Sukuma Sayings

741. BHAGOYANGI BHADINA MBINA NDO.

Akahayile kenako, kalolile bhabhini bha mbina abho bhagitanagwa bhagoyangi. Abhabhini bhenabho, bhagafunyama nzoka ulu bhandya ugubhina mbina jabho. Abhanhu bhenabho, bhaga muchalo jilebhe bhugajifunya nzoka jabho jinijo, aliyo bhali hoyi bhanhu bhadadu duhu ahenaho.

Hunagwene abhanhu aho bhabhona chene bhagayomba giki, “bhagoyangi bhadina mbina ndo.” Ubhunubho huna bhub’iza wandijo bho kahayile kenako, kunguno, abhab’ini abhangi bhagafunyaga nzoka ulu bhanhu bhukwila aha mbina yiniyo.

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumilaga nguzu ningi, ku jikolo jidoo, nulu umugutumama nimo ndoo, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adulile nulu gubhucha ngong’ho gujupigila mhumbi, kunguno adadebhile ugulinganija ijilanga jakwe ni ndimu iyo aligibhulaga. Uweyi agatumamaga imilimo yakwe gitumo alitogelwa, kunguno ya wangu bhokwe bho gupelana, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga na bhagoyangi abho bhagafunyaga nzoka ulu bhandya ugubhina nulu bhagab’iza bhalihoyi bhanhu bhatatu du hoyi, kunguno nuweyi agatumilaga nguzu ningi nulu alitumama nimo ndoo duhu. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki,  “bhagoyangi bhadina mbina ndo.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na masala ga gulinganija chiza imiliimo yabho, umukikalile kabho, kugiki bhadizumala nguzu jabho sagala, umuwikaji bhobho.

Mathayo 18:20.

Mathayo 13:31.

WAGOYANGI HAWA NA NGOMA NDOGO.

Msemo huo, ulianzia kwa wacheza ngoma wanaoitwa wagoyangi. Wagoyangi hayo ni wana mchezo wa ngoma ya kutumia nyoka. Watu hao, huwatoa hao nyoka wanapoanza tu kucheza. Hivyo, watu hao walifika kwenye kijiji kimoja, ambapo waliwatoa nje hao nyoka nje wakati watu waliokuwepo hapo walikuwa wawili tu.

Ndiyo maana watu walipoona hivyo, walisema, “wagoyangi hawana ngoma ndogo.” Huo ndiyo ukawa mwanzo wa msemo huo, kwa sababu wachezaji wa makundi wengine, husubiri mpaka wawepo watu wengi zaidi, ndipo hufikia hatua ya kuwatoa nje hayo nyoka.

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutumia nguvu kubwa kwenye kitu kidogo, katika maisha yake. Mtu huyo, aweza hata kuchukua bunduki kwenda kuulia panzi, kwa sababu yeye hajui kulinganisha silaha zake na kitu anachoenda kukiua, maishani makwe.  Yeye hufanya kazi zake kwa kadiri anavyotaka, kwa sababu ya wepesi wake wa kukasilia.

Mtu huyo, hufanana na wagoyangi ambao hutoa nyoka nje kata kama kuna watu watatu tu kwenye ngoma yao, kwa sababu naye hutumia nguvu kubwa kwenye kazi ndogo, pia hukasilishwa hata na jambo dogo zaidi. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “wagoyangi hawana ngoma ndogo.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na akili ya kuwawezesha kutumia nguvu inayolingana na kazi wanazozifanya, katika maisha yao, ili wasizipoteze bure nguvu zao, maishani mwao.

Mathayo 18:20. “Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao.””

Mathayo 13:31. “Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa Mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua akaipanda shambani mwake.””

