stories

556. NANCHIMA UNG’WANA MHELA ILINDA.

Imbuki ya kahayile kenako ilolile bhuching’wa bho ng’wana o mhela iyo ilinda. Ubhuching’wa bhunubho bhuli bho guchima jisumva jibhili, kunguno uyo alinda, ibhize mhela nulu munhu, agabhizaga alina ng’wiye umugati yakwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘nanchima ung’wana mhela ilinda’.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinsabhi o jikolo ja mbika ningi aha ng’wakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga na sabho ningi ijo agajitumilaga nulu agalabhuka munhu ahakaya yakwe gumpija. Uweyi agajigufunyaga duhu, kunguno ojipandika ijikolo ijo jili jingi noyi umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agiikolaga nu munhu uyo  alinda, nulu ndimu iyo ilinda, kunguno n’uweyi alina sabho ijo agajitumilaga nulu kunchala ng’wiye uyo ominyikaga kusibhitali. Hunagwene abhanhu bhagayombaa giki, ‘nanchima ung’wana mhela ilinda.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu kubhiza na wisagizu bho gupandika jikolo bhuli ng’wene ijo alijichola umubhutumami bho milimo yakwe, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho umukikalile kabho.

(Mathayo 7:7-8; Luka 11:9-10; Luka 11:13).

KISWAHILI: NIMEMCHOMA MWANA KIFARU ANA HIMILA.

Chanzo cha msemo huu chaangalia kuchomwa kwa  kifaru ambaye ana mimba. Kuchomwa huko kwa kifaru mwenye himila ni hali ya kuumizwa kwa viumbe wawili, kwa sababu mwenye himila, awe mwanadamu au mnyama, ana mtoto ndani ya tumbo lake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘nimemchoma mwana kifaru ana himila.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni tajiri mwenye mali nyingi nyumbani kwake. Mtu huyo huzitumia mali zake hizo katika kutatua matatizo mbalimbali katika familia yake. Wingi wa mali hizo huweza kumsaidia hata mtu akiumia nyumbani kwake; huchukua mali hizo na kumuwahisha kwenye matibabu hospitalini. Mtu huyo hufanana na yule kiumbe mwenye himila aliyeumia, kwa sababu naye anazo mali ambazo huonekana anapozitumia wakati wa kutatua tatizo fulani katika familia yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘nimemchoma mwana kifaru ana himila.’

Msemo huu hufundisha watu kuwa na matumaini ya kupata mafanikio makubwa kila mmoja wao anayejibidisha kutafuta katika utekelezaji wa makukumu yake, ili aweze kuishi kwa amani na wenzake maishani.

(Mathayo 7:7-8; Luka 11:9-10; Luka 11:13).

nsabhi masai

mhela

ENGLISH: I HAVE STABED A BABY IN A PREGNANT RHINO.

The origin of this saying is stabbing of a baby in a pregnant creature. This is a traumatic experience for two beings, because a pregnant being, whether human or animal, has a baby inside her womb. That is why people say, ‘I have stabbed a baby in a pregnant rhino.’

The saying is used comparatively to refer to a rich person with many possessions in his home. The person uses his/her wealth to solve various problems in his/her family. The wealth can even help a person when he or she is injured to get treated in a hospital. This person is like a pregnant creature, because his/her wealth is useful in solving problems in his/her family. That is why people say, ‘I have stabbed a baby in a pregnant rhino.’

The saying teaches people to hope for the greatest success as long as they execute their responsibilities as they should, so that they can live in peace with their peers.

(Matthew 7: 7-8; Luke 11: 9-10).

555. UYO AGAFUGAGA MABHELE NGOKO JIDINAHILA ADALALAGA.

Imbuki ya lusumo lunulo yingilile kubhufugi bho mabhele. Amabhele  genayo, gagafugagwa nulu gagasegesagwa mpaga gapya chiza. Aliyo lulu, ulu galisegeswa chiniko gagamalaga likanza lilihu gagufugagwa, nulu gagusegesagwa huna gapya. Ulu gupya gagisungulaga amaguta gabhiza galihigulya amabhele gasaga hasi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘uyo agufugaga mabhele ngoko jidinahila adalalaga.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo olagana, uyo atogilwe gwigusha n’ung’wiye uyo bhitolile nawe bhujiku pe. Umunhu ng’wunuyo agadumamaga ugutumama imilimo yakwe ulu wela ubhujiku, kunguno ya gwikala na tulo ningi iyo adaimalile ibhujiku. Uweyi agikolaga n’unsegesi o mabhele uyo adalalaga kunguno ya gugwandya unimo guniyo ngoko jidinahila, kulwakubhiza n’uweyi igigushashaga n’uyo bhitolile nawe bhujiku pe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga agutindilaga ilimi, kunguno adalalile ibhujiku. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘uyo agufugaga mabhele ngoko jidinahila adalalaga.’

