zakaria Kashinje

776. SHILI MU MHINDA YA NG’WIYO UTUSHIMANA.

Imbuki ya lusumo lunulo, ilolile bhudamu bho gujimana iginhu ijo jili mumhinda ya ng’wiyo. Iginhu jinijo, jigikalaga jibhisile ukubhanhu abho bhali bhadibhinhikile mhinda yiniyo, kunguno bhadajidebhile ijo jatuulwa moyi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “shili mu mhinda ya ng’wiyo utushimana.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali na widohya bho gugadegeleka amiganiko ga bhanhu bhakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agahoyaga chiza na bhiye kunguno adebhile igiki galihoyi miganiko miza umumioyo ya bhiye bhenabho ayo adagadebhile. Uweyi agatumamaga milimo kihamo na bhiye bhenebho, kunguno ya widohya bhokwe.

Ijokolo ijo jili mumhinda ya ng’wiyo jinijo, jigikolaga na miganiko ayo gali mumoyo go ng’wiyo, kunguno nago udugamana mpaka ubhize na widohya bho gubhadegeleka abhiyo umumahoya gabho. Umunhu uyo alina widohya agabhadegelekaga abhiye umumahoya gakwe. Hunagwene agabhawilaga abhiye bhenabho giki, “shili mu nhinda ya ng’wiyo utushimana.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na widohya bho gwikala na bhichabho chiza, umukikalile kabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umubhutumami bho milimo yabho, shigu jose.

1 Wakorintho 2:11-12.

KISWAHILI: KILICHOMO MFUKONI MWA MWENZAKO HUTAKIFAHAMU.

Chanzo cha methali huo, chaangalia ugumu wa kukihafahamu kitu kilichomo mfukoni mwa mwenzako. Kitu hicho, huwa kimefikichika kwa wengine kwa sababu hawafahamu kile kilichowekwa ndani yake. Kitu hicho hufahamika kwa yule aliyeweka kwenye mfuko huo, ambaye ndiye mwenye mfuko huo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “klichomo mfukoni mwa mwenzako hutakifahamu.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana unyenyekevu wa kuyasikiliza mawazo ya watu wake, katika maisha yake. Mtu huyo, huongea na wenzake vizuri, kwa sababu anafahamu kwamba mawazo yaliyomo ndani ya mioyo ya wenzake hao hawezi kuyafahamu, asipoongea nao na kuwasikiliza kwa makini. Yeye hufanya kazi zake kwa ushirikiano na wenzake kwa sababu ya unyenyekevu wake huo.

Vitu vilivyomo mfukoni mwa wenzako, hufanana na mawazo yaliyomo moyoni mwa mwenzako, kwa sababu nayo huyafahamu mpaka uwe na unyenyekevu wa kumsikiliza vizuri. Mtu mwenye unyenyekevu huo, huwasikiliza wenzake katika maongezi yao. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “kilichomo mfukoni mwa mwenzako hutakifahamu.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na unyenyekevu wa kuishi na wenzao vizuri, katika maisha yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika utekelezaji wa majukumu yao, siku zote.

1Wakorintho 2:11-12.

ENGLISH: YOU WILL NEVER KNOW WHAT IS IN YOUR FELLOW’S POCKET.

 

The above proverb looks at the difficulty of recognizing something which is in your partner’s pocket. Such object is hidden from others because they do not know it. It is however known to the person who placed it in such pocket, who is the owner of it. That is why people say, “You will never know what is in your fellow’s pocket.”

This proverb is likened to a man who has humility to listen to thoughts of his people, in his life. He in turn, communicates well with his colleagues, because he realizes that the thoughts that are in the hearts of his colleagues cannot be understood, unless he speaks to them and listens attentively. He performs his duties in cooperation with his colleagues because of his humility.

The things which in your partner’s pocket are similar to the thoughts which in your partner’s heart, because you also cannot understand them until you have the humility to listen to him or her well. Such humble person listens to others during their conversations. That is why he tells people that, “you will never know what is in your fellow’s pocket.”

This proverb teaches people on how to be humble enough to live well with others, in their lives, so that they may always be more successful in carrying out their daily responsibilities.

