proverbs

264. GWEJA MINO DAHOYA.

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile mino ga bhanhu bhab’ili abho bhalihoya. Umumahoya gabho geneyo, bhagab’izaga bhisekela guti giki bhalolecha mino, kunguno bhuling’wene aligabhona amino ga ng’wiye, aliyo iyoilihoyi umugati yakwe umunhu ng’wunuyo, uungi adudula uguibhona. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘gweja mino dahoya.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agikalaga usekela bhanhu bho golecha mino duhu ukubhoyi, aliyo umung’holo yakwe agab’izaga apelanile na adabhatogilwe abhiye. Umunhu ng’wunuyo agayombaga mihayo ya wiza, aliyo umung’holo yakwe, aliganika gwita mihayo yabhub’i ukubhiye. Umumahoya genayo, abhiye bhagayombaga giki, ‘gweja mino dahoya.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu  gubhatogwa abhanhu abho bhalihoya nabho. Ubhutogwa bhunubho bhugubhambilija abhanhu bhenabho ijinagwikala bho mholele na bhananzendo bhichab’o.

(Yohana 2: 2:23 – 225)

KISWAHILI: KWA WEUPE WA MENO, TUMEONGEA.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia meno ya watu wawili wanaoongea pamoja. Katika maongezi yao hayo, watu hao huwa wakioneshana meno kwa kuchekeana kana kwamba wanaonesha meno, kwa sababu kila mmoja huona meno ya mwenzake, lakini hawezi kuona mawazo yaliyomo moyoni mwa mwenzake huyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kwa weupe wa meno, tumeongea.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa akiwachekelea watu kwa kuonesha kwao meno tu, lakini huwa amekasirika moyoni mwake na hapendi wenzake. Katika maongezi hayo wenzake humwambia hivi, ‘weupe wa meno tumeongea.

Methali hiyo hufundisha watu  kuwapenda wenzao wanaoongea nao. Upendo huo utawasaidia watu wao katika kuishi kwa amani na wanakijiji wenzao kwa ajili ya kujiletea maendeleo mengi maishani mwao.

(Yohana 2: 2:23 – 225).

angolan

ENGLISH: BY THE WHITENESS OF THE TEETH, WE HAVE HAD A GREAT TALK.

The origin of this proverb is the teeth of two people talking together. In their conversations, these people expose their teeth as if they were displaying them, because they see each other’s teeth, but they cannot see the thoughts that are in each other’s heart. That is why people say, ‘By the whiteness of the teeth, we have had a great talk.’

The proverb is used comparatively with reference to people who make fun of other people by just showing their teeth, but they are angry deep inside their hearts and they do not like their colleagues. In conversations, their colleagues who suspect their hypocricy tell them, ‘By the whiteness of the teeth, we have had a great talk’.

The proverb teaches people to love the people they talk to. This love will help their people live in peace with their fellow villagers for the sake of improving their lives in various ways.

(John 2: 2:23 – 225).

263. NINENILE IMBUGA.

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile mbuga iyo munhu aliibhitila. Umunhu ng’wunuyo agasiminzaga lugendo lulihu umumbuga yiniyo. Hangi iganojaga kunguno ya wingi bho masalu umo gagamanaga gulibhila amagulu gakwe. Imbuga yiniyo iganojaga noyi umunhu ng’wunuyo. Ulu oyifuma imbuga yiniyo agayegaga noyi. Hunagwene agayombaga giki, ‘ninenile imbuga.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo olimumakoye ahashigu ijojab’itile. Ihaha lulu wingile umumakoye genayo, alimugati ya bhuyegi bhutale. Umunhu ng’wunuyo agabhalomelaga abhiye igiki ogamalile amakoye genayo. Alimubhuyegi bho gulumbilija giki okindile chiza. Hunagwene, agayombaga giki, “ninenile imbuga”. Ukwene huguhaya giki ogamalile amakoye ayo gankoyaga, wandije guyega duhu ihaha.

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu gwiyumilija gutumama milimo na bhukamu bhutale, kugiki bhapandike matwajo mingi umuwikaji bhobho. Ulu bhalagapandike amatwajo genayo, bhuling’wene aguhaya nawe giki, ‘ninenile imbuga.’

(2Timotheo 2:9-11; 2Timotheo 4:7-8).