728. NAMUGI ADAB´IHAJA.

Akahayile kenako, kalolile munhu uyo alintale, nulu uyo ali namugi aha kaya yakwe. Olihoyi namhala umo uyo adimaga mitugo na bhana bhakwe. Lushigu lumo agajimija ng’ombe ubhabhuja abhana bhakwe, “nani uijimijije ing’ombe?” ung’wana ushosha, “ima lulu.” Unamhala ubhawila, “jaji mugaichole mpaga muyibhone.” Aho bhagaibhona bhudebha igiki unamhala huyo aijimija ng’ombe yiniyo, bhuyomba giki, “namugi adab’ihaja.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumilaga bhutale bhokwe bho gubhaluhya abhanhu bhakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhutumilaga ubhutale bhunubho bho gubhubhisa ubhunhana, kunguno ya kulang’hana ikujo lwakwe. Uweyi agitaga giko bho gubhasayila salaga abhanhu bhakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu namhala uyo agajimija ng’ombe ubhasayila na gubhaluhya abhana bhakwe, kunguno nu weyi agabhaluhyaga abhanhu bhakwe bho gubhubhisa ubhung’hana. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “namugi agab’ihaga.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhutumila chiza ubhutale bhobho, kugiki abhanhu bhabho bhadule gwikala na mholele ya gubhambilija guitumama chiza imilimo yabho. Abhanhu bhenabho igelelilwe bhabhize ni kujo kubhanhu bhose.

Zaburi 2:1-12.

Waebrania 6.1-4.

Ayubu 32:6b-7.

MZEE WA FAMILIA HAKOSEI.

Msemo huo, huangalia mtu yule ambaye ni mwenye madaraka au baba wa familia. Alikuwepo mzee mmoja aliyekuwa anachunga mifugo na watoto wake. Siku moja, alipoteza ng’ombe akawauliza watoto wake, “nani amepoteza ng’ombe?” Mmoja wa watoto akajibu, “simfahamu?” Akawambia, “nendeni mukamtafute mpaka mmuone.” Walipomuona waligundua kwamba, baba yao ndiye aliyempotea huyo ng’ombe, wakasema, “mzee wa familia hakosei.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatumia madaraka yake kwa kuwakandamiza watu wake. Mtu huyo, hutumia madaraka au nafasi yake hiyo katika kuuficha ukweli, kwa lengo la kulinda heshima yake mbele ya watu. Yeye huwalaimu hovyo watu wake.

Mtu huyo, hufanana na mzee mwenye watoto aliyepoteza ng’ombe akawasingizia watoto wake, kwa sababu naye huitumia nafasi yake ya ukubwa katika kuwakadamiza wale walioko chini yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba,  “mzee wa familia hakosei.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuitumia vizuri nafasi yao ya uongozi, ili waweze kuishi kwa amani ya kuwezesha kuyatekeleza vizuri majukumu yao. Watu hao, wanatakiwa kuwa na heshima kwa watu wote wanaoishi nao.

Zaburi 2:1-12. “Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na mataifa kula njama bure? Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya BWANA na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. Wanasema, ‘‘Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.’’ Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, “Nimemweka Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.’’ Nitatangaza amri ya BWANA : yeye aliniambia, “Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa Baba yako. Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa mali yako. Utawatawala kwa fimbo ya kifalme ya chumana kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.’’ Kwa hiyo, ninyi wafalme, iweni na hekima, mwonyeke, enyi watawala wa dunia. Mtumikieni BWANA kwa hofu na mshangilieni kwa kutetemeka. Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.”

Yoshua Bin Sira 3:12-14. “Mwanangu, umsaidia baba yako katika uzee wake, wala usipate kumhuzunisha siku zote za maisha yake. Akiwa amepungukiwa na ufahamu umwie kwa upole, wala usimdharau iwapo wewe u mzima sana; kwa maana sadaka apewayo baba haitaswahauliwa, na badala ya dhambi itahesabiwa kwa kukuthibitisha; ”

Waebrania 6.1-4. “Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Kristo na tusonge mbele ili tufikie utimilifu, si kuweka tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, yaani, mafundisho kuhusu mabatizo, kuwekea watu mikono, ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. Mungu akitujalia tutafanya hivyo. Kwa kuwa ni vigumu kuwarejeza tena katika toba wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho Mtakatifu.”

