kufumila umo bhusuluja bhokwe. Agiyangula gulima lingunda lya bhulubha. Kubahati ya wiza, UShikalo agapona noi gubhitilija.

Nanghwe uigimba gubhitilija. Agayomba, “Ihaha,  nahilile nali mhola gete, nali ngosha namala makoye. Ihaha nahilile.” Inhungulume uluiguta, igahilaga. Naise bhanhu uludupandika dugahilaga, dugigimbaga, dugadosoga kubhitilija mpaga nulu gung’wibha UMulungu, ihaha nahilile.

Aliyo UMulungu agang’wila, “Ubhebhe uli mbuuli gubhitilija ali? Lelo bhujiku inholo yako igusolwa. Ighinhu jinijo ijo wikumingila gigubhiza ja ng’wanani?” Ukujileka jibhunile fungo, utuja najo.

KISWAHILI: HADITHI YA ZAKARIA

Alikuwepo mtu mmoja mkristu aliyebatizwa zamani, jina lake Zakaria Shikolo, alikuwa mfanya biashara mawazo yake yote yalielekea kwenye biashara yake tu. Hata siku za jumapili yeye Shikolo hakupata nafasi ya kwenda kusali.

Wakristo wenzake walipo fika kwake ili kumshauri asali, hakuwajali hata kidogo, akawajibu, “Mimi sina nafasi shughuli ni nyingi, tena sikuja hapa kutangaza injili (kubeja lina) maisha ni mali tu.”

Sasa mwishowe Shikolo alipata mali nyingi kutokana na hiyo biashara yake. Akaamua kulima shamba la pamba, kwa bahati nzuri Shikolo akavuna mno kupita kiasi.

Naye akajivuna mno kupita kiasi, akasema, “Sasa nimewika, ni mzima kabisa, nimwamume nimemaliza matatizo.” Sasa nimewika, jogoo akishiba anawika, hata sisi watu tukipata tunawika, tunajigamba, tunajivuna kupita kiasi hata kumsahau Mungu, (Ihaha nahilile) Sasa nimewika.

Lakini Mungu akamwambia, ‘Wewe ni mjinga wa kiasi gani? Leo usiku roho yako itachukuliwa na vitu vile vyote ulivyojikusanyia vitakuwa vya nani?’ Utaviacha vikiwa vimezidisha uzito wake kwenye vining’iniza vyakula, hutaenda navyo.

man-3

adult-1

 

ENGLISH: THE STOTY OF ZACHARIA THE TRADER

There was a newly baptized Christian, named Zacharia Shikolo, who was a businessman. He was was always thinking about his business. Even on Sunday, Shikolo did not have time to pray.

When his fellow Christians came to him to advise him, he did not care at all. He replied, “I have no time. There are so many things to do., I have not come here to preach the gospel (to make a name).”

Now, Shikolo finally got a lot of wealth from his business. He decided to grow cotton in a big farm.Fortunately, Shikolo harvested a lot that year.

As a result, he became so arrogant. He said, “Now I have got wealth and excellent life. I have finished all the trouble. Now I have got wealth. I am like the cock that has eaten to satisfaction. I can crow.  Even we people when we get wealth, we can crow. Now I have got wealth. Everything is over.”

But God said to him, “How foolish you are. Today in the evening, your soul will be taken away and for whom will all the things you have gathered be? You will leave them behind.” Luke 12:15-21.

129. NG’WANIKI MARIA

Collected by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey  (African Proverbs, Sayings and Stories)

Olihoi ng’waniki umo ilina lwakwe, Maria, uyo olina miaka ikumi nitandatu. Agikala musi ya Misri. Umo wikaji bhokwe olina nhungwa mbi noi ya bhulamba. Agabhiza agubhalondejaga bhanajeshi bhuli kwene uko bhajaga.

Nhangala ninghi witanagwa nu Mulungu anshokele aliyo kulwa gutongelwa na wikumbwa bhokwe bhubhi agaduuma.

Lushugu lumo agaja kuliKelesiya lwa Yerusalemu mulikanisa lwa ng’wa ntakatifu Ana. Ahoogema hangi na hangi ugunshindeka umunanyango kulo nguzu aliyo hei! Yalihoi nguzu iyo yanemejaga ugwingila.

Aho obhona giki odumaga ugwingila umu likelesia, agaja kusanamu ya ng’wa Bikira Maria, iyo yalibihi nu wei. Utuja mazwi na gulomba wambilijiwe kugiki apandike gugalucha inhungwa jakwe ijabhubhi.