KISWAHILI: NIMEIVUKA MBUGA.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia mbuga ambayo mtu anatembea juu yake. Mtu huyo hutembea kwa mwendo mrefu kwenye mbuga hiyo kwa sababu ya ukubwa wake. Zaidi ya hayo, yeye huchoka kwa sababu ya wingi wa mchanga uliomo ndani yake ambao huifanya miguu yake ididimie kwenye mchanga huo. Mbuga hiyo huzidi kumchosha sana mtu huyo. Hivyo akiimaliza mbuga hiyo mtu huyo atafurahi sana. Ndiyo maana yeye husema kwamba, ‘nimeivuka imbuga.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye alikuwa kwenye matatizo makubwa siku zilizopita. Hivyo kwa sasa yuko kwenye furaha kubwa kwa sababu emeyamaliza matatizo yale. Anafanana na mtu aliyeivuka mbuga hiyo kubwa na ndefu. Mtu huyo huwasimulia wenzake kwamba alikuwa na matatizo makubwa, lakini sasa amayamaliza. Ameshinda hivyo anafurahia ushindi huo. Ndiyo maana mtu huyo husema kwamba, ‘nimeivuka mbuga.’ Ndiyo kusema kuwa, ameyamaliza matatizo yaliyokuwa yakimsumbua, kwa sasa anafurahia ushindi huo.

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuvumilia katika kufanya kazi kwa bidii kubwa ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao. Wakiyapata mafanikio hayo kila mmoja atasema hivi, ‘nimeivuka mbuga.’

(2Timotheo 2:9-11; 2Timotheo 4:7-8).

 

desert

ENGLISH: I HAVE CROSSED THE PLAIN.

The origin of this proverb is a plain on which someone was walking. Such a person had a long walk from one side of the plain to the other because of its humongous size. A person walking on a humongous plain gets tired because of its size and the amount of mud that keeps his/her feet sinking into the plain. As such, the plain is very tiring. Thus, when the person finishes the journey to cross it will be very happy. That’s why he/she says, ‘I have crossed the plain.’

The proverb is comparatively used with reference to a person who was in serious trouble in the past and is now in great joy because he/she has solved the problem. He/she is like a person who crossed a vast plain. The person tells his/her colleagues that he/she had serious problems, but he/she has now gone them and it is all the past. He has won so he enjoys the victory. That is why the man says, ‘I have crossed the park.’ That is, he has solved the problems that were bothering him, and now he enjoys the victory.

The proverb teaches people to persevere in working hard so that they can get the most out of their lives. When they achieve that, everyone will say, ‘I have crossed the park.’

(2Timothy 2: 9-11; 2Timothy 4: 7-8)

262. WADUDIMILA HIBAMBASI

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile ndimi o mitugo. Undimi ng’wunuyo agajichilulaga imitugo jinijo ogatuula hibala ilya nduhu amaswa. Ahenaho ilihang’wape guti hibambasi. Imitugo jinijo jigashogaka kaya jidigutile, kunguno jadimilagwa hibambasi. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga undimi ng’wunuyo giki, ojidimilaga hibambasi. Mumho ojishoshaga kaya imitugo jinijo jidigutule.

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagazugilagwa jiliwa bhalya aliyo bhakija ugwiguta. Unzugi obho agikolaga nu ndimi uomitugo uyo ojidimilaga hibambasi jukija ugwiguta. Hunagwene abhanhu bhenabho abho bhakijaga ugwiguta ijiliwa, bhagang’wilaga unzugi obho giki, ‘wadudimila hibambasi.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu  gubhagola chiza abhanhu bhabho. Ubhugoji bhunubho bhulikihamo na gub’inha jiliwa ja gubhatosha abhanhu bhabho, na gub’inha malezi gagubhatosha abhana bhabho gub’iza na kikalile kawiza umuwikaji bhobho.

(Yohana 10:11-13; Ezekiel 34:1-2).

KISWAHILI: UMETUCHUNGIA KWENYE ARDHI TASA.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia mchungaji wa mifugo. Mchungaji huyo huwachungia mifugo wake kwenye eneo jeupe, yaani, lisilo na majani. Hapo ni peusi kama kwenye bambasi au sehemu isiyoota nyasi. Mifugo hao hurudi nyumbani bila kushiba kwa sababu wamechungiwa kwenye bambasi. Ndiyo maana watu husema kwamba, amewachungia kwenye bambasi. Maana yake mifugo hao hawajashiba.

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wale ambao huwapikia chakula kisichowatosha watu wao. Hao ni watu wasiowapatia watu wao mahitaji ya kutosha kuwawezesha kuishi inavyotakia. Watu hao hufanana na mchungaji wa mifugo awachungiaye mifugo wake kwenye bambasi wakashindwa kushiba. Ndiyo maana watu hao, ambao hawajashiba chakula, humwambia mpishi wao kwamba, ‘umetuchungia kwenye bambasi.’

