Sukuma Riddles

336. KALAGU – KIZE. IGAGI LYA HA LUB’IMBI UDULIB’UTA – ILUMBUYO

Imbuki ya kalagu yiniyo yingilile kub’ub’uti wigagi lya halub’imbi. Iligagi linilo, lilijimanijkijo ja ngelelo go kikolo ja ng’wa munhu, na wandijo  b’ojikolo ja ng’wa ungi. Ulu munhu ulib’inza iligagi linilo mumho ojijimija ijimanikijo jinijo. Hunagwene abhanhu bhagaganaga giki, ‘igagi lya halub’imbi udulib’inza.’ Uungi oshosha giki, ilumbuyo.

Ikalagu yiniyo igalenganijiyagwa kuli munhu uyo aliha guntola ilumbuye. Uilumbuye ng’wunuyo alisawa nigapi linilo ilyaha lub’imbi. Gashinaga lulu, ilemejiwe uguntola munhu uyo alinduguye ogubyalwa munda yimo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga kiki, ‘igagi lya ha ulub’imbi udulibuta:- Dada yako.’

Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu higulya ya kudiimila malagilo gali wiza umuchalo jabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho.

Mambo ya walawi 8:9.

Mambo ya walawi 20:17.

2 Samweli 13:11 – 12.

Waroma 27:22.

KISWAHILI: KITENDAWILI  – TEGA

MUWA WA MPAKANI HUUKATI: – DADA YAKO

Chanzo cha kitendawili hicho chatokea kwenye ukataji wa muwa wa mpakani. Muwa huo ni kitambulisho cha pale ambapo mali ya mtu inaishia na pale inapoanzia mali ya mtu mwingine. Mtu akiukata muwa huo, maana yake ameiondoa alama ya kitambulisho cha mpaka huo. Ndiyo maana watu huambiana kwamba, ‘muwa wa mpakani huukati: mwingine hujibu – dada yako.’

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa mtu ambaye hutaka kumuoa dada yake. Dada huyo ni sawa na muwa huo wa mpakani. Kumbe basi, mtu haruhusiwi kumuoa ndugu yake wa tumbo moja. Ndiyo maana watu huambiana kwamba, ‘muwa wa mpakani huukati: mwenzake hujibu, dada yako.’

Kitendawili hicho hufundisha watu juu ya kushika maagizo yaliyomema katika jamii, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao.

Mambo ya walawi 8:9.

Mambo ya walawi 20:17.

2 Samweli 13:11 – 12.

Waroma 27:22.

cane

277. NYAMA YA MBOKU UDILYA

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile nyama ya ng’wa munhu uyo alimboku. Inyama ya ng’wa munhu ng’wunuyo, igikalaga na mapalala mingi, kunguno uwei adabhonaga. Kuyiniyo lulu, inyama yiniyo igazuganijiyagwa na mapalala gayo genayo, ayogagib’ipyaga. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘nyama ya mboku udilya.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhali na miito gabhubhi. Amiito genayo gagigaluchaga ni mihayo yabho yab’iza mib’i. Amiito genayo amabhi, gikolile nu mpoku. Imihayo imibhi ikolile ni nyama iyo ilina mapalala. Hunawene abhanhu bhagabhawilaga abha miito gabhubhi bhenabho giki, ‘nyama ya mboku udilya.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kuleka gwita miito ga bhubhi, kunguno amiito genayo gagaib’ipyaga ni mihayo yabho. Gashinaga lulu, yigelelilwe gwita miito ga wiza, ayo gagayib’ejaga ni mihayo yabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho abhanhu bhenabho.’

Mathayo 23:26.

