608. NG’HOLO YA NHAB’I IDABYALAGA.

Imbuki ya lusumo lunulo, yililola bhujidabyala bho ng’holo ya nhab’i.  Ing’holo yiniyo, iya nhab’i uyo alinayo imo duhu, igabhizaga ilolilwe na bhuli katumamile, guti nzala nulu gugenihwa na bhageni. Iyoyi igatumamilagwa duhu haho itali nugubyala. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ng’holo ya nhab’i idabyalaga.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adina jikolo ahakaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ung’wunuyo, agabhizaga na makoye mingi, kunguno akambiligije kakwe kali kamakoye.

Uweyi agapandikaga jikolo ijo agajimalaga bho likanza liguhi duhu, guti nu nhab’i uyo agaitumilaga ing’holo yakwe, haho itali nulu gubyala, kunguno ya gwisongwa na makoye mingi aha ng’wakwe. Hunagwene abhanhu abhagayombaga giki, ‘ng’holo ya nhab’i idabyalaga.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija guchola jikolo bho guitumama imilimo yabho na bhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika sabho ijagubhambilija ugwinja amakoye, umukilalile kabho. Yigelelilwe abhanhu bhenabho bhaleke ugwisanya jikolo jigehu ijo bhalijo.

2Samweli 2:2-3.

Ezra 9:7.

Mathayo 13:12.

Marko 4:25.

Luka 8:18.

KISWAHILI: KONDOO WA FUKARA HAZAI.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia kutozaa kwa kondoo wa maskini. Kondoo huyo, ambaye ni wa fukara mwenye naye mmoja tu, hutegemewa kutumika kwenye kila shida, kama vile kununua chakula, na kuandaa mboga ya wageni. Yeye hutumiwa hata kabla hajazaa. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kondoo wa fukara hazai.’

Methali huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hana vitu kama vile mali kwenye familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, hukumbwa na matatizo mengi sana maishani mwake, kwa sababu ya kukosa mali ya kumsaidia katika kuyatatua matatizo hayo.

Yeye hupata mali kidogo tu ambazo huzimaliza kwa muda mfupi, kama yule fukara atumiavyo kondoo wake hata kabla hajazaa, kwa sababu ya kusongwa na matatizo mengi kwenye familia yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kondoo wa fukara hazai.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kutafuta mali kwa kufanya kazi zao kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mali ya kuwaondolea matatizo, katika maisha yao. Yafaa watu hao, waache tabia ya kutegemea kitu kidogo walicho nacho.

2Samweli 2:2-3.

Ezra 9:7.

Mathayo 13:12.

Marko 4:25.

Luka 8:18.

ng'holo3

ng'holo

 

ENGLISH: THE SHEEP OF THE POOR CANNOT REPRODUCE .

The source of this saying is the fertility of the poor’s sheep. The poor’s sheep is the only possession he/she has and he/she depends on it if he/she faces a problem such as shortage of food in his/her family. The poor’s sheep will end up being used before it multiplies. Therefore, whatever little he/she can have in life cannot multiply to make him/her a successful person. In such a context, people came with the saying that ‘The sheep of the poor cannot reproduce.’

The saying can be compared to a person who does not have anything in his/her family. This person can suffer for lacking something to support his/her life. Even the little resource he/she can manage to get can last only for few days.

This saying teaches people to work hard to get rich. They need to work hard and avoid giving up easily in their struggle.

2Samuel 2: 2-3, Ezra 9: 7, Matthew 13:12, Mark 4:25, Luke 8:18.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.