Imbuki ya lusumo lunulo, ilolile bhutumami bho liso. Iliso linilo, ligabhonaga ginhu jose jose, jibhize jisoga, nulu jib’i. Ulu lyubhona mihayo misoga, lyuguyeja noyi kunguno imihayo yiniyo yigagulungujaga umoyo.
Aliyo lulu, iliso linilo ulu lyubhona mihayo mib´i, lyugusunduhaja kunguno imihayo yiniyo yigawinjaga ubhuyegi ubho bhulihoyi umu moyo goko. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “liso lidab’isaga mihayo.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agagatumililaga chiza amiso gakwe bho gubhona mihayo misoga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agayegaga ulu oyibhona imihayo iyo ili miza, kunguno igang’wenhelala matwajo gagujibheja chiza ikaya ja bhanhu. Uweyi agagalemejaga amiso gakwe ugubhona imihayo imib’i, kunguno igenhaga makoye umukikalile ka bhanhu.
Umunhu ng’wunuyo, agabhalangaga abhiye inzila ja gugatumila chiza amiso gabho bho gubhona mihayo miza iyo igenhaga matwajo miza, umukikalile kabho. Hunagwene uweyi agabhabhilaga abhanhu giki, “liso lidab’isaga mihayo.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gugatumamila chiza amiso gabho bho gubhona mihayo miza na guyileka imib’i, umukikalile kabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Mathayo 20:15.
Luka 2:30.
Luka 11:34.
2 Wakorintho 3:7.
KISWAHILI: JICHO HALIFICHI MANENO.
Chanzo cha methali hiyo, chaangalia utendaji kazi wa jicho. Jicho hilo, huona kitu chochote kiwe kizuri au kibaya. Likiona kitu kizuri litakufurahisha sana kwa sababu kitu hicho hufariji moyo.
Lakini jicho hilo, likiona kitu kibaya, hukuhudhunisha kwa sababu kitu hicho, huyiondoa furaha iliyomo moyoni mwako. Ndiyo maana watu husema kwamba, “jicho halifichi maneno.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatumia macho yake kwa kuona vitu vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, hufurahi akiona kitu kizuri kwa sababu kitu hicho huleta maendeleo kwenye familia za watu. Yeye huyazuia macho yake kuona vitu vibaya kwa sababu vinaleta matatizo kwenye maisha ya watu.
Mtu huyo, huwafundisha wenzake namna ya kuyatumia vizuri macho yao kwa kuona vitu vinavyowaletea maendeleo katika maisha yao. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “jicho halifichi maneno.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyatumia vizuri macho yao kwa kuangalia vitu vizuri na kuyazuia kuangalia vitu vibaya, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.
Mathayo 20:15. “Je, sina haki yangu kufanya kile nitakacho na mali yangu mwenyewe? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’”
Luka 2:30. “Kwa maana macho yangu yameuona wokovu Wako,…”
Luka 11:34. “Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote umejaa giza.”
2 Wakorintho 3:7. “Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, ile iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata ikawa Waisraeli hawawezi kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule utukufu wake, ingawa ulikuwa ni wa kufifia,…”
ENGLISH: AN EYE DOES NOT HIDE WORDS.
The foundation of the above saying looks at the functions of an eye. The eye sees anything whether it is good or bad. Seeing something good will make you happy because it makes you feel good.
However, when the same eye sees something wrong, it bothers you because that thing, takes away the joy that is in your heart. That is why people say, “An eye does not hide words.”
The saying is likened with a man who uses his eyes to see good things in his life. He is happy to see something good because that thing brings development to people’s families. He keeps his eyes away from looking at things that are bad because they bring trouble on his people’s lives.
This person teaches his colleagues on how to make good use of their eyes by seeing the things that improve their lives. That is why he tells people that, “an eye does not hide words.”
This proverb teaches people how to use well their eyes by looking at good things and preventing them from looking at the evil ones.
Matthew 20:15.
Luke 2:30.
Luke 11:34.
2 Corinthians 3: 7.