myth

243. LIGELE LYA B’AKENGEJI LILIMBA LYIMBO LYA B’ULUMBI KULI MULUNGU NU KUB’ANZILISHI B’AB’UKENGEJI

LIGELE LYA B’AKENGEJI LILIMBA LYIMBO LYA B’ULUMBI KULI MULUNGU NU KUB’ANZILISHI B’AB’UKENGEJI.

Balikihamo na bha: Rev. Joseph Healey, (Ng’wana Healey), Rev. Donald Sybertz, (Ng’wana Helena), Rev. Sandu, Martin,  Mabula, Clement na bhangi b’ingi.

 

KISWAHILI: KIKUNDI CHA KAMATI YA UTAFITI NDOLELEJI, KIKIIMBA WIMBO WA SHUKRANI KWA MUNGU, NA KWA WAANZILISHI WA UTAFITI.

Hao ni pamoja na: Rev. Joseph Healey, (Ng’wana Healey), Rev. Donald Sybertz, (Ng’wana Helena), Rev. Sandu, Martin, Mabula, Clement na wengine wengi.

ENGLISH: NDOLELEJI RESEARCH COMMITTEE GROUP SINGING A GRATITUDE SONG TO GOD AS WELL AS TO THE RESEARCH FOUNDERS. Video

They include: Rev. Joseph Healey, (Ng’wana Healey), Rev. Donald Sybertz, (Ng’wana Helena), Rev. Sandu, Martin, Mabula, Clement and others. Video of the research committee group singing.

 

 

 

 

242. NG’WIJINJA INGONG’HO NG’WAGULA NG’HOME

Imbuki ya kahayile kenako ilolile ngong’ho na ng’home. Ingong’ho igalenganijiyagwa na ginhu ijo jilijasolob’o, ing’home igalenganijiyagwa na ginhu ija sagara.

 Kuyiniyo lulu, akahayile kenako kalolile bhanhu abho bhagajinjaga ginhu ijo jilinasolobho nhale guti lishamba. Aliyo lulu, ihela jinijo bhagajigulilaga ginhu ijo jidina solobho, guti gujinja ishamba na gugula pigipigi.

Abhanhu bhenab’o b’agagulaga ginhu ja sagara. Hunagwene bhagawilagwa na b’ichab’o bho kahayile kenako ulu b’ajijinja iginhu ja solob’o na gugula ginhu ija sagala.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagajikenagulaga ijikolo jabho ku ginhu ijo jidinasolobho. B’agajitumamilaga isab’o jab’o jinijo b’o gujigulila ginhu ijo jili jasagara. Abhichab’o bhagab’ahugulaga abhanhu bhenabho bho gubhawila giki, ‘bhajinja ngong’ho b’agula ng’home.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gujitumila isab’o jabho bhogujigulila ginhu ijo jilinasolobho. Kab’alemeja abhanhu bhenabho ugujikenagula isab’o jinijo kugiki jidule gub’ambilija ahashigu ijahab’utongi.

KISWAHILI: MMEUZA BUNDUKI MMENUNUA RUNGU

Chanzo cha msemo huo huangalia Bunduki na Rungu. Bunduki hulinganishwa na kitu cha thamani kama shamba, na Rungu hulinganishwa na kitu kisicho na thamani kama pikipiki ikilinganishwa na shamba. Hicho ni kitu cha hovyo.

Kwa hiyo basi, msemo huo huangalia watu wale wauzao vitu vya thamani kubwa na kuitumia pesa hiyo kwa kununulia kitu cha hovyo, yaani kitu kisicho na thamani.

Watu hao huambiwa na wenzao wakionywa kwa kutumia msemo huo wauzapo vitu vya thamani na kuitumia vibaya hela hiyo waliyoipata. Wenzao hao husema, “mmeuza Bunduki mmenunua Rungu!”

Msemo huo hulinganishwa kwa watu wale watumiao vizuri mali zao kwa kuzinunulia vitu visivyo na thamani. Watu hao huzitumia mali zao kwa kununulia vitu vya hovyo. Wenzao huwaonya kwa kuutumia msemo huo wakisema, ‘mmeuza Bunduki na mmenunua Rungu.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kutumia mali zao kwa kununulia vitu vyenye thamani badala ya kuziharibu kwa kuzitumia kwenye mambo ya hovyo.

