758. KUB´ISA SHILI UGUFUMBULWA MAKOLE.

Imbuki ya lusumo lunulo, ingilile ha bhalandi bha shili. Bhalihoyi bhanhu abho bhagaja gujulanda shili habhuzenganwa bhaliyomba, “lulilanda shili ahakaya yiniyi.” Unzenganwa obho ng’wunuyo agashosha, “unene nadinajo ishili.”

Aliyo gashinaga, lushigu lumo aho ojitula ishili jinijo ahagandya gujihehela hanze iki jidahehelagwa mukaya. Huna bhumhona abhanhu abho oloo bhima. Haho agamanyikila igiki gashinaga aling’wiming’holo. Hunagwene bhagang’wila giki, “kub’isa shili ugufumlulwa makole.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo aling’wiming’holo umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhimaga abhiye ijikolo jakwe ulubhanhomba bho gubhawila giki adinajo, aliyo gashinaga jilihoyi umukaya yakwe. Uweyi agamanyikaga ukubhanhu abho oliobhima ulu lyashiga ilikanza lya gujitumamila ijikolo jinijo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agabhabhima shili abho bhanhandaga wiza ufumbulwa makole, aho lyashiga ilikanza lya gujiheha, kunguno nu weyi agabhimaga abhiye wiza omanyika ulu lyashiga ilikanza lya gujitumamila ijikolo jakwe jinijo. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagang’wilaga giki, “kub’isa shili ugufumlulwa makole.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja wiming’holo umukilalile kabho, kugiki bhadule gwiyambilija chiza ugujibheja ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 10:26-27.

Luka 12:2-3.

KISWAHILI: KUFICHA KUNDE UTAFICHULIWA MAGANDA.

Chanzo cha methali hiyo, kilitokea kwenye uazimaji wa kunde. Walikuwepo watu walioenda kuazima kunde kwa jirani yao wakisema, ‘tunaazima kunde kwenye familia hii.’ Jirani yao huyo aliwajibu, ‘mimi sina kunde.’

Lakini kumbe, siku moja alipozipiga kunde hizo akaanza kuzipepetea nje kwa vile hazipepetewi ndani ya nyumba. Ndipo watu wale aliowanyima kunde hizo wakagundua kuwa mtu huyo ni mchoyo. Ndiyo maana wakamwambia kwamba, “kuficha kunde utafichuliwa maganda.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mchoyo katika maisha yake. Mtu huyo, huwanyima wenzake wanaomuomba vitu vyake kwa kuwaambia kwamba, hana, kumbe anavyo vitu hivyo ndani ya nyumba yake. Yeye hujulikana kwa watu hao kuwa aliwanyima unapofika wakati wa kuvitumia vitu hivyo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyewanyima kunde majirani zake walimuomba, akafichuliwa maganda, kwa sababu naye huwanyima wenzake vitu vyake wanamuomba, ambavyo huonekana unapofika wakati wa kuvitumia. Ndiyo maana watu hao humwambia kwamba, “kuficha kunde utafichuliwa maganda.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuachana na tabia za uchoyo katika maisha yao, ili waweze kusaidiana vizuri katika kuziletea maendeleo familia zao, maishani mwao.

Mathayo 10:26-27. ““Kwa hiyo msiwaogope hao, kwa maana hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna siri ambayo haitajulikana. Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe na lile mnalosikia likinong’onwa, masikioni mwenu, lihubirini kwenye paa la nyumba.”

Luka 12:2-3. ‘‘Hakuna jambo lo lote lililositirika ambalo halitafunuliwa au lililofichwa ambalo halitajulikana. Kwa hiyo, lo lote mlilosema gizani litasikiwa nuruni na kile mlichonong’ona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa.”

kunde beans

kunde beans-

kunde string-beans

ENGLISH: HE, WHO HIDES COWPEAS, WILL BE BETRAYED BY THEIR CHAFFS.

The basis of this proverb came from asking for cowpeas .There were people who went to ask for cowpeas from their neighbour saying, ‘we are asking for cowpeas from this family.’ The neighbour replied, ‘I don’t have any cowpeas.’

However, one day when he had thrashed the cowpeas he began to sift them out as they could not be sifted inside the house. Then the people who had asked for those cowpeas and were denied by him realized that the man was greedy. That is why they told him that, “he, who hides cowpeas, will be betrayed by their chaffs.”

This proverb is compared with a person who is greedy. Such man deprives his colleagues of his possessions by telling them that he does not have them, but he has them in his house. He is known to those people that he denied them when it came time to use those things.

He is like the one who refused his neighbours of the cowpeas they had asked for, but who was betrayed by their chaffs .This is because he also denies his fellows of the things they ask for him of which he says he does not have but which appear when the time for using them comes. That is why these people tell him that, “he, who hides cowpeas, will be betrayed by their chaffs.”

This proverb teaches people about not being greedy so that they can help each other better in bringing development to their families.

Matthew 10: 26-27 Luke 12: 2-3.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.