Imbuki ya lusumo lunulo yingilile kubhuli bho masangu bho kaya. Ubhuli bho masangu bhunubho bhub’ukilile ha mbina ya b’akima. Imbina yiniyo ulushigu ulo igushulaga, b’alyaga masangu na gubalasana. Hunagwene ulu bhanhu bhali kihamo ulu b’ubalasana, abhanhu bhagayombaga giki, ‘kaya yalile masangu.’
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanu abho bhali b’itolile, ulu b’iduma kaya yabho ucha, b’agahayaga giki, ikaya yiniyo yalile masangu. Gashinaga ikaya ugulya masangu, mumho gwiduma na gub’ulaga kaya yabho yiniyo. Hunagwene abhanhu ulu bhubhona b’itoji widumile na gub’ulaga kaya yab’o, bhagayombaga giki, ‘kaya yalile masangu.’
Ulusumo lunulo lolanga b’itoji higulya ya kuleka widumi bho gub’ulaga kaya yabho, kugiki bhadule gwikala b’itolile pye shigu ja wikaji bhobho.
Yeremia 3:18.
Isaya 50:1.
Malaki 2:14-16.
Ezra 10:3.
KISWAHILI: KAYA IMEKULA MAKANDE.
Chanzo cha methali hiyo chatokea kwenye ulaji wa makande wa kaya. Ulaji huo wa makande ulianzia kwenye mchezo wa wanawake. Mchezo huo au ngoma hiyo, ilikuwa na desturi ya kula makande siku ya kumaliza mchezo. Baada ya kula walisambaa kila mmoja kwenda nyumbani kwake. Ndiyo maana watu wakiona wenzao waliokuwa pamoja wamesambaa, husema kwamba, ‘kaya imekula makande.’
Methali hiyo hulinganishwa kwa watu waliooana, wakakosana na kuachana, kwa maana ya kuvunja mji. Mji huo huelezewa kwamba umekula makande. Kumbe kula makande ni kuvunja mji, baada ya kukosana kwa waliooana hao. Ndiyo maana watu wakiona watu walioona wamekosana na kuachana, husema kwamba, ‘kaya imekula makande.’
Methali hiyo hufundisha watu walioona juu ya kuacha ugomvi wa kuvunja mji wao, ili waweze kuishi pamoja siku zote za maisha yao.
Yeremia 3:18.
Isaya 50:1.
Malaki 2:14-16.
Ezra 10:3.
ENGLISH: THE FAMILY HAS EATEN MASANGU/ (MIXED MAIZE AND BEANS).
The source of this saying comes from eating cooked grains. The saying can be traced from the female dance where people were accustomed of eating cooked grains (masangu) at the end of the dance. After eating, each one of them could find his/her own way; leave the place. It is through this departure; going back to their respective homes that people can say ‘the family has eaten cooked grains (masangu)’ to mean departure.
The saying can be compared to married people, who appear to quarrel and finally separate. Their separation can be described by the saying that ‘the family has eaten cooked grains (masangu)’ to mean break up in marriage.
The saying teaches people about not involving in quarrelsome acts that may result into break ups in friendship or marriage. In so doing, they will be able to live together in peace and harmony throughout in their lives.
Jeremiah 3:18.
Isaiah 50: 1.
Malachi 2: 14-16.
Ezra 10: 3.