KISWAHILI: NYAMA YA KIPOFU HUTAILA

Chanzo cha methali hiyo chaangalia nyama ya mtu ambaye ni kipofu. Nyama hiyo huwa na takataka nyingi, kwa sababu ya yeye kuwa na hali ya kutoona. Hivyo yeye huwa hawezi kukiandaa vizuri chakula chake, ndiyo maana chakula hicho huwa kina takataka nyingi. Ndiyo maana pia watu husema kwamba, ‘nyama ya kipofu hutaila.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wenye matendo mabaya. Matendo hayo husababisha kwa watu hao pia kuwa na maneno mabaya. Matendo mabaya hayo hufanana na kipofu. Maneno mabaya hufanana na nyama hiyo ya kipofu, yenye takataka nyingi. Ndiyo maana watu huwaambia watu hao wenye matendo mabaya kwamba, ‘nyama ya kipofu hutaila.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha kutenda matendo maovu, kwa sababu matendo hayo maovu husababisha pia kwao kuwa na maneno mabaya.  Kumbe basi, yafaa kutenda matendo mema ambayo huzaa maneno mazuri, yatakiwayo kwa ajili ya maendeleo ya familia zao.

Mathayo 23:26.

meat food

 

 

184. KALAGU – KIZE. AKASIMINZILE KAKWE HAKAB’INILE KAKWE – B’AMBU

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Imbuki ya kalagu yiniyo ilolile jisumbwa ijo jigitanagwa B’ambu. IB’ambu ili shinu iyo igasiminzaga ukunu yukagija guti ilib’ina, aliyo gashinaga nigujaga. Umukajile kenako, ib’ambu yiniyo, nose igashigaga uko ijile. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, akasimizile kayo ib’ambu, hakajile kayo.

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe bho bhukalalwa na bhulingiji bhutale. Umunhu ng’wunuyo agadulaga uguimala chiza imilimo yakwe yiniyo.

Gashinaga, igelelilwe abhanhu b’ab’ize na bhukalalwa bho guitumama chiza imilimo yabho na guimala gitumo idakililwe gub’iza. Umugwita chiniko, bhagudula gupandika matwajo mingi agubhambilija ugujibheja chiza ikaya ni jumuiya jabho.

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya kub’iza na bhukalalwa bho guitumama chiza imilimo yabho mpaga guimala. Ubhukalalwa bhunub’o, bhugubhenhela matwajo mingi ayogadulile kubhinha bhupandiki bhutale, bho jikolo, umuwikaji b’ob’o.

Ijinagongeja, ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gub’iza na bhulingiji bho guitumama chiza imilimo yabho mpaga guishisha aha nhalikilo yajo. Umugwita chinicho, bhagudula gukwabha sabho ningi ijagujisabhya ikaya ni jumuiya jabho, umuwikaji b’ob’o.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

KUTEMBEA KWAKE NDIVYO KUCHEZA KWAKE – KINYONGA.

Chanzo cha kitendawili hicho chaangalia kiumbe kinachoitwa Kinyonga. Kinyonga ni mdudu ambaye hutembea kwa kusitasita, kama anacheza kumbe ndivyo asafirivyo. Katika kuenenda kwake hivyo, yeye hufaulu kufika kule aendeko. Ndiyo maana watu husema kwamba, kutembea kwakwe kinyonga ndivyo kucheza kwake.

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa mtu ambaye hufanya kazi zake kwa uangalifu na umakini mkubwa. Mtu huyo huweza kuzitekeleza vizuri kazi zake. Kumbe yafaa watu wawe na uangalifu wa kutosha kuzitekeleza kazi zao kama itakiwavyo. Kwa kufanya hivyo, wataweza kupata maendeleo mengi katika familia na jumuiya zao.

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na uangalifu wa kuwawezesha kuzitekeleza vizuri shughuli na kazi zao zote. Uangalifu huo utawaletea mafanikio mengi yawezayo kuwasaidia katika kuzijenga familia na jumuiya zao, maishani mwao.

Zaidi ya hayo, kitendawili hicho hufundisha watu juu ya kuwa na umakini katika utekelezaji wa majukumu na shughuli zao zote. Umakini huo utawawezesha, kupata mali nyingi ziwezazo kuzitajirisha familia na jumuiya zao maishani mwao.

