Justina

1544. SUKUMA: IKAYA IYO IGASALILAGA KIHAMO IGIKALAGA KIHAMO.

Olihoyi munhu uyo osalilaga kihamo ni kaya yakwe. Uweyi obhakomelejaga abha ha kaya yakwe gusalila rozari kubhulingisilo bho gubhalumanya chiza abhanhu bhakwe umuwikaji bhokwe. Ubhulingisilo bhokwe bhunubho bhugabhambilija abhanhu bhakwe gwikala kihamo umuwikaji bhobho. Hunagwene agayomba giki, “ikaya iyo igasalilaga kihamo igikalaga kihamo.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agantongejaga Mulungu aha kaya yakwe. Umunhu ng’wunuyo, obhakomelejaga gusalila kihamo abhanhu bhakwe bho gung’wisanya Mulungu umukakoye nu mubhuyegi, na gwilekeja kunguno ya gunzunya mulungu umukikalile kakwe. Uweyi agadujaga ugubhalela chiza abhanhu bha ha kaya yakwe kunguno ya gung’wisanya Mulungu umuwikaji bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo osalilaga kihamo ni kaya yakwe mpaka ubhambilija gwikala kihamo abhanhu bhakwe kunguno nuweyi agang’wisanya Mulungu mpaga obhalela chiza abhanhu bhakwe umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “ikaya iyo igasalilaga kihamo ikikalaga kihamo.”

Ulusumo lunulo lobhalanga abhanhu gubhiza na witegeleja bho gung’wisanya Mulungu na gwitogwa umubhuzunya bhobho kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Yoshua 24:15.

Mathayo 18:20.

Wakolosai 3:13-14.

Waefeso 6:1-4.

Zaburi 127:1.

Matendo 2:46–47.

SWAHILI: FAMILIA INAYOSALI PAMOJA HUDUMU PAMOJA.

Kulikuwa na mtu aliyesali pamoja na familia yake. Alihimiza wanafamilia wake kusali sala ya familia, hasa Rozari, kupitia Rozari ya Familia kwa lengo la kuwaunganisha wanafamilia wote maishani mwao. Lengo lake liliwawezesha wanafamilia kubaki wameungana pamoja maishani mwao. Ndiyo maana yeye alisema kwamba, “familia inayosali pamoja hudumu pamoja.”

Methali hii hulinganishwa kwa mtu yule anayemtanguliza Mungu katika familia yake. Mtu kama huyo huwatia moyo wanafamilia wake wa kusali pamoja, kumwamini Mungu wakati wa furaha na shida, kusameheana, na kuimarisha umoja wa familia kupitia imani. Yeye aliweza kuwalea vyema wanafamilia wake kwa sababu ya kumtanguliza Mungu katika maisha ya familia yake.

Mtu huyu hufanana na yule aliyesali pamoja na familia yake vya kutosha kuiwezesha familia yake kukaa pamoja, kwa sababu ya kumweka Mungu mahali pa kwanza katika familia yake hadi kufikia hatua ya kuwalea vyema wanafamilia maishani mwake. Yeye huiongoza familia kwa imani na mfano mzuri wa kuigwa na huleta amani na upatanisho kwenye migogoro inapotokea, kwa kuhimiza upendo, heshima kwa wanafamilia wote. Yeye pia humtegemea Mungu badala ya nguvu za kibinadamu pekee kwa ajili ya kujenga familia yenye maadili ya kiroho na utii kwa Mungu. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “familia inayosali pamoja hudumu pamoja.”

Methali hii huwafundisha watu kuhusu kumweka Mungu mahali pa kwanza katika familia zao kwa kukuza sala ya familia, umoja, kuamini mwongozo wa Mungu, ulinzi, upendo, utunzaji wa pamoja miongoni mwa wanafamilia, na nguvu ya imani katika kushinda changamoto, ili waweze kujenga familia imara juu ya msingi wa kiroho badala ya kimwili tu katika maisha yao.

Yoshua 24:15. “Mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana.”

Mathayo 18:20. “Kwa maana walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu, mimi nipo hapo pamoja nao.”

