Imbuki ya lusumo lunulo yingilile kubhufugi bho mabhele. Amabhele genayo, gagafugagwa nulu gagasegesagwa mpaga gapya chiza. Aliyo lulu, ulu galisegeswa chiniko gagamalaga likanza lilihu gagufugagwa, nulu gagusegesagwa huna gapya. Ulu gupya gagisungulaga amaguta gabhiza galihigulya amabhele gasaga hasi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘uyo agufugaga mabhele ngoko jidinahila adalalaga.’
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo olagana, uyo atogilwe gwigusha n’ung’wiye uyo bhitolile nawe bhujiku pe. Umunhu ng’wunuyo agadumamaga ugutumama imilimo yakwe ulu wela ubhujiku, kunguno ya gwikala na tulo ningi iyo adaimalile ibhujiku. Uweyi agikolaga n’unsegesi o mabhele uyo adalalaga kunguno ya gugwandya unimo guniyo ngoko jidinahila, kulwakubhiza n’uweyi igigushashaga n’uyo bhitolile nawe bhujiku pe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga agutindilaga ilimi, kunguno adalalile ibhujiku. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘uyo agufugaga mabhele ngoko jidinahila adalalaga.’
Ulusumo lunuyo lolanga bhanhu gubhiza n’ikanza lya gwibhegeleja uigutumama imilimo yabho iyo igabhapandikalaga jililwa, kugiki bhadule gwinja makoye ga nzala aha kaya jabho.
(Marko 13:36-37).
KISWAHILI: ACHEKECHAYE MAZIWA KABLA YA JOGOO KUWIKA HUWA HALALI.
Chanzo cha methali hii chatokea kwenye uchekechaji wa maziwa. Maziwa huchekechwa kwa muda mrefu sana ndipo yaive. Kuiva kwake ni kufikia hatua ya kujitenga mafuta kuwa juu ya maziwa. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘achekechaye maziwa kabla ya jogoo kuwika huwa halali.’
Methali hii hulinganishwa kwa mwana ndoa ambaye hucheza na mwenzi wake usiku kucha. Mtu huyo hushindwa kufanya kazi kesho yake, kwa sababu ya kuwa na usingizi mwingi ambao hakuumaliza vizuri usiku uliopita. Yeye hufanana na yule anayechekecha maziwa kabla ya jogoo kuwika maana hufanya kazi hiyo usiku kucha bila kulala, kwa sababu naye hucheza na mwenzake wa ndoa usiku kucha, hali ambayo hunfanya aonekane mchovu wakati wa mchana. Mtu huyo hushinda kutwa nzima akisinzia kwa sababu ya kutolala vizuri usiku uliopita. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘achekechaye maziwa kabla ya jogoo kuwika huwa halali.’
Methali hii hufundisha watu kutenga muda wa maandalizi yatakayowawezesha kuyatekeleza vizuri majukumu yao yanayowawezesha kupata chakula, ili waweze kupata mafanikio mengi katika kuzijenga vizuri familia zao. Muda wa maandalizi hayo utawawezesha kuondoa tatizo la njaa kwenye familia zao.
(Marko 13:36-37).
ENGLISH: HE WHO SHAKES MILK BEFORE COCKCROW NEVER SLEEPS.
The origin of this proverb is the act of shaking curdled milk to separate it from fat. This is done for a relatively very long time until the fat comes on top of the milk. That is why people say, ‘He who shakes milk before cockcrow never sleeps.’
The proverb is used comparatively to warn a married person who plays with his/her spouse all night long to desist from that behavior, because that person would always be unable to work the next day due to lots of sleep from the previous night. That person is like the one who shakes milk before cockcrow who does that all night without sleeping as he/she, too, plays with his/her spouse all night, which makes him/ look tired in during daytime. That person succumbs to sleeping all day because of not sleeping well the night before. That is why people tell him/her, ‘He who shakes milk before cockcrow never sleeps.’
The proverb teaches people to set aside time to prepare for their activities that bring food on the table, so that they can be more successful in building better families. Preparations will allow them to eliminate the problem of hunger in their families.
(Mark 13: 36-37).