Mathayo 6:1-8.

Mathayo 24:36-44.

Matendo 2:14-18.

chameleon-

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME…

IT WALKS AS IT PLAYS – CHAMELEON

The overhead riddle focuses on the peculiar locomotion of a cameleon, a creature that walks as if it is dancing. Indeed, it reaches its destination successfully, by use of that style.

The riddle is comparable to a person who does his/her work keenly and with the seriousness it deserves. The end result here would be work well done. It is not only important but also appropriate for people to carry out their duties with care. By doing so, their families and communities are bound to benefit more in terms of development and progress.

That paradox enlightens people about the need for diligence in undertaking their obligations and tasks. Taking caution brings about many positive achievements that can help build their families as well as their communities.

In addition, the riddle instills in people the important quality of being focused in the execution of their roles and responsibilities. Such keenness and perceptiveness can enable them to effectively harness resources that can be used to uplift their lives, their families and their communities.

Matthew 6: 1-8.

Matthew 24: 36-44.

Acts 2: 14-18.

183. KALAGU – KIZE NG’WANA O MUJILUGU ADATULAGWA MBULA- NG’WANA UYO ALI MUNDA.

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Imbuki ya kalagu yiniyo ililola ng’wana uyo alimunda, nulu uyo atali ugubyalwa. Ung’wana ng’wunuyo adiko nulu gutulwa mbula, kunguyo uwei agikalaga wib’isile mugati ya ng’wa nina. Kuyiniyo lulu, nulu igandya gutula mbula, agutulwa nu nina duhu.  Ung’wana ng’wunuyo, huyo ali o mujuligu, uyo adatulagwa mbula.

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agikalaga ashegijiwe na munhu ungi umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhizaga alinawe nkhingi okwe. Ung’winuyo huyo gaganshigilaga amakoye gosegose. Gashinaga lulu, unkhingi okwe, ukuliweli, aliguti nina ong’wana uyo atali munda.

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya kubhalanhana chiza abho bhali hasilili yab’o. Abhanhu bhenabho bhali guti bhabyaji umo igelelelilwe bhabhalanhane chiza abhana bhabho, gitu nkima uyo alibhudito umo aganhanghanilaga ung’wana okwe uyo atali munda yakwe. Abhanebho lulu, ha bhana abha mujulugu, abho bhadatulagwa mbula.

Ijinagongela, ikalagu yiniyo yabhalanga abhabyaji higulya ya gubhambilija chiza abhana bhabho, abho bhatali ugutola, nulu ugutolwa, kunguno abhenabho bhatali mujulugu. Yigelelilwe bhab’agunane bho gub’inha bhulangwa bho wiza ubho gudula ugub’inja umumakoye gosegose.

Kuyiniyo, yigelelilwe abhanhu bhikale muli Mulungu uyo alijulugu ja kubhalanghana bhadizutulwa mbula. Imbula yiniyo, yadula gulinganijiwa na shetani. Abho abhazunya gwikala mukati ya ng’wa Yesu, agub’alanghana bho gwilanga muliwei. UYesu agub’inja umubhusese bho ng’wa shetani.

KISWAHILI: KTENDAWILI – TEGA

MTOTO ALIYE PANGONI HANYESHEWI MVUA- MTOTO ALIYEKO TUMBONI.

Chanzo cha kitendawili hicho chaangalia mtoto ambaye bado yumo ndani ya tumbo la mama yake. Mtoto huyo ni yule ambaye bado hajazaliwa. Kwa hiyo, mtoto huyo hawezi kunyeshewe mvua, kwa sababu yeye huwa amejificha tumboni mwa mama yake. Atakayenyeshewa na mvua hiyo, ni mama yake, ambaye kwake, mama huyo ni kama pango lake alimojificha, ili asipatwe na matatizo yoyote. Kwa maana hiyo, mtoto huyo hawezi kunyeshewa mvua kwa sababu yumo pangoni mwa mama yake.