Ayubu 32:6b-7. “Mimi ni mdogo kwa umri, ninyi ni wazee, ndiyo sababu niliogopa, sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua. Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’”

672. HANGAYA YABHELEKA.

Imbuki ya kahayile kenako, yingilile ku Sonda iyo igafumaga dilu makingilima Isonda yiniyo, uluyafuma  igamanyichaga giki ubhujuku wela, kugiki abhanhu bhaje ku milimo iki wizaga bhupe. Ubhupe bhunubho, bhugolechaga ikanza lya gwandya kutumama milimo, kunguno bhuli ng’wene agadulaga ugubhona chiza. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Hangaya yabheleka.’

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ntumami ogwipunha dilu oja ukumilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agalitumilaga chiza ilikanza ilya Limi, bho gwanguha gujigulambija gutumama milimo yakwe yiniyo. Uweyi adebhile isolobho ya gulitumila chiza ilikanza lyake lya Limi linilo. Isolobho jinijo, jilikihamo na gwipandikila matwajo mingi, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolola ni sonda iyo igabhelekaga dulu, kunguno nuweyi agipunhaga dulu makingilima, ogigulambija gutumama milimo yakwe, iyo igang’winhaga matwajo mingi, umuwikaji bhokwe.

Uweyi agabhinhaga nabhiye bhulangwa bho gulitumila ilikanza lya limi jinagwigulambija uguitumama imilimo yabho yiniyo chiza, umukikalile kabho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘Hangaya yabheleka.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gulitumila ilikanza lyabho ilyalimi bho gwigulambija guitumama na bhukamu bhutale imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo agagujibheja chiza ikaya jabho.

Luka 1:73.

Mathayo 16:3.

2 Wakorintho 6:1.

Luka 2:32.

Waebarania 1:1…

KISWAHILI: SAYARI/NYOTA IMETOKEA.

Chanzo cha msemo huo, chatokea kwenye Nyota ile inayotoka asubuhi na mapema. Nyota hiyo, ikitokea huonesha kwamba usiku umekucha, ili watu waende kufanya kazi kwa vile mwanga umekuja.

Mwanga huo, huonesha wakati wa kuanza kufanya kazi, kwa sababu ya kila mmoja kuweza kuona vizuri. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘Sayari/Nyota imetokea.’

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mfanya kazi anayeamka asubuhi na mapema, na kwenda kufanya kazi zake, katika maisha yake. Mtu huyo, huutumia vizuri muda wake wa mchana, kwa kujibidisha kuyatekeleza  kwa bidii majukumu yake hayo. Yeye anafahamu faida ya kuutumia vizuri muda wake huo wa mchana. Faida hizo, ni pamoja na kujipatia mafanikio mengi, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na Nyota ile inayotokeza asubuhi, kwa sababu naye hujilawa asubuhi na mapema kwenda kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yake, yanayompatia mafanikio mengi, katika maisha yake.

Yeye pia huwapatia mafundisho wenzake, ya kuutumia muda wao wa mchana, katika kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao vizuri, katika maisha yao. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘Sayari/Nyota imetokea.’

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuutumia muda wao wa mchana kwa kujibidisha kuyatekeleza kwa bidii kubwa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio ya kuziendeleza vizuri familia zao.

Luka 1:73.

Mathayo 16:3.

2 Wakorintho 6:1.

Luka 2:32.

Waebarania 1:1…

star

star2

bhakima bhatumami

 

ENGLISH: THE MORNING STAR HAS APPEARED.

The source of this saying is the morning star that communicates that a new day has come. When this star appears it sweeps away darkness and invites light to mean that people have to wake up and continue with their daily activities. This scenario of making people wake up and proceed with their daily routine can be described using the saying that ‘the morning star has appeared.’

This saying can be compared to a person who wakes up early in the morning and goes to work. Such a person values time and knows when to wake up and what to do. People of this nature are likely to have achievements in life because of the way they are organized in their responsibilities. They also teach others about valuing time.

The saying teaches people about how to use their time in their daily activities. People have to work hard in order to achieve success in life.

Luke 1:73. Matthew 16: 3. 2 Corinthians 6: 1. Luke 2:32. Hebrews 1: 1.

