1524. SUKUMA: AMIITO GALIMIZA GULEB’A IMIHAYO.

Imbuki ya lusumo lunulo yifumilile kuli nimi uyo wikalaga muchalo ja Sanjo. Unimi ng’wunuyo, omishiga diyu ogandya gulima mpaka lyagwa ilimi kunguno oliamanile igiki “ijito jigayombaga noyi kulebha imihayo.” Hunagwene abhanhu abho bhamujaga inguno ya gwita chiniko obhashogejaga giki, “amiito galimiza gulebha imihayo.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinikujo lwa golecha bhutungulija nu bhutogwa bhokwe bho gubhitila imilimo iyo agayitaga duhu. Umunhu ng’wunuyo, agiitaga yose iyo ilimubhulagani bhokwe na kajile kakwe kunguno ya likujo lyakwe linilo umuwikaji bhokwe. Uweyi agasabhaga sabho ningi noyi ahakaya yakwe yiniyo kunguno ya likujo lyakwe linilo ilyaguitimija imilimo yakwe bho gwigulambija guitumama chiza, umuwikaji bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo otumamaga milimo yakwe gwingila diyu mpaka lyagagwa ilimi kunguno nuweyi agigulambijaga gutumama milimo yakwe mpaga osabha sabho ningi aha kaya yakwe yiniyo umuwikaji bhokwe. Uweyi alintongeji ntungulija uyo agabholekeja abhanhu bhakwe nzila ya wiza bho gutumama milimo chiza, adiogutumila mihayo duhu. Hunagwene agayombaga giki, “amiito galimiza gulebha imihayo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya bhutungilija na wigulambija bho gutumama imilimo midamu. Lubhalanga gudebha igiki mihayo duhu idadulile gubheja bhutungulija kugiki bhadule guyimalamaja bho miito gabho iyo bhagayiyombaga, umuwikaji bhobho.

Yakobo 2:17.

Mathayo 7:16.

1 Yohana 3:18.

Mithali 14:23.

SWAHILI: VITENDO NI BORA KULIKO MANENO.

Asili ya methali hii ilianzia kutoka kwa mkulima aliyeishi katika kijiji cha Sanjo. Mkulima huyo alikuwa akiamka mapema asubuhi na kuanza kufanya kazi kuanzia asubuhi hadi jioni kwa sababu alijua kwamba “matendo huzungumza zaidi kuliko maneno.” Ndiyo maana watu walipomuuliza sababu ya kufanya hivyo, alijibu kwa kusema kwamba, “matendo ni bora kuliko maneno.”

Methali hii hulinganishwa kwa mtu mwenye hekima ya kuthibitisha wema wake, uaminifu, upendo, au bidii kwa kupitia kile anachofanya badala ya kile anachosema tu. Mtu kama huyo hutimiza ahadi zake na kuonesha tabia njema kwa matendo ambayo huwatendea wengine kwa sababu ya hekima yake hiyo maishani mwake.  Yeye hutajirika sana katika familia yake kwa sababu ya hekima yake hiyo ya kutekeleza anachosema kwa kufanya kazi kwa bidii katika maisha yake hayo ya kila siku.

Mtu huyo hufanana na yule mkulima aliyefanya kazi zake kuanzia asubuhi hadi jioni kwa sababu naye pia hufanya kazi zake kwa bidii hadi kufikia hatua ya kuwa tajiri katika familia yake. Yeye ni kiongozi anayewahudumia watu kwa uaminifu badala ya kutoa ahadi tupu. Ndiyo maana husema kwamba “matendo ni bora kuliko maneno.”

Methali hii huwafundisha watu kuhusu: uwajibikaji, uaminifu, kuwa na bidii ya kufanya kazi ngumu. Kuelewa kuwa maneno pekee hayawezi kujenga uaminifu isipokuwa yanaungwa mkono na matendo. Kwa hiyo, watu wanapaswa kuishi kulingana na yale wanayoyasema na kuyatekeleza yale wanayohubiri.

Yakobo 2:17 “Imani yenyewe, ikiwa haina matendo, imekufa.”

Mathayo 7:16 “Kwa matunda yao mtawatambua.”

1 Yohana 3:18 “Tusipende kwa maneno au kwa usemi bali kwa matendo na kweli.”

Mithali 14:23 “Kila kazi ngumu huleta faida, lakini maneno matupu huleta umaskini.”

ENGLISH: ACTIONS ARE BETTER THAN WORDS

The original of this proverb started from a farmer who lived at Sanjo village. This farmer used to wake up and start working from morning to evening because he knew that “actions speak louder than words.” That why when people asked him a reason of doing so, he answered “actions are better than words.”

This proverb is equaled to a person who has wisdom of proving his goodness, honesty, love, or hard work through what he does instead of what he merely says. Such a person fulfills promises and demonstrates character by deeds which he does to others because of his wisdom in life. He becomes so rich at his family because of his wisdom of practicing what he says by working hard in his daily life.

This person resembles a farmer who did his works from morning to evening because he also works hard to the point of becoming rich at his family. He is a leader who serves people faithfully instead of making empty promises.That is why he says “actions are better than words.”

This proverb teaches people about: honesty, responsibility, faithfulness, and hard work. Words alone cannot build trust unless they are supported by actions. People should live according to what they say and practice what they preach.

James 2:17 “Faith by itself, if it does not have works, is dead.”

Matthew 7:16 “By their fruits you will know them.”

1John 3:18 “Let us not love with words or speech but with actions and in truth.”

Proverbs 14:23 “All hard work brings a profit, but mere talk leads only to poverty.”

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.