1 Corinthians 2: 11-12.

775. NUMBU YA WIZA IDAPUNZAGWA.

Ulusumo lunulo lolola numbu iyo iliyawiza. Inumbu yiniyo, idapunzagwa kugunno idina nzuka. Gashinaga lulu, inumbu ijo jili na nzuka jiginginjiyagwa tamu inzuka jinijo, na jazugwa lulu. Ukulwande ulungi, inumbu iyo iliyawiza igasimbagwa na guzugwa duhu kunguno idinamadudu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “numbu ya wiza idapunzagwa.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina nungwa ja wiza umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, olangwa umana uyuitumama chiza imilimo yakwe, kunguno agikalaga chiza na bhanhu.  Uweyi agabhalangaga abhanhu bhakwe ahigulya ya guitumama chiza imilimo yabho bho gwikala chiza nabho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni numbu iyo iliyawiza, kunguno nuweyi aliowiza umukikalile kakwe na bhanhu. Uweyi alina mito ga wiza ukubhiye. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “numbu ya wiza idapunzagwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na nhungwa ja wiza ijo jidulile gubhambilija ugwikala chiza na bhichabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho. Yigeleliwe bhikomeje gwita mito ga wiza shigu jose.

Wagalatia 5:16-17.

KISWAHILI:  KIAZI KIZURI HAKIMENYWI.

Methali hiyo, yaangalia kiazi ambacho ni kizuri. Kiazi hicho, huwa hakimenywi kwa sababu hakikuingiliwa na wadudu. Kumbe basi, kiazi kilicho na wadudu huwa kinamenywa kwanza kwa ajili ya kuondoa sehemu yenye wadudu, ndipo kinapigwa. Kwa upande mwingine, kiazi kizuri huchimbwa na kupikwa tu, kwa sababu hakina na wadudu. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kiazi kizuri hakimenywi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye tabia njema, katika maisha yake. Mtu huyo, alishafundishwa namna ya kufanya kazi zake vizuri, kwa sababu ya yeye kuishi vizuri na watu. Yeye huwafundisha watu namna ya kuyatekeleza majukumu yao kwa kuishi nao vizuri.

Mtu huyo, hufanana na kile kiazi kizuri, kwa sababu naye ana tabia njema ya kuishi vizuri na wenzake. Ndiyo maana watu humwita kwamba, “kiazi kizuri hakimenywi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema ya kutenda mema, ili waweze kuishi vizuri wenzao na kupata mafanikio mengi maishani mwao. Wanatakiwa kuendelea kutenda mema siku zote.

Wagalatia 5:16-17.

potato1

sweet-potatoes

sweet-potato-

ENGLISH: A NICE POTATO IS NEVER PEELED.

This proverb looks at a potato that is good. Such potato is not peeled because it has not been invaded by insects. In fact, the insect-infested potato is first peeled to remove the insect-infested part, then it can be eaten. On the other hand, a good potato is dug and cooked only, because it is free from insects. That is why people say, “a nice potato is never peeled.”

This proverb is compared to a person who is well-mannered in his life. Such man was taught on how to fulfill well his daily activities. He is a model to others because of his sound behavior that instruct on how to behave in the societies. He teaches people how to fulfill their responsibilities by living well with them.

This person is like a good potato, because he also has a good habit of living well with his people. That is why those people call him, “a nice potato is never peeled.”

This proverb teaches people on how to have good morals, so that they can live well with each other and achieve great success in their lives. They should continue to do good things to their people always.

Galatians 5: 16-17.

774. YAPAMA BHUGONG’HO HUNA WA KOBHA MASANZU.

Ulusumo lunulo, lwandija kuli nsabhi o mitugo uyo oliadagitile chiza ulugutu imitugo jinijo. Umunhu ng’wunuyo olina mbuli ijo jikalaga mlugutu ulo nduhu mazangu.

Lushigu lumo, igingila subhi umulutu lo mbuli jakwe jinijo, yuyidima imo. Aho isubhi yiniyo yayisolwa imbuli yakwe, huna wandya guchola masanzu gaguluchibhila ulugutu lokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “yapama bhugong’ho huna wakobha masanzu.”