Wakolosai 3:13-14. Mtakatifu Paulo anawaita waumini kusameheana na kuvaa upendo, ambao hufunga kila kitu pamoja katika umoja kamili.

Waefeso 6:1-4 inawafundisha watoto na wazazi kuishi katika utii, upendo, na nidhamu ya kimungu.

Zaburi 127:1. “Bwana asipoijenga nyumba, wajenzi wanafanya kazi bure.”

Matendo 2:46–47. Waumini wa mwanzo walikutana pamoja kwa umoja, maombi, na ushirika, wakionesha nguvu inayotokana na imani ya pamoja.

Kwa hiyo, methali hii “Familia inayosali pamoja huduma pamoja” inatukumbusha kwamba umoja wa kudumu wa familia hujengwa juu ya uhusiano wa pamoja na Mungu. Familia zinazosali pamoja hujenga vifungo imara vya upendo, uaminifu, msamaha, na kuwawezesha kukabiliana na changamoto za maisha kwa imani na matumaini.

ENGLISH: A FAMILY THAT PRAYS TOGETHER STAYS TOGETHER.

There was a person who prayed together with his family. He promoted family prayer, especially the Rosary, through the Family Rosary because of aiming at uniting all family members on the way to God. His aim enabled the famiy members to stay united together in his life. That is why he said “a family that prays together stays together.”

This proverb is compared to a person who places God at the center of his family life. Such a person encourages family members to pray together, trust God in times of joy and difficulty, forgive one another, and strengthen family unity through faith. He managed to nicely nurture his family members because of placing God at the center of the family in his life.

This person resembles the one who prayed together with his family enough to enable his family stay together, because of placing God at the center of his family to the point of nurturing well the family members in his life.  He leads the family by faith and good example and brings peace and reconciliation whenever conflicts arise by encouraging love, respect, and mutual support among family members. He also depends on God rather than human strength alone by building a home founded on spiritual values and obedience to God. That is why he says, “a family that prays together stays together.”

This proverb teaches people about of placing God at the center of their family by promoting family prayer, unity, hormany, trust in God’s guidance, protection, love, fogiviness, mutual care among family members, and power of faith in overcoming challenges, so that they can build a strong family on spiritual rather than material foundation in their lives.

Joshua 24:15. “As for me and my house, we will serve the Lord.”

Matthew 18:20. “For where two or three gather in my name, there am I with them.”

Colossians 3:13–14.  St. Paul calls believers to forgive one another and put on love, which binds everything together in perfect unity.

Ephesians 6:1–4. teaches children and parents to live in obedience, love, and godly discipline.

Psalm 127:1. “Unless the Lord builds the house, the builders labor in vain.”

Acts 2:46–47. The early believers met together in unity, prayer, and fellowship, demonstrating the strength that comes from shared faith.

Therefore, this proverb a Family that prays together stays together” reminds us that lasting family unity is built on a shared relationship with God. Families that pray together develop stronger bonds of love, trust, forgiveness, and mutual support, enabling them to face life’s challenges with faith and hope.

1539. SUKUMA: LILONDA LYA MUNHOLO LIDABHONAGWA BHO MISO.

Ulusumo lunulo lwingilile kusumo ja jiafrica. Lulimhoyela munhu uyo agakoyiyagwa ni lilolanda lya mugati ya mholo yakwe ilo lidabhonagwa ubho miso na bhiye. Ililonda linilo ligaminyaga uweyi bho sele sele duhu kunguno abhanhu bhadalibhonaga. Hunagwene agayombaga giki, “lilonda lya munholo lidabhonagwa bho miso.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agolechaga bhuyeji bho bhanze aliyo alina makoye umugati yakwe, umuwikaji bhokwe bhunubho. Umungu ng’wunuyo, agayegana na gwigela giki alina nguzu bho hanze ukunu alina bhupina bhutale umunholo yakwe kunguno ya bhusatu bho makoye gakwe genayo ayo bhadagabhonabho abhiye umukikalile kakwe. Uweyi agiyumilijaga bho sele sele uguyilela ikaya yakwe kunguno nduhu uyo agagabhonaga amakoye gakwe genayo umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo wiyumilijaga bhusadu bho lilonda lyakwe, kunguno nuweyi agagiyumilija amakoye agaguyilela chiza ikaya yakwe yiniyo umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “lilonda lya munholo lidabhonagwa bho miso.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na lisungu lya gubhambilija abhanhu abho bhali na makoye kugiki bhadule gupandika mbango ja gwikala na bhuyegi umukaya jabho jinijo.

