Ulusumo lunulo luhoyelile giki ubhumani ying’wene bhudatoshije mpaka wambilije bhanhu gwikala chiza. Umulikujo lya jiafrica, nono abhamuchalo, abhanhu bhanhiyagwa likujo bho gujilanija numo alibhutumamila ubhumani bhokwe ijinagubheja kaya iyalange lisoga, idi bho bhumani duhu.
Itala iyo idina mafuta idadulile gufunya lisana, giko lulu, nu bhumani ubho bhudina miito bhudadulile gwambilija bhanbhu gwikala chiza. Hunagwene abhanhu abhakikujo bhagayomba giki, “bhulangwa bho nduhu miito bhuli guti tala iyo idina maguta.”
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo wilanga mihayo mingi mushule, mukanika nulu mubhananzengo bhiye, aliyo lulu adumile uguitumamila umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agayombaga mihayo ikujo aliyo adikalaga muwikaji wikujo kunguno ya nhungwa jakwe gubhiza ja bhubhi, umukajile kakwe. Uweyi agadumaga uguyilela chiza ikaya yakwe kunguno ya nhungwa jakwe ijabhubhi jinijo, umukikalile kakwe kenako.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo alinibala litale aliyo adalilimaga kunguno nuweyi alinabhumani bho mihayo mingi aliyo adabhutumamilaga umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “bhulangwa bho nduhu miito bhuli guti tala iyo idina maguta.”
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya solobho ya kubhutumamila chiza ubhulangwa ubho bhabhupandika kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.
Yakobo 1:22.
Mathayo 5:16.
Mhubiri 9:10.
Luka 11:33.
SWAHILI: ELIMU BILA MATENDO NI KAMA TAA ISIYO NA MAFUTA.
Methali hii huzungumzia kwamba maarifa pekee hayatoshi isipokuwa yaemetekelezwa. Katika hekima ya kitamaduni ya Kiafrika, haswa katika jamii nyingi za vijijini, watu walimthamini mtu si tu kwa kile alichokijua, bali pia kwa jinsi alivyotumia maarifa yake katika kuwasaidia wengine vya kutosha kuboresha maisha yao. Taa isiyo na mafuta haiwezi kutoa mwanga; vivyo hivyo, elimu isiyo na matendo haiwezi kuinufaisha jamii. Ndiyo maana wenye busara walisema “elimu bila matendo ni kama taa isiyo na mafuta.”
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye amejifunza mambo mengi shuleni, kanisani, au katika jamii, lakini anashindwa kutumia maarifa hayo katika maisha ya kila siku. Mtu kama huyo huzungumza kwa busara lakini haishi kwa busara kwa sababu ya mwenendo wake mbaya. Yeye hushindwa kuwalea vizuri wanafamilia wake kwa sababu ya kuzungumza kwa busara bila kuishi kwa busara katika maisha yake.
Mtu huyo hufanana na mtu yule ambaye anamiliki zana za kilimo lakini halimi kamwe ardhi, au mtu ambaye hubeba Biblia kila siku lakini halitii Neno la Mungu. Maarifa ya mtu huyo hayana maana bila ya kutekelezwa kwa matendo yaboreshayo maisha ya watu. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “elimu bila matendo ni kama taa isiyo na mafuta.”
Methali hii huwafundisha watu kuhusu: umuhimu wa kutumia elimu katika vitendo, kutumia hekima kuitumikia jamii, kuishi kulingana na kile ambacho mtu amejifunza, uwajibikaji na tabia njema na thamani ya maarifa ya vitendo maishani mwao, ili waweze kufanikiwa maishani mwao.
Yakobo 1:22. “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, mkijidanganya nafsi zenu.”
Mathayo 5:16. “Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema.”
Mhubiri 9:10. “Lolote mkono wako utakalopata kulifanya, lifanye kwa nguvu zako zote.”
Luka 11:33. “Hakuna mtu awashaye taa na kuificha.”
Mistari hii huonesha kwamba hekima na elimu ya kweli lazima izae matendo mema yanayowanufaisha wengine.
ENGLISH: EDUCATION WITHOUT ACTION IS LIKE A LAMP WITHOUT OIL.
This proverb talks about that knowledge alone is not enough unless it is put into practice. In traditional African wisdom, especially in many village communities, people valued a person not only for what he knew, but for how he used his knowledge to help others enough to improve their lives. A lamp without oil cannot produce light; likewise, education without action cannot benefit society. That is why the wise said “education without action is like a lamp without oil.”
This saying is compared to a person who has learned many things in school, church, or society, but fails to apply that knowledge in daily life. Such a person talks wisely but does not live wisely because of his wicked conduct. He fails to nurture well his family members because of speaking wisely without living wisely in his life.
This person resembles someone who owns farming tools but never cultivates the land, or a person who carries a Bible every day but never obeys the Word of God. Knowledge becomes useless when it is not practiced. That is why people tell him that, “education without action is like a lamp without oil.”
This proverb teaches people about: the importance of putting education into action, using wisdom to serve society, living according to what one has learned, responsibility and good character and the value of practical knowledge in life.
James 1:22. “But be ye doers of the word, and not hearers only, deceiving your own selves.”
Matthew 5:16. “Let your light so shine before men, that they may see your good works.”
Ecclesiastes 9:10. “Whatever your hand finds to do, do it with all your might.”
Luke 11:33. “No one lights a lamp and hides it.”
These verses show that true wisdom and education must produce good actions that benefit others.