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu ambaye huwa amekingwa na mtu mwingine maishani mwake. Mtu huyo, ni yule ambaye yuko chini ya mtu mwingine anayemtegemea kumtunza katika kujipatia mahitaji yake, yakiwemo yale ya kupata: chakula, mavazi na malazi yake.

Matatizo mbalimbali huwa yanamfikia yule aliye juu yake, hayamfikii yule aliyeko chini. Yule aliyeko chini hubaki salama, kwa sababu ya yeye kukingwa na yule aliyeko juu yake. Ndiyo kusema, mtoto aliyeko pangoni hanyeshewi mvua. Huyo ndiye mtoto aliyeko tumboni.

Kitendawili hicho hufundisha watu juu ya kuwalinda vizuri wale waliyoko chini yao, wakiwemo watoto wao, wanafunzi wao, wananchi wao, na kadhalika. Watu hayo, ni pamoja na wazazi ambao hutakiwa kuwalinda watoto wao ili wasipatwe na matatizo. Walimu pia hutakiwa kuwalinda kwa kuwafundisha vizuri wanafunzi wao, ili wasipatwe na matatizo ya kushindwa mitihani yao. Hao ni sawa na mapango yawakingayo watoto hao kunyeshewa mvua.

Zaidi ya hayo, kitendawili hicho, huwafundisha wazazi juu ya kuendelea kuwasaidia watoto wao ambao hawajafikia umri wa kuoa au kuolewa,  kwa kuwapatia malezi mema yawazeyo kuwakinga na matatizo mbali mbali maishani mwao.

Kwa hiyo, yafaa watu wakae ndani ya Muumba wao ambaye ni Mungu ili wasije wakanyeshewa mvua. Mvua hiyo huweza kufananishwa na shetani. Ndiyo maana, Yesu huwaita watu wamwendee yeye, ili awapumuzishe, kutoka kwenye matatizo yatokanayo na wao kubaki kwenye utumwa wa shetani. Yesu huwaondoa utumwani mwa shetani, wale wamwaminiyo, na kukaa ndani yake. Na sisi twaitwa kwenda kukaa  ndani ya Yesu Kristo, ili tusihangaike maishani.

Mathayo 11:28-30.

Isaya 49:15-16.

Zaburi 17:8-14.

Zaburi 91:1-6.

Isaya 66:12-13.

Zaburi 61:

belly-

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME

A CHILD WHO IS BURROWED IN THE CAVE DOES NOT GET RAINED ON – A CHILD IN THE MOTHER’S WOMB

The above riddle is about a baby who is still in the mother’s womb. In the event of rain, the baby cannot be reached by the rain because it is hidden in the safety of the mother’s womb. The mother, who is like a cave, gets rained on but shields the baby from any such stress.woman-pregnant

This puzzle is likened to a situation where someone is given support and protection by someone else in his/her life. The dependant person rides on the good will of his/her benefactor to secure his/her own needs, including food, clothing and shelter.

By virtue of taking responsibility for other people’s welfare, the person encounters various challenges. Meanwhile, the one who draws protection from him/her remains secure, just like the baby who is burrowed in the comfort of the cave that is its mother’s womb.

Such riddle teaches people about the importance of offering protection to those under their care, including their children, students, citizens, among others. For instance, parents are supposed to protect their children from harm; teachers are required to protect their students by imparting in them the necessary knowledge and skills to enable them excel in their examinations. Such people are like caves that protect the children from the rain.pregnant-beauty

In addition, the riddle tends to encourage parents to consistently care for and support their children throughout their youthful years. This would help them keep problems at bay.

Therefore, it is necessary for people to dwell in God, their Creator, so that they do not get wet from rain. The rain can be compared to the devil. That is why Jesus calls people to come to Him, so that He can give them liberation from the bondage of the devil. Jesus removes the bondage of Satan from those who believe and abide in Him. And we are called to dwell in Jesus Christ, so that we do not worry about life.

Matthew 11: 28-30.