Mithali 14:10.

Zaburi 34:18.

1Samweli 16:7.

Mathayo 11:28.

Zaburi 147:3.

SWAHILI: KIDONDA CHA MOYO HAKIONEKANI KWA MACHO.

Asili ya methali hii inapatikana katika mila na misemo mingi yenye hekima za Kiafrika. Inaelezea ukweli kwamba maumivu ya kihisia, kiroho, na kisaikolojia hayawezi kuonekana kwa nje kama kidonda cha mwilini, lakini yanaweza kuwa ya kina na yenye uchungu zaidi. Mtu aliye na kidonda hicho ndani yake huteseka kimya kimya maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “kidonda cha moyo halionekani kwa macho.”

Methali hii hulinganishwa kwa mtu yule anayeonekana mwenye furaha lakini ana majeraha ndani yake maishani mwake. Mtu huyu hutabasamu na kuonekana mwenye nguvu kwa nje huku akiwa na huzuni kubwa maishani mwake kwa sababu ya kuwa na huzuni, na maumivu ya kihisia ndani ya maisha yake. Yeye huvumilia mateso kimya kimya katika kuwalea wanafamilia wake kwa sababu hakuna anayeweza kuona maumivu yaliyomo moyoni mwake.

Mtu huyo hufanana na mtu aliyeteseka kutokana na maumivu yake, kwa sababu naye pia huteseka kutokana na maumivu ya kihisia maishani mwake. Yeye ni kama mtu ambaye mwili wake unaonekana kuwa na afya njema, lakini moyo wake umelemewa na kukataliwa, usaliti, upweke, hatia, au hasara. Wengine wanaweza wasigundue maumivu hayo kwa sababu yamefichwa ndani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “kidonda cha moyo halionekani kwa macho.”

Methali hii huwafundisha watu kuhusu: Kuwa na huruma na uelewa kwa wengine. Kuepuka hukumu za haraka kwa sababu hatujui wengine wanapitia nini. Umuhimu wa kuwafariji na kuwatia moyo wale wanaoumia. Kutafuta uponyaji kwa majeraha ya kihisia na kiroho. Kuonesha wema, kwa kuwa maumivu yaliyofichwa mara nyingi ni makubwa kuliko maumivu yanayoonekana.

Mithali 14:10. “Moyo hujua uchungu wake, wala mgeni hashiriki furaha yake.” Mstari huu unafundisha kwamba maumivu mengine hujulikana tu kwa mtu anayeyapitia.

Zaburi 34:18. “Bwana yuko karibu nao waliovunjika moyo, huwaokoa waliopondeka roho.” Mungu huona na huponya majeraha ambayo macho ya wanadamu hayawezi kuona.

1Samweli 16:7. “Mwanadamu hutazama sura ya nje, bali Bwana hutazama moyo.” Wakati watu wanaona nje, Mungu huona hali iliyofichwa ya moyo.

Mathayo 11:28. “Njooni kwangu, ninyi nyote mlio na kazi na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Yesu anawaalika wale waliobeba mizigo isiyoonekana kupata faraja kwake.

Zaburi 147:3. “Huwaponya waliovunjika moyo na kuyafunga majeraha yao.” Mungu ndiye mponyaji wa majeraha yanayoonekana na yasiyoonekana.

Jeraha la kimwili linaweza kuonekana na kila mtu, lakini jeraha la moyoni mara nyingi hufichwa. Kwa hivyo, tunapaswa kuwatendea wengine kwa wema, uvumilivu, na upendo, tukikumbuka kwamba ni Mungu pekee anayejua kikamilifu maumivu ambayo watu hubeba ndani yao.

ENGLISH: A HEART WOUND IS INVISIBLE TO THE EYES.

