sayings

405. ULAFULWA LYA NG’WIPOLU NA MAPEMBE GALYO.

Imbuki ya kahayile  kenako yingilile kubhubolwa bho jisumva na lilimu lya ng’wipolu na mapembe galyo. Ijisumva jinijo jigalyaga noyi ijiliwa. Aliyo lulu jidigutaga wangu.

Ijoyi jigikikumbagwa nulu gulilya lilimu igima kihamo na mapembe galyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki ,’ulafulwa lya ng’wipolu na mapembe galyo.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinlaku o gulya jiliwa. Umunhu ng’wunuyo adigutaga ulu bhang’winha ijiliwa, mumo alile. Hamo ulu utengelwa ilimu lya ng’wipolu lizugile na mapembe galyo ulya, adulile gwiguta. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘’ulafulwa lya ng’wipolu na mapembe galyo.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka bhulaku bho gulya jiliwa, umuwikaji bhobho, kugiki bhadizub’ahaga abhichabho, ulub’alilya ijiliwa jinijo.

marko 8: 36-37.

Wagalatia 5:19-21.

KISWAHILI: UTAGONGWA LA POLINI NA PEMBE ZAKE.

Chanzo cha msemo huo chaangalia kugongwa kwa kiumbe na mnyama poli mwenye pembe zake. Kiumbe hicho hula sana chakula. Lakini basi, huwa hakishibi. Chenyewe hutamani hata kula mnyama poli pamoja na pembe zake, ambaye ni mkubwa sana. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘utagongwa la polini na pembe zake.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mlafi wa kula chakula. Mtu huyo huwa hashibi wanapompatia chakula. Labda wakimtengea mnyama poli na pembe zake, aliyepikwa na kumla pengine atashiba. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘utagongwa la polini na pembe zake.’

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha ulafi wa kula chakula, ili wasiwapunje wenzao walapo chakula hicho.

Marko 8: 36-37.

Wagalatia 5:19-21.

bufalo

 

ENGLISH: YOU WILL BE KNOCKED BY A HORNED-WILD ANIMAL.

The origin of the above saying is a knock between a certain creature and a horned-wild animal. The creature eats a lot of food with no satisfaction. It even desires to eat big horned-animals for satisfaction. Such a creature is being warned by the proverb that ‘you will be knocked by a horned-wild animal.’

The saying can be compared to a greedy person who doesn’t get satisfaction in his/her eating.

The saying teaches people to stop being greed. They need to be considerate when eating by thinking about others that they also need to eat.

Mark 8: 36-37.

Galatians 5: 19-21.

392. GULYA NYAGOKO.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kukalille ka jiliwa, ka ngoko. Ingoko yiniyo, igalyaga ijiliwa bho gujisesagula na gujisalambanya, ijiliwa jinijo.

Igajibalasanyaga jab’iza guti jashilaga nulu jilijingi. Hunagwene abhanhu ulu bhumhona unii ojiliwa uyo alilya chiniko, bhagang’wilaga giki atogilwe ‘gulya nyagoko.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalyaga ijiliwa ukunhu ujisondola, kugiki achagule ijiliwa ijisoga. Umunhu ng’wunuyo agajidimagulaga ijiliwa jinijo guti ujidosaga ijingi. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, uweyi atogilwe ‘gulya nyagoko.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka gujidimagula sagala ijiliwa ulu bhalilya, kugiki bhadule gujilya ijiliwa jinijo, ni nikujo ukubhichabho.

1 Wakorintho 11:27 – 30.

Tito 1:12.

KISWAHILI: KULA KIMTINDO WA KUKU.

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye mtindo autumiao kuku alapo chakula. Kuku huyo, hula chakula kwa kukisambaza akitumia miguu yake.

Hukisanmbaza chakula hicho, mpaka kinaonekana kama kimeisha hata kama kilikuwa kingi zaidi. Ndiyo maana watu wakimuona mlaji wa chakula ambaye hula kwa mtindo huo, humwambia kwamba yeye apenda ‘kula kimtindo wa kuku.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu ambaye hula chakula kwa kukichambua kwa lengo la kutafuta kile kilicho kizuri zaidi. Mtu huyo hukishikashika chakula hicho kama amekidharau kile kingine. Ndiyo maana watu humwambia mtu huyo kwamba, yeye apenda ‘kula kimtindo wa kuku.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kukishishika chakula wanapokula, ili waweze kukila kwa heshima, na kuwaheshimu pia wenzao.