Isaiah 49: 15-16.

Psalm 17: 8-14.

Psalm 91: 1-6.

Isaiah 66: 12-13.

Psalm 61: 4.

180. KALAGU – KIZE NG’OMBE JA NG’WIZE JAGUDIMA JISWAGILILE – MISO

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Imbuki ya kalagu yiniyo ililola miso ayo gagatumamaga milimo yako bho nduhu ugwinga umumili. Amiso genayo gagab’onaga bhuli kwene uko ulola ubhona duhu. Aliyo gagab’izaga galumanile numili mu makanza gose. Amiso genayo gadiko ugwinga aha mili uyo gulinago. Gagabhizaga gali haho duhu.

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga miliyo yakwe ukunu alikihamo na bhiye. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga kihamo na bhiye umub’utumami bho miliyo yakwe yose. Agatumamaga chiza imilimo yakwe pye niyo aginhiyagwa na bhatale bhakwe.

Ijinagongeja, umunhu ng’wunuyo agajidililaga chiza ijikolo jakwe,  nija bhiye. Yigelelilwe umunhu ajilanghane chiza ijikolo ijo alijipandika umuwikaji bhokwe, kugiki ijikolo jinijo jidule ugung’wambilija ahashiku ijaha bhutongi.

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwikala na bhumo na bhichabho umubhutumami bho milimo yabho. Ubhumo bhunub’o bhudulile gubhambilija umuguitumama chiza imilimo yabho, kunguno bhuli ng’wene agubhiza na bhukalalwa bhogupandika matwajo mingi ayo gadulile gujambilija ikaya, jumuiya ni si jabo, bho makanza malihu.

Ijinagongeja, ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gudimila chiza ijikolo jabho giti umo gagagulabhililaga amiso umili. Yigelelilwe abhanhu bhilange halumo inzila ja gujilanghana chiza ijikolo jabho nija mumakaya gabho.

KITENDEWILI – TEGA

NG’OMBE WA KWETU HUCHUNGIA ZIZINI –

MACHO

Chanzo cha kitendawili hicho chaangalia macho ambayo hufanya kazi zake bila kuondoka kwenye mwili. Macho hayo huona kila upande utakaongalia bila kuachana na mwili huo. Hivyo huwa yameungana vizuri na mwili huo kwa muda wote. Hayawezi kuondoka kwenye mwili ulionayo. Huwa yapo tu kwenye mwili huo.

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa mtu ambaye hufanya kazi zake akiwa ameungana vizuri na wenzake. Mtu huyo huwa na umoja na wenzake katika utekelezaji wa majukumu yake yote. Huzifanya kazi hizo apewazo na wakubwa au watu wa nyumbani kwake, vizuri.

Zaidi ya hayo, mtu huyo huvilinda vizuri vitu avipatavyo maishani mwake. Huvilinda pia vile ambavyo nivya wenzake, ili viweze kuwasaidia wote katika siku za mbeleni. Huwafundisha pia wenzake namna ya kuvitunza vizuri hivyo vitu vyao.

Kitendawili hicho hufundisha watu juu ya kuwa na umoja na wenzao katika utendaji wao wa kazi za kila siku. Umoja huo waweza kuwasaidia katika kuishi kwa amani na kuvitunza vizuri vitu wavipatavyo maishani mwao. Umoja huo pia huleta maendeleo katika familia, jumuiya na nchi zao.

Zaidi ya hayo, kitendawili hicho, chafundisha watu juu ya kuvitunza vizuri vitu wavipatavyo, kama vile macho yautunzavyo mwili muda wote yatekelezapo majukumu yake. Yafaa watu wafundishane vizuri namna ya kuzitunza vizuri mali zao na za jumuiya zao.

Mathayo 6:22-23.

Mathayo 13:16-17.

2Wakorintho 10:7.

Waefeso 1:18.

