Kashinje Zacharia

455. MAKUNZA ADAJAGA NG’WAMASAGINGHI NG’WIYE.

Imbuki ya lusumo lunulo yilolile kikalile ka ng’wa makunja ako kali ka heke. Uweyi olialemile ugukaleka akikalile kakwe, ako kagang’wenheleja kubhiza masaginghi.

Umunhu ng’wunuyo oliadajaga ukuli masaginghi ng’wiye. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘makunja adajaga ng’wa masaginghi ng’wiye.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile igiki, bhuli ginhu jili na jimile jajo. Umunhu ng’wunuyo, agalenganijiyagwa na makunja uyo adajaga ng’wa masaginghi ng’wiye, kunguno nanghwe agajisomelaga iginhu giti numo jili, umujimile jajo.

Uweyi agikalaga akadimilile akajile kakwe kenako, guti nu makunja umo oliakadimililile akajile kakwe. Adajigaluchaga iginhu jinijo, kugiki jifade akimile kakwe uweyi, agajilekaga numo jili. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga, ‘makunja adajaga ng’wa masaginghi ng’wine.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyabhi, bho gujitumila chiza ijinhiwa jabho, kugiki bhadule kupandika matwazo mingi, umuwikaji bhobho.

Yohana 3:12.

1 Wakorintho 12:12.

KISWAHILI: MAKUNJA HAENDI KWA MASAGINGHI MWENZAKE.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia maisha ya makunja yalivyokuwa ya pekee. Yeye alikuwa hataki kuacha mwenendo wake huo wa maisha, ambao ulimfanya aitwe masaginghi, yaani mtu wa pekee.

Mtu huyo alikuwa haendi kwa masaginghi mwenzake, kwa maana ya kuiacha namna yake yakuishi, iliyompatia mafanikio mengi maishani mwake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘makunja haendi kwa masaginghi mwenzake.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule anayeelewa kwamba, kila kitu kina asili yake. Mtu huyo hulinganishwa na makunja asiyeenda kwa masaginghi mwenzake, kwa sababu naye huvisoma vitu hivyo katika asili yake, ili aweze kuuelewa ukweli wa vitu hivyo.

Yeye huwa havibadilishi vitu hivyo, vifuate alivyo yeye, bali huviacha vibaki vilivyo. Ndiyo maana watu humwambia mtu huyo kwamba, ‘makunja haendi kwa masaginghi mwenzake.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na uhuru wa kuvitumia vizuri vipaji vyao, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao.

Yohana 3:12.

1Wakorintho 12:12.

zambia-

ENGLISH: MAKUNJA DOES NOT GO TO HIS FELLOW MASAGINGHI.

The source of this proverb looks at Makunja’s unique life style. He did not want to change his style of life and people labelled him (Masaginghi) a special person. This kind of life made him a successful person. This is why people can use the proverb ‘Makunja does not go to his fellow Masaginghi’ to communicate how one with success in life cannot easily give up in struggle for fear of losing his/her richness.

The proverb can be compared to a person who understands that everything has its origin. Such a person is compared to Makunja who do not go to fellow Masaginghi because he can read by himself and be able to understand the world in its natural state.

The proverb teaches people about the freedom to make the best use of their talents. This can make one have the best kind of life determined by him/her.

John 3:12.

1 Corinthians 12:12.

454. WICHEMBA INGELE WANIJIMBA.

Imbuki ya lusumo lunulo yilolile bhuchembi bho ngele, ubhogubhajimba abhangi. Umunhu uyo alijinja ginhu ulu uichemba ingele iyo agapimilaga, aguyubhajimba abho bhalingulia. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘wichemba ingele wanijimba.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo aling’wiming’holo, umubhusuluja bhokwe. Umunhu ng’wunuyo agabhajimbaga abhanhu abho agabhajingijjga.

Uweyi agalenganijiyagwa na munhu uyo oyichemba ingele yakwe, kunguno, nanghwe abhagapunjaga abhaguji bha jikolo jakwe, bho nyashilimu. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘wichemba ingele wanijimba.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja wiming’holo, umubhusuluja bhobho, kugiki bhadizubhajimba abhaguji bha jikolo jabho.

Amosi 8:4-6.

 1 Wathesalonike 4:6.

ULIKIKATA KIPIMO UMENIPUNJA.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia ukataji wa kipimo anachokitumia mtu katika biashara yake, kwa lengo la kuwapunja wateja wake.

Mtu akikikata kipimo chake hicho cha kufanyia biashara yake, atawapunja wale wanaonunua vitu vyake. Ndiyo maana watu hao wakigundua kwamba anawapunja kwa sababu ya kukipunguza kipimo chake, humwambia kwamba, ‘ulikikata kipimo umenipunja.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mchoyo katika uendeshaji wa biashara zake. Mtu huyo huwapunja wale anaowauzia vitu vyake, kwa kutumia ujanja wa namna mbalimbali.

