Sukuma Sayings

982. MZIDUNGEMA B’USESE.

Akahayile kenako, kahoyelile higulya ya gugeng’wa b’usese bho ng’wa munhu nhebhe. Ub’usese bhunubho, b’uli bhuluhiwa bho ng’wa munhu uyo agaja ha kaya iyo igang’winha milimo midamu guti nsese, kunguno ya gukayiwa bhutogwa ukuli munhu ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga abha ha kaya yiniyo giki “mzidungema b’usese.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli nkima uyo otolwa ha kaya iyo idantogilwe, umukikalile kayo. Ikaya yiniyo, igamanaga yuntuma unkima ng’wunuyo, guja gujutumama milimo midimu bho mduhu ugwifula, kunguno ya gung’wiganikila guti giki ali nsese oyo. Unkima ng’wunuyo, agikalaga anogile bhuli makanza kunguno ya gutumamiwa milimo midimu yiniyo bhuli makanza, umukikalile kakwe.

Unkima ng’wunuyo, agikolaga nu munhu uyo agaja hakaya iyo yang’winhaga milimo midimu bhuli makanza, kunguno nuweyi agatumagwa gujutumama milimo midimu bhuli makanza ni kaya yiniyo aho otolelwa. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga abhanhu bha ha kaya yiniyo giki, “mzidungema b’usese.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya guleka gub’agema b’usese abhanhu bho gub’inha ikujo pye abhose, kulwa bhu munhu bhobho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Kutoka 20:8-11.

Kutoka 21:1-11.

Kutoka 1:8-14.

 

KISWAHILI: MSIMJARIBU MTUMWA.

Msemo huo, huongelea juu ya kufanywa mtumwa kwa mtu fulani. Utumwa huo, ni hali ya kuteswa kwa mtu aliyeenda kwenye familia ambayo watu wake walimtumikisha kwa kumpatia kazi ngumu kama mtumwa, kwa sababu ya kukosa upendo kwake mtu huyo. Ndiyo maana watu waliwaambia wanafamilia hayo kwamba, “msimjaribu mtumwa.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mwanamke aliyeolewa kwenye familia isiyompenda. Familia hiyo, huwa ina mtuma mwanamke huyo kwenda kufanya kazi ngumu bila hata kupumzika, kwa sababu ya kumfikiria kama mtumwa wa hapo. Mwanamke huyo, huwa amechoka kila wakati kwa sababu ya kutumikishwa kwa kupewa kazi hizo mgumu, mara kwa mara, katika maisha yake.

Mwanamke huyo, hufanana na yule mtu aliyeenda kwenye familia iliyomtumikisha kwenye kazi ngumu kama mtumwa, kwa sababu naye hutumikishwa kwa kufanyishwa kazi ngumu, na familia hiyo alipoolewa. Ndiyo maana watu huwaambia wanafamilia hao kwamba, “msimjaribu mtumwa.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kuwatumikisha watu kama watumwa, kwa kuwaheshimu watu wote kwa sababu ya utu wao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao.

Kutoka 20:8-11.

Kutoka 21:1-11.

Kutoka 1:8-14.

woman-SLAVE

slave-castle-

ghana-1

 

ENGLISH: DO NOT MAKE HIM/HER SLAVE.

This saying refers to enslavement of a person. Slavery is a state of torture to a person who went to a family members who enslaved him by giving him hard works as a slave, because they did not love him. That is why the people told those family members that, “Do not make him/her slave.”

This saying is equated to a married woman in a family that does not love her. This family often sends the woman to work in difficult activities without even resting, because of considering her as a slave. This woman is constantly exhausted because of being tortured by such frequent difficult tasks in her life.

This woman is like the person who went to a family that tortured him as a slave, because she was also forced to work in difficult tasks by the family members where she got married. That is why people say to those family members that, “Do not make him/her slave.”

This saying imparts in people a clue on stopping habit of enslaving people, by respecting all people because of their dignity, so that they can peacefully live in their families.

Exodus 20: 8-11.

Exodus 21: 1-11.

Exodus 1: 8-14.

981. OZUB’ANGAGA.

Olihoyi nkima umo uyo ozugaga jiliwa. Unkima ng’wunuyo, ogazuga jiliwa jib’isi kunguno ya bhuzuki bhokwe ubho sagala bhunubho. Uweyi agenheleja bhanhu gwikala na nzala kunguno ya guduma ugujilya ijiliwa jakwe ijib’isi jinijo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “ozub’angaga.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adatumamaga chiza imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga sagala sagala imilimo, iyo ilikihamo na bhulimi, na bhusuluja, kunguno ya gugayiwa bhudiliji bho milimo yakwe yiniyo. Uweyi agagayiyagwa ijiliwa jagulya aha kaya yakwe, kunguno ya gugayiwa bhudiliji bho milimo yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nkima uyo agazuga jiliwa jib’isi, kunguno nu weyi agatumamaga sagala sagala bho nduhu uguidilila chiza imilimo yakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ozub’angaga.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija guitumama imilimo yabho bho guidilila chiza, kugiki bhadule gupandika jiliwa na sabho ja gubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Warumi 12:11.