Methali hiyo hufundisha watu  kuwatunza vizuri watu wao, wakiwemo wafanyakazi na watoto wao. Matunzo hayo yatawasaidia wafanya kazi wao katika kupata haki zao vizuri, na watoto wao kupata malezi yawezayo kuwajengea tabia njema maishani mwao.

Yohana 10:11-13.

Ezekiel 34:1-2.

 

burkina-children

ENGLISH: YOU HAVE GRAZED US ON A BARREN LAND.

The origin of this proverb is a herdsperson. The person grazed his flock on a plain land with barren vegetation. This is usually a grass-free place and, therefore, not suitable for pasture. Thus, the animals returned home hungry and unsatisfied because they had been grazed on a barren vegetation area. That is why people, usually unsatisfied, say, ‘you have grazed us on a barren land’. It means that they have not have not been satisfied.

The proverb is used to tell those who cook inadequate food for their people. They are people who do not provide enough food for their people to survive. These people are like a herdsman who grazes his herds on a barren land. That is why unsatisfied people tell their cooks, ‘you have grazed us on a barren land.’

The proverb teaches people about taking good care of their people, including workers and their children. This care will help the workers have free access to their rights, and their children to receive training for building their future lives.

John 10: 11-13.

Ezekiel 34: 1-2.

261. WADIMA NZWI WALEKA UGUGULU.

Imbuki ya kahayile kenako ingilile kujigano ja ng’wa Sayayi na Shimba. Ijigano jinijo jihayile giki, Usayayi b’agikenya ni Shimba, uwei upelela mujigulu. Ugingila na usanganijiwa moyi uding’wa ugugulu. Aho oding’wa uwei uhaya giki, ‘wadima nzwi waleka ugugulu.’

Umunashinda aho wigwa chene, ugulekela ugugulu alihaya owilagwa go ng’hana, igiki linzwi.  Akoyi akaSayayi kukolob’ela mugati, kub’iza kapila ugubhulagwa. Hunakub’iza kahayile giki, ‘wadima nzwi waleka ugugulu.’

Akahayile kenako kakalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumilaga masala gakwe ijinagwipija umumakoye. Umunhu ng’wunuyo adebhile uguginja amakoye  ayo alinago, bho gutumila wiganiki bho masala mingi. Umunhu ng’wunuyo hangi adeb’ile ugubhambilija ab’iye ugugatumila amasala geneyo bhogwipija mumakoye.

Akahayile kenako kalanga bhanhu  gumana ugugatumila chiza amasala gabho bho gwipija na gwiyinja mumakoye. Ubhumani bhunubho bhugub’ambilija bhanhu bhingi uguginja amakoye ayo bhalinago.

(1 Samweli 16:18; Mathayo 10:17-18)

KISWAHILI: UMESHIKA MZIZI UKAACHA MGUU.

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye hadithi ya Sungura na Simba. Hadithi hiyo yaeleza kwamba, Sungura na Simba waligombana. Sungura akakimbia kwenda kujificha kwenye kichuguu. Kabla hajaingia vizuri kwenye kichuguu, Simba alimpata akamshika mguu. Sungura aliposhikwa mguu, alisema hivi, ‘umeshika mzizi ukaacha mguu.’ Simba aliposikia hivyo, alimwachia akifikiri kuwa kweli ni mzizi. Sungura alitokomea ndani akapona au akasalimika. Ndiyo ukawa msemo kwamba, ‘umeshika mzizi ukaacha mguu.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule atumiaye akili zake vizuri katika kujitatulia matatizo. Mtu huyo afahamu namna ya kujiondolea matatizo aliyo nayo maishani mwake kwa kutumia akili zaidi. Zaidi ya hayo, mtu huyo huwafundisha pia wengine njia za kujiondolea matatizo yanayowakumba.

Msemo huo hufundisha watu  kuelewa namna ya kuzitumia vizuri akili zao katika kujitatulia matatizo maishani mwao. Uelewa huo utawasaidia watu wengi katika kujiondolea matatizo yawakumbayo maishani mwao.

(1 Samweli 16:18; Mathayo 10:17-18).

 

african lion

rabbit

ENGLISH: YOU GOT HOLD OF A ROOT AND LEFT THE LEG.

The origin of this saying is a tale about the Rabbit and the Lion. The tale has it that the two had a fight. As a result, the Rabbit ran to take cover in an anthill. The Lion chased and caught the Rabbit by the leg before entering the anthill.