662. BHUKULU WISINDI BHUGAYA NDETE.

Imbuki ya kahayile kenako, yilolile bhutale wi sindi ilo lidina ndete.  Ilisindi linilo, lilitale noyi ubho gulilola. Umunhu uyo alichola ndete ugulipelela wangu kugiki adule gupandika ndete ja gulanga na gujilwa. Aliyo lulu, ilyoyi kihamo nubhutale bholyo bhunubho, lidina ndete. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘bhukulu wi sindi bhugaya ndete.’

 Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ntale, aliyo adina masala, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agiiganikaga weyi duhu bhung’wene, kunguno ya masala gakwe ayo gadadulile uguilanghana chiza ikaya yakwe. Uweyi nulu agapandika sabho agajikenagulaga bho gujing’wela walwa, ukunu ikaya yakwe ililalila kuguno ya kugaiwa ijiliwa.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu bhutale uwisindi ilo lidina ndete, kunguno nuweyi alintale, aliyo adina masala agagujitumila isabho bho uguidilila chiza ikaya yakwe. Uweyi adadebhile ugubhalanja abhanhu bhakwe, akikalile akawiza. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘bhukulu wisindi bhugaya ndete.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza na masala gagujilanghanila chiza ikaya yabho, bho gujitumamila chiza isabho jabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho.

Yeremia 4:22.

Mhubiri 10:3.

Yakobo 1:4.

Yakobo 1:5.

KISWAHILI: UKUBWA WA MUMUNYA KUKOSA MBEGU.

Chanzo cha msemo huo, chaangalia ukubwa wa mumunya ambalo halina mbegu ndani yake. Mumunya hilo ni kubwa kwa kuliangalia kwa macho. Mtu anayetafuta mbegu za kukaanga na kula anaweza kulikimbilia haraka sana. Lakini basi, lenyewe pamoja na ukubwa wake huo, halina mbegu ndani yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘ukubwa wa mumunya kukosa mbegu.’

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mkubwa kwa umbo, lakini hana akili, maishani mwake. Mtu huyo, hujifikiria yeye mwenyewe tu, badala ya kuwafikiria watu wake, kwa sababu ya kukosa akili za kuitunza vizuri familia yake hiyo. Yeye akipata mali, huzimalizia kwenye matumizi ya hovyo, yakiwemo yale ya kuzinyewe pombe, badala ya kuisaidia familia yake hiyo.

Mtu huyo, hufanana na ukubwa wa mumunya ambalo halina mbegu, kwa sababu naye ni mkubwa, lakini hana akili za kumwezesha kuzitumia mali katika kuitunza familia  yake hiyo. Yeye hafahamu kuifundisha familia yake hiyo, mwenendo ulio mwema. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘ukubwa wa mumunya kukosa mbegu.’

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na akili za kuzilinda familia zao, kwa kuzitumia mali zao katika kuzitunza vizuri, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao hizo, maishani mwao.

Yeremia 4:22.

Mhubiri 10:3.

Yakobo 1:4.

Yakobo 1:5.

water-melon-1068293__480

isindi

maasai-herdsman

 

ENGLISH: THE BIGGER THE SIZE OF WATERMELON DOES NOT MEAN THE HIGHER THE NUMBER OF ITS SEEDS.

The source of this proverb is the watermelon and its seeds. In its appearance, a watermelon can appear to be very big in size to the extent of confusing someone, who doesn’t know them well, that they have a good number of seeds. To describe this scenario, people can use the proverb that ‘the bigger the size of watermelon does not mean the higher the number of its seeds.’

This proverb can be compared to a person who appears to be matured enough to carry out his/her responsibilities but, unfortunately, he/she is not clever enough to handle those responsilities. This person can spend much of the time thinking about himself/herself with no consideration of others. He/she likely even to fail in taking care of his/her family because of not having good management of resources available. People of this nature can spend much of their time spending the little they have instead of accumulating more for future use. Such people can die without leaving any legacy to their families.

The proverb teaches people about having a mind to protect their families. They have to use the available resources to take good care of themselves and their children.

