Ulusumo lunulo lyingilile kubhukengeji bho ginhu umo jasumbilwa. Unti gugikalaga gupanga kunguno ya mizwi yago. Imizwi yiniyo igagwinhaga unti gunuyo minze, jiliwa, na bhudamu. Unti ulugujimija imizwi yago, gugumaga na gucha. Imizwi yiniyo igolechaga likujo lilange lya gwikala chiza na bhanhu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “unti uyo gudina mizwi gugumaga.”
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agawibhaga ubhulangwa bho nhungwa ja gwikala chiza nu Mulungu umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agatumamaga imilimo yakwe bho gwisendamila weyi ng’winikili duhu kunguno ya gugibha amalagiko ga ng’wa Mulungu, umuwikaji bhokwe. Uweyi adadumaga uguimala chiza imilimo yakwe kunguno ya gulyibha ililange ilo ligabhejaga nhungwa ja wiza, umukikalile kakwe.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nu nti uyo gudina mizwi kunguno nuweyi agaligumanija ilikujo lya bhulangwa bho gwikala chiza mpaga oduma uguimala chiza imilimo yakwe, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “unti uyo gudina mizwi gugumaga.”
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya solobho ya guwikalana chiza ubhulangwa bho gwikala chiza ni kaya jabho, kugiki bhadule kujilela chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.
Yeremia 17:7–8.
Zaburi 1:3.
Wakolosai 2:7.
Mathayo 7:24–27.
SWAHILI: MTI USIO NA MIZIZI HUKAUKA.
Methali hii inatokana na uchunguzi wa maumbile. Mti huishi kwa sababu ya mizizi yake. Mizizi huupa mti maji, nguvu, lishe, na uthabiti. Mti unapopoteza mizizi yake, hukauka na hatimaye hufa. Katika hekima ya kitamaduni ya Kiafrika, mizizi huashiria asili, utamaduni, familia, imani, na msingi wa maadili. Ndiyo maana watu husema kwamba “mti usio na mizizi hukauka.”
Methali hii hulinganishwa kwa mtu yule ambaye husahau historia yake, hupuuza mafundisho mazuri, huacha nidhamu, au hujitenga na Mungu na maadili ya familia. Mtu huyu hufanya mambo ikiwa ni pamoja na kazi zake kwa kujitegemea mwenyewe tu badala ya kutegemea nguvu za Mungu kwa sababu ya kupuuza mafundisho mazuri yakiwemo yale ya amri za Mungu maishani mwake. Yeye hushindwa kufikia malengo yake kwa sababu ya kupuuza mafundisho mazuri ambayo yaweza kumsaidia maishani. Mtu kama huyo huanguka kwa urahisi katika mkanganyiko, majaribu, na hushindwa kwa sababu hana msingi imara.
Mtu huyo hufanana na ule mti ambao hauna mizizi kwa sababu naye pia hupuuza hekima itakayo kwenye mafundisho mazuri ikiwa ni pamoja na yale ya Mungu hadi kufikia hatua ya kushindwa kufikia malengo yake maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mti usio na mizizi hukauka.”
Methali hiyo huwafundisha watu Kuhusu: umuhimu wa kuwa na misingi imara katika maisha, kuheshimu utamaduni, familia, na maadili mema, na kushikamana na Mungu na maadili ya kiroho.
Mtu asiye na kanuni ni kama mti usio na mizizi, hawezi kusimama imara wakati wa dhoruba.
Yeremia 17:7–8 “Lakini heri amwaminiye Bwana… Watakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji.”
Zaburi 1:3 “Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda yake kwa wakati wake.”
Wakolosai 2:7 “Mmetiwa mizizi na kujengwa ndani yake, mmeimarishwa katika imani.”
Mathayo 7:24–27 Yesu anafundisha kwamba mtu anayejenga juu ya msingi imara atasimama imara dhoruba zinapokuja.
ENGLISH: A TREE WITHOUT ROOTS WITHERS
This proverb originates from the observation of nature. A tree survives because of its roots. The roots give the tree water, strength, nourishment, and stability. When a tree loses its roots, it dries up and eventually dies. In African traditional wisdom, roots symbolize origin, culture, family, faith, and moral foundation.That is why people say “a tree without roots withers.”
This proverb is compared to a person who forgets his background, ignores good teachings, abandons discipline, or separates himself from God and family values. This person does things including his works by depending on himself instead of on relying on God’s power because of ignoring good teaching including God’s commandments in his life. He fails to actualize his goals because of ignoring good teachings which can assist him in life. Such a person easily falls into confusion, temptation, and failure because he has no strong foundation.
This person resembles the tree that has no roots because he also ignores wisdom from good teaching including those of God to the point of failing to actualize his goals in his life. That is why people tell him, “a tree without roots withers.”
This Proverb Teaches People About: The importance of strong foundations in life, respecting culture, family, and good morals, remaining connected to God and spiritual values, remembering one’s origin and identity, and living a stable and disciplined life.
A person without principles is like a tree without roots, he cannot stand firm during storms.
Jeremiah 17:7–8 “But blessed is the one who trusts in the Lord… They will be like a tree planted by the water.”
Psalm 1:3 “That person is like a tree planted by streams of water, which yields its fruit in season.”
Colossians 2:7 “Rooted and built up in Him, strengthened in the faith.”
Matthew 7:24–27 Jesus teaches that a person who builds on a strong foundation will stand firm when storms come.