Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile solobho ya wanguhi bho guja hanhu. Umunhu uyo wanguhaga gushiga hanhu agikomanigijaga aha wikalo, kunguno agasangaga uwikalo bhulihoyi, na masumbi galihoyi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘uyo aganguhaga agakomanyaga aha ng’wa gwikala.’
Ulusumo lunulo lukalenganijiyagwa kuli munhu uyo aganguhaga uguja ukumilimo, nulu uko libhilingilo. Umunhu ng’wunyo, agapandikaga solobho ya gugutumama hatale unimo gunuyo, ulu ojaga kumilimo yakwe, Uweyi adulile nulu guzengela numba yakwe hasoga, kunguno ya wanguhi bhokwe bhunubho, ubhogushiga hoyi.
Uweyi agabhalanjaga na bhiye ugwanguha uguja ukumilimo yabho, nulu uko bhalija, kugiki, bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho. Hunagwene agabhawilaga abhanhu bhakwe giki, ‘uyo aganguhaga agakomanyaga aha ng’wa gwikala.’
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu gubhiza na nhungwa ja gwanguha ugujuitumama imilimo yabho, nulu uko wibhilingilo bhobho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho.
(Mathayo 25:1-13; Mathayo 24:36-44; Luka 13:24-25).
KISWAHILI: AWAHIYE NDIYE HUCHAGUA PA KUKAA.
Chanzo cha methali hii chaangalia faida ya kuwahi kufika mahali fulani. Mtu akiwahi kufika mahali alikotakiwa kwenda, hupata nafasi ya kujichagulia sehemu ya kukaa, kwa sababu ya yeye kukuta nafasi nyingi zikiwa bado zingali wazi, na viti vingi vikiwa wazi pia. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘awahiye ndiye huchagua pa kukaa.’
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwahi kwenda kazini au kwenye mkutano fulani. Mtu huyo hupata nafasi ya kuyatekeleza majukumu yake kwa mafanikio makubwa. Mafanikio hayo humpatia maendeleo kwenye familia yake.
Yeye hufaulu hata kujengea nyumba yakesehemu iliyo nzuri, kwa sababu ya kuwahi kwake huko. Yeye huwafundisha pia wenzake namna ya kupata mafanikio hayo, kwa kuwahimiza kundelea kuwahi katika kazi zao. Ndiyo maana huwaambia watu wake kwamba, ‘awahiye ndiye huchagua pa kukaa.’
Methali hiyo hufundisha watu kuwa na tabia ya kuwahi kwenda kuyatekeleza majukumu yao, au kuwahi kwenda kule wanakotakiwa, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao.
(Mathayo 25:1-13; Mathayo 24:36-44; Luka 13:24-25).
ENGLISH: HE WHO ARRIVES EARLIER CHOOSES WHERE TO SIT.
The origin of this proverb is the benefits of arriving at some place earlier than others. When a person arrives earlier at that place, he or she gets a chance to choose a where to sit or even stay, because he/she will find many vacancies. That is why people say, ‘He who arrives earlier chooses where to sit.’
The proverb is comparatively used to urge people to go early to their working or meeting places because a person who arrives earlier has the opportunity to carry out his/her duties with great success. That success improves his/her family wellbeing.
Such a person can even manage to build his/her residence on a beautiful scenary, because of his/her early arrival at the place. He also teaches his colleagues how to achieve this, by encouraging them to be always early at their working places. That is why he/she tells them, ‘He who arrives earlier chooses where to sit.’
The proverb teaches people to develop the habit of going early to their jobs or elsewhere where they are needed, so that they can achieve more in their lives.
(Matthew 25: 1-13; Matthew 24: 36-44; Luke 13: 24-25).