Ulusumo lunulo, lugalenganiyagwa kuli munhu uyo adibhegelejaga chiza hayo gatali ugumpandika amakoye, umukikalile kakwe. Umunhu ung’winuyo, agadumaga uguginja makoye genayo ulu gansanga, kunguno ya wilendeja bhokwe. Uweyi adatumamaga chiza imilimo yakwe, ulu gashigaga amakanza ga guja kumilimo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nsabhi o mitugo uyo agasojiwa mbuli yakwe na subhi, kunguno nuweyi adibhegelejaga haho gatali ugunpandika amakoye, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “yapama bhugong’ho huna wakobha masanzu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwibhegeleja chiza haho bhatali ugupandika amakaye, umukikalile kabho, kugiki bhadule gugahangija amakoye ayo galabhapandike, umuwikaji bhobho.

1 Petro 5:8-9.

KISWAHLI: AMEGONGA MLANGO NDIYO UMETAFUTA MIIBA.

Methali hiyo, ilianzia kwa tajiri wa mifugo ambaye hakulijenga vizuri zizi lake. Mtu huyo, alikuwa na mbuzi waliokuwa wakiishi kwenye zizi lisilokuwa na mlango.

Siku moja, aliingia chui kwenye zizi hilo akachukua mbuzi mmoja. Chui huyo alipompeleka yule mbuzi, ndipo yule tajiri akaanza kutafuta miiba ya kufungia kwenye mlango wa mbuzi wake hao. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “Amegonga mlango ndiyo unatafuta miiba.”

Methali hiyo, hulinganisha kwa mtu yule ambaye hajiandai vizuri kabla hajapata matatizo, katika maisha yake. Mtu huyo, hushindwa kuyatatua matatizo yanayompata kwa sababu ya kujisahau kwake. Yeye hafanyi kazi unapofika wakati wa kuzitekeleza kazi hizo.

Mtu huyo, hufanana na yule ambaye chui alimchukulia mbuzi wake, kutokana na kujisahau kwake, kwa sababu naye hujisahau kujiandaa mpaka matatizo yanamkuta, ndipo anaanza kuhangaika kutafuta ufumbuzi. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “amegonga mlango ndiyo unatafuta miiba.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujiandaa vizuri kukabiriana na matatizo mbalimbali kabla hayajawapata katika maisha yao, ili waweze kuyatatua yanapowakuta, maishani mwao.

1 Petro 5:8-9.

 

leopard subhu

goats

goats2

ENGLISH: IT HAS KNOCKED ON THE DOOR WOODS THEN YOU HAVE LOOKED FOR DOOR CLOSING THORNS (ONE SHOULD BE RESPONSIBLE FOR ONE’S ACTIONS).

The overhead proverb began with a wealthy cattle man who did not build his barn well. He had goats that lived in a barracks without a door.

One day, a leopard entered into the barn and took one of the goats. Then such rich man began to look for thorns to lock in the door of his goats. That is why people said to him, “it has knocked on the door woods then you have looked for door closing thorns.”

This proverb is compared to a person who is unprepared before he/she has a problem, in life. Such person, in turn, becomes unable to solve those problems that befall him/her because of his/her forgetfulness. He/she does not work when it comes time to carry out those tasks.

This person is similar to the one whom the leopard took from him his goat, due to his forgetfulness, because he also forgets to prepare himself until problems befall him then he begins to struggle to find a solution. That is why people say to him, “it has knocked on the door woods then you have looked for door closing thorns.”

This proverb teaches people on how to prepare well to deal with various problems before they get into their lives, so that they can solve them when they find them, in their lives.

1 Peter 5: 8-9.

 

772. NTI GO MHELA GUTAPILILAGWA KABHILI.

Ulusumo lunulo lulolile munhu uyo obhitaga ng’wipolu lya ndimu nhali. Abhiye bhagang’wila, “udizubhite ung’wipolu linilo kunguno jilihoyi ndimu nhali noyi.” Uweyi agashosha, “ulujunitula nagupela.” Umunhu ng’wunuyo, ahongila duhu moyi, agatulya na ndimi mhali upela mpaka ugapilila ha nti go mhela.