1Yohana 1:1.

african-kenyan

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME

COWS OF OUR HOME FEED WHILE THEY ARE IN THE COWSHED – EYES

The literal meaning of the overhead proverb is about eyes and the way they function without leaving their sockets. Eyes can see every place where one focuses them, but they won’t leave one’s body; they are firmly attached to it throughout. They cannot leave the body; they are part of it.

That paradox is likened to a person who engages in his/her work effectively in collaboration with others. He/she is able to accomplish his/her responsibilities using a united approach with colleagues. Such a person satisfactorily undertakes the tasks assigned to him/her by family members.

In addition, the person is able to safeguard the things that he/she acquires in life, including those of other people, for posterity. He/she also teaches people how to diligently safeguard what they possess.

The puzzle imparts in people the necessity of being united with their peers in their daily activities. Such unity can help them live peacefully, besides affording them the ability to safeguard their valuable possessions in life. Also, progress in the family, in the community and in the country is brought about by unity.

Moreover, the proverb also teaches people on how to take care of the things they acquire, just like the eyes take care of the body throughout their vigilance function. People ought to understand how to diligently protect their own property and that of their communities.

Matthew 6: 22-23.

Matthew 13: 16-17.

2 Corinthians 10: 7.

Ephesians 1:18.

1 John 1: 1.

174. KALAGU – KIZE. DIKOYELA NA NG’WANA MIGU NOSE NAMPONYA: – IGONGOTE ILILILINA MANDEGE NULU NYAMA YI GUHA

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Imbuki ya kalagu yiniyo ililola, munhu uyo alilya lindege. Agumanaulipilimula pilimula alililya, nose agulimaja amandege galyo, uliponya iligongote. Nuku nyama yiguha nigiko, kunguno uni onyama agumana uilya inyama iyo ilihigulya ya liguha, nose agulimaja inyama na aguliponya iliguha linilo.

Ikalagu yiniyo igalenganijiyagwa kulimunhu uyo alinabhulingisiji bho guisolanya imihayo iyo iliyawiza, iyo idulile gubhambilija abhanhu ugujibheja ikaya jabho, na guileka mihayo iyo idinasolobho ijinagujibheja ikaya jinijo. Ilichiza umunhu abhize na bhumani bho guisolanya imihayo iyasolobho ahalili, na guileka iyo idinasolobho umuwikaji bho bhanhu.

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya kuisolanya imihayo iyo ilinasolobho, aho bhalili, umuwikaji bhobho, na guyileka iyo idinasobho. Ilichiza abhanhu ugubhiza na bhumani ubho guikomanya imihayo iyasolobho yiniyo, kugiki bhadule ugujibheja chiza ikaya jabho.

Ijinagonjeja, ikalagu yiniyo yalanga giki bhuli nimo gwene dugagwandyaga bho gukoyakoya, nose ukubhutongi gugadenhelaga solobho. Guti gulima, nguno ahabhutongi jiliwa jigupya.

Hangi, ikalagu yiniyo, yabhalanga abhanhu higulya ya kub’iza na wiyumilija ubho bhudulile,  nulu gung’wambilija umunhu ugugushisha chiza unimo, guti gwingila mubhulangwa bho gunkub’ija Yesu gushiga nose agupandika bhatisimu. Uwiyumilija bhunubho bhugenhaga nguzu jagugushisha unimo aha nhalikilo yago. Umunhu ng’wunuyo agaiponyaga igiti iyi olinayo, na agingilaga ng’wisana.

KITENDAWILI – TEGA.

TUMEHANGAIKIANA NA MWANA MIGU HATIMAYE NIMEMWANGUSHA – GUNZI LILILO NA MAHINDI AU NYAMA YA MFUPA.

Chanzo cha kitendawili hicho chaangalia mtu alaye mhindi. Mtu huyo, huula mhindi huo huku akiugeuzageuza, mwishowe mahindi huisha na kulitupa lile gunzi. Vivyo hivyo kwa upande wa mfupa, kwa sababu mlaji wa nyama huendelea kuila mpaka ikaisha na kubakia mfupa ambao huutupa.