Ulusumo lunuyo lolanga bhanhu gubhiza n’ikanza lya gwibhegeleja uigutumama imilimo yabho iyo igabhapandikalaga jililwa, kugiki bhadule gwinja makoye ga nzala aha kaya jabho.

(Marko 13:36-37).

KISWAHILI: ACHEKECHAYE MAZIWA KABLA YA JOGOO KUWIKA HUWA HALALI.

Chanzo cha methali hii chatokea kwenye uchekechaji wa maziwa. Maziwa huchekechwa kwa muda mrefu sana ndipo yaive. Kuiva kwake ni kufikia hatua ya kujitenga mafuta kuwa juu ya maziwa. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘achekechaye maziwa kabla ya jogoo kuwika huwa halali.’

Methali hii hulinganishwa kwa mwana ndoa ambaye hucheza na mwenzi wake usiku kucha. Mtu huyo hushindwa kufanya kazi kesho yake, kwa sababu ya kuwa na usingizi mwingi ambao hakuumaliza vizuri usiku uliopita. Yeye hufanana na yule anayechekecha maziwa kabla ya jogoo kuwika maana hufanya kazi hiyo usiku kucha bila kulala, kwa sababu naye hucheza na mwenzake wa ndoa usiku kucha, hali ambayo hunfanya aonekane mchovu wakati wa mchana. Mtu huyo hushinda kutwa nzima akisinzia kwa sababu ya kutolala vizuri usiku uliopita. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘achekechaye maziwa kabla ya jogoo kuwika huwa halali.’

Methali hii hufundisha watu kutenga muda wa maandalizi yatakayowawezesha kuyatekeleza vizuri majukumu yao yanayowawezesha kupata chakula, ili waweze kupata mafanikio mengi katika kuzijenga vizuri familia zao. Muda wa maandalizi hayo utawawezesha kuondoa tatizo la njaa kwenye familia zao.

(Marko 13:36-37).

nhungulume2

african-couple

 

ENGLISH: HE WHO SHAKES MILK BEFORE COCKCROW NEVER SLEEPS.

The origin of this proverb is the act of shaking curdled milk to separate it from fat. This is done for a relatively very long time until the fat comes on top of the milk. That is why people say, ‘He who shakes milk before cockcrow never sleeps.’

The proverb is used comparatively to warn a married person who plays with his/her spouse all night long to desist from that behavior, because that person would always be unable to work the next day due to lots of sleep from the previous night. That person is like the one who shakes milk before cockcrow who does that all night without sleeping as he/she, too, plays with his/her spouse all night, which makes him/ look tired in during daytime. That person succumbs to sleeping all day because of not sleeping well the night before. That is why people tell him/her, ‘He who shakes milk before cockcrow never sleeps.’

The proverb teaches people to set aside time to prepare for their activities that bring food on the table, so that they can be more successful in building better families. Preparations will allow them to eliminate the problem of hunger in their families.

(Mark 13: 36-37).

554. ABHABHILI BHALI BHABHILI.

Imbuki ya kahayile kenako yilolile bhanhu abho bhali bhabhili umubhutumami bhobho. Abhanhu bhanebho bhagadulaga gugumala nimo uyo guli ntale bho gutumila likanza liguhi, kunguno ya wilunguja bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘abhabhili bhali bhabhili.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhali na wiyambilija bhutale umubhutumami bho milimo yabho. Abhanhu bhenabho bhagilungujaga ijinaguitumama imilimo yabho bho wanguwangu na chiza, mpaga bhadula guimala bho likanza liguhi noyi, kunguno ya wilunguja bhobho bhunubho.

Uwilunguja bhobho bhunubho, bhugabhinhaga nguzu bhuli ng’wene ija gwigulyambija gutumama milimo, kunguno ya wilunguja bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagayomgaga giki, ‘abhabhili bhali bhabhili.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu gubhiza kihamo ijinagwiyambilija uguyitumama imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi ayo gadulile gujibheja chiza ikaya jabho.

KISWAHILI: WAWILI NI WAWILI.

Chanzo cha msemo huu chaangalia watu ambao ni wawili katika utekelezaji wa majukumu yao. Watu hao huweza kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi na kuimaliza, kwa sababu ya umoja wao huo wa kusaidiana vizuri. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘wawili ni wawili.’