Abhanhu bhung’wila hangi giki adizubhite hangi ung’wipolu linilo, kunguno unti uyo upilila gunuyo, gutapililagwa kabhili. Hunagwene bhagang’wila giki, “nti go mhela gutapililagwa kabhili.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo oliohubha ulekejiwa, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, aho ohubha adalomba bhulekejiwa, ubhupandika. Aliyo lulu, agabhiza atali uhadikija guhubha hangi, kunguno ya wikolosha bhokwe. Uweyi agabhikoloshaga abhiye kunguno ya gwiganika giki bhagunhekeja duhu.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agatulwa na ndimu ugapilila hanti go mhela, kunguno  nuweyi agahubha uelekejiwa, umukikalile kakwe. Aliyo lulu, agabhiza atali ubhikolosha abhiye agwiganikaga giki, agulomba alekejiwe hangi. Hunawene abhanhu bhagang’wilaga giki, “nti go mhela gudapiligwa kabhili.”

Ulusumo lunulo, lolanda bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja gubhikolosha abhichabho, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho bhenebho, umuwikaji bhobho.

Luka 17:11-19.

KISWAHILI: MTI WA KIFARU HAUPONEWI MARA MBILI.

Methali hiyo, humwangalia mtu yule aliyekuwa akipita kwenye poli la wanayama wakali. Wenzake walimwambia, “usipite kwenye poli hilo kwa sababu kuna wanyama wakali.” Yeye alijibu, “wakinifuata nitakimbia.”  Mtu huyo, alipoingia kwenye poli hilo, alifukuzwa na mkali akaenda kuponea kwenye mti wa kifaru.

Watu walimwambia kwamba asipite tena kwenye poli hilo la wanyama wakali, kwa sababu hawezi kuponea tena kwenye mti huo. Ndiyo  maana watu hao walimwambia kwamba, “mti wa kifaru hauponewi mara mbili.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye alikosea, kwa mara ya kwanza akasamehewa, maishani mwake. Mtu huyo, alipokosea aliomba msamaha, akaupata. Lakini basi, alikuwa bado akifanya makosa tena kwa sababu ya ukolofi wake. Yeye huwachokoza wenzake kwa sababu ya kufikiria kwamba, wenzake hao watamsamehe tu.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyefukuzwa na mnyama mkali akaponea kwenye mti wa kifaru, kwa sababu naye alikosa akasamehewa, matika maisha yake. Lakini ja ajabu bado anawachokoza wenzake akifikiria kwamba atasamehewa tena. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mti wa kifaru hauponewi mara mbili.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia za uchokozi, katika maisha yao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.

Luka 17:11-19.

rhenox.1

man1

tree-3842194__480

ENGLISH: THE RHINOCEROS TREE CANNOT SAVE SOMEONE TWICE (GOLDEN CHANCE NEVER COMES TWICE).

The above proverb looks at the man who was passing through the forest of wild beasts. His colleagues told him, “Don’t pass through that forest because there are wild animals.” He replied, “If they follow me, I will run away.” When he entered it Rhino chased him until he escaped by climbing at a tree.

People told him not to go back through that wild beast forest, because he could not escape from death by using that tree again. That is why the people told him, “the rhinoceros tree cannot save twice.”

The proverb is likened to a man who did wrong for the first time and got forgiveness in his lifetime. Such man apologized after doing wrong. But then he was still making mistakes again because of his cruelty. He irritates his colleagues because of thinking that they would only forgive him.

The man is like the one who was chased away by the wild beast and escaped by climbing at the rhinoceros tree, because he too had sinned and was forgiven, in the course of his life. But strangely enough, he still provokes his colleagues, thinking that he will be forgiven again. That is why people say to him, “the rhinoceros tree cannot save twice.”

This proverb teaches people to stop aggressive behavior, in their lives, so that they can live in peace with each other, in their lives.

Luke 17: 11-19.