Mathayo 24:13.

KISWAHILI: UMEHARIBU.

Alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa akipika chakula. Mwanzake huyo, alipika hovyo chakula hicho kikawa kibichi kwa sababu ya kukosa umakini wa kujali vizuri kazi yake. Yeye alisababisha watu kushinda na njaa kwa sababu ya kushindwa kukila chakula chake hicho kibichi. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “umeharibu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule asiyeyatekeleza vizuri majukumu yake, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya kazi zake hovyo hovyo, ambazo ni pamoja na zile za kilimo na biashara, kwa sababu ya kutokujali kwake kazi zake hizo. Yeye hukosa chakula nyumbani kwake kwa sababu ya kukosa umakini wake huo, katika utekelezaji wa majukumu yake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule mwanamke aliyepika hovyo chakula chake kikawa kibichi, kwa sababu naye hufanya kazi zake hovyo, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “umeharibu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao kwa kuyajali vizuri, ili waweze kupata mafanikio mengi zaidi, maishani mwao.

Warumi 12:11.

Mathayo 24:13.

woman-212

ENGLISH: YOU HAVE SPOILT EVERYTHING.

There was a woman who was cooking. Nonetheless she spoilt her food because she did not pay attention to her works. She caused the people to go hungry because they could not eat her raw food. That is why they told her that, “You have spoilt everything.”

This saying is compared to a person who does not fulfill his/her responsibilities well in life. This person performs his/her duties negligently, including those of agriculture and trade, because of laziness. He/she misses food at home because of such lack of focus in the discharge of his/her responsibilities in life.

This person is like the woman who spoilt food in her way of cooking, because he/she also does not pay attention in his/her works. That is why people say to his/her that, “You have spoilt everything.”

This saying teaches people on how to work hard enough to fulfill well their responsibilities by taking good care of them, so that they can have more success in their lives.

Romans 12:11.

Matthew 24:13.

980. DALINDA GUGUMIWA.

Ugugumiwa jili jilipo ja ng’wa munhu uyo amalaga gutumama nimo nheb’e. Bhalihoyi bhatumami bha jipande umu ngese ya nimi umo. Abhatumami bhenabho, bhagailimila injese yiniyo mpaga bhuyimala chiza, kunguno ya bhukamu bhobho ubho gutumama milimo bhunubho. Aho bhamala ugujilimila ijipande jabho, bhagalindila gulipya ihela jabho ukuli nimi ng’wunuyo. Hunagwene bhangayomba giki, “dalinda gugumiwa.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe bho jelwa ng’holo mpaga oyimala chiza, umubhutumami bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agamishaga diyu ogigulambija gutumama milimo iyo ilikihamo na gulima, na gwinja jiliwa jakwe gufumila mumigunda yakwe, kunguno wisagiji bhokwe bho kuli Mulungu uyo adulile gung’winha sabho ningi ulu umala chiza imilimo yakwe yiniyo. Uweyi agapandikaga sabho ningi umuwigulambija bho gutumama milimo yake yiniyo, kunguno ya wigagiji bhokwe bhunubho ubho ukuli Mulungu, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhatumami abhajipande abho bhagalimila ngese mpaga bhujimala chiza ijipande jabho, kunguno nu weyi agigulambijaga gutumama milimo yakwe mpaga oyimala chiza, ukunhu wisagililwe gwinhiwa sabho ningi na Mulungu, umukikalile kakwe. Hunagwene agayombaga giki, “dalinda gugumiwa.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bho gung’wisanya Mulungu, kugiki bhadule gwinhiwa sabho ningi, umutumami bhobho.

2Thimotheo 2:6.

Mathayo 20:1-16.

KISWAHILI: TUMESUBIRI UJIRA.