Msemo huou hulinganishwa kwa watu wale ambao hufanya kazi zao kwa kushirikiana vizuri. Watu hao hujibidisha kufanya kazi zao kwa haraka na vizuri hadi hufaulu kuzimaliza kwa muda mfupi, kwa sababu ya umoja wao huo.

Umoja huo huwapa nguvu kila mmoja wao za kujibidisha kufanya kazi, kwa sababu ya faraja yao hiyo ya kuwa pamoja. Umoja huo pia huwawezesha kushirikiana katika kuyatatua matatizo mbalimbali katika maisha yao. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘wawili ni wawili.’

Msemo huu hufundisha watu kuwa na umoja wa kuwawezesha kusaidiana katika kuyatekeleza vizuri majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio ya kuziendeleza vizuri familia zao.

modelo-mocambicana

bhashule

ENGLISH: THE TWO ARE TWO.

The orogin of this saying is individuals who are two in execution of their responsibilities. Such individuals can do a great job in a short period of time and finish it because of their unity and support. That’s why people say, ‘The two are two.’

The saying is used comparatively to refer to people who do their jobs in good cooperation. Such people do their work quickly and efficiently, until they are able to finish it within the shortes time possible, because of their unity.

The union empowers each of them to work hard, because of shared comfort. The union also allows them to work together to solve various problems in life. That’s why people say, ‘the two are two.’

The saying teaches people about being united to enable them to help each other in fulfilling their responsibilities, so that they can find success for the betterment their families.

553. NDEGE YA HASI.

Imbuki ya kahayile kenako yilolile ndege iyo yili ya hasi. Indege yiniyo idalalaga ung’wigulya guti umo jigalalilaga indege ijingi. Iyoyi igapelelaga hasi pye amakanza gayo. Hunagwene abhanhu bhagiyiitanaga giki, ‘ndege ya hasi.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitaga bhukengeji bhogudebha ijenheleja ja jito jitale ijo jigigelaga umuchalo jakwe. Umunhu ng’wunuyo, agagatumilaga chiza amasala gakwe, mpaga obhupandika ubhung’hana bho jito jinijo. Uweyi agikolaga n’indege ya hasi, kunguno nuweyi agabhucholaga ubhung’hana bho musilili, kugiki abhanhu bhakije ugundebha igiki alikengela mhayo nebhe. Hunagwene agiitanaga giki, ‘Ndege ya hasi.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu gudebha gwita bhukengeji ubho bhudulile gubhambilija ugubhudebha ubhung’hana bho mihayo iyo igigelaga umuchalo jabho, kugiki bhadule gwikala  bho mholele na bhichabho umukikalile kabho.

(Mathayo 2:1-5; Mathayo 2:16-17).

KISWAHILI: NDEGE YA CHINI.

Chanzo cha msemo huu chaangalia ndege ambayo huwa chini. Ndiyo hiyo, hairuki kama zirukavyo ndege zingine. Yenyewe hukimbia ikiwa chini wakati wote. Ndiyo maana watu huiita kwamba ni ‘ndege ya chini.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya utafiti wa kumwezesha kuelewa chanzo cha matukio makubwa ya kijijjini kwake. Mtu huyo hutumia vizuri akili zake zote, hadi anafikia hatua ya kupata ukweli wa tukio hilo lililotukia kijijini kwake. Yeye hufanana na ndege ya chini, kwa sababu naye hufanya utafiti kwa kuchungua kisirisiri chanzo cha matukio ya pale kijijini kwake. Yeye hufanya kazi hiyo chinichini, ili wengine wasiweze kumtambua kuwa anafuatilia tukio fulani la pale kijijini kwao. Ndiyo maana yeye hujiita kwamba ni ‘ndege ya chini.’

Msemo huu hufundisha watu kuelewa namna ya kufanya utafiti wa kuwawezesha kuelewa chanzo cha matukio ya kwenye maeneo yao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao katika maisha yao.

(Mathayo 2:1-5; Mathayo 2:16-17).

ndege

ndege1

 

ENGLISH: A GROUND PLANE.

The origin of this saying is a plane that stays on the ground. Yes, it does not fly like other planes. It runs on the ground all the time. That is why people call it ‘a ground plane.’

The saying is used comparatively to refer to a person who conducts research to understand the cause of major events in his village. The person makes good use of all his senses until he/she finds out what happened. He/she is like a ground pplane, because he/she conduct his/her research secretly. He/she works undercover so that others may not recognize that he/she is persuing a local event in their village. That is why he/she calls himself a ‘ground plane.’

The saying teaches people about understanding how to do research to enable them understand the cause of events in their environment, so that they can live in harmony with their peers.