Jeremiah 4:22. Ecclesiastes 10: 3. James 1: 4. James 1: 5

660. WABHEJA WATWINHA MAGULU. WATUKUNGILA JILATU.

Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile bhulumbi bho bhasiminzi abho bhinhagwa magulu. Uwinhiwa bho magulu bhunubho, bhuli bho guzugilwa jiliwa abhanhu abho bhalimugendo bhenabho. Ijiliwa jinijo, jigabhinhaga nguzu ja gudula gusiminza mpaga bhushika uko bhajile.

Hunagwene abhasiminzi bhenabho, ulu bhuzugilwa jiliwa aha kaya ndebhe,  bhujilwa mpaga bhiguta, bhagalagaga bho gulumbilija giki, ‘wabheja watwinha magulu. Watukungila jilatu.’ Ulu bhuyomba chiniko, bhagandyaga gusiminza bhajile umulugendo lwabho.

Lusumo lunulo, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali na wizanholo bho gubhakalibhusha abhageni na gulumbilija ulu witilagwa ya wiza na bhiye, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikalaga na bhanhu chiza bho gubhagalila abho bhalimugendo, kugiki bhadule gwifula aha ng’wakwe, na gupandika jiliwa ija gudula gubhinha nguzu chiza. Uweyi agabhabhonelaga isungu abhanhu abho bhali na makoye, umuwikaji bhobho.

Umunhu ng’wunuyo, wikolile nu ngaliji obhageni uyo agabhazugilaga jiliwa, kunguno nuweyi agabhakalibhushaga abhageni aha ng’wakwe na gubhagalila chiza. Uweyi agabhalangaga nabhiye ahigulya ya gubhiza bhizanholo bho gubhagalila jiliwa abhageni bhabho.

“Ulusumo lunulo lugatumilagwa na bhanhu abho bhalifunya bhulumbi aho bhamala gulya. Ugudinha magulu lunu ugutubhegeja jilatu mumho: “Oduzugilaga jiliwa ijo jadinhaga nguzu ja gusimizila.”” Hunagwene abhageni bhenabho bhaganumbaga bho guyomba giki, ‘wabheja wa twinha magulu. Watukungila jilatu.’  Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 46.

‘Kueneza Injili kwa methali’ jili jitabho ijo jigandikwa na Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey, M.M., ijojigachapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Lusumo lunulo, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza na wizanholo bho gubhakalibhusha abhageni aha kaya jabho, kugiki bhadule gubhinha nguzu ja gubhashisha uko bhajile.

“Ekaristi mumho gulumba. UmuEkaristia duganumbaga Mulungu ku wiza bhose ubho oditila.

Ulu ijiliwa jigadinhaga nguzu ja gusiminza dushiga ukodujile bho nduhu makoye, Ekaristia igadinhaga nguzu ja gushiga kuli Mulungu bho nduhu makoye. Umu Sakramenti ya Ekaristia UYesu Kristo odinhaga magulu, odubhegejeaga jilatu, giki odinhaga jiliwa ijagudulagudushia ng’wigulu bho nduhu makoye.

Kuyiniyo dadakilwa kunhumbilija USebha Wise UYesu Kristo na gung’wila: “Obheja, Baba, odinha magulu, odubhegeja jilatu.”” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 46.

Yohane 6:54.

kutoka 16:35.

Kumbukumbu 8:10.

Zaburi 139:14.

2 Wathesalonike 1:3.

KISWAHILI: ASANTE UMETUPATIA MIGUU. UMETUTENGENEZEA VIATU,

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia utoaji wa shukrani wa wasafiri waliopewa miguu. Upewaji huo wa miguu, ni wa watu waliyoko safarini kukaribishwa kwenye mji fulani na kupikiwa chakula. Chakula hicho, huwapa nguvu za kuendelea tena na safari yao kiasi cha kutosha kuwafikisha kule waendako.

Ndiyo maana wasafiri hao huishukuru familia hiyo, na kuiaga kwa kusema kwamba, ‘asante umetupatia miguu. Umetutengenezea viatu.’ Baada ya kusema hivyo, huendelea na safari yao ya kwenda kule waendako.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule mwenye ukarimu wa kuwakaribisha wageni na kuwashukuru wale waliomtendea wema, maishani mwake. Mtu huyo, huishi na watu vizuri kwa kuwatunza wale walioko safarini, ili waweze kupumzika kwake na kuwapatia chakula chakuwaongezea nguvu vizuri. Yeye huwahurumia wale walioko kwenye matatizo mbalimbali, maishani mwao.