The original of this proverb is found in many African traditions and wisdom sayings. It expresses the truth that emotional, spiritual, and psychological pain cannot be seen outwardly like a physical wound, yet it can be deeper and more painful. The person who has inner wounds suffers silently in his life. That is why he says, “a heart wound is invisible to the eyes.”

This proverb is compared to a person who appears happily but has wounds within him in life. This person smiles and appears strong on the outside while carrying deep sorrow in his life because of having disappointment, grief, and emotional pain within himself in life. He endures sufferings silently in nurturing his family members because no one can see the wounds which are in his heart.

This person resembles the person who suffers from his wounds, because he also suffers from emotional pain in his life. He is like someone whose body appears healthy, but whose heart is burdened by rejection, betrayal, loneliness, guilt, or loss. Others may not notice the pain because it is hidden inside. That is why people say about him “a heart wound is invisible to the eyes.”

This proverb teaches people about: Being compassionate and understanding toward others. Avoiding quick judgments because we do not know what others are going through. The importance of comforting and encouraging those who are hurting. Seeking healing for emotional and spiritual wounds. Showing kindness, since hidden pain is often greater than visible pain.

Proverbs 14:10. “The heart knows its own bitterness, and no stranger shares its joy.” This verse teaches that some pains are known only to the person experiencing them.

Psalm 34:18. “The Lord is near to the brokenhearted and saves the crushed in spirit.” God sees and heals wounds that human eyes cannot see.

1Samuel 16:7. “Man looks at the outward appearance, but the Lord looks at the heart.” While people see the outside, God sees the hidden condition of the heart.

Matthew 11:28. “Come to me, all who labor and are heavy laden, and I will give you rest.” Jesus invites those carrying invisible burdens to find comfort in Him.

Psalm 147:3. “He heals the brokenhearted and binds up their wounds.” God is the healer of both visible and invisible wounds.

A physical wound may be seen by everyone, but a wound in the heart is often hidden. Therefore, we should treat others with kindness, patience, and love, remembering that only God fully knows the pain that people carry within.

1529. SUKUMA: UYO ADIZUKAGA UKO OFUMILA, AGAJIMILAGA UKO AJILE.

Ulusumo lunulo lulolile likujo lya kihalile ka jiafrika. Abhanhu bhalangagwa gwizuka imbuki ya kaya jabho, kikalile, ni nhungwa ijawiza. Abhatale bhalibhamana igiki umunhu uyo agibhaga imbuki ya mizwi yakwe agajimilaga wangu umuwikaji bhokwe. Hunagwene bhagang’wilaga giki “uyo adizukaga uko ofumila, agajimilaga uko ajile.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalekaga imbuki ya kikalile ka bhatale bhakwe nu bhulangwa ubho bhonkuja, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, alinanhinda ja gubhulema ubhushauli bho gwita mihayo ya sagala kunguno ya gubhudalahija ubhulangwa bho bhatale bhakwe umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agadumaga uguimala imilimo ya ha kaya yakwe kunguno ya guleka gubhudilila chiza ubhulangwa bho bhatale bhakwe, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agayibhaga imizwi ya bhatale bhakwe mpaka ojimila, kunguno nuweyi agabhudalahijaga ubhulangwa bho bhatale bhakwe mpaka oduma uguyimala chiza imilimo yakwe yiniyo, aha kaya yakwe, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “uyo adizukaga uko ofumila, agajimilaga uko ajile.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya: gwizuka isumo yabho, bho gubhakuja abhabyaji bhabho, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Kumbukumbu la Torati 8:2.

Mithali 22:28.

Luka 15:17-18.

Zaburi 78:4.

Yeremia 6:16.

SWAHILI: ASIYEKUMBUKA ALIPOTOKA, HUPOTEA AENDAKO.

Methali hii inatokana na hekima ya kitamaduni ya Kiafrika. Katika jamii nyingi za Kiafrika, watu walifundishwa kukumbuka historia ya familia zao, utamaduni, mila, na maadili. Wazee waliamini kwamba mtu anayesahau mizizi yake hupoteza mwelekeo maishani kwa urahisi. Methali hiyo ilitumika sana kuwakumbusha vijana kuheshimu historia yao, wazazi, mila, na imani. Ndiyo maana wazee walimwambia yule anayesahau mizizi yake kwamba, “asiyekumbuka alipotoka, hupotea aendako.”