When the Rabbit learnt that it had been caught by its leg, it said to the Lion, ‘You got hold of a root and left the leg.’ On hearing that, the Lion thought it was true and, therefore, left the leg thereby allowing the Rabbit to vanish into the anthill and survive his attack. Thereafter, it became a saying, ‘You got hold of a root and left the leg.’

The saying is used comparatively to refer to people who use their brains well in solving problems. Such people know how to get rid of problems they have in their lives by simply using common sense. In addition, such people also teach others how to get out of their problems using their brains.

The saying teaches people about understanding how to use their senses to solve problems in their lives. This understanding will help many people to get rid of the problems they are going through in their lives.

(1 Samuel 16:18; Matthew 10: 17-18).

260. GUCHING’WA NO IDI GUCHA.

Imbuki ya lusumo lunulo ingilile kuli munhu uyo ochimagwa ginhu jugi, guti linti, nulu ichimu na bhibhoneji hakaya yakwe. Umunhu ng’unuyo aguminyika kunguno ya kupandika ilonda aho ochimilagwa.  Aliyo lulu, umunhu ng’unuyo, idigiki agucha duhu, kunguno adulile gulagulwa ililonda linilo mpaga nulu lyupila. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘guching’wa no idi gucha.’

Ulusomo lunulo lugalenganijiwa kubhanhu abho bhagabhadililaga bhasadu bhabho bho gubhachala kusibhitali, bhagapandika bhugota bho gudula gubhapija wangu, kugiki bhadule gwendelea kutumama milimo yabho chiza.

Abhanhu bhenab’o bhagab’izaga na bhutogwa bhutale kubhichab’o. Gub’itila bhutogwa bhunubho bhagadulaga gubhambilija abhanhu bhabho bho kutumila nulu sabho jabho. Bhagitaga giko, kunguno bhamanile igiki, ‘guching’wa no idi gucha.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu kudilila bhanhu abho bhali na makoye, guti ga bhusadu na gangi, kugiki bhadule gupila wangu. Ubhudiliji bhunubho bhugubhambilija bhanhu bhingi abho bhali makoye guti ga bhusadu, uguginja wangu.

KISWAHILI: KUCHOMWA MNO SI KUFA.

Chanzo cha methali hii ni mtu aliyechomwa na kitu chenye ncha kali, kama vile mti au mkuki na watu waonevu, akiwa nyumbani kwake. Mtu huyo huumia kwa sababu ya hupata jeraha kwenye sehemu aliyochomwa na kitu hicho. Hata hivyo, mtu huyo aweza kutibiwa jeraha hilo mpaka akapona vizuri. Kuchomwa hadi kupata jeraha kama hilo si kwamba kutatamsababishia kifo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kuchomwa mno si kufa.’

Methali hii hulinganishwa kwa watu wenye upendo wa kuwajali wagonjwa kwa kuwapeleka hospitalini ili wakapatiwe matibabu ya kuwawezesha kupona haraka ya kutosha kuendelea na kazi zao vizuri.

Upendo walio nao watu hao huwawezesha kuwatatulia watu hao matatizo yao kwa sababu kupitia upendo huo, watu hao hufikia hata hatua ya kutumia mali zao katika kuwawezesha watu wao kupona haraka magonjwa au majereha ya aina mbalimbali.  Watu hao hufanya hivyo kwa sababu wafahamu kwamba, ‘kuchomwa mno si kufa.’

Methali hiyo hufundisha watu  kuwa na upendo wa kuwajali watu walio na matatizo mbalimbali, yakiwemo yale ya ugonjwa na mengine, ili waweze kupona haraka. Upendo huo utawawezesha watu hao kutatua matatizo ya watu wengi wanaohitaji msaada huo.

sickness sadness-

spear

ENGLISH: TO BE STABBED HARD IS NOT TO DIE.

The origin of this proverb is a person who got pireced with a sharp object such as a pointed tree branch or a spear at his or her home by cruel people and got badly wounded. Such wounded person could be treated and got well again. Thus, being stabbed does not necessarily translate to one’s death. That is why people say, ‘to be stabbed hard is not to die.’

The proverb is comparatively used to encourage people who take care of the sick by taking them to the hospital for treatment to enable them recover quickly enough to healthly continue with their jobs.

The love that these people have allows them to solve other peoples’ problems. Through that love, these people even go as far as using their resources to facilitate other peoples’ quick recovery from various illnesses, wounds or injuries. These people do this because they know that ”to be stabbed hard is not to die.’

The proverb teaches people to show love to people with a variety of problems, including those of illness and others, so that they can recover quickly. Such love will enable those people to solve problems of many needy people.