762. JANDUGUYO JANUKULAGE NA BHUYEGI: ULIHAYA JIGABU WALIMA NANGHWE?

Imbuki ya lusumo lunulo, ingilile kuli munhu uyo aginhiwa jikolo na ng’wiye uyo olinduguye. Aho winhiwa ijikolo jinijo, agakija ugulumba kunguno uliojidalahija. Uweyi wigongejaga gwinhiwa jikolo ijo jidulile gokala mujigabu guti giki bhajilima nanghwe umunhu ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “janduguyo janukulage na bhuyegi: ulihaya jigabu walima nanghwe?”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adina bhulumbi ukubhiye abho bhagangunanaga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhadalahijaga abhiye abho bhagangunanaga bho gujibyedeleja ijikolo ijo bhagang’winhaga. Uweyi agajibhonaga jidololo bhuli jene ijo bhaling’winha abhiye, kunguno agigongejaga winhiwe jikolo jitale gukila ijo bhang’winhaga jinijo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo aginhiwa jikolo na nduguye, ujidalahija, bho gwigongeja winhiwe ijo jokalile mujigabu, kunguno nuweyi adalumbaga ulu bhang’wambilija abhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene bhagang’wilaga giki, “janduguyo janukulage na bhuyegi: ulihaya jigabu walima nanghwe?”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhulumbilija ulu bhinhiwagwa jikolo nulu jigabhiza jigehu na ginehe, kugiki bhadule gwikala chiza na bhanhu bhabho, umuwikaji bhobho. Idichiza ugujidalahija ijikolo ija gwinhiwa na bhichabho.

Bhaebrania 12:28.

KISWAHILI: CHA NDUGUYO KIPOKEE KWA FURAHA (KATIKA TUNGA):  WATAKA KAPU ULILIMA NAYE?

Chanzo cha methali hiyo, kilianzia kwa mtu aliyepewa kitu na ndugu yake. Alipopewa kitu kicho hakushukuru kwa sababu alikidharau, kuwa ni kidogo. Alitaka apewe kitu kikubwa cha kuweza kujaa kwenye kapu kana kwamba, walilima naye ndugu yake huyo. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “cha nduguyo kipokee kwa furaha (katika tunga): wataka kapu ulilima naye?”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hana shukrani kwa wenzake wanaomsaidia, katika maisha yake. Mtu huyo, hukidharau kitu anachosaidiwa kwa kupewa na wenzake. Yeye huviona kuwa ni kidogo kila kitu anachopewa na wenzake, kwa sababu ya kutaka apewe kikubwa zaidi kupita kile alichopewa.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyepewa kitu na ndugu yake, akakidharau, kwa kutaka apewe kikubwa cha kujaa kapu, kwa sababu naye hashukuru anapopewa vitu na wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “cha nduguyo kipokee kwa furaha (katika tunga): wataka kapu ulilima naye?”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na moyo wa shukrani kwa wale wanaowasaidia kwa kuwapatia vitu mbalimbali, hata kama vikiwa vidogo kiasi gani, ili waweze kuishi vizuri na wenzao, maishani mwao. Siyo vizuri kukidharau kitu cha kupewa na wenzao.

Waebrania 12:28.

farmer2

farmer african-girl

african-women-walking-along-road

ENGLISH: BE  CONTENT  TO  RECEIVE  WHATEVER  THE  AMOUNT  OF  SOMETHING  YOU  ARE  GIVEN.  THIS IS BECAUSE  YOU  DID NOT WORK   FOR  IT (RECEIVE THOSE OF YOUR RELATIVES WITH JOY: YOU WANT THE BASKET DID YOU CULTIVATE WITH THEM?)

The overhead proverb originated from a man who was given a gift by his brother. He was was not grateful because he despised such gift by considering it as a small thing. He wanted to be given a big one enough to fill the basket as if he cultivated together with his brother. That is why people said to him that, “be  content  to  receive  whatever  the  amount  of  something  you  are  given.  This is because  you  did not work   for  it.”

The proverb is likened to a man who has no appreciation to his fellow human beings who help him, in his life. Such person, in turn, despises the gifts that are given to him by his peers. He considers them as small things, because he wants to be given more than what he received.

This person resembles the one who despised what his brother gave to him, by remanding something bigger than that, because he also did not appreciate the gifts which were given to him by his fellows. That is why people tell him, “be  content  to  receive  whatever  the  amount  of  something  you  are  given.  This is because you did not work   for  it.”

This proverb instills in people an idea on how to be grateful to those who help them in various ways, no matter how small their helps can be, so that they can live well with each other, in their lives. It is not good to look down on others.

Hebrews 12:28.