Imbuki ya lusumo lunulo yilolile bhuchembi bho ngele, ubhogubhajimba abhangi. Umunhu uyo alijinja ginhu ulu uichemba ingele iyo agapimilaga, aguyubhajimba abho bhalingulia. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘wichemba ingele wanijimba.’
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo aling’wiming’holo, umubhusuluja bhokwe. Umunhu ng’wunuyo agabhajimbaga abhanhu abho agabhajingijjga.
Uweyi agalenganijiyagwa na munhu uyo oyichemba ingele yakwe, kunguno, nanghwe abhagapunjaga abhaguji bha jikolo jakwe, bho nyashilimu. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘wichemba ingele wanijimba.’
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja wiming’holo, umubhusuluja bhobho, kugiki bhadizubhajimba abhaguji bha jikolo jabho.
Amosi 8:4-6.
1 Wathesalonike 4:6.
ULIKIKATA KIPIMO UMENIPUNJA.
Chanzo cha methali hiyo chaangalia ukataji wa kipimo anachokitumia mtu katika biashara yake, kwa lengo la kuwapunja wateja wake.
Mtu akikikata kipimo chake hicho cha kufanyia biashara yake, atawapunja wale wanaonunua vitu vyake. Ndiyo maana watu hao wakigundua kwamba anawapunja kwa sababu ya kukipunguza kipimo chake, humwambia kwamba, ‘ulikikata kipimo umenipunja.’
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mchoyo katika uendeshaji wa biashara zake. Mtu huyo huwapunja wale anaowauzia vitu vyake, kwa kutumia ujanja wa namna mbalimbali.
Yeye hulinganishwa na mtu aliyekikata kipimo chake cha kufanyia biashara, kwa sababu, naye hutumia ujanja wa kuwapunja wale wanaonunua vitu vyake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘ulikikata kipimo umenipunja.’
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha tabia za uchoyo wa kuwapunja watu katika biashara zao, ili waache kuwadhulumu wateja wao.
Amosi 8:4-6.
1Wathesalonike 4:6.
ENGLISH: YOU HAVE CUT THE SCALE; YOU HAVE GIVEN ME LITTLE.
The source of this saying is the use of scale in business activities. A business person can cut his/her measuring scale in order to generate more profit in his/her business. If some one does so, he/she is likely to chase his/her customers and therefore destructing his/her own business. He/she can be accused of stealing from customers.
This saying can be compared to a person who is greedy in running his/her business. The person manipulates the goods he or she sells using a variety of tactics.
He/she is compared to a person who dismisses his/her business through fooling his/her customers.
The saying teaches people to stop being greed rather stick to principles of trustworthy that can enable them live better with others in the society.
Amos 8: 4-6.
1Thessalonians 4: 6.