Ujira ni malipo kwa mtu aliyemaliza kutekeleja kazi fulani aliyopewa na mhusika. Walikuwepo wafanya kazi wa vibarua kwenye palizi ya mkulima fulani. Wafanya kazi hao, waliipalilia palizi hiyo mpaga wakaimaliza vizuri, kwa sababu ya bidii yao ya kufanya kazi. Walipomaliza kibarua hicho, walisuburi malipo ya pesa zao kwa mkulima huyo. Ndiyo maana walisema kwamba, “tumesubiri ujira.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatekeleza vizuri majukumu ya kazi zake, katika utendaji wake. Mtu huyo, huamuka asubuhi na kujibidisha kufanya kazi zake ambazo ni pamoja na kulima na kuvuna mavuno, kutoka mashambani mwake, kwa sababu ya matumaini yake ya kupewa mali nyingi na Mungu kutoka kwenye kazi zake hizo. Yeye hupata mali nyingi katika kujibidisha kwake kufanya kazi hizo, kwa sababu ya matumaini yake hayo kwa Mungu, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na wafanya kazi wa vibarua waliopalilia palizi mpaga wakakimaliza kibarua chao vizuri, kwa sababu naye hujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yake mpaga anayamaliza, huku akitumaini kupewa mali nyingi na Mungu, katika maisha yake. Ndiyo maana husema kwamba, “tumesubiri ujira.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yao, kwa kumtegemea Mungu, ili waweze kupewa mali nyingi, katika maisha yao.

2Thimotheo 2:6.

Mathayo 20:1-16.

farm-lady-

ENGLISH: WE ARE WAITING FOR WAGES.

A wage is a payment to a person who has completed a particular task which has been assigned to him or her by a concerned. There were laborers on the farmer’s weed who finished weeding it well, because of their hard working. When they finished the job, they waited for the money to the farmer to be paid by him. That is why they said that, “We are waiting for wages.”

This saying is equated to the person who performs his duties well, in his enactment. This man wakes up in the morning and labors to do his work, which includes plowing and reaping, from his fields, because of his hope of being given many riches by God from his efforts. He gains much wealth in his efforts enough to get many progresses because of his trust in God.

This man is like the laborers who finished weeding out the weeds well enough to wait for wages from the farmers, because he also strives to fulfill his responsibilities in life while hoping to be richly rewarded by God, in his life. That is why he says that “We are waiting for wages.”

This saying instills in people a clue on how to work hard enough to fulfill their responsibilities well by depending on God, so that they can be given more wealth for running their lives.

2 Timothy 2: 6.

Matthew 20: 1-16.

972. DALINYHIWA MIHAYO YA NGELEGENZO.

Imihayo iya ngelegenzo ili mihayo ya ng’heni iyo igayombagwa bho mbisila aliyo uyo aliwilwa alihaho. Imihayo yiniyo, igayombagwa kubhanhu bhangi aliyo ili nhoyela munhu umo uyo bhiguma nang’hwe kunguno ya bhupelani ubho bhuli mu ng’holo jabho. Ulu uyigwa mihayo yiniyo umunhu uyo ali ng’wanishi okwe ogapelanaga. Hunagwene agayombaga giki, “dalinyhiwa mihayo ya ngelegenzo.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo atogilwe mihayo ya gwiduma na bhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adatogagwa ugudegeleka mihayo ya ng’wiye uyo bhigumile nang’hwe, kunguno ya bhupelanu bhokwe bhunubho. Uweyi agatumilaga mihayo ya ngheni bho gub’itila bhiye aliyo ali nhoyela ng’wanishi okwe, kunguno ya gugayiwa bhutogwa ukuli ng’wiye ng’wunuyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunyo, alindamu ugubhalekaja abhanhu abho widuma nabho umukikalile kakwe. Uweyi agayiganikilaga shib’i imihayo iyo aliiyomba ung’wanishi okwe. Hunagwene agayombaga giki, “dalinyhiwa mihayo ya ngelegenzo.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kuleka gwiyitila mihayo ya bhub’i, bho gwilekeja ulu bhidumaga, kugiki bhadule gwikala bho mholele, umu kaya jabho.

Wagalatia 5:16-26.

KISWAHILI: TUMEANZWA MANENO YA KUZUNGUKWA.

Maneno ya kuzungukwa ni maneno ya mafumbo yanazumgumzwa kwa wengine wakati mlengwa yuko kwenye kundi hilo. Maneno hayo, humuongelea mtu waliyekosana naye kwa sababu ya hasira iyomo ndani ya mioyo yao. Yule anayeongelewa akigundua hukasilika. Ndiyo maana husema kwamba, “tumeanzwa maneno ya kuzungukwa.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule anayependa kukosana na wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hapendi kusikiliza maneno ya yule anayemchukia, kwa sababu ya hasira yake hiyo. Yeye hutumia maneno ya mafumbo kupitia wengine, kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa adui yake huyo, kwa sababu ya kukosa upendo kwa mwenzake huyo, maishani mwake.

Mtu huyo, huwa mgumu kuwasamehe watu aliokosana nao, katika maisha yake. Yeye huyafikiria vibaya maneno anayoyaongea yule anayemchukia. Ndiyo maana husema kwamba, “tumeanzwa maneno ya kuzungukwa.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kutendeana maovu, kwa kusameheana pale wanaposekeana, ili waweze kuishi kwa amani, maishani mwao.