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa mtu mwenye umakini wa kuchambua kilicho kizuri pale alipo ambacho chaweza kuwasaidia watu katika kujenga familia zao, na kuyaacha yale ambayo hayana faida katika ujenzi wa familia hizo. Yafaa mtu awe na umakini wa kuchambua maneno na matendo yenye faida pale alipo, na kuyaacha yale ambayo hayana faida katika maisha ya mwanadamu.

Kitendawili hicho, chafundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuchagua maneno na matendo yawezayo kuleta maendeleo katika familia za zao, na kuyaacha yale ambayo hayana faida maishani mwa watu. Mtu atakiwa kuwa na umakini wa kumwezesha kuchagua kile kilicho cha maana katika kujenga familia yake, na kiyaacha yote yawezayo kuibomoa familia yake hiyo.

Zaidi ya hayo, kitendawili hicho, chafundisha watu, juu ya kuwa na ufuatiliaji mzuri wa kazi zao ili waweza kuzifikisha kwenye mwisho wake uwezao kuwapatia maendeleo pale walipo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, watu huhangaika kwanza, ndipo wanayafikia mafanikio yao. Mfano wa mkulima, ambaye huvumilia mahangaiko ya kulima, mpaka anapata mavuno yake.

Kitendawili hicho pia hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu, uwawezeshao kuyafikia malengo yao, kama vile mwanafunzi aanzavyo mafundisho ya kumfuata Yesu, mpaka anabatizwa. Huyo kutoka gizani na kuingia kwenye mwanza. Kwa hiyo, mtu huyo, ametoa giza na kuupokea mwanza.

1Wakorintho 10:13.

Waefeso 2:1.

Waefeso 2:4-6.

Waefeso 6:10-14.

corn-

ENGLISH: I HAVE RIDDLE – LET IT COME

I HAVE WRESTLED WITH MIGU AND I HAVE EVENTUALLY THROWN HIM DOWN – MAIZE ON COB/STEAK ON BONE

The above riddle refers to a situation when a person eats maize on a maize cob. The person would eat the grain, all the while turning the cob around. When he/she is done, the bereft cob is discarded. The same is true with bone meat, whereupon the person would throw away the bone after methodically eating off its steak.lamb

The paradox is likened to a person who is meticulous enough to determine what is of value in regard to building the family, and what is worthless. It is necessary for a person to possess the capacity to analyze words and deeds, and to be able to disregard those that are worthless in human life.

That riddle teaches people about the importance of making careful choice of words and actions, which can bring prosperity in the family, and about ignoring what is worthless in people’s lives. One should be keen enough to choose what is worthwhile in building one’s family, and leave out everything that can destroy it.corn-on-the-cob

In addition, the riddle educates people about fidelity to their work all through, which is bound to ensure progress. That is due to the fact that people shall first endure trials and tribulations before achieving success, just like a farmer would endure the anxieties of cultivation before he gets his harvest.

Such paradox also instills in people the virtue of patience, a quality that enables them to achieve their goals, like a disciple who follows the teachings of Jesus until he gets baptized. Such a person leaves darkness and enters into the light, that is, the beginning of a new life.

1 Corinthians 10:13.

Ephesians 2: 1.

Ephesians 2: 4-6.

Ephesians 6: 10-14

173. KALAGU – KIZE ULU OLILA UMAMA AB’ANHU B’AYEGA B’AYIKINDIKA NA B’UYENGI – NGOMA/NDONO

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Imbuki ya jigano jinijo ililola b’ab’ini b’a mbina. Abhanhu bhenabho bhagatulaga ng’oma. Ing’oma yiniyo igalilaga b’o gutulwa b’o nguzu, aliyo ab’ab’ini bhayo b’agayegaga noyi, nduhu nulu gusunduhala igiki untuji aliiminya ing’oma yiniyo.

