502. KALAGU – KIZE. AMANILE UGOLA ALIYO ADAMANILE IJOALOLA:- NGOKU.

Imbuki ya kalagu yiniyo ilolile kasiminzile ka ngoku. Ingoku ulu ilisiminza igalekaga bholange umo ilibhitila. Hangi nu lugendo loyo, lulilogwigondagonda, kunguno ludasululaga. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘amanile ugola aliyo adamanile ijoalola’ bashosha giki ‘ngoku’.

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo, agalekaga jigemelo ja wiza umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhalungujaga chiza abho bhali mumakoye. Uweyi agatumamaga milimo yakwe, bho nduhu uhadikijiwa, nulu gulindila gwizukijiwa na ungi, kunguno aidebhile ingelelo ya milimo yakwe.

Uweyi agikolaga ni ngoku, kunguno nanghwe agolaga ginhu jilebhe, ijo abhiye bhagilangaga gutumama milimo yabho, chiza gubhitila wikaji bhokwe. Hunagwene agabhaganilaga abhanhu giki, ‘amanile ugola aliyo adamanile iji alola’ bhashosha, ‘ ngoku.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu  kuwalekela abhanhu bhabho, meng’ho ja gudula gubhakomeleja guitumama imilimo yabho, bho bhuyegi bhutale, kugiki bhadule ugujibheja chiza ikaya jabho.

(Zaburi 23:1-4. Mathayo 11:25-30. 1Petro 5:8-11)

 

KISWAHILI: KITENDAWILI    –   TEGA: ANAJUA KUCHORA LAKINI HAJUI AKICHORACHO – KONOKONO.

Chanzo cha kitendawili hiki ni utembeaji wa konokono. Konokono akitembea, huchora mchoro anamopitia. Pia mwendo wake ni wa kupindapinda; si ule ulionyooka. Ndiyo maana watu hutegeana kitendawili kwamba ‘anajua kuchora lakini hajui akichoracho’ na kutoa jibu la ‘konokono’.

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye, huacha mfano mzuri wa kuishi vizuri na watu, kupitia maisha yake. Mtu huyo, huwafariji vizuri wale walioko kwenye matatizo mbalimbali. Yeye pia hutekeleza majukumu yake, bila kulazimishwa wala kusubiri kuambiwa na mwingine, kwa sababu anayaelewa vizuri, yalivyo, na namna ya kuyatekeleza.

Mtu huyo, hufanana na konokono achoravyo kwa bidii, kwa sababu naye huchora kitu fulani ambacho wenzake, hukiona na kujifunza namna ya kuyatekeleza majukumu yao vizuri, kupitia maisha yake. Ndiyo maana yeye huwahadithia watu wake kwamba, ‘anafahamu kuchora lakini hajui kile anachokichora’ na kujibu, ‘ konokono.’

Kitendawili hicho, chafundisha watu  kuacha alama za kuwahimiza wenzao kuyatekeleza majukumu yao, kwa furaha kubwa, kupitia maisha yao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao.

Zaburi 23:1-4. Mathayo 11:25-30. 1Petro 5:8-11.

 

ngoku

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME: HE KNOWS HOW TO DRAW BUT DOESN’T KNOW WHAT HE DRAWS – A SNAIL.

The origin of this riddle is the snail walk. As the snail walks, it leaves drawings along its passage. Also, its motion is not a straight one. That is why people pose a riddle, ‘He knows how to draw but doesn’t know what he draws‘ and reply ‘a snail’.

This riddle, compared to the individual, leaves a good example of how to live well with people, through his life. The person, in turn, comfort those in distress. He also carries out his duties, without being forced or waiting to be told by another, because he understands them well, what they are, and how to carry them out.

The man is like a hard-working snail, because he also draws on something his colleagues see, and learn how to carry out their duties, through his life. That is why he tells his people that, ‘it knows how to draw but it doesn’t know what it draws: – a snail.’

This riddle, teaches people about leaving markers to encourage their peers to carry out their responsibilities, with great joy, through their lives, so that they can better their families.

(Psalm 23: 1-4; Matthew 11: 25-30; 1Peter 5: 8-11)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.