Imbuki ya kahayile kenako ingilile kujigano ja ng’wa Sayayi na Shimba. Ijigano jinijo jihayile giki, Usayayi b’agikenya ni Shimba, uwei upelela mujigulu. Ugingila na usanganijiwa moyi uding’wa ugugulu. Aho oding’wa uwei uhaya giki, ‘wadima nzwi waleka ugugulu.’
Umunashinda aho wigwa chene, ugulekela ugugulu alihaya owilagwa go ng’hana, igiki linzwi. Akoyi akaSayayi kukolob’ela mugati, kub’iza kapila ugubhulagwa. Hunakub’iza kahayile giki, ‘wadima nzwi waleka ugugulu.’
Akahayile kenako kakalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumilaga masala gakwe ijinagwipija umumakoye. Umunhu ng’wunuyo adebhile uguginja amakoye ayo alinago, bho gutumila wiganiki bho masala mingi. Umunhu ng’wunuyo hangi adeb’ile ugubhambilija ab’iye ugugatumila amasala geneyo bhogwipija mumakoye.
Akahayile kenako kalanga bhanhu gumana ugugatumila chiza amasala gabho bho gwipija na gwiyinja mumakoye. Ubhumani bhunubho bhugub’ambilija bhanhu bhingi uguginja amakoye ayo bhalinago.
(1 Samweli 16:18; Mathayo 10:17-18)
KISWAHILI: UMESHIKA MZIZI UKAACHA MGUU.
Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye hadithi ya Sungura na Simba. Hadithi hiyo yaeleza kwamba, Sungura na Simba waligombana. Sungura akakimbia kwenda kujificha kwenye kichuguu. Kabla hajaingia vizuri kwenye kichuguu, Simba alimpata akamshika mguu. Sungura aliposhikwa mguu, alisema hivi, ‘umeshika mzizi ukaacha mguu.’ Simba aliposikia hivyo, alimwachia akifikiri kuwa kweli ni mzizi. Sungura alitokomea ndani akapona au akasalimika. Ndiyo ukawa msemo kwamba, ‘umeshika mzizi ukaacha mguu.’
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule atumiaye akili zake vizuri katika kujitatulia matatizo. Mtu huyo afahamu namna ya kujiondolea matatizo aliyo nayo maishani mwake kwa kutumia akili zaidi. Zaidi ya hayo, mtu huyo huwafundisha pia wengine njia za kujiondolea matatizo yanayowakumba.
Msemo huo hufundisha watu kuelewa namna ya kuzitumia vizuri akili zao katika kujitatulia matatizo maishani mwao. Uelewa huo utawasaidia watu wengi katika kujiondolea matatizo yawakumbayo maishani mwao.
(1 Samweli 16:18; Mathayo 10:17-18).
ENGLISH: YOU GOT HOLD OF A ROOT AND LEFT THE LEG.
The origin of this saying is a tale about the Rabbit and the Lion. The tale has it that the two had a fight. As a result, the Rabbit ran to take cover in an anthill. The Lion chased and caught the Rabbit by the leg before entering the anthill.
When the Rabbit learnt that it had been caught by its leg, it said to the Lion, ‘You got hold of a root and left the leg.’ On hearing that, the Lion thought it was true and, therefore, left the leg thereby allowing the Rabbit to vanish into the anthill and survive his attack. Thereafter, it became a saying, ‘You got hold of a root and left the leg.’
The saying is used comparatively to refer to people who use their brains well in solving problems. Such people know how to get rid of problems they have in their lives by simply using common sense. In addition, such people also teach others how to get out of their problems using their brains.
The saying teaches people about understanding how to use their senses to solve problems in their lives. This understanding will help many people to get rid of the problems they are going through in their lives.
(1 Samuel 16:18; Matthew 10: 17-18).