Methali hii hulinganishwa kwa mtu yule anayeacha mila zake kwa kupuuza ushauri mzuri kutoka kwa wazee ulioyaunda maisha yake. Mtu kama huyo huwa na kiburi kimpelekeacho kuwa na hali kuchanganyikiwa, au kufanya maamuzi mabaya kwa sababu hakumbuki tena msingi wa maisha yake. Yeye hushindwa kutimiza malengo yake katika familia yake kwa sababu ya kupuuza ushauri mzuri kutoka kwa wazee wake katika maisha yake.

Mtu huyu hufanana na yule mtu aliyesahau mizizi yake akapokea, kama msafiri anayetembea msituni bila kujua njia aliyotumia kuingia. Kwa kuwa amesahau njia aliyotoka, anapotea na hawezi kupata mwelekeo sahihi kwa urahisi. Ndiyo maana watu humuonya kwa kusema kwamba, “asiyekumbuka alipotoka, hupotea aendako.”

Methali hii huwafundisha watu kuhusu: kukumbuka asili na historia yao, kwa kuwaheshimu wazazi, wazee, na mila, kujifunza kutokana na uzoefu wa zamani, kubaki wanyenyekevu hata baada ya mafanikio, na kudumisha imani na maadili popote wanapokwenda, ili waweze kufanikiwa katika kuwalea wanafamilia wao, katika maisha yao.

Methali huwafundisha watu kwamba, mtu anayekumbuka asili yake atakuwa na hekima, mwongozo, na utulivu maishani.

Kumbukumbu la Torati 8:2. “Kumbuka jinsi Bwana, Mungu wako, alivyokuongoza njia yote jangwani miaka hii arobaini.” Mstari huu unawafundisha watu kutosahau mahali ambapo Mungu amewaleta kutoka.

Mithali 22:28. “Usiondoe mawe ya mpaka wa zamani yaliyowekwa na mababu zako.” Hii inawakumbusha watu kuheshimu misingi na mila zilizorithiwa na mababu zao.

Luka 15:17-18. Mwana mpotevu alikumbuka nyumba ya baba yake baada ya kupotea katika maisha ya dhambi. Kukumbuka nyumba yake kulimsaidia kurudi kwenye njia sahihi.

Zaburi 78:4. “Tutawaambia kizazi kijacho matendo ya sifa ya Bwana.” Mstari huu unawahimiza watu kukumbuka na kuhifadhi historia na imani yao.

Yeremia 6:16. “Simama kwenye makutano ya barabara mkaone; uliza njia za kale, uliza njia iliyo njema iko wapi, na uifuate.” Hii inawafundisha watu kufuata njia nzuri na hekima ya zamani.

ENGLISH: HE WHO DOES NOT REMEMBER WHERE HE COMES FROM, HE GETS LOST WHERE HE GOES.

This proverb originates from traditional African wisdom. In many African communities, people were taught to remember their family background, culture, traditions, and values. Elders believed that a person who forgets his roots easily loses direction in life. The proverb was commonly used to remind young people to respect their history, parents, customs, and faith. That is why the elders told the one who forgets his roots “he who does not remember where he comes from, he gets lost where he goes.”

This proverb is compared to a person who abandons his traditions, ignores good advice from elders, and forgets the struggles that shaped his life. Such a person may become proud, confused, or make wrong decisions because he no longer remembers the foundation of his life. He fails to actualize his goals at his family because of ignoring good advice from elders in his life.

This person resembles the traveler who walks into a forest without knowing the path he used to enter. Since he has forgotten the way he came from, he becomes lost and cannot easily find the right direction. That is why people warm him saying “he who does not remember where he comes from, he gets lost where he goes.”

This proverb teaches people about: remembering their roots and background, by respecting parents, elders, and traditions, learning from past experiences, staying humble even after success, and keeping faith and moral values wherever the go, so that they be successfully in nurturing their family members, in their lives.

