1519. SUKUMA: NOMO LOMO AGULISAMULAGA.

Akahayile kenako kahoyelile munhu nomo lomo uyo agasambajaga mihayo ya bhulongo kubhangi. Umunhu ng’wunuyo agaponanjaga mihayo ya bhulongo kubhangi iyo igasambalaga wangu kunguno ya kuiyombela habhanhu bhingi giti munhu uyo agalutaga mawe bho nduhu ugumana uko galigwila. Hunagwene abhanhu bhaganhayaga giki, “nomo lomo agulisamulaga.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agasambajaga wangu mihayo ya bhulomo lomo bho nduhu ugudilila amafumilo gayo, umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, adayiganikaga chiza iyo idulile gwenhelejiwa na mihayo yakwe iya bhulongo yiniyo kunguno ya nhungwa jakwe ijabhubhi jinijo umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agayiminyaga sagala ikaya yakwe kunguno ya kusambaja mihayo ya bhulongo iyo igenhaga widumi ukubhanhu bhakwe bhenabho, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nomo lomo uyo oyombaga mihayo ya bhulongo bho nduhu ugudebha amafumilo gayo, kunguno nuweyi agayombaga mihayo ya bhulongo mpaga obhenheleja gwiduma abhanhu bhakwe bhenabho umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhakwe bhaganhayaga giki, “nomo lomo agulisamulaga.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho kuleka kuyomba mihayo ya bhulongo ukubhichabho, kugiki bhadule kujilanga chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mithali 12:22.

Waefeso 4:25.

Yakobo 3:5.

Katika Mithali 12:19.

SWAHILI: MUONGO ANALIRUSHA.

Msemo huu unamzungumzia mwongo anayeeneza maneno ya uongo kwa wengine. Mtu huyu hutupa maneno yake ya uongo kwa wengine ambayo huenea haraka kwa sababu ya kuzungumza mbele ya watu kama mtu anayetupa mawe bila kujua yatatua wapi. Ndiyo maana watu husema “muongo analirusha.”

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hueneza uongo haraka na bila kujali matokeo yake, katika maisha yake. Mtu kama huyo hafikirii madhara ambayo maneno yake yanaweza kusababisha kwa wengine kwa sababu ya tabia yake hiyo mbaya maishani mwake. Yeye huwajeruhi wanafamilia wake kwa sababu ya kuwatupia maneno hayo ya uongo ambayo husababisha migogoro na mgawanyiko kati yao, katika maisha yake.

Mtu huyo hufanana yule muongo aliyesema maneno ya uongo bila kujua matokeo yake, kwa sababu naye pia hufurahia kusema uongo unaowadhuru wanafamilia wake hadi kusababisha mkanganyiko na mgawanyiko kwao kati yao. Ndiyo maana wanafamilia wake hao husema kwamba “muongo analirusha.”

Msemo huu huwafundisha watu kuhusu hatari ya kusema uongo na kusambaza taarifa za uongo. Inaonya kwamba uongo unaweza kusafiri haraka na kusababisha madhara makubwa, hata unaposemwa kwa upole. Inahimiza ukweli, uwajibikaji katika usemi, na kufikiria kwa makini kabla ya kusema.

Mithali 12:22 “Bwana huchukia midomo ya uongo, bali hupendezwa na watu waaminifu.”

Waefeso 4:25 “Kwa hiyo kila mtu aache uongo na aseme kweli na jirani yake.”

Yakobo 3:5 “Ulimi ni kiungo kidogo cha mwili, lakini hujisifu sana.” Ulimi unaelezewa kuwa mdogo lakini wenye nguvu, unaoweza kusababisha madhara makubwa, kama moto.

Katika Mithali 12:19 “Midomo ya kweli hudumu milele, bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.”

Msemo huu unatukumbusha kwamba maneno yana nguvu yakitolewa, hayawezi kudhibitiwa kwa urahisi. Kwa hivyo, hekima iko katika kusema ukweli na kulinda ulimi wa mtu.

ENGLISH: THE LIE IS THROWING IT

This saying talks about a liar who spreads false words to others. This person throws his false words to others which spreads quicks because of speaking infront of people like someone who throws stones without knowing where they will land. That is why people say “the lie is throwing it.”

This saying is compared to a person who spreads lies quickly and carelessly, in his life. Such a person does not consider the harm their words may cause to others because of his wicked behavior in life. He injures his family members because of throwing those false words to them which cause conflicts and division to them, in his life.

This person resembles the liar who spoke false words without knowing their consequences, because he also enjoys speaking lies which injure his family members to the point of causing confusion and division to them. That is why his family members say “the lie is throwing it.”

This proverb teaches people about the danger of lying and spreading false information. It warns that lies can travel fast and cause great harm, even when spoken lightly. It encourages truthfulness, responsibility in speech, and careful thinking before speaking.

Proverbs 12:22 “The Lord detests lying lips, but he delights in people who are trustworthy.”

Ephesians 4:25 “Therefore each of you must put off falsehood and speak truthfully to your neighbor.”

James 3:5 “The tongue is a small part of the body, but it makes great boasts.” The tongue is described as small but powerful, capable of causing great harm, like a fire.

In Proverbs 12:19 “Truthful lips endure forever, but a lying tongue lasts only a moment.”

This saying reminds us that words have power once released, they cannot be easily controlled. Therefore, wisdom lies in speaking the truth and guarding one’s tongue.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.