(Matthew 2: 1-5; Matthew 2: 16-17).

552. LUBHUNDA MIYAGA.

Imbuki ya kahayile kenako ilolile bhubhundi bho miyaga bho jivumva jilebhe, nu bho ningi uyo alinduja. Ubhubhundi bho miyaga bhunubho bhuli bho jisumva ijo jigasamaga huna lwingila luyaga umuno gojo. Ijoyi jigihayaga giki jilina bhudula bho gulubhugila luyaga lutale.

 Ulu ningi nduja ubhakinda abhiye agihaya giki n’uweyi agabhundaga miyaga, kunguno adahebhagwa umumbina jakwe. Hungwene agiitanaga umugiji o miyaga ng’wunuyo giki, ‘Lub’unda miyaga.’

Akahayile kenako kagalenganijiyaga kuli munhu uyo alina nguzu ja gutumama milimo iyo igamalilaga makoye umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga milimo ya gubhatongela chiza abhiye, kugiki bhadebhe ugugamala amakoye gabho bho gutumama milimo yabho chiza.

Uweyi agikolaga nu lubhunda miyaga, kunguno n’uweyi alina nguzu ja guyihebha imilimo yakwe chiza. Imilimo yiniyo igamalilaga makoye aha ng’wakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, ‘Lubhunda miyaga.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu gubhiza na nguzu ja guyitumama imilimo yabho chiza, kugiki bhadule gubhingija abhanhu bhabho makoye ga gugayiwa jiliwa umuwikaji bhobho.

(Mathayo 27:45-54; Marko 1:21-28; Matendo ya Mitume 16:2; 1Wathesalonike 4:11-12).

KISWAHILI: MBUGIA UPEPO.

Chanzo cha msemo huu chaangalia ubugiaji wa upepo wa kiumbe fulani au wa manju ambaye huwashinda wenzake katika michezo ya ngoma. Ubhugiaji huo ni wa kiumbe ambacho huachana ili kuruhusu upepo ungie mdomoni. Chenyewe hujidai kuwa na uwezo wa kubugia kimbunga kiwezacho kuzoa vitu mbalimbali.

Hali hiyo hutokea wakati manju anayesifika akiwashinda wenzake kwenye michezo ya ngoma, anajitapa. Yeye hujiita majina ya kuonesha kwamba ana uwezo mkubwa kuwazidi wenzake, ili waendelee kumwogopa. Ndiyo maana yeye hujiita kwamba ni ‘mbugia upepo.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye nguvu za kumwezesha kufanya kazi zile ziwezazo kumuondolea matatizo kwa haraka maishani mwake. Mtu huyo huyatekeleza majukumu yake ya kuwaongoza vizuri wenzake, ili waelewe namna ya kuyatatua matatizo yao kwa kufanya kazi vizuri na kwa bidii.

Yeye hufanana na mbugia upepo, kwa sababu naye ana nguvu za kuzitekeleza kazi zake vizuri hadi kuzimaliza. Kazi hizo humsaidia katika kuyatatua vizuri matatizo yake. Ndiyo maana watu humwita kwamba ni ‘mbugia upepo.’

Msemo huu hufundisha watu kuwa na nguvu za kuyatekelezea majukumu yao vizuri, ili waweze kupata mafanikio yawezazo kuwatatulia matatizo mbalimbali maishani mwao.

(Mathayo 27:45-54; Marko 1:21-28; Matendo ya Mitume 16:2; 1Wathesalonike 4:11-12).

nkima ntumami

ntumami

 

ENGLISH: A WIND SWALLOWER.

The origin of this saying is ghostly nature of a particular creature or a maestro that overpowers his/her colleagues in dance competitions. The creature opens its mouth to allow wind to enter. It claims to be able to swallow a storm, which can take on many objects.

The self praise happens a maestro beats his/her contestants. When it so happens, he/she calls himself/herself praise names to show that he/she has great powers over his/her contestants so that they will always be scared of him/her. That is why he/she calls himself/herself ‘a wind swallower.’

The saying is used comparatively to refer to a person who has the power to do tasks that can get him out of trouble quickly in life. The person carries out his/her responsibilities to properly guide others to understand how to solve their problems, by working effectively and diligently. He/she is like a wind swallower, because he/she also has the power to carry out his tasks well. Such activities help him/her to solve his/her problems properly. That is why people call him ‘a wind swallower.’

The saying teaches people to carry out their tasks properly, so that they can achieve the best they can to solve a variety of problems in their lives.

(Matthew 27: 45-54; Mark 1: 21-28; Acts 16: 2; 1Thessalonians 4: 11-12).