760. LISO TALA YA MILI.

Imbuki ya lusumo lunulo, ilolile nimo go liso ugo gugutimila imili. Iliso linilo, ligagutimilaga umili bhogubhona ginhu jose jose ijo jilihabhutongi bholyo. Ulu munhu ulitumila chiza iliso lwakwe umili gokwe gugwikala mhola.

Aliyo lulu, umunhu uyo ulitumila bho gubhola mihayo mib’i, umili gokwe gugupandika makoye kunguno imihayo yiniyo yigagutulaga mugiti umili. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “liso tala ya mili.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agagatumililaga chiza amiso gakwe bho gubhona mihayo misoga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agayegaga ulu oyibhona imihayo iyo ili miza, kunguno igang’wenhelala matwajo gagujibheja chiza ikaya ja bhanhu bhakwe. Uweyi agagalemejaga amiso gakwe ugubhona imihayo imib’i, kunguno igenhaga makoye umukikalile ka bhanhu.

Umunhu ng’wunuyo, agabhalangaga abhiye inzila ja gugatumila chiza amiso gabho bho gubhona mihayo miza iyo igenhaga matwajo miza, umukikalile kabho kugiki nabho bhikali mulisana. Hunagwene uweyi agabhabhilaga abhanhu giki, “liso tala ya mili.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gugatumamila chiza amiso gabho bho gubhona mihayo miza na guyileka imib’i, umukikalile kabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 20:15.

Luka 2:30.

Luka 11:34.

2 Wakorintho 3:7.

KISWAHILI: JICHO NI TAA YA MWILI.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia kazi ya jicho katika kuumulikia mwili. Jicho hilo, huumulikia mwili kwa kuangalia kitu chochote ambacho kiko mbele yake. Mtu atayelitumia jicho lake vizuri mwili wake utakuwa salama.

Lakini basi, mtu huyo akilitumia vibaya jicho lake kwa kuona vitu vibaya, mwili wake utapata matatizo, kwa sababu vitu hivyo huuweka mwili gizani. Ndiyo maana watu husema kwamba, “jicho ni taa ya mwili.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatumia vizuri macho yake kwa kuona vitu vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, hufurahi akiona kitu kizuri kwa sababu kitu hicho huleta maendeleo kwenye familia za watu wake. Yeye huyazuia macho yake kuona vitu vibaya kwa sababu vinaleta matatizo kwenye maisha ya watu kwa kuiweka miili yao gizani.

Mtu huyo, huwafundisha wenzake namna ya kuyatumia vizuri macho yao kwa kuona vitu vinavyowaletea maendeleo katika maisha yao, ili miili yao isiishi gizani. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “jicho ni taa ya mwili.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyatumia vizuri macho yao kwa kuangalia vitu vizuri na kuyazuia kuangalia vitu vibaya, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao kwa kuishi katika mwanga, maishani mwao.

Mathayo 20:15. “Je, sina haki yangu kufanya kile nitakacho na mali yangu mwenyewe? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’”

Luka 2:30. “Kwa maana macho yangu yameuona wokovu Wako,…”

Luka 11:34. “Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote umejaa giza.”

2 Wakorintho 3:7. “Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, ile iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata ikawa Waisraeli hawawezi kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule utukufu wake, ingawa ulikuwa ni wa kufifia,…”

eyes girl

Eyes child-

eyes african-child

ENGLISH: THE EYE IS THE LIGHT OF THE BODY.

The essence of the above proverb looks at the function of the eye which is to illuminate the body. The eye illuminates the body by looking at anything that is in front of it. A person who uses his eye well, his body will be safe.

But if a person misuses his eye by looking at evil things, his body will suffer, because those things keep the body in the darkness. That is why people say that, “the eye is the light of the body.”

Such proverb is likened with a person who makes good use of his or her eyes to make them see good things in his life. Such person is happy to see something good because it brings development to the families of his people. He keeps his eyes away from seeing evils because they bring trouble to people’s lives as they keep their bodies in darkness.

This person teaches his colleagues on how to make good use of their eyes by seeing the things that can bring them progress in their lives, so that their bodies do not live in darkness. That is why he tells people that, “the eye is the lamp of the body.”

This proverb teaches people on how to use their eyes properly by looking at good things and preventing them from watching evil things.

Matthew 20:15.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.