Yeye hulinganishwa na mtu aliyekikata kipimo chake cha kufanyia biashara, kwa sababu, naye hutumia ujanja wa kuwapunja wale wanaonunua vitu vyake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘ulikikata kipimo umenipunja.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha tabia za uchoyo wa kuwapunja watu katika biashara zao, ili waache kuwadhulumu wateja wao.

Amosi 8:4-6.

1Wathesalonike 4:6.

scale

ENGLISH: YOU HAVE CUT THE SCALE; YOU HAVE GIVEN ME LITTLE.

The source of this saying is the use of scale in business activities. A business person can cut his/her measuring scale in order to generate more profit in his/her business. If some one does so, he/she is likely to chase his/her customers and therefore destructing his/her own business. He/she can be accused of stealing from customers.

This saying can be compared to a person who is greedy in running his/her business. The person manipulates the goods he or she sells using a variety of tactics.

He/she is compared to a person who dismisses his/her business through fooling his/her customers.

The saying teaches people to stop being greed rather stick to principles of trustworthy that can enable them live better with others in the society.

Amos 8: 4-6.

1Thessalonians 4: 6.

453. KWILUNGU BHADAJAGA LWA KABHILI.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhuzugi bho walwa ubho bhudapile. Ulu walwa bhuzuga, aliyo bhukija ugupya chiza, ilihumbi lyabho lidashokejiyagwa. Gashinaga lulu, ibhelelile bhuzugwe bhungi uwalwa bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘kwilungu bhadajaga lwa kabhili.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitaga mihayo, nulu milimo yakwe, bho nduhu ugwita bhukengeji bho gudula gung’wambilija uguimala chiza.

Uweyi agitimbukilagwa wandyaga nimo, nulu mhayo, bho nduhu ugugamana amakoye ayo gadulile gwilonga, umunimo, nulu mhayo gunuyo. Hunagwene abhanhu, ulu gigela makoye umunimo gokwe, bhagayomgaga giki, ‘kwilungu bhadajaga lwa kabhili.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwita bhukengeji bho milimo yabho chiza, haho bhatali ugwitumama, kugiki bhadule ugugiliga amakoye ayo gakomile gwigela, umubhutumami bho milimo yabho.

Waeb 9:12.

 Mark 14:25.

KISWAHILI: MPIKO WA POMBE YA KIENYEJI HAURUDIWI MARA YA PILI.

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye upikaji wa pombe ambayo haijaiva. Pombe ikipikwa ikakosewa kupikwa ikawa haijaiva vizuri, hairudiwi kupikwa tena. Kumbe basi, yafaa ipikwe pombe nyingine. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘mpiko wa pombe ya kienyeji haurudiwi mara ya pili.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule, ambaye hufanya kazi zake bila kufanya utafiti wa kumwezesha kuzimaliza vizuri.

Mtu huyo, hufanya kazi zake kwa kukurupuka, bila kuangalia kwanza matatizo ambayo, yaweza kutokea kwenye kazi hiyo, ili kuzifahamu njia za kuyatatulia.

Ndiyo maana akitapata matatizo kwenye kazi anayoifahanya mtu huyo, watu husema kwamba, ‘mpiko wa pombe ya kienyeji haurudiwi mara ya pili.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kufanya utafiti wa kazi wanazotaka kuzifanya, kabla ya kuzianza, ili waweze kuyakwepa matatizo ambayo yanaweza kutokea kwenye kazi hizo.

Waeb 9:12.

 Mark 14:25.

IMG_20190709_111321_5

ENGLISH: THE COOKING OF THE TRADITIONAL BREW IS NOT REPEATED.

The source of the saying comes from half-cooked local brew. If a cook hasn’t cooked properly her local brew, there is no possibility of orrecting the mistake. The solution is to cook another brew. This is why people say ‘the cooking of the traditional beer is not repeated’.

The saying can be compared to a person who performs his/her tasks without doing research that can enable him/her to finish it properly. Such people perform their tasks without first looking at problems that may arise and find ways to resolve them.

The saying teaches people about researching before engaging in actual performance of tasks one wants to do. This can help them to avoid problems in future.

Heb 9:12.

Mark 14:25.

452. ICHEMBILE INGELE.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kungele iyo yatinwa yugeha. Ingele jilijipimilo ja wiguliji bho jiliwa guti: bhusiga, mandege,  ng’haranga na jingi ningi.

Ingele yiniyo, ulu yutinwa igadohaga yilema ugutumilwa hangi, kunguno ulu yupimilwa, idulile gubhagopa abhiguliji. Hunagwene abhanhu bhagayomba giki, ‘ichembile ingele.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adina masala. Umunhu ng’wunuyo, agawilagwa giko bho mbisila, kunguno, ulu umana igiki aliwilwa adina go amasala, adulile gukolwa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, umunhu ng’wunuyo ‘ichembile ingele.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza ni kujo, lya guichagula mihayo iyo iliyawiza, ulu bhalihoya na bhichabho, kugiki bhadule ugwikala chiza nabho.