The proverb teaches that a person who remembers his origin will have wisdom, direction, and stability in life.

Deuteronomy 8:2. “Remember how the Lord your God led you all the way in the wilderness these forty years.” This verse teaches people not to forget where God has brought them from.

Proverbs 22:28. “Do not move the ancient boundary stones set up by your ancestors.” This reminds people to respect the foundations and traditions handed down by their forefathers.

Luke 15:17-18. The prodigal son remembered his father’s house after getting lost in sinful living. Remembering his home helped him return to the right path.

Psalm 78:4. “We will tell the next generation the praiseworthy deeds of the Lord.” This verse encourages people to remember and preserve their history and faith.

Jeremiah 6:16. “Stand at the crossroads and look; ask for the ancient paths, ask where the good way is, and walk in it.” This teaches people to follow the good paths and wisdom from the past.

 

 

 

 

1528. SUKUMA: NZILAMAKA IGANJIMIJAGA UNSIMINZI.

Ulusumo lunulo lufumilile kulikujo lya kale ilya Africa. Ikale abhasiminzi wasiminzaga bho magulu bhalibhitila mumapolu, mabhonde na mumachalo bho mduhu ramani. Abhanhu bhenabho bhashikaga aha nzilamaka bhajimija ijilunga. Hunagwene bhagayomba giki, “njilamaka iganjimijaga unsiminzi.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhonaga wiza wingi oduma uguchagula nulu jimo umuwikaji bhokwe bhunubho. Umunhu ng’wunuyo, agadumaga uguchagula josejose ulu ubhonaga majikolo mingi agawiza kunguno ya gugawila bhumani wikujo lya kikalile kiza umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agajimijaga ijilunga ja guitongela chiza ikaya yakwe kunguno ya gugaiwa bhulangwa bho guchagula chiza, umuwikaji bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nabhasiminzi bha mumapoli abho bhagajimija ijilunga, kunguno nuweyi agajimijaga amasala ga guchagula chiza mpaga oduma uguitongela chiza ikaya yakwe ulu obhonaga majikolo mingi agawiza, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki “njizamaka iganjimijaga unsiminzi.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho guchagula gwikala chiza ulubhabhonaga majikolo mingi agawiza, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umukaya yabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mithali 3:5–6.

Mathayo 7:13–14.

Yakobo 1:5.

1Wakorintho 14:33.

SWAHILI: NJIA PANDA HUMCHANGANYA MSAFIRI.

Methali hii inatokana na hekima ya jadi ya Kiafrika na pia inaakisiwa katika tamaduni nyingi kote ulimwenguni. Zamani, wasafiri walisafiri kwa miguu kupitia misitu, mabonde, na vijiji bila ramani. Walipofika kwenye barabara nyingi zinazovuka yaani njia panda, waliweza kuchanganyikiwa kwa urahisi na kupoteza mwelekeo. Kwa hivyo methali hiyo iliundwa ili kuwafundisha watu umuhimu wa hekima, mwongozo, na kufanya maamuzi yaliyo wazi maishani mwao. Ndiyo maana walisema kwamba, “njia panda humchanganya msafiri.”

Methali hii hulinganishwa kwa mtu yule hukabiliwa na chaguzi nyingi maishani na hajui ni njia gani ya kufuata maishani mwake. Mtu kama huyo huweza kuchanganyikiwa kwa sababu ya maoni mengi, vishawishi, au fursa nyingi maishani. Yeye hupoteza mwelekeo wa kuongoza familia yake vizuri kwa sababu ya kukosa hekima, mwongozo, na uwezo wa kufanya maamuzi mazuri maishani mwake.

Mtu huyu hufanana na wale watu waliokosa mwongozo na hekima sahihi hadi kufikia hatua ya kupoteza mwelekeo wao kwa sababu naye pia hufuata maelekezo mengi kwa wakati mmoja na hatimaye hupoteza umakini katika kuongoza familia yake hiyo maishani mwake. Kama vile msafiri anavyoweza kupotea kwenye njia panda, mtu asiye na kusudi wazi anaweza kupotea kiroho, kimaadili, au kijamii maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “njia panda humchanganya msafiri.”