Msemo huo huwakataza watu hao kuziharibu hovyo mali zao ili ziweze kuwasaidia baadaye kwa kuwaletea maendeleo maishani mwao. Wasiuze vitu vya thamani kama shamba na kununua pikipiki.

Mdo 2:36-39.

241. LYIMBO LYA GUNNUMBILIJA MULUNGU

YUSTINA DEUS O JIKUNDI JA B’AKENGEJI B’A KAMATI YA NDOLELEJI ALIMBA LYIMBO LYA GUNUMBILIJA MULUNGU UYO AGAMPIJA PADRI DONALD SYBERTS NG’WANAHELENA OHO OLIOSADA.

KISWAHILI: WIMBO WA SHUKRANI KWA KWA MUNGU

YUSTINA DEUS WA KIKUNDI CHA KAMATI YA UTAFITI CHA NDOLELEJI AKIIMBA WIMBO WA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA PADRI DONALD NG’WANAHELENA ALIYEKUWA MGONJWA.

ENGLISH: A THANKSGIVING SONG TO GOD

YUSTINA DEUS OF NDOLELEJI RESEARCH COMMITEE GROUP, SINGING A THANKSGIVING SONGVIDEO TO GOD FOR HEALING FR. DONALD SYBERTZ WHO WAS SICK.

 

SAMIKE ADADULILE UGUHUMULA

B’ULUMBI

Samike olintongezi o mbina ya Bagalu, uyo olinduja noyi na okindaga b’ojinagu umuwikindi bhokwe na luganda lo mbina ya B’agika. Uluganda lo B’agika lugab’iza na wilu, na lugachola nzila ja gudula gunhabhula USamike. Aho magemero mingi gaduma, lushugu lumo umujilabhu ja walwa, abhanishi wakwe bhaganlabhula USamike ub’iza nsadu noyi. Unfumu okwe uomakanza genayo, adadulile ugunlagula. Huna uja kubhafumu bhangi nabho bhugaduma ugunlagula.

Nose aho wikala adalile kulikanza lya shugu itano, na giko uduma ugusiminza, USamike agabhuchiwa na bhahemba bhakwe mpaga gukaya ya nfumu ntale uyo agapijaga witanagwa, Luhumbika, huko agaja ugalagulilwa mpaga upila.

Aho opijiwa, USamike agapandika bhuyegi bhutale noyi mpaga utunda na lyimbo lya bhulumbi kuli Luhumbika. Agasiminza bhuli kwene alilyimba ilyimbo linili ilya bhukumilija na bhulumbi. USamike adadulile uguhumula, aliyo umuwikindi bho mbina agendelea ugubhawila abhanhu ginhu jitale ijo ULuhumbika ong’witila. Agimba:

Ugusada idigucha. Napandika hambohambo gete. Napijiwa. Bhana b’ane, yegagi kihamo nane. Luhumbika huyo unipija. Nalilomba wikale bhulunga kele! Uwei alinfumu ntale uyo agapijaga. Ubhugota bhokwe bhulibho nhana bhulina nguzu noyi ikibhugahangijaga abhanishi bhaduma ugunilabhula. Bhugota bhokwe bhuli na nguzu kukila abhanishi. Ulu nioliadiweyi ninacha. Ninadimhola mpaga lelo.

Yalinduhu inzila yingi ukuli nene. Oliadiho munhu ungi uyo ninansanga. Luhumbika aganifyadula guti umoagitilaga umeja omadafari ulualilubha b’ulolo b’upya b’o madafari, guti giki nafuma munda muli mayu one.” Uk. 95, mujitabho ja Jigano za Jiafrika, ku bhahubiri  na b’ang’walimu, jandikwa na Joseph G. Healey, MM. Jakengelwa na Bakengeji bhusuguma bha Bujora.