Mtu huyo, hufanana na mtunzaji wa wageni anayewapikia chakula, kwa sababu naye huwakaribisha wageni na kuwaandalia chakula nyumbani kwake. Yeye huwafundisha pia wenzake juu ya kuwa na ukarimu wa kuwakaribisha wageni wao, na kuwaandalia chakula.

“Methali hii hutumika kwa watu ambao wanatoa shukrani baada ya kula. Kutupa miguu au kututengenezea viatu ina maana: “Umetupikia chakula ambacho kinatupa nguzu za kusafiri.” Ndiyo maana wageni hao, humshukuru kwa kusema kwamba, ‘asante umepatia miguu. Umetugengezea viatu.’ Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 46.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti, Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwakaribisha wageni kwenye familia zao, ili waweze kuwapatia nguvu za kuwawezesha kuendelea na safari yao, hadi kuwafikisha kule waendako.

“Maana ye Ekaristi ni kushukuru. Katika Ekaristi tunamshukuru Mungu kwa mema yote ambayo ametutemdea.

Kama chakula hutupa nguvu ya kusafiri tufike tunakokwenda bila shida, Ekaristi hutupa nguvu ya kufika kwa Mungu bila shida. Katika Sakramenti ya Ekaristi Yesu Kristo ametupa miguu, ametutengenezea viatu, yaani ametupa chakula kinachotuwezesha kufika mbinguni bila shida. Kwa hiyo yatupasa kumshukuru Bwana Wetu Yesu Kristo na kumwambia: “Asante, Baba, umetupa miguu, umetutengenezea viatu.”” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 46.

Yohane 6:54. “Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho.”

kutoka 16:35. “Waisraeli wakala mana kwa miaka arobaini, mpaka walipofika katika nchi iliyokaliwa na watu. Walikula mana mpaka walipofika mpakani mwa Kanaani.”

Kumbukumbu 8:10. “Wakati mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni BWANA Mungu wenu kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa.”

Zaburi 139:14. “Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha, kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu.”

food1

food2

food3

ENGLISH: THANK YOU FOR GIVING US FEET; YOU MADE US SHOES.

The source of this saying is thanksgiving for travelers after being well received by their host and being given food. The food they get is considered as feet to mean more strength that can enable them to continue walking until they reach their set destination. As a way to appreciate their host for the kindness they can use the saying that ‘thank you for giving  us feet; You made us shoes.’

The saying can be likened to a generous person who welcomes strangers and extends thanks to those who have done good in his/her life. The person lives with the people well by taking care of those on the journey. He/she does so by providing them with accommodation and food. People of this nature teaches others about kindness and hospitality to others.

This proverb can be applied to people who express gratitude after eating. Giving us feet or shoes means “You have cooked a meal that gives us strength to continue walking until we reach the planned destination.” This is why visitors can thank someone saying, ‘Thank you for giving us feet; You have made shoes for us’ to show their appreciation. You can also refer to Kueneza Injili kwa Methali which is translated as Spreading the Gospel in Proverbs, page 46. written by Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M. and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

The proverb teaches people to be hospitable to their visitors. They need to provide them with whatever help they can manage. In so doing, they help them gain more strength to continue with their journey.

Human beings have to thank God for the gift of Eucharist.  In the Eucharist we thank God for all the good that He has done for us.

As food gives us the strength to travel to our destination without difficulty, the Eucharist gives us the power to reach God without difficulty. In the sacrament of the Eucharist Jesus Christ has given us feet, made us shoes, that is, He has given us food that enables us to get to Heaven without difficulty. So we should thank our Lord Jesus Christ and say: “Thank you, Father, you have given us feet; you have made us shoes.” Refer to Kueneza Injili kwa Methali page 46.

John 6:54. Exodus 16:35. Deuteronomy 8:10. Psalm 139:14.