Methali hii huwafundisha watu kuhusu: umuhimu wa hekima katika kufanya maamuzi, kutafuta mwongozo kabla ya kuchagua njia, kubaki makini maishani, kuepuka mkanganyiko unaosababishwa na mawazo mengi yanayokinzana, na kuamini uongozi na mwelekeo mzuri. Inawakumbusha watu kwamba maisha yana njia nyingi, na chaguo baya zaweza kusababisha matatizo huku chaguo za busara zikiongoza kwenye mafanikio na amani maishani mwao.

Mithali 3:5–6. “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mtii, naye atanyosha mapito yako.” Mstari huu unafundisha kwamba Mungu hutoa mwongozo wakati barabara za maisha zinaonekana kuchanganyikiwa.

Mathayo 7:13–14. “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba… mlango ni mdogo, na njia nyembamba iendayo uzimani.” Yesu anafundisha kwamba kuna njia nyingi maishani, lakini njia sahihi tu ndiyo inayoongoza kwenye uzima wa milele.

Yakobo 1:5. “Lakini mtu yeyote kati yenu akipungukiwa na hekima, na amwombe Mungu, awapaye wote kwa ukarimu.” Watu wanapokabiliwa na maamuzi yanayochanganya, wanapaswa kutafuta hekima kutoka kwa Mungu.

1Wakorintho 14:33. “Maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani.” Mungu anatamani watu wake watembee katika uwazi, amani, na mwelekeo sahihi badala ya mkanganyiko.

Methali “njia panda humchanganya msafiri” hufundisha kwamba maisha yamejaa chaguzi na njia panda. Bila hekima, mwongozo, na imani katika Mungu, mtu anaweza kupoteza mwelekeo kwa urahisi. Watu wenye busara hutafuta ushauri, huomba uelewa, na kwa uangalifu.

ENGLISH: “INTERSECTION OF ROADS CONFUSES THE TRAVELER.”

This proverb comes from traditional African wisdom and is also reflected in many cultures around the world. In ancient times, travelers journeyed on foot through forests, valleys, and villages without maps. When they reached many crossing roads, they could easily become confused and lose direction. The proverb was therefore created to teach people the importance of wisdom, guidance, and clear decision-making in life. That is why they said, “Intersection of roads confuses the traveler.”

This proverb is compared to a person who faces many choices in life and does not know which path to follow in life. Such a person may become confused because of too many opinions, temptations, or opportunities. He loses direction of leading well his family because of lacking wisdom, guidance, and clear decision-making in life.

This person resembles those people who lacked proper guidance and wisdom to the point of losing their directions because he also follows many directions at the same time and finally loses focus in leading his family in life.

Just as a traveler can become lost at roads intersection, a person without clear purpose can become lost spiritually, morally, or socially. That is why people tell him that, “Intersection of roads confuses the traveler.”

This proverb teaches people about: the importance of wisdom in making decisions, seeking guidance before choosing a path, remaining focused in life, avoiding confusion caused by many conflicting ideas, and trusting good leadership and direction. It reminds people that life has many crossroads, and wrong choices can lead to trouble while wise choices lead to success and peace.

Proverbs 3:5–6. “Trust in the Lord with all your heart and lean not on your own understanding; in all your ways submit to Him, and He will make your paths straight.” This verse teaches that God gives direction when life’s roads seem confusing.

Matthew 7:13–14. “Enter through the narrow gate… small is the gate and narrow the road that leads to life.” Jesus teaches that there are many paths in life, but only the right path leads to eternal life.

James 1:5. “If any of you lacks wisdom, you should ask God, who gives generously to all.” When people face confusing decisions, they should seek wisdom from God.

1Corinthians 14:33.“For God is not a God of confusion but of peace.” God desires His people to walk in clarity, peace, and right direction rather than confusion.

The proverb “intersections of roads confuse the traveler” teaches that life is full of choices and crossroads. Without wisdom, guidance, and faith in God, a person can easily lose direction. Wise people seek counsel, pray for understanding, and carefully.