KISWAHILI: SAMIKE HAKUWEZA KUNYAMAZA

SHUKRANI

“Samike alikuwa ni kiongozi wa ngoma ya Bagalu aliyefanikiwa sana na ambaye alishinda kwa urahisi mashindano dhidi ya Kikundi cha Ngoma ya Bagika. Kikundi cha Bagika kikawa na wivu, na husuda na kutafuta njia ya kuweza kumdhuru Samike. Baada ya majaribio mengi kushindwa, siku moja katika klabu ya pombe, adui zake walimdhuru Samike na akawa mgonjwa sana. Mganga wake wa wakati ule hakuweza kumtibu. Ndipo akawaendea  baadhi ya waganga wengine ambao nao pia walishindwa.

Hatimaye, baada ya kushinda  bila kula kwa muda wa siku tano, na hivyo akashindwa kutembea, Samike alibebwa na wafuasi wake hadi nyumbani kwa mganga mkuu wa uponyaji, aitwaye Luhumbika, ambako ndiko alikotibiwa na kupona.

Baada ya kuponywa hivyo, Samike alijawa na furaha kubwa ilioje hata akatunga wimbo wa shukrani kwa Luhumbika. Alisafiri kila mahali huku akiuimba wimbo huo wa sifa na shukrani kwa Luhumbika. Samike hakuweza kunyamaza, lakini katika mashindano ya ngoma aliendelea kuwaambia watu juu ya mambo makuu ambayo Luhumbika alimtendea. Aliimba:

Kuugua siyo kufa. Nimepata nafuu kabisa. Nimeponywa. Watoto wangu, furahini pamoja nami. Luhumbika ndiye aliyeniponya. Naomba aishi milele! Yeye ni mpanga mkuu mponyaji. Dawa yake ya kweli ina nguvu sana kwani huwafanya maadui washindwe kunidhuru. Dawa yake ina nguvu zaidi kuliko ya maadui. Kama asingekuwa yeye ningekuwa nimekufa. Nisingekuwa hai bado.

Hapakuwepo na njia nyingive kwangu. Hakakuwepo na mtu mwingine ambaye ningemwendea. Luhumbika aliniinua kutoka kwenye kitanda. Aliniponyesha. Luhumbika alinifyatua kama afanyavyo mtengenezaji wa tofali anavyokanda udongo mpya wa matofali kana kwamba nilitoka tumboni mwa mama yangu.” Uk. 95, wa kitabu cha Hadhithi za Kiafrica, kwa Wahubiri na Walimu, cha Joseph G. Healey, MM. kilichotafitiwa na Kamati ya Utafiti ya Wasukuma, Bujora, Tanzania.

ENGLISH: SAMIKE COULDN’T KEEP SILINT

THANKSGIVING,

 Samike was a very successful dance leader of Bagalu group and would easily win the competitions against the Bagika Dance Group. The Bagika became very jealous, envious and looked for ways to harm Samike. After several unsuccessful attempts, one day at a local beer party, his enemies bewitched Samike and he became seriously ill. His regular diviner-healer could not cure him. Then he went to several other ordinary diviner-healers who also failed to cure him.

Finally, after going without food for five days and being unable to walk, Samike was carried by his disciples to the home of the great divine-healer, Luhumbika where he was eventually cured. After his recovery, Samike was overcome with joy and composed a song of thanksgiving to Luhumbika. He traveled everywhere singing this song of praise and thanksgiving. Samike could not keep silent, but at dance competitions he kept telling people the great things that Luhumbika had done for him. He sang:

To be sick is not to die. I am completely better. I am healed. My children, rejoice with me. Luhumbika is the one who healed me. May he live forever? He is a real divine-healer. His magical medicine is so powerful that it is impossible for the witches to harm me. His medicine is more powerful than the sorcerers. If it were not for him I would be dead. I would have no life in me.

There was no way out for me. I had no one else to turn to. I was in a hopeless situation. I was like one dead or lost. Luhumbika raised me up from my sick bed. He healed me. Luhumbika refashioned me like a brick maker makes a new mud brick as if I had just come from my mother’s womb.

African Stories For Preachers and Teachers (2005), p.95, compiled Joseph G. Healey, MM. It was researched by Bujora Committee Research Group.  It is also found in the www.afriprov.org.

