1520. SUKUMA: B’IZAGA NA SUNGE YA NG’HANA.

Imbuki ya kahayile kenako ifumilile kukikalile kabhasuguma. Abhanhu bhenabho bhabhuchaga sunge ya jiliwa guti mandege, busiga nulu jiliwa jingi ulubhajile ku nimo guti go winga bho bhazenganwa bhabho. Hunagwene bhagiwilaga bhuli ng’wene giki, “b’izaga na sunge ya ng’hana.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agayegaga nijo alinajo na adikalaga na wiminholo umuwikaji bhokwe bhunubho. Umunhu guti ng’wunuyo, agalonjaga mbango, bho gutumama milimo yakwe bho bhutungilija na wizanholo kunguno ya nhungwa jakwe ijawiza jinijo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agabhalelaga chiza abhanhu bha ha kaya yakwe yiniyo kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhasuguma abho bhagachala sunge ukuwinga bho mazenganwa bhabho, kunguno nuweyi agabhalelaga chiza abhanhu bha ha kaya yakwe mpaka bhakula chiza, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agang’wilaga bhuli ng’wene giki, “b’izaga na sunge ya ng’hana.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutungilija bho guyega na ginhu ijo bhalinajo, na kutumama milimo yabho bho wizanholo na widohya, kugiki bhadule kujilela chiza ikaya jabho umuwikaji bhobho bhunubho.

Wafilipi 4:11–12.

1 Timotheo 6:6.

Waebrania 13:5.

Mithali 15:16.

SWAHILI: UWE NA ZAWADI YA KURIDHISHA.

Asili ya msemo huo inaweza kufuatiliwa hadi kwenye maisha ya kitamaduni ya wasukuma. Watu hawa hubeba chakula kwenye ndoo zao wanapoenda kwenye sherehe za majirani zao zikiwemo zile za harusi kama michango yao kwenye sherehe hizo. Ndiyo maana wao huambiana kwamba “uwe na zawadi ya kuridhisha.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huridhika na kile alicho nacho na haishi na uchoyo au wivu usioisha maishani mwake. Mtu kama huyo huthamini baraka, hufanya kazi kwa uaminifu, na huepuka malalamiko yasiyo ya lazima kwa sababu ya tabia yake hizo njema maishani mwake. Yeye huwalea vyema wanafamilia wake kwa sababu ya uaminifu wake huo katika maisha yake ya kila siku.

Mtu huyo hufanana na wale wasukuma waliotuma zawadi nzuri kwenye harusi za majirani zao kwa sababu naye pia huwalea vyema wanafamilia wake kama zawadi yake kwao, maishani mwake. Ndiyo maana huwafundisha kwa kusema “uwe na zawadi ya kuridhisha.”

Msemo huo huwafundisha watu kuhusu kuridhika, kuwa na shukrani, unyenyekevu, na amani ya moyo. Unawakumbusha kwamba kuridhika huleta furaha, huku uchoyo mara nyingi ukileta migogoro, wivu, na huzuni. Mtu mwenye shukrani huthamini baraka za Mungu na anaheshimu ustawi wa wengine.

Wafilipi 4:11–12. “Nimejifunza kuridhika katika hali yoyote.”

1 Timotheo 6:6. “Utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.”

Waebrania 13:5. “Ridhika na ulicho nacho.”

Mithali 15:16. “Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, kuliko kuwa na mali nyingi pamoja na masumbufu.”

ENGLISH: HAVE A GIFT OF SATISFACTION.

The origin of this saying can be traced back to the traditional life of the Sukuma people. These people carry food in their bucket while going to their ceremonies like weddings of their neighbors as their contributions to such party. That is why they encourage one another by saying “have a gift of satisfaction.”

This saying is compared to a person who is content with what he or she has and does not live with endless greed or jealousy in life. Such a person appreciates blessings, works honestly, and avoids unnecessary complaints because of his sound behavior in life. He nicely nurtures his family members because of his being honest in his daily life.

This person resembles those who sent nice gifts to the weddings of their neighbors because of he also nurtures well his family members in his life. That is why he encourage them by saying “have a gift of satisfaction.”

This saying teaches people about contentment, gratitude, humility, and peace of heart. It reminds them that satisfaction brings happiness, while greed often brings conflict, envy, and sorrow. A thankful person values God’s blessings and respects the welfare of others.

Philippians 4:11–12. “I have learned to be content whatever the circumstances.”

1 Timothy 6:6. “Godliness with contentment is great gain.”

Hebrews 13:5. “Be content with what you have.”

Proverbs 15:16. “Better a little with the fear of the Lord than great wealth with turmoil.”

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.