 

 

 

850. NZUB’I ADAB’ITILAGA ILAMBO.

Ulusumo lunulo, lulilola nzub’i o shi, nulu ndilo uyo agaja ogazub’a bhuli hilambo lyene mpaga abhite hoyi, gujilola ishi. Unzub’i ng’wunuyo, agitaga giko kunguno ahayile apandike ndilo nyingi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “nzub’i adab’itilaga ilambo.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agasulujaga jikolo jilebhe, uyo agab’itaga bhuli kaya yene, umubhusuluja bhokwe. Unsuluja ng’wunuyo, agajaga uliga bhuli aha kaya yene iyo aliyibhona ilugulile unyango, kunguno atogilwe amale gujijinja pye ijikolo ijo alijisuluja, umunimo gokwe gunuyo. Uweyi agapandikaga solobho mhale noyi umubhusuluja bhokwe bhunubho kunguno ya wikomeja bhokwe ubho gubhita bhuli kaya, umutumami bho milimo yakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nzub’i o ndilo uyo agabhitaga bhuli ilambo, kunguno nu weyi agajaga ubhita bhuli kaya, umubhusuluja bhokwe bhunubho. Uweyi abhalangaga abhanhu bhakwe inzila ja guhoya na bhanhu bhingi umubhutumami bhobho, kugiki bhadule gupandika sabho ningi, umumilimo yabho. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “nzub’i adab’itilaga ilambo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija gubhutumila pye uwasa ubho bhali nabho umubhutumami bho milimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Luka 24:47.

Matendo ya mitume 1:8.

Warumi 10:18.

Marko 16:15-16.

KISWAHILI: MVUVI HAACHI KUPITIA BWAWANI.

Methali hiyo, humwangalia mvuvi wa samaki ambaye hupitia kwenye kila bwawa akitafuta samaki. Mvuvi huyo, hufanya hivyo kwa sababu anataka kupata mafanikio ya kuvua samaki wengi. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mvuvi haachi kupitia bwawani.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huuza vitu fulani, kwa hupitia kwenye kila familia, katika uuzaji wa biashana yake. Mfanya biashana huyo, huenda akiingia kwenye kila familia ambayo anauona mlango wake uko wazi, kwa sababu anapenda kuuza vitu vyake vyote, katika biashara yake hiyo. Yeye hupata faida kubwa sana katika kazi yake hiyo, kwa sababu ya bidii yake ya kupitia kwenye kila familia, katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mtu huyo, hufanana na yule mvuvi wa samaki aliyepitia kwenye kila bwawa, kwa sababu naye huenda akiingia kwenye kila familia, katika biashara yake hiyo. Yeye huwafundisha pia watu wake namna ya kuongea na watu wengi katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika kazi zao. Ndiyo maana huwa anawaambia watu kwamba, “mvuvi haachi kupitia bwawani.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuzitumia fursa zote walizo nazo, katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Luka 24:47.

Matendo ya mitume 1:8.

Warumi 10:18.

Marko 16:15-16.

fisherman-1

people-with fish

visser-fishing zanzibar

fishpond-

ENGLISH: THE FISHER-PERSON DOES NOT JUMP A FISHPOND (TRADITIONS ARE LIKE A  LAW).

This proverb focuses on a fisherman who goes through each pond in searching for fish. He does this because he wants to be successful in catching more fish. That is why people say that, “the fisher-person does not jump a fishpond.”

This proverb is compared to the man who sells certain things by passing through every family in his trade. Such trader enters at every family which he sees that its door is open, because he likes to sell all his goods. He gets a lot of benefits from his work, because of his persistence of passing through each family that can buy his goods.

This man is like the fisherman who passed through every pond, because he too goes into every family that can buy his goods. He also teaches his people on how to communicate with many people in fulfilling their duties, so that they may be more successful in their daily activities. That is why he often tells people that, “the fisher-person does not jump a fishpond (traditions are like a law).”

This proverb teaches people on how to strive to use all the opportunities which they have in fulfilling their daily responsibilities, so that they may have more successes in their families.

Luke 24:47.

Acts 1: 8.

Romans 10:18.

Mark 16: 15-16.