480. KITENDAWILI – TEGA. MODOKA YANE IDAMALAGA MAGUTA:- MAGULU

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola magulu. Bhuli munhu alina magulu gakwe, aliyo lulu, ulu uhaya gwandya lugendo agubhuka duhu na gwadya gusiminza, bho nduhu ni giki, aguditila maguta, umumagulu gakwe yenayo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘modaka yane idamalaga maguta:- magulu.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu, uyo ashikanile umubhutumami bho milimo yakwe. Umunhu ng’wunuyo, alina bhushikanu bho guja gujutumama milimo makanza gosegose, guti na magulu ayo gagandyaga lugengo, bho nduhu gulinda guditilwa maguta.

Uweyi agabhalangaga nabhiye, ahigulya ya kubhiza na bhushikanu bhunubho, ubho gutumama milimo yabho chiza. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, ‘modaka yane idamalaga maguta:- magulu.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya kubhiza na bhushikanu bhutale, ubho bhudulile gubhambilija uguitumama imilimo yabho chiza, kugiki bhadule gujibheja chiza, ikaya jabho.

Mathayo 26:41.

Mathayo 25:13.

Mathayo 10:22.

Zaburi 119:89-91.

KISWAHILI: KITENDAWILI  – TEGA

MOTOKAA YANGU HAIMALIZI MAFUTA:- MIGUU

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia miguu. Kila mtu ana miguu yake, ambayo huitumia akitaka kutembea sehemu fulani, bila hata kuweka mafuta, kwenye miguu yake hiyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘motokaa yangu haimalizi mafuta:- miguu.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule aliyekamilika katika utekelezaji wa kazi zake. Mtu huyo, ana bidii ambayo humwezesha kuzifanya kazi kwa utayari mzuri. Yeye yuko tayari wakati wowote, kutekeleza majukumu yake, kama miguu ilivyo tayari kuanza safari, bila kusubiri kuwekewa mafuta.

Yeye huwafundisha pia wenzake, namna ya kuwa na utayari huo wa kuyatimiza vizuri majukumu yao kila wakati. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, ‘motokaa yangu haimalizi mafuta:- miguu.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na utayari mkubwa wa kuyatekeleza majukumu yao vizuri, na kwa bidii kubwa, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao.

Mathayo 26:41.

Mathayo 25:13.

Mathayo 10:22.

Zaburi 119:89-91.

magulu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.