1 Wakorintho 11:27 – 30.

Tito 1:12.

chickens

 

eat-chips

ENGLISH: TO EAT LIKE CHICKEN.

The source of the above saying comes from chicken eating style. The chicken will eat the food by spreading it on its feet. It spreads the food to the extent of making it appear as if it is finished, but in actual fact, they eat by sorting out some of the unwanted things. In describing people with this kind of behaviour, people can use this saying that ‘to eat like chicken.’

The saying can be compared to a person who eats food by sorting out some of the unwanted things thus looking for the best incredients of food. Such people are always looked at as someone who dislikes food and thus described by the saying that ‘to eat like chicken.’

The saying teaches people to stop bad eating habits when they eat. They need to respect the food they eat and the people who prepared it.

1 Corinthians 11:27 – 30.

Titus 1:12.

391. GULYA GWA NKANI LELO.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kukalile ka jiliwa ka jisunva ijo jigajibhonaga ijiliwa jinijo, jinonu gulebha ijo jab’ita. Ijisunnva jinijo jigalyaga bhuli lushigu, na jihayile gujimala bhuli jiliwa ijo jilinhiwa, kunguno jigajibhonagaga jinonu kuleb’a ijaigolo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘gulya gwa nkani lelo.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalyaga jiliwa jinonu bho nduhu ugub’izuka abhiye. Umunhu ng’wunuyo agiizukaga weyi duhu. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘gulya gwa nkani lelo.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gub’adilila na bhichab’o ulu bhalilya ijiliwa jabho, kugiki bhadule gwiguta pye  abhose.

Mathayo 6:8-11.

 1 Wafalme 17: 8-16.

KISWAHILI: KULA KILA SIKU HASA LEO.

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye ulaji wa chakula wa kiumbe ambacho hukiona chakula hicho kuwa kitamu kipita kile cha siku iliyo pita.

Kiumbe hicho, hula chakula kila siku, na hutaka kukimaliza kila chakula kipewacho, kwa sababu ya kukiona chakula hicho, kuwa kitamu kupita kile cha jana. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kula kila siku hasa leo.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu ambaye hula chakula kitamu bila kuwakumbuka wenzake. Mtu huyo hujikumbuka yeye mwenyewe tu. Ndiyo maana watu humwambia mtu huyo kwamba, ‘kula kila siku hasa leo.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwajali wenzao wakati wanapokula chakula chao, ili waweze kushiba wote.

Mathayo 6:8-11.

 1Wafalme 17: 8-16.

EATING

vintage3

 

ENGLISH: EATING MORE THAN PREVIOUS DAYS.

The source of the above saying comes from food intake of an organism that considers the food to be sweeter than the previous day. Such a creature that is used to eat everyday will want to finish every food given because it will find the food always sweeter than the one given other times. The eating habit of such a creature can be described by the saying that ‘eating more than previous days.’

The saying can be compared to someone who eats sweet food without considering his/her colleagues. That person only remembers himself/herself. The behaviour of such people can be described by this saying that ‘eating more than previous days.’

The proverb teaches people to care for others when they eat their food. This wil help them to have a good relationship built on care and love.

Matthew 6: 8-11.

1Kings 17: 8-16.

390. GULYA JILYANI.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhuli bho jiliwa ubho bhuli bho kihamo. Ulu bhanhu bhali na kajile kawikole, bhagatogagwa gwikala halumo, na gulya jiliwa jabho halumo, kugiki bhikale bhaguhoyaga kumakanza malihu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘gulya jilyani.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhazenganwa abho b’itogilwe. Abhanhu bhenabho bhagalyaga jililwa jabho halumo, kunguno ya witogwi bhobho b’unub’o.

 Abhoyi bhagiyambilijaga nu gutumama imilimo yabho halumo. Bhadeb’ile ugubhalanga nab’ichab’o, ahigulya ya gulya na gutumama halumo, umuwikaji bhobho. Hunagwene bhagab’awilaga abhanhu bhikomeje ‘gulya jilyani.’

Akahayike kenako kalanga bhanhu higulya ya gub’iza na witogwi na bhazenganwa bhab’o, kugiki bhadule gutumama milimo yabho halumo, na ‘gulya jilyani.’

Marko 4:8.

 Mathayo 4:32.

 Kutoka 12:4.

KISWAHILI: KULA UJIRANI.

