sayings

323. B’ANENE

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kujisumva ijo jiidilile joyi duhu. Ijisumva jinijo jigikumilijaga joyi bhung’wene, jidahayile akumilijiwe ungi. Hangi jitogilwe jipandike joyi duhu, abhangi bhagayiwe. Hunagwene abhanhu bhagabhitanaga abhanajisumva bhenabho giki, ‘b’anene.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adahayile abhiye b’apandike. Umunhu ng’winuyo ahayile apandike weyi duhu.  Atogilwe gwihaya giki uweyi amanile yose na adugije pye iyose. Agamanaga wikumilija weyi bhung’wene. Hunagwene abhanhu bhagabhitanaga abhanhu bhenabho giki, ‘b’anene.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gulekana na nhungwa ja wiming’holo na wihayi bho sagala, umuwikaji bhobho.

1Timotheo 6:6-10.

Luka 18:9-12.

KISWAHILI: WAMIMI

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye kiumbe ambacho hujijali chenyewe tu. Kiumbe hicho hujisifu chenyewe, hakitaki asifiwe mwingine. Zaidi ya hayo, kinapenda kipate kitu au mafanikio chenyewe tu, wengine wakose. Ndiyo maana watu huviita viumbe kama hivyo, ‘wamimi.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule asiyependa wenzake wapate kitu au mafanikio. Mtu huyo hutaka apate yeye tu. Yeye hupenda kujitapa kwamba ajua yote na aweza yote. Huwa anajisifu mwenyewe kwa sababu ya ubinafsi wake. Ndiyo kusema kwamba, yeye ni mbinafsi. Ndiyo maana watu huwaita watu kama hao kwamba ni ‘wamimi.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuachana na tabia za ubinafsi na uchoyo wa kujidai hovyo, maishani mwao.

1Timotheo 6:6-10.

Luka 18:9-12.

selfish ones

me

 

ENGLISH: EVERYTHING FOR ME

This saying comes from a person that cares about himself or herself only. Such a person will always boast himself/herself and he/she does not want another person to be praised. The person wants only him/her to achieve everything.That is why people call him/her that, “everything for me.”

The saying is compared to someone who does not want others to achieve in life. He/ she only wants to achive alone. He/she likes to boast that he/she knows everything and he/she can do everything. Such a person is proud of himself for his/her selfishness.That is why people call such people “everything for me.”

The saying teaches people to break free from selfish thinking or selfish habits in their lives.

1Timothy 6: 6-10.

Luke 18: 9-12.

322. OCHA KAB’IMBA KANGI

Imbuki ya kahayile kenako yililole ngi. Ingi ulu yutulwa yugwa hasi bho nduhu ugutinwa, igagwaga kakanza kadololo yapimbuka. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ocha kab’imba kangi.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu ulu utulwa mpaga ugwa na gufelwa wikanza liguhi upila. Abhanhu bhagayombaga giki, ‘ocha kab’imba kangi.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka gutula bhanhu bho gubhibhonela umuwikaji bhobho. Hangi yigelelilwe gubhachala kustali abho bhaminyikaga kugiki bhadule gupila wangu.

Waefeso 2:1-4.

KISWAHILI: AMEZIRAI KIMTINGO WA  INZI

Chanzo cha msemo huo chaangalia inzi. Inzi akipigwa na kuanguka bila kupasuka huzirai kwa muda kidogo, baadaye huzinduka. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘amezirai kimtindo wa inzi.’

 Msemo huo hulinganishwa kwa mtu aliyepigwa akaanguka na kuzirai kwa mda mfupi halafu akazinduka. Ndiyo maana watu husema kwa mtu huyo kwamba, ‘amezirai kimtindo wa inzi.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha tabia za kuonea watu kwa namna mbalimbali, zikiwemo zile za kuwapiga. Yafaa pia kuwapeleka hospitalini wale walioumizwa, ili waweze kupona haraka.

Waefeso 2:1-4.

 

girl

vintage2

 

 

ENGLISH: HE/SHE HAS FAINTED IN A FLY’S STYLE

The origin of this saying is the behaviour of flies. When a fly is hit and falls down uncontrollably it lasts for a while then wakes up. That is why people say, “he/she has fainted in a fly’s style.”

