Imbuki ya kahayile kenako yingilile kukikalile ka mbiti. Imbiti yiniyo ingalyaga ijiliwa jayo bho nyasalasala, kunguno imanile igiki ulu yubhonwa igupejiwa.
Ulu yuhaya gudima ntugo halebhe, igajaga bho gukungila, kugiki adizibhona ung’winikili o ntugo gunuyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘mbiti yamana kalile.’
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu, uyo agajaga ulilila jiliwa, mumakaya ga bhanhu, nyasalasala. Umunhu ng’wunuyo, agalenganijiyagwa na mbiti, kunguno nayo idajaga bho lolele, mpaga ikunge kunge nayije. Yiyoyi igagaja bho gukungila, kugiki idule ugugudima untugo gunuyo.
Uniliji nang’hwe agajaga bho gulola meng’ho, kugiki abhanhu bhadizumbadija. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga umunhu ng’wunuyo giki, ali ‘mbiti yamana kalile.’
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja guja bhulilila jiliwa, mukaya ja bhichabho, kugiki bhatumame milimo, iyo idulile gubhapandikila jiliwa jagubhatosha gulya, mukaya jabho.
Mathayo 1:18.
2 Wathesalonike 3:6-10.
KISWAHILI: FISI ALIYEFAHAMU NAMNA YA KULA.
Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye namna alavyo fisi. Fisi hula chakula chake kwa akili ya ujanja ujanja, kwa sababu aelewa kwamba, akionwa atafukuzwa.
Akitaka kushika mfugo sehemu fulani, huenda kwa kunyemelea, ili asionwe na mwenye mfugo huo. Ndiyo maana watu husema kwamba, yeye ni ‘fisi aliyefahamu namna ya kula.’
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule aliye na tabia ya kwenda kula chakula, kwenye familia za watu, kwa kutumia akili za ujanja ujanja.
Mtu huyo, hulinganishwa na fisi, kwa sababu naye haendi kwa wazi, mpaka aangalie kwanza ndipo aende. Yeye huenda kwa kunyemelea, ili aweze kuukamata mfugo huo.
Mlaji wa kwenye familia za watu naye, huenda kwa kuangalia alama za nyakati, ili watu wasimgundue. Ndiyo maana watu humwita mtu huyo kwamba, yeye ni ‘fisi aliyefahamu namna ya kula.’
Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha tabia za kunyemelea kwenda kula chakula, kwenye familia za watu, ili waweze kufanya kazi zile ziwezazo kuwapatia chakula cha kutosha, kuwalisha kwenye familia zao.
Mathayo 1:18.
2 Wathesalonike 3:6-10.
ENGLISH: THE HYENA HAS KNOWN THE MANNER OF EATING.
The source of the saying comes from the manner of eating of a hyena. Hyenas eat food with a cunning mind, because they know that when seen by human beings they can be chased and sometimes killed. So, if a hyena wants to eat a certain domestic animal, it has to sneak in a manner that it cannot be seen.
The saying can be compared to a person who has a tendency to go out to eat, in people’s families, using clever tactics. This person might be going secretly to eat in other peoples’ families. He/she knows the time when food is served and therefore sneakingly goes to join them in eating. Such people are being described using the saying that ‘the hyena has known the manner of eating.’
The saying teaches people to stop the habit of eating from other peoples’ families rather work hard and be self-sufficient in order to feed oneself and his/her family as a whole.
Matthew 1:18.
2 Thessalonians 3: 6-10.