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye ulaji wa chakula ambao ni wa pamoja. Watu wakiwa na maisha yanayofanana, hupenda kuishi wakiwa pamoja, na kula chakula chao kwa pamoja, ili wakae wakiongea kwa muda mrefu. Ndiyo maana watu hao husema kwamba, ‘kula ujirani.’

Msemo huo hulinganishwa kwa majirani wanaopendana. Watu hao hula chakula chao kwa pamoja kwa sababu ya upendo walio nao kati yao.

Wao husaidiana hata kufanya kazi zao kwa pamoja. Wanafahamu namna ya kuwafundisha pia wenzao jinsi ya kula na kufanya kazi zao hizo kwa pamoja. Ndiyo maana watu hao huwahimiza wenzao kwa kusema ‘kula ujirani.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na upendo kwa majirani zao, ili waweze kufanya kazi zao kwa pamoja, na ‘kula ujirani.’

Marko 4:8.

Mathayo 4:32.

 Kutoka 12:4.

eat

ENGLISH: TO EAT IN THE NEIGHBORHOOD.

The source of the above saying comes from communal food eating style. People with similar life standards can tend to live together; eat their meal together and therefore, they are able to have long conversations about their society. Such a strong bond among people in the nearbourhood is described by the saying that ‘to eat in the nearbourhood.’

The saying can be compared to nearbours who love one another. These people eat their meals together. They also help each other to do their jobs together and they know how to teach their fellows how to eat and do their jobs together. This is why people are encouraged to maintain togetherness by using this saying that ‘to eat in the nearbourhood.’

The saying teaches people about loving their neighbours so that they can work together and love each other.

Mark 4: 8.

Matthew 4:32.

 Exodus 12: 4.

389. JISINZA JILYA B’IYE.

Imbuki ya kahayile kenako yilolile jisinza na bhuli bhojo. Ijisinza jinijo, jilinhu jidamu ijo jidulile gub’alya ab’ichajo, alijoyi jusaga mumo jilili. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘jisinza jilya b’iye.’

Akahayile kenako kagalenganijniyagwa kuli munhu uyo atogilwe gulya jiliwa ja b’iye, alijakwe alemile uguliwa na b’iye b’enabho.

Umunhu ng’wunuyo adatogilwe ugub’akalib’usha abhiye ahakaya yakwe, kunguno ya gogoha gumajiwa ijiliwa jakwe. Abhanhu abho bajideb’ile inhungwa jakwe jinijo bhagang’wilaga giki, ‘jisinza jilya b’iye.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka wiming’holo, kugiki bhadule ugub’itila abhichab’o iyo bhatogilwe ugutilwa abhoyi, umuwikaji b’ob’o.

Luka 11:46.

Daniel 2:40.

Mathayo 5:27-32.

Yoshua Bin Sira 9:19.

KISWAHILI: CHUMA HULA WENZAKE.

Chanzo cha msemo huo chaangalia chuma na ulaji wake. Chuma hicho ni kitu kilicho kigumu ambacho kinauwezo wa kula wenzake, chenyewe kikabaki kama kilivyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘chuma hula wenzake.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu ambaye hupenda kula kwa wenzake, lakini kwake hataki wenzake hao wale kwake. Mtu huyo hapendi kuwakaribisha wenzake kula chakula chake nyumbani kwake, kwa sababu ya kuogopa kukimaliza chakula chake hicho. Watu wale ambao wanaifahamu tabia yake hiyo, humwambia kwamba, ‘chuma hula wenzake.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha uchoyo maishani mwao, ili waweze kuwatendea wenzao yale ambayo wao wenyewe, hupenda kutendewa na wao.

Luka 11:46.

Daniel 2:40.

Mathayo 5:27-32.

Yoshua Bin Sira 9:19.

saw

tools-

 

ENGLISH: IRON EATS ITS FELLOWS.

The origin of the above saying is how metals survive by feeding on fellow metals. There are some metals that are hard enough and they are capable of feeding on other metals. In describing such metals people can say ‘iron eats its fellows.’

The saying can be compared to a person who likes eating food from others but doesn’t entertain others to eat his/her food. Such a person is likely to deny others from visiting his/her home for fear of eating his/her food. People of this behaviour are being warned by telling them that ‘Iron eats its fellows.’

The saying teaches people to stop being selfish in their lives rather they need to treat others in a way that they would themselves want to be treated.

Luke 11:46.

Daniel 2:40.

Matthew 5: 27-32.

Joshua Bin Sira 9:19.