The saying is compared to a person who has been hit and faint for a short time and then wake up. That is why people say, “he/she has fainted in a fly’s style.”

The saying teaches people to stop bullying behaviours such as beating others. It is also necessary to rush a person to hospital if he/she is injured so that he/she can recover quickly.

Ephesians 2: 1-4.

 

313. WAGOBYA NILO (B’ULILO)

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhuchoji bho jiliwa. Ijiliwa jinijo jigategagwa, guti ndimu nulo ndilo. Uluojigobya unchoji ojo ng’wunuyo agayegaga, uweyi kihamo na bhiye. Hunagwene abhiye bhagang’wilaga giki, ‘wagobya nilo (b’ulilo).’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo opandikaga milimo ya gung’wenhela jiliwa. Umunhu ng’wunuyo agayegaga noyi ulu oyipandika imilimo yiniyo, kunguno ya b’upandiki bhokwe, bho aho ng’wagulila ijiliwa. Abhazenganwa bhakwe nabho bhagayegaga ugumona ng’wichabho opandikaga aho ng’ wagulila ijiliwa. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagang’wilaga giki, ‘wagobya nilo (b’ulilo).

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guchola milimo ya gubhenhela jiliwa, na guyega kihamo ulu bhayipandika imilimo yiniyo.

1Wakorintho 9:13-14.

KISWAHILI: UMEKAMATA PA KULIA

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye utafutaji wa chakula. Chakula hicho hupatikana kwa njia mbalimbali zikiwemo zile za kutafuta kazi, kuvua samaki, kuwinda wanyama na kuwatega kwa mtego. Akipata chakula hicho mtu huyo hufurahi sana, yeye pamoja na wenzake. Ndiyo maana wenzake humwambia kwamba, ‘umekamata pa kulia.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule aliyepata kazi ya kumletea chakula. Mtu huyo hufurahi sana apatapo kazi hiyo, kwa sababu kazi hiyo humletea chakula. Majirani zake nao pia hufurahi kumuona mwenzao amepata pa kulia. Ndiyo maana watu hao, humwambia hivi, ‘umekamata pa kulia.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kutafuta kazi za kuwaletea chakula, na kufurahi kwa pamoja wazipatapo kazi hizo.

1Wakorintho 9:13-14.

buffalo

 

ENGLISH: YOU TRAPPED SOMETHING TO EAT

The source of this saying is a search for food. Such food is available by trapping animals or fishing. When someone finds such food he/she becomes very happy with his/her companions. That is why his/her companions can tell him/her, “you have trapped something to eat.”

The saying is compared to a person who got a new job that will bring him or her food. Such a person becomes very happy when he/she gets such a job. The neighbours of that person also become happy for him/her. That is why those people can say, ‘you have trapped something to eat.’’

The proverb teaches people about finding jobs that can bring them food and make them happy.

1 Corinthians 9: 13-14.

309. NANGULO GO MVA

Imbuki ya kahayile kenako ingilile kukikalile kamva. Imva igikalaga igashije duhu, kunguno idajaga nulu kumilimo. Aliyo ijiliwa igalyaga duhu, bho nduhu nugumana nuko jigafumilaga ilijiwa jinijo, kunguno iyoyi igikalaga ifulile duhu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘nangulo go mva.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agikalaga wigashije bho nduhu ninga gutumama milimo. Umunhu ng’wunuyo agalenganijiyagwa nimva, kunguno nanghwe adajaga ukunimo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘nangulo go mva.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gub’iza na nhungwa ja gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule abhanhu bhenabho, ugujenhela maendeleo ikaya jabho.

2Wathesalonike 3:10-11.

KISWAHILI: PUMZIKO LA MBWA

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye maisha ya mbwa. Mbwa huishi bila kufanya kazi, Yeye hupumzika tu, kwa sababu haendi wala kazini. Lakini chakula huwa anakula tu bila kuelewa kule kilichotoka chakula hicho, kwa sababu yeye huishi kwa kupumzika tu. Ndiyo maana watu husema, ‘pumziko la mbwa.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huishi kwa kukaa bila kwenda kufanya kazi. Mtu huyo hulinganishwa na mbwa, kwa sababu naye huwa hafanyi kazi. Ndiyo maana watu humwita, ‘pumziko la mbwa.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii ili watu hao waweze kuziletea maendeleo familia zao.