Wagalatia 5:16-26.

people-women

models-1

ENGLISH: WE HAVE NOW STARTED TO BE TOLD IMPLICIT WORDS.

Implicit words are figurative words which are spoken by someone to others while the target is tell one who is within that group. These words are spoken to the person with whom they have quarreled for expressing an anger which is in their hearts. The one has been been talked about finds it annoying. That’s why this one says that, “We have now started to be told implicit words.”

This saying is compared to a person who likes to quarrel with others in life. This person does not like to listen to the words of the person whom he/she hates, because of his/her anger. He/she uses figurative language through others, for the purpose of conveying a message to his/her enemy because of an absence of love for enemies.

This person has difficult in forgiving the people who have wronged him/her in life. He/she misinterprets the words which are spoken by someone whom he/she hates. That’s why he/she says that, “We have now started to be told implicit words.”

This saying imparts in people an idea of stopping treating each other badly, by forgiving each other after offending each other, so that they can live peacefully in their lives.

Galatians 5: 16-26.

women-11

971. UNG’WENUYO NG’WANA ONDELA.

Ung’wana ondela ali ng’wana ONtemi. Ung’wana ng’wunuyo, agikilaga na kajile kawiza kunguno nawe alintemi duhu aha shigu ijahabhutongi. Uweyi ligashikaga likanza lya gwinhiwa bhutemi kunguno ikale untemi ulu ucha, ung’wana okwe winhiwagwa ubhutemi b’unubho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “ung’wenuyo ng’wana ondela.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe bho ng’holo yawiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajilanijaga na malagilo ga bhatale agawiza, kunguno ya bhutogwa bhokwe ukubhanhu bhakwe. Uweyi agambilijaga bhanhu bhingi ugugamala wangu amakoye gabho, kunguno ya kajile kakwe kenako aka gwigulambija gutumama milimo bho ng’holo yawiza giko, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu ng’wana ondela uyo agadimaga malagilo miza ga bhatale bhakwe, kunguno nuweyi agatumamaga milimo yakwe bho ng’holo yawiza, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “ung’wenuyo ng’wana ondela.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kutumama milimo yabho bho ng’holo niza, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi ga gubhalanhanila chiza abhanhu bhabho, umuwikaji bhobho.

Wakolosai 3:20-21.

Wakolosai 4:1.

KISWAHILI: HUYU NI MTOTO WA MFALME.

Mtoto wa mfalme huitwa mfalme wa baadaye kwa sababu ya mwenendo wake kuwa mwema. Mtoto huyo, huwa na tabia njema kwa sababu ya kutunza maadili yake yatakayo muwezesha kupewa ufalme. Yeye huwa anapewa ufalme huo baadaye kwa sababu, zamani mfalme akifa, mtoto wake, alipewa ufalme huo. Ndiyo maana watu humuita kwamba, “huyu ni mtoto wa mfalme.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatekeleja majukumu yake kwa moyo mwema, katika maisha yake. Mtu huyo, huishi kwa kufuata maadili mema ya wakubwa wake, kwa sababu ya upendo wake kwa wake. Yeye huwasaidia watu wengi katika kuyatatua matatizo yao, kwa sababu ya tabia yake hiyo njema ya kujituma kufanya kazi vizuri, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na mtoto wa mfalme anayeyaishi vizuri maadili mema ya wakubwa wake, kwa sababu naye huyaendeleza maadili hayo mema ya kuyatekeleza majukumu yake kwa moyo mwema, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humuita kwamba, “huyu ni mtoto wa mfalme.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuyatekeleza majukumu yao, kwa moyo mwema, ili waweze kupata mafanikio mengi ya kuwatunzia watu wao, maishani mwao.

Wakolosai 3:20-21.

Wakolosai 4:1.

ENGLISH: THIS IS THE KING’S CHILD.

This saying speaks about the Son who is called the future king because of his good conduct. This child has good manners because he maintains the values ​​that will enable him to be given the kingdom of his father. He will later be given such kingdom after passing away of his father. That is why people say to him that, “this is the king’s child.”

This saying is equaled to a person who carries out his duties with a good heart in his life. Such man lives by the good morals of his leaders because of his love for his people. He helps many people in solving their problems because of his good work ethic in his life.

This person is like a prince who lives up to the moral standards of his father, because he also develops the noble character of performing his duties with a good heart in his life. That is why people speak about him that, “this is the king’s child.”

This saying teaches people on how to carry out their responsibilities in good faith, so that they can have more successes in taking care of their people in their lives.

Colossians 3: 20-21

Colossians 4: 1.