Imbuki ya ulusumo lunuyo ifumilile kubhana bha mabhasa abho bhitanagwa bha Kulwa na Dotto. Uumo obhana bhenabho uli obyalwa na mili ntale gulebha ung’wiye uyo ali na mili ndoo. Abhanhu abho bhabhabhonaga bhagabhudebha ubhuheke bhobho. Hunagwene bhagang’wila uyo ali na mili ntale giki, “ong’welela ung’wiyo.”
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumilaga wiza, milimo nulu bhutengeke bho ng’wa munhu bho gwicholela solobho yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agatumilaga bhunwani nulu ubhukihamo umo idi nhana mpaga wenheleja makoye ukubhiye kunguno ya gwicholela solobho jakwe ng’winikili umuwikaji bhokwe. Uweyi agabhenhelaga makoye abhanhu bha ha kaya yakwe yiniyo kunguno ya gwitogisha bho gwilola weyi ng’winikili umukikalile kakwe kenako.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuumo obhana abha mabhasa uyo alina mili ntale kulebha ung’wiye, kunguno nuweyi agabhapunjaga abhanhu bha ha kaya yakwe bho gubhalilila jiliwa mpaga bhapandika makoye, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki “umempunja mwenzako.”
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhunhana, bhutungilija ni kujo kubhichabho, kugiki bhadule gwikala na bhuyegi umukaya jabho. Lulibhalemeja ugugwikala na wiminholo, wibhoneji, na gwicholela solobho jabho yiyene umuwikaji bhobho bhunubho, kugiki bhadule kujibheja chiza ikaya yakwe jinijo.
Wagalatia 6:2.
Mithali 22:16.
Mika 6:8.
Luka 6:31.
SWAHILI: UMEMPUNJA MWENZAKO.
Methali hii inatokana na mapacha yaani Kulwa na Dotto. Mmojawapo ya mapacha hao alizaliwa akiwa na mwili mkubwa kuliko yule mwingine ambaye mwili wake ulikuwa mdogo. Watu waliowaona waliona tafauti kubwa kati yao. Ndiyo maana walimwambia yule pacha aliyekuwa na mwili mkubwa kwamba, “Umempunja mwenzako.”
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutumia wema, udhaifu, kazi, au uaminifu wa mtu mwingine kwa manufaa yake binafsi maishani mwake. Mtu kama huyo hutumia urafiki au ushirikiano isivyo haki na kuacha mateso kwa wengine kwa sababu ya ubinafsi wake huo maishani mwake. Yeye husababisha mateso kwa wanafamilia wake kwa sababu ya ubinafsi wake huo wa kula peke yake huku wengine wakiwa na njaa, maishani mwake.
Mtu huyo hufanana na yule pacha aliyezaliwa akiwa na mwili mkubwa kuliko yule mwingine aliyekuwa na mwili ndogo, kwa sababu naye pia huwapunja wanafamilia wake hadi kuwasababishia mateso maishani. Yeye hula peke yake huku wengine wakiwa na njaa, kama kiongozi anayewalemea wengine lakini anakataa kuwasaidia.
Yeye hufanana pia na mfanyabiashara asiye mwaminifu anayepata faida kwa kuwadanganya wenzake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “Umempunja mwenzako.”
Methali hiyo huwapa watu mawazo kuhusu, haki, uaminifu, na heshima kwa wengine. Huonya dhidi ya uchoyo, uonevu, na ubinafsi katika mahusiano, familia, mahali pa kazi, na jamii. Inawahimiza watu kuishi kwa huruma na usawa.
Wagalatia 6:2. “Chukueni mizigo ya kila mmoja, na hivyo kuitimiza sheria ya Kristo.”
Mithali 22:16. “Anayemdhulumu maskini kwa ajili ya faida yake mwenyewe atakuwa maskini.”
Mika 6:8. “Fanya haki, penda rehema, na uende kwa unyenyekevu na Mungu wako.”
Luka 6:31. “Watendee wengine kama vile ungependa wakutendee.”
ENGLISH: YOU HAVE EXPLOITED YOUR COMPANION.
This proverb is originated from the twings namely Kulwa and Dotto. One of these twings was born with bigger body than the other one whose body was small. The people who saw them noticed such difference between them. That is why they told the twing who had bigger body, “You have exploited your companion.”
This saying is matched to a person who takes advantage of another person’s kindness, weakness, labor, or trust for selfish benefit in life. Such a person uses friendship or partnership unfairly and leaves the other suffering because of his selfishness in life. He causes sufferings to his family members because of his selfishness of eating alone while others are hungry, in life.
This person resembles the twin who was born with bigger body than the other one, because he also takes advantage of his family members to the point of causing sufferings to them, in life. He eats alone while others are hungry like a leader who burdens others but refuses to help them.
He also resembles a dishonest trader who gains profit by cheating companions. That is why people tell him, “You have exploited your companion.”
This proverb imparts in people ideas about justice, fairness, honesty, and respect for others. It warns against greed, oppression, and selfishness in relationships, families, workplaces, and communities. It encourages people to live with compassion and equality.
Galatians 6:2. “Bear one another’s burdens, and so fulfill the law of Christ.”
Proverbs 22:16. “Whoever oppresses the poor for his own increase will come to poverty.”
Micah 6:8. “Do justice, love mercy, and walk humbly with your God.”
Luke 6:31. “Do to others as you would have them do to you.”