240. MUGULYA MANUNHYIWA NEGELE

Imbuki ya kahayile kenako ilolile ilange lya namhala uyo alikomeleja b’ana b’akwe b’atumame milimo ya yabho na nguvu, kugiki bhadule gupandika jiliwa jingi, b’atizub’iza na gukob’eleja jiliwa ja gwisoleleja. Ijiliwa ijagwisoleleja jinijo jigalenganijiyagwa nijo jiganunhiyagwa na negele.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagafunyaga ilange lya wiza ukubhanhu bhabho. Ililange linilo ligenhaga ukubhanhu bhabho ikujo, bhukamu bho gutumama milimo, na nhungwa ya kudula gwikala na bhanhu chiza umuwikaji b’ob’o.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhalela abhanhu bhao chiza, kugiki bhadizupandika makoye gagugayiwa jiliwa aha kaya jabho. Akalele kenako kagub’inha matwajo mingi agagudula gub’eng’hela upandiki wingi umuwikaji b’ob’o. Kagub’ingija makoye gagwisoleleja jiliwa.

MTAKULA YANUSWAYO NUNDA

Chanzo cha msemo huo huangalia malezi ya mzee yule ahimizaye watoto wake kufanya kazi kwa nguzu, ili waweze kupata chakula kingi kiwezacho kuwaondolea mahangaiko ya kutafutiza chakula kwa kuokoteza. Hali hiyo ya kuhangaika kwa kuokoteza chakula, hufananishwa na chakula kinuswacho na nunda.

Msemo huo hulinganishwa kwa watu wale watoao malezi mema kwa watu wao. Malezi hayo huleta tabia njema ya kujitegemea, hekima, bidii ya kufanya kazi na ufahamu wa kuishi na watu vizuri, kwa watu wao. Malezi hayo huwaondolea watu wao mahangaiko ya njaa kwa sababu ya kukosa chakula.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwalea vyema watu wao ili waweze kujitegemea kwa kufanya kazi kwa bidii ya kutosha kuwapatia chakula na mahitaji yao yote yaliyoyalazima maishani mwao.

Malezi hayo yatawaletea watu wao maendeleo yakuweza kuziendesha vizuri familia zao maishani mwao. Watakuwa na bidii ya kufukuza njaa majumbani mwao kiasi cha kutosha kuepukana na vyakula vya kuokoteza huko na huko.

Mw 3: 17-19 Mw 2:15.

239. ULU NHIGAMANAGWA NINADIZILE

Imbuki ya kahaile kenako ilolile munhu uyo ajaga hanhu alinawisagiji bho gupandikika matwazo masoga. Aliyo lulu, ahooshika koyi ugapandika makoye badala ya mafumilo miza. Gashinaga lulu, akahayile kenako agayombaga munhu uyo oigaiyagwa iyo olikobhaga.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhadibhegelejaga chiza haho bhatali uguitumama imilimo yabho, guti gwita bhukengeji bho gudula gudebha chiza amafumilo ga milimo yabho yiniyo. Ugukija gwita b’ukengeji guti bhunubho haho bhatali uguitumama imilimo yabho, gugabhenghelejaga gugayigwa iyo bhaliicholaga, na guyomba giki, ‘ulu nhigamanagwa ninadizile.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwita bhukengeji bhutale bho milimo yabho, haho bhatali uguitumama imilimo yiniyo. Ubhukengeji bhunubho b’ugubhambilija uguimana na guitumama imilimo iyo idulile gubhenhela matwajo mingi umuwikaji b’ob’o.

Yohane 11:21.

NINGEJUA NISINGEKUJA

Chanzo cha msemo huo chaangalia mtu aliyeenda sehemu fulani akiwa na matumaini ya kupata maendeleo mazuri. Lakini basi, alipofika huko alipata matatizo badala ya mafanikio. Kumbe basi, msemo huo husemwa na mtu aliyekosa kile alichokuwa akikitafuta.

Msemo huo hulinganishwa kwa watu wasiojiandaa vizuri kabla ya kufanya kazi zao, kama vile, kufanya utafiti wa kutosha kuzifahamu kazi ziwezazo kuwaletea maendeleo maishani mwao. Kutokufanya utafiti kama huo, kabla ya kuzifanya kazi zao, hupelekea kwao kukosa kile walichokuwa wakikitafuta, na kusema, ‘ningejua nisingekuja.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kufanya utafiti wa kina kabla ya kuzifanya kazi zao. Utafiti huo utawawezesha watu hao kuzifahamu na kuzitekeleza vizuri kazi zile ziwezazo kuwaletea maendeleo maishani mwao.

