Akahayile akajisuguma kenako kingilile kuwikaji bha bhasuguma abho bhagikalaga lwande lo suguma ng’weli ya Tanzania. Aho wandijo ubhugota bholibhudolechaga miti ya gupija duhu, aliyo hangi bholechaga bhupija bho moyo, ni kujo lya gumala makoye kubhanhu. Umunhu uyo alinabhugota bho mbiga ningi wigelaga giki alina nguzu, bhugagaja, na wibhegeleja bho heke. Umunhu ng’wunuyo winhagwa ikujo na bhanhu bhakwe kunguno ya gugamala amakoye gabho chiza. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “umunhu uyu ali nsabhi o bhugota.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali na bhumani wingi wa gugamala amakoye umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, adadumaga ugugamala amakoye kunguno ya bhumani bhokwe bhunubho umukikalile kakwe. Uweyi agadulaga ugubhalela chiza abhanhu bha aha kaya yakwe kunguno ya bhumani bhokwe bhunubho ubho gugamala amakoye chiza, umuwikaji bhokwe bhunubho.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nu nsabhi obhugota bho gupija bhanhu kunguno nuweyi alina bhumani bho gugamala chiza amakoye ga bhanhu bha aha kaya yakwe umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhakwe bhaganhayaga giki, “umunhu uyu ali nsabhi o bhugota.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya solobho ya gwibhegeleja bho gupandika bhumani, na bhugagaja umuwikaji bhobho kugiki bhadule gugamala chiza amakoye gabho umuwikaji bhobho bhunubho.
Katika Mithali 24:5.
Katika Mhubiri 7:12.
Katika Yakobo 1:5.
SWAHILI: MTU HUYU NI TAJIRI WA DAWA.
Msemo huu wa Kisukuma unatokana na maisha ya kijamii ya Wasukuma wanaoishi sehemu ya kaskazini magharibi mwa Tanzania. Hapo awali, “dawa” haikumaanisha tu mimea ya kuponya magonjwa, bali pia ilijumuisha tiba za kiroho, na hekima ya kushughulikia matatizo ya maisha. Mtu aliyekuwa na aina nyingi za dawa alionekana kuwa na nguvu, mbunifu, na aliyejiandaa vyema kwa hali tofauti. Mtu kama huyo aliheshimiwa na wanajamii kwa sababu ya kuwa na suluhisho la changamoto mbalimbali. Ndiyo maana watu walisema “mtu huyu ni tajiri wa dawa.”
Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana ujuzi, maarifa, au rasilimali kadhaa za kutatua matatizo maishani mwake. Mtu huyu hashindwi kirahisi na matatizo kwa sababu ya “kuwa na utalaamu” kwa njia kadhaa kimwili, kiakili, au kiroho maishani. Yeye hufanikiwa kuwalea vyema wanafamilia wake kwa sababu ya ujuzi wake huo wa kutatua matatizo mbalimbali maishani mwake.
Mtu huyu hufanana na yule aliyekuwa na dawa kadhaa za kuponya watu kwa sababu naye pia ana ujuzi wa kutatua matatizo ya wanafamilia wake maishani. Ndiyo maana wanafamilia wake hao husema kwamba “mtu huyu ni tajiri wa dawa.”
Msemo huu huwafundisha watu kuhusu umuhimu wa kujitayarisha kwa kujipatia ujuzi, na ubunifu maishani. Huwatia watu moyo wa kutafuta hekima, kujifunza ujuzi tofauti, na kujiimarisha kiroho na kijamii. Yenyewe pia huwakumbusha kwamba “utajiri” wa kweli si utajiri wa kimwili tu bali pia uwezo wa kushughulikia changamoto za maisha kwa ufanisi.
Katika Mithali 24:5 “Mtu mwenye hekima ana nguvu nyingi, na mtu mwenye maarifa huongeza nguvu zake.” Hii inaonyesha kwamba maarifa na hekima ni aina za nguvu za kweli.
Katika Mhubiri 7:12 “Hekima huwahifadhi walio nayo.” Kama vile dawa inavyolinda mwili, hekima hulinda uhai.
Katika Yakobo 1:5 “Mtu yeyote kati yenu akipungukiwa na hekima, na amwombe Mungu.” Hii inasisitiza kwamba “dawa” ya kiroho hutoka kwa Mungu.
Kwa ujumla, msemo unasisitiza kwamba mtu “aliye tajiri wa dawa” ni yule ambaye ana hekima nyingi, maandalizi, na uwezo wa kushinda magumu ya maisha.
ENGLISH: THIS PERSON IS RICH IN MEDICINES.
This Sukuma saying comes from community life of the Sukuma people who live in the northwestern part of Tanzania. In the past, “medicine” did not only mean herbs for healing sickness, but also included spiritual remedies, and wisdom for dealing with life’s problems. A person who possessed many kinds of medicine was seen as powerful, resourceful, and well-prepared for different situations. Such a person was respected by societal members because of having solutions to various challenges. That is why people said “this person is rich in medicines.”
This saying is compared to a person who has several skills, knowledge, or resources of solving problems in his life. This person is not easily defeated by difficulties because of being “equipped” in several ways physically, mentally, or spiritually in life. He succeeded in nicely nurturing his family members because of his skills for solving various difficulties in his life.
This person resembles the one who possessed several medicines for healing people because he also has skills for solving problems of his family members in life. That is why his family members say “this person is rich in medicines.”
This saying teaches people about the importance of being prepared, knowledgeable, and resourceful in life. It encourages people to seek wisdom, learn different skills, and strengthen themselves spiritually and socially. It also reminds them that true “richness” is not only material wealth but also the ability to handle life’s challenges effectively.
In Proverbs 24:5 “A wise man is full of strength, and a man of knowledge enhances his might.” This shows that knowledge and wisdom are forms of true strength.
In Ecclesiastes 7:12 “Wisdom preserves those who have it.” Just like medicine protects the body, wisdom protects life.
In James 1:5 “If any of you lacks wisdom, you should ask God.” This highlights that spiritual “medicine” comes from God.
Overall, the saying emphasizes that a person who is “rich in medicines” is one who is rich in wisdom, preparation, and the ability to overcome life’s difficulties.