2Wathesalonike 3:10-11.

dog3

dog2

ENGLISH: A DOG NEVER WORK, YET IS SATISFIED

This proverb originates from the dog’s life. The dog does not work. It spends most of its life resting. It also eats food without knowing where that food comes from. That is why people say, “a dog never work, yet is satisfied.”

The saying is compared to a person who lives by doing nothing. Such person is likened to a dog because he/she does not work but he/she is contented with such life. That is why people tell him, “a dog never work, yet is satisfied.”

The saying discourages people from living without work. They should work hard so as to improve their lives and their families.

2Thessalonians 3: 10-11.

305. GUNANGA GULU GUSHIGA UNSHINDIKE

Imbuki ya kahayile kenako ingilile kuli munhu uyo unangaga munhu uyo aligulu. Umunhu ng´wunuyo, agadebha igiki, ugulu ng´wunuyo adelelwa ulu adakumiwe nang´hwe. Aho onkumya, agabhona igiki ugulu ng´wunuyo aliidebha iyo aling´wila, kunguno agalab´ula ukuli unangi, uyo agatumila makono ugunanga mpaga welelwa, ugulu ng´wunuyo. Hunagwene abhanhu bhagayomba giki, ´gunanga gulu gushiga unshindike.´

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile nzila ningi ija gubhalanga abhanhu abho bhalina jika, umuwikaji bhobho. Umunhu ng´wunuyo agabhalangaga na bhanhu bhakwe ahigulya ya gujitumila inzila jinijo, kugiki bhajidebhe nabho, bhogubhawila giki, ´gunanga gulu gushiga unshindike.´

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gub´iza na nzila ningi ijagudula gubhalangija abhanhu bhabho abho bhali na jika, umuwikaji bhobho.

Wagalatia 3:1-3.

Luka 7:31-32.

KISWAHILI: KUMFUNDISHA BUBU MPAKA UMSUKUME

Chanzo cha msemo huo chatokea kwa mtu aliyekuwa anamfundisha mtu aliyekuwa bubu. Mtu huyo aligundua kwamba, bubu huyo asingekielewa kile alichokuwa akimfundisha, bila kumgusa mwenyewe. Alipomgusa, mtu huyo aliyekuwa bubu, alianza kuelewa kile alichokuwa akimfundisha, kwa sababu baada ya kumgusa aligeuka kumwangalia, naye akamweleza kwa kutumia ishara za mikono. Ndiyo maana watu husema kwamba, ´kumfundisha bubu mpaka umsukume.´

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu ambaye afahamu njia nyingi za kuwafundishia watu wenye vilema mbalimbali, maishani mwao. Mtu huyo huwafundisha pia wenzake juu ya njia hizo kwa kuwaambia kwamba, ´kumfundisha bubu mpaka umsukume.´

Msemo huo hufundisha watu juu ya kutumia njia nyingi za kuweza kuwafundishia watu wenye ulemavu mbalimbali, maishani mwao, ili waweze kuufikisha vizuri ujumbe wao kwao.

Wagalatia 3:1-3.

Luka 7:31-32.

women

mute

ENGLISH: TEACHING A DEAF PERSON, YOU NEED TO TOUCH HIM/HER

This saying originates from a person who was teaching a deaf person. The teacher realized that the deaf could not understand what he/she was teaching without touching him/her. When the teacher touched him/her, he/she began to understand the teachings because, after he/she had touched him/her, he/she turned to look at the teacher and the teacher explained to him/her by using gestures. That is why people say, “Teaching a deaf person, you need to touch him/her.”

The saying is compared to someone who knows different ways of teaching people with disabilities. Such a person also teaches his/her companions about these ways by telling them, “Teaching a deaf person, you need to touch him/her.”

The above saying teaches people about using different ways of teaching people with disabilities so that they can understand the subject.

Galatians 3: 1-3.

Luke 7: 31-32.