Yohane 11:21.

236. MEJA O BHUGOTA ADILAMBAGA MAKONO

Imbuki ya kahayile kenako ilolile munhu uyo alib’ejaga b’ugota. Umunhu ng’winuyo agab’ub’ejaga ub’ugota bhenubho, ukunu alibhudimagula bho makono gakwe, kugiki b’ub’ele chiza.

Aliyo lulu, ub’ugota bhunub’o b’ugab’izaga b’ululu, kunguno yiniyo, adilamba amakono gakwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘meja o b’ugota adilambaga makono.’

 Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho b’agab’ejaga ginhu jab’o na witegeleja. Abhanhu bheneb’o bhadeb’ile igiki, ijo bhalijib’eja jidulile gwenha solobho ukubhanhu ulub’ujitumamila chiza, aliyo lulu, ulubhujitumamila shib’i, jidulile gwenha makoye ukubhanhu bhenabho.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja  bhutale ulu bhalib’eja ginhu josejose, kugiki iginhu jinijo, jidule gubhenhela solob’o umuwikaji b’ob’o.

1Petro 5:8.

KISWAHILI: MTENGENEZA DAWA HAJILAMBI MIKONO

Chanzo cha msemo huo huangalia mtu yule atengenezaye dawa. Mtu huyo hutengeneza dawa hiyo huku akiishika kwa mikono yake ili aweze kuhakikisha kwamba dawa hiyo inakuwa nzuri.

Lakini basi, dawa hiyo huwa chungu, kwa sababu hiyo, mtu huyo huhakikisha kwamba hajilambi mikono yake. Ndiyo maana watu husema, ‘mtengeneza dawa hajilambi mikolo.’

Msemo huo hulinganishwa kwa watu wale wafanyao kazi au watengenezao kitu fulani kwa umakini wa hali ya juu. Watu hao waelewa kwamba, kile watengenezacho huweza kuleka faida kwa watu kikitumiwa vizuri, lakini kikitumiwa vibaya, chaweza kuleta matatizo kwa watu hao.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na umakini mkubwa wakati watengenepo kitu chochote, ili kitu hicho kiweze kuleta faida katika maisha yao na wenzao.

1Petro 5:8.

234. NTUMAMILA JAKWE ADILAMBAGA MAKONO

Imbuki ya kahayile kenako ilolile munhu uyo alitumamila sabho jakwe. Umunhu ng’wunuyo agajitumamilaga na wisandazu bhutale isabho jinijo, kunguno adebhile umo ojikoyakeyelaga ugujipandika.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagaitumamaga imilimo bhobhukamu mpaka bhajipandika isabho. Abhanhu bhenabho bhagajitumamigala isabho jinijo bho wisandazu bhutale, kunguno jilisabho jabho.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhukamu bho gutumama milimo kugiki bhadule gupandika sabho jabho. Isabho jinijo hijo bhagujitumamila na wisandazu, kunguno untumamila jakwe adilambaga makono.

Mathayo 20:1-16.

Walawi 19:13.

Kumbukumbu 24:15.

KISWAHILI: MTUMIA ZA KWAKE HAJILAMBI MIKONO

Chanzo cha msemo huo huangalia mtu atumiaye mali zake. Mtu huyo huzitumia mali hizo kwa uhuru mkubwa, kwa sababu afahamu jimsi alivyozihangaikia katika kuzipata.

Msemo huo hulinganishwa kwa watu wale wafanyao kazi kwa bidii sana mpaka kufikia hatua ya kupata mali. Watu hao huzitumia mali hizo kwa uhuru mkubwa kwa sababu ni zao wenyewe.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kutosha kufanya kazi ziwezao kuwapatia mali na mafanikio makubwa maishani mwao. Mali hizo huwapa nafasi ya kuzitumia kwa furaha, kwa sababu atumiaye mali zake hajilambi mikono.

Mathayo 20:1-16.

Walawi 19:13.

Kumbukumbu 24:15.