Agagaluka nghana. Agandya gulila kunguno ya shibhi jakwe. Gwandija lushiku lunulo, ugwigwa moto go bhutogwa bho ng’wa Yesu umugati yakwe.

Agajileka ishibhi jakwe, na agandamiila Yesu Kristo. Agaja mulibambasi gujiluhya na gusalila.

Agabhiza Ntakatifu na aginhiwa jipaji ja gubhatongela bhanhu higulya ya gwikala wikaji bhutakatifu. Bhamsenyele na bha Badri bhagaja gujumona na gundegeleka. Agang’wizuka Yesu.

Bhuli lushiku isala yakwe, yali Yesu! Yesu! Yesu! Niyabhiza bhuyegi ile duligwe Ililaka lwako.

KISWAHILI: MCHANA MARIA

Alikuwepo msichana mmoja jina lake Maria, mwenye umri wa miaka kumi na sita. Aliishi katika nchi ya Misri. Katika maisha yake alikuwa na tabia mbaya sana ya umalaya. Akawa anawafuata wanajeshi kila mahali wanapokwenda.

Mara nyingi aliitwa na Mungu kutubu na kumrudia, lakini kwa sababu ya kutawaliwa na tamaa mbaya alishindwa. Siku moja alikwenda Yerusalemu kwenye kanisa la Mtakatifu Anna.

Alipofika kwenye mlango wa kanisa hilo, alijaribu kuingia lakini alishindwa. Alijaribu tena na tena kuusukuma mlango kwa nguvu lakini wapi! Kulikuwepo na nguvu iliyomzuia kuingia. Alipoona ameshindwa kuingia kanisani, akaenda kwenye sanamu ya Bikira Maria, iliyokuwa karibu naye, akapiga magoti na kumwomba msaada ili apate kubadili tabia yake mbaya.

Alibadilika kweli, akaanza kulia kwa sababu ya dhambi zake. Tangu siku hiyo, aliusikia moto wa upendo wa Yesu ndani yake. Akaziacha dhambi zake, na akamng’ang’ania Yesu  Kristo.

Akaenda jangwani kujitesa kwa kufunga na kusali. Akawa mtakatifu na akapewa kipaji cha kuwaongoza watu namna ya kuishi maisha ya Utakatifu. Maaskofu na mapadri walikwenda kumwona na kumsikiliza. Alimkumbuka Yesu. Kila  siku sala yake ilikuwa Yesu! Yesu! Yesu! Ingekuwa heri leo tusikie sauti yako.

madonna-

 

ENGLISH: THE CALLED GIRL MARY

There was a girl named Mary, who was sixteen years old. She lived in  Egypt. She lived life of prostitution. She followed the soldiers everywhere they went.

She was often called by God to repent and return to Him, but because of her evil desires, she failed. One day, she visited Jerusalem particularly the church of Saint Anna.

When she came to the church door, she tried to enter but she failed. She tried again and again to push the door with all her power but she failed! There was a force that prevented her from entering. When she saw that she was not able to enter the church, she went to the image of the Virgin Mary that was next to her. She knelt down and asked to help to change her bad conduct.

She truly changed and began to cry as repentance of her sins. From that day, she felt the fire of Jesus love in her. She left her sins, and looked upon Jesus Christ for guidance.

She could go to the wilderness to fast and pray. She became holy and was given the gift of leading people to live a holy life. The bishops and priests frequently went to see her and listen to her. She always remembered Jesus. Every day, her prayer was Jesus! Jesus! Jesus! It would be better today for us to hear your voice.

 

128. NAMHALA NGUGU

Collected by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey  (African Proverbs, Sayings and Stories)

Myaka minghi yabhitaga ihaha. Olihoi namhala umo uyo olingugu noi. Akanamhala akagugu kenoko kagazumalika umusi. Agachalwa kumoto kulwa nguno ya bhugugu bhokwe.

Ahenaho UMulungu na bhamalaika abhalindi bha namhala ng’wunuyo bhagachola ulu lilihoi lyito limo ilyawiiza ilo akanamhala akagugu kagapandika gulyita umubhulamu bhokene.

Bhagabhulucha giki lushigu lumo umu wikaji bhokwe agang’winha munhu nhabhi nti go jitungulu jimo jaguhamba bho nduhu gulomba ja gulipwa. Mulungu agantuma malaika asole nti gojitungulu kugiki gung’hilija unamhala ungugu ukumoto kugiki adimile na gwipija gwinga mumoto.