Yeremia 4:26.

Muhubiri 10:3.

KISWAHILI: KIPIMO KIMEKATWA.

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye kipimo kilichokatwa kikapungua ukubwa wake. Kipimo ni kitu kinachotumika wakati wa kuuziana mazao ya chakula kama vile: mtama, mahindi, karanga na vingine vingi.

Kipimo hicho kikikatwa hupungua ukubwa wake. Hali hiyo hukifanya kisifae tena kutumika katika kupimiana mauziano, vinginevyo watapunjana wale wanaouziana kitu hicho. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kipimo kimekatwa.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hana akili. Mtu huyo huambiwa hivyo, kwa mafumbo na wenzake, kwa sababu akigundua kuwa, watu wanamwambia kuwa, hana akili, atakasirika. Ndiyo maana watu kusema kwamba, mtu huyo ‘kipimo kimekatwa.’

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na hekima ya kuchagua maneno yaliyo mazuri, wakati wanaongea na wenzao, ili waweze kuishi vizuri nao.

Yeremia 4:26.

Muhubiri 10:3.

horizontal-scale1

african ichembile

ENGLISH: THE SCALE HAS BEEN CUT.

The source of the saying comes from a cut-off dimension. The scale is something used when selling food products such as: sorghum, maize, nuts and many others.

When the scale is cut, it decreases its size. This makes it no longer useful for measuring the items to be sold. That’s why people can say, ‘the scale has been cut’ to mean reduction of its actual size.

The saying can be compared to a person who has no sense. Such a person is told in parables in order to make him/her not understand that his/her ability to think is relatively low. The saying teaches people about the wisdom of choosing the right words when talking to their peers. This can help them to have peace all the time.

Jeremiah 4:26.

Ecclesiastes 10:3.

451. CHEMBELAGA AHA IKAYA YANE NHALE.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhanhu abho bhaligabhanha nyama. Aliyo lulu, umubhugabhani bho nyama yiniyo, uumo obho aligongeja guchembelwa nyama nhale, gitumo atogelilwe uweyi. Hunagwene agayombaga giki, ‘chembelaga aha ikaya yane nhale.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalombaga ginhu bho lugoto, nulu bho gung’ang’anila. Uweyi ahayile nulu gwisolela nu wei ng’winikili, kunguno ya wigongeja bhokwe, ubho guhaya apandike iginhu ginijo, gitumo atogelilwe weyi. Hunagwene umunhu ng’wunuyo, agayombaga giki. ‘chembelaga aha ikaya yane nhale.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka gulomba ginhu bho gung’ang’anila, kugiki bhadule gwinhiwa ijo bhalijilomba. Igeleliwe abhanhu bhenabho, bhabhizuke na bhichabho, ulu bhalilomba ginhu jilebhe.

Zaburi 78:15.

Yakobo 1:15.

2Petro 3:3.

Yuda 1:18-21.

KATIA HAPA MJI WANGU NI MKUBWA.

Chanzo cha msemo huo chatokea kwa watu wanaogawana nyama kwa kukatiana. Lakini basi, katika kugawiana kwa nyama hiyo, mmoja wao hutaka kukatiwa kipande kikubwa kama atakavyo yeye. Ndiyo maana yeye husema kwamba, ‘katia hapa mji wangu ni mkubwa.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huomba kitu kwa kung’ang’ania. Yeye hutaka hata kujichukulia mwenyewe, badala ya kusubiri kupewa na mhusika, kwa sababu ya ung’ang’nizi wake.

Yeye hutaka kupewa kipande kikubwa cha nyama hiyo, kama atakavyo yeye, bila kuwajali wenzake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, ‘katia hapa mji wangu ni mkubwa.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha tabia za kuomba kitu kwa kung’ang’ania bila kuwajali watu wengine, ili waweze kupewa kile wanachokiomba. Yafaa pia watu hao, wawajali wenzao, wanapoomba kitu fulani.

Zaburi 78:15.

 Yakobo 1:15.

 2Petro 3:3.

 Yuda 1:18-21.

cut-meat

ham

ENGLISH: CUT IT HERE, MY FAMILY IS BIG.

The source of the saying comes from people who share meat. In the distribution of the meat, one of them wants to cut as big piece of it because of having a big family to feed. That is why he/she says, ‘cut it here, my family is big.’

The saying can be compared to aperson who asks for something persistently. He/she even wants to take it upon himself/herself rather than waiting to be given by the distributor in a fairly manner. Such a person can be labelled as selfish; he/she doesn’t consider his/her fellow in the distribution of available resources.

The saying teaches people to stop the tendency of being selfish rather care for others as well. In so doing people will be able to respect each other thus creating a very peaceful society.

Psalm 78:15.

James 1:15.

2 Peter 3: 3.

Jude 1: 18-21.