Ijigano jinijo jigalenganijiyagwa kuli munhu uyo agakoyakoyaga bho gutumama miliyo yakwe bho nguzu ningi, kugiki abhanhu bhakwe, bhapandike bhuyegi. Igelelilwe munhu umo wifunye jinagumama milimo yiniyo iyo idulile gubhenhela b’uyegi abhangi abho bhang’wisanije.

Ijigano jinijo jalanga bhanhu higulya ya gwifunya gubhambilija bhangi bho gutumama miliyo iyo idulile gubhenhela bhuyegi abhanhu bhabho b’enab’o. Ib’elelile umunhu aho alili, abhambilije abhanhu bhake, nulu namugi igelelilwe  atumame b’o nguzu jakwe b’o gwifunya gubhambilija abhanhu bhakwe, kugiki bhadule gupandika bhuyegi.

Ijinagongeja, ijigano jinijo jalanga bhanhu higulya ya gukub’ija inzila ya ng’wa Yesu uyo agaluha na kucha ha nsalabha, kugiki abhapije abho bhalinzunya. Ib’elelile abho danzunya wei duyege bho gub’ina chiza ulu datulilwa ing’oma nu Yesu.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

BIBI ANAPOLIA WATU WANAFURAHI WANARUKA KWA FURAHA- NGOMA/ZEZE

Chanzo cha kitendawili hicho chaangalia wacheza ngoma. Watu hao hupiga ngoma ambayo hulia kwa kupigwa kwa nguvu. Lakini wachezaji wake hufurahia mno, wala hawahuzuniki kwamba mpigaji wake anaiumiza hiyo ngoma.

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa mtu ambaye huhangaika katika kufanya kazi zake kwa nguvu nyingi, ili watu wake wapate kufurahi. Yatakiwa mmoja ajitoe kwa kufanya kazi hizo ziwezazo kuwaletea furaha watu wengi wamtegemeao.

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kujitoa kuwasaidia watu wengi kwa kufanya kazi ziwezazo kuwaletea furaha watu hao. Mtu apaswa kuwasaidia wake watu pale alipo, kama vile mzee katika familia atakiwavyo kujituma kwa nguvu zake katika kujitoa kuwafanyia kazi watu wake hao ili waweze kupata furaha.

Zaidi ya hayo, kitendawili hicho hufundisha watu juu ya kufuata njia ya Yesu aliyeteseka na kufa msalabani kwa ajili ya kuwakomboa wale wamwaminio. Twatakiwa wale tumwaminio yeye kufurahi kwa kucheza anapotupigia ngoma hiyo Bwana wetu Yesu Kristo.

Mathayo 11:16-17.

Mathayo 20:28.

Yohana 3:16-17.

1Wakorintho 14:1.

2Wathesalonike 2:15-16.

drum

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

WHEN THE GRANDMOTHER CRIES PEOPLE BECOME HAPPY AND THEY JUMP JOYOUSLY– DRUM/CALABASH MUSIC

The foundation of the above riddle is about music and dance. When the drummist beats the drum harder, the dancers grow more excited and the dancing gets more frenzied with the rising drum beat. The dancers do not get angry at the drummist for beating the drum hard.drummer

The puzzle is likened to a person who, through struggle and great energy, works hard so that his dependants can enjoy the fruits of his labour. It is a noble thing for someone to sacrifice and undertake difficult tasks for the sake of bringing happiness to those who rely on him/her.

The riddle teaches about the commitment to help others by undertaking tasks that can bring joy to them. One ought to help one’s people wherever one is, just as an elder in the family would be required to play a lead role in his/her commitment to work hard enough and guarantee success and happiness to his/her people.

Above all, the riddle enlightens people about the need to follow Jesus’ way of suffering and dying on the Cross for the salvation of those who believe in Him. We need to rejoice when our Lord Jesus Christ invites us to dance to His drum – by following His commandments.

Matthew 11: 16-17.

Matthew 20:28.

John 3: 16-17.

1 Corinthians 14: 1.

2 Thessalonians 2: 15-16.