Umalaika agatimija giko, nu namhala ungugu ng’wunuyo agipija umumoto. Gashinaga abhangi ukumoto kunuko aho bhabhona wasa bhunubho bhogwipija, bhagidamilija kukanamhala.

Ahenaho ubhugugu bhokene bhugang’wiziila hangi. Witingisha na gubhapanda bho magulu abhangi mpaga bhakije ugubhupandika uwasa bhunubho ubho gugudima unti ugojitungulu na bhakije ugwiningeleja ukuliwei.

Kulwa nguno ya witingisha bho namhala ungugu, unti gugatinika na bhose bhagagwa hangi mumoto. Ubhukamu bho ng’wa malaika bhugabhiza bhule gete. Unamhala ungugu adadulile ugupila.

UYesu agaduhugula dubhize na nholo ya gwilekeja. “Mudizulamula, naying’we mudulamulwa, mudizusaila, naying’we mudusailwa, lekelaji, naying’we mugukelwa, bhinhagi abhanhu ghinhu, naying’we mugwinhiwa…kulwa nguno, ingele iyo mulibhagelekela hiiyo mlagelekelelwa.”

Dimana aise ulu dugekelelwa ingele iise iya wimi nholo, na whiilu na bhukolwa! Dudadulile ugupila. Kuyiniyo, makanza gose dizuke, uMulungu adaladulekeja aise uludukije ugubhalekeja abhadugu bhise bho nholo.

KISWAHILI: KIZEE BAHILI

Miaka mingi imepita sasa kulikuwa na mzee mmoja aliyekuwa bahili sana. Kizee huyo Bahili alifariki dunia, akapelekwa motoni  kwa sababu ya ubahili wake.

Hapo Mungu na  malaika mlinzi wa mzee huyo walitafuta kama kuna tendo moja jema ambalo mzee bahili alipata kulitenda wakati wa uhai wake. Waligundua kwamba siku moja katika maisha yake alimpa maskini mche wa kitunguu bila ya kudai malipo.

Mungu akamtuma malaika achukue mche wa kitunguu ili kumnyoshea mzee bahili kule motoni ili akishike na kujiokoa kutoka motoni. Malaika akatekelaza hivyo, na yule mzee bahili akajiokoa katika moto.

Kumbe wengine huko motoni walipoiona nafasi hii ya kuokoka, wakajibandika kwa mzee. Hapo ubahili wake ukamjia tena. Akajitikisa na kuwakanyaga kwa miguu hata wengine wasipate nafasi ya kushika ule mche wa kitunguu wala kujishikiza kwake.

Kwa sababu ya  mtikisiko wa mzee bahili, ule mche ulikatika na wote wakaanguka tena motoni. Bidii ya malaika ilikuwa ni bure kabisa. Mzee bahili hakuweza kuokoka.

Yesu anatuonya kuwa na moyo wa kusameheana: Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa, msilaumu, nanyi hamtalaumiwa, acheni, nanyi mtaachiliwa, wapeni watu vitu, nanyi mtapewa….. kwa kuwa  kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

Ole wetu tukipimiwa kipimo chetu cha uchoyo, na wivu na chuki! Hatuwezi kuokoka. Kwa hiyo daima tukumbuke, Mungu hatatusamehe sisi tusipowasamehe ndugu zetu  kwa moyo.

closeup

begging-

 ENGLISH: THE STINGY OLD MAN

Many years have passed since there was an old man who was very stingy. One day, such a stingy old man died. He was taken to hell for his stinginess.

Then God and the guardian angel of the old man sought if there was one good act that the old man had done in his lifetime. They found that one day in his life he gave a small piece of onion to the poor without demanding a payback.

God sent the guardian angel to take a piece onion seedling to the old man in the fire. Should he catch it, he could save himself from the fire. The angel did so, and the stingy old man saved himself from the fire.

While some other people in the fire saw this opportunity to be saved, they attached themselves to the old man. Then his stinginess came to him again. He shook and kicked them with his feet until others did not have a chance to touch the onion.

As a result of shaking, the stingy old man fell and all other people fell back into the fire. The angel’s commitment was completely useless. The stingy old man could not be saved.

Jesus warns us to have a forgiving heart: Judge ye not, and ye shall not be judged; condemn ye not, and ye shall not be condemned; the measure you use to others is the same one which will be applied to you.

Woe to us when we have greed, envy and hatred! We cannot be saved. So let us always remember, God will not forgive us unless we forgive our brothers by heart.