Joe Healey

544. JILUTULA MBANGA.

Imbuki ya kahayile kenako yingile ku jisumva ijo jili na nguzu umukikalile kajo. Ijisumva jinijo, jigabhitaga hosehose kunguno ya nguzu jajo. Hunagwene abhanhu bhagajitanaga giki, ‘jilutula mbanga.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo midimu bho wiyumilija mpaga oyimala. Umunhu ng’wunuyo adulile nulu gusenga ipolu lya manti matale mpaka upandika ngunda goguyulima hoyi jiliwa. Uweyi agalimaga migunda mitale iyo idulile gubhalisha bhanhu bhingi umuwikaji bhobho.

Umunhu ng’wunuyo agabhizaga jigemelo ukubhiye ja gutumama milimo bho bhukamu bhutale, kunguno ya bhukalalwa bhokwe ubho gutumama milimo bho gwiyambilija chiza na bhiye. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, ‘jilutula mbanga.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu gujitumila inguzu jabho bho gwigulyambija gutumama milimo yabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho umukikalile kabho.

(Kutoka 7:8-13; 1Wafalme 18:20-39; Matendo ya mitume 8:9-25).

KISWAHILI: BINGWA WA MAPAMBANO.

Chanzo cha msemo huu chaangalia kiumbe kile ambacho kina nguvu maishani mwake. Kiumbe hicho hupita popote pale kwa sababu ya nguvu zake hizo. Ndiyo maana watu hukiita ‘bingwa wa mapambano.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi ngumu kwa uvumilivu hadi kuzimaliza. Mtu huyo anaweza hata kufyeka pori lenye miti mikubwa mpaka akapata shamba la kulimia mazao yake. Yeye hulima mashamba makubwa ambayo humwezesha kuwalisha watu wengi katika maisha yake.

Mtu huyo huwa mfano wa kuigwa na wenzake katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa sababu ya kupenda kwake kufanya kazi kwa kusaidiana na wenzake. Ndiyo maana watu humwita, ‘bingwa wa mapambano.’

Msemo huu hufundisha watu kuzitumia nguvu zao kwa kusaidiana katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao katika maisha yao.

(Kutoka 7:8-13; 1Wafalme 18:20-39; Matendo ya Mitume 8:9).

ferry-of zambia

worker1

 

ENGLISH: A WAR CHAMPION.

The origin of this saying is a powerful creature. That creature passes anywhere because of its powers. That is why people call it ‘A war champion.’

The saying is used comparatively to refer to any individual who works hard patiently for the purpose of finishing it. The individual may even clear a forest to get a farm for cultivating crops. The individual cultivates large fields, which enables him/her to feed many people.

Such a person becomes a role model for his or her colleagues in the execution of their responsibilities, because of their willingness to work in support of their colleagues. That is why people call him/her, ‘A war champion.’

The saying teaches people how to use their power to help each other in fulfilling their responsibilities, so that they can better support their families in their lives.

(Exodus 7: 8-13; 1Kings 18: 20-39; Acts 8: 9).

543. SUHA YA BHUKI IDAMALAGA BHUNONU.

Imbuki ya kahayile kenako, yilolile bhuki. Ubhuki bhunubho bhuli bhunonu noyi, nulu bhugatulwa musuha, isuha yiniyo igunona nayo, kunguno ubhuki bhugamililaga umugati yayo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘suha ya bhuki idamalaga bhunonu.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina nhungwa ja wiza umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agayombaga mihayo ya wiza, kunguno yigenhaga mholele ya gwitogwa na bhiye umumahoya gakwe.

Imihayo yakwe yiniyo igabhizaga minonu guti bhuki, kunguno idasukaga ukubhadegeleki bhayo. Abhanhu bhagikalaga na ng’humbu ya gundegeleka umunhu ng’wunuyo, kugiki bhadule guyimana iyo aliiyombaga. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘suha ya bhuki idamalaga bhunonu.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu gubhiza na nhungwa ja wiza umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho umuwikaji bhobho.

(1Wakorintho 16:13-14; Zaburi 119:89-91).

KISWAHILI: KIBUYU CHA ASALI HAKIISHIWI UTAMU.

Chanzo cha msemo huu chaangalia uwekaji wa asali kwenye kibuyu. Asali ni tamu sana, hata ukiiweka kwenye kibuyu, utamu wake utabakia humo kwa sababu huwa inang’ang’ania ndani yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kibuyu cha asali hakiishiwi utamu.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye, ni mwenye tabia njema katika maisha yake. Mtu huyo huongea maneno mazuri yenye amani na upendo kwa wenzake katika maongezi yake.

Maneno hayo huwa matamu kama asali, kwa sababu huwa hayaishiwi utamu wake kwa wasikilizaji wake. Watu huwa na hamu ya kuendelea kumsikiliza mtu huyo, ili waweze kuyaelewa yale anayoyaongea. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘kibuyu cha asali hakiishiwi utamu.’

Msemo huu hufundisha watu kuwa na tabia njema katika namna yao ya kuishi kwao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao maishani mwao.

(1Wakorintho 16:13-14; Zaburi 119:89-91).

honey-bhuki

ENGLISH: A HONEYCALABASH NEVER LACKS SWEETNESS.

The origin of this saying is storage of honey in a calabash. Honey is very sweet, even if you put it in a syrup, its sweetness will remain there because it sticks in it. That is why people say, ‘Honeycalabash never lacks sweetness.’

The saying is used comparatively to refer to any person with good character in life. That person speaks sweet words of peace and love to his/her fellows in his/her conversation. These words are as sweet as honey, because they are not confined to their audience. People are eager to keep listening to that person, so they can understand what he or she is saying. That is why people tell him, ‘Honeycalabash never lacks sweetness.’

The saying teaches people to be good in their ways of living, so that they can live in harmony with others.

(1Corinthians 16: 13-14; Psalm 119: 89-91).

542. LUGENGO LO SHIMBA YOMBO MUNZENGO.

Imbuki ya kahayile kenako yilolile shimba. Ishimba ili ndimu iyo iling’hali noyi umukikalile kayo. Iyoyi uluyingila mulugali gwikolela jiliwa, igabhizaga yombo nhale umuchalo jinijo, kunguno ya makanji gayo. Igikindikaga nulu mulugutu yapula ng’ombe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki ‘lugendo lo shimba yombo munzengo.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhizaga nsambo umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agabhinzaga milyango ya bhanhu, wingila gwibha sabho jabho. Uweyi ulu wibha jikolo ja bhanhu, yigabhizaga yombo umunzengo, guti ni shimba iyo igenhaga yombo bho gupula mitugo ja bhanhu umuchalo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘lugendo lo shimba yombo munzengo.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu guleka kajile kawibhi umukikalile kabho, kugiki bhadizenha yombo umunzengo gobho umuwikaji bhobho.

(Matendo ya Mitume 9:19-25; Mithali 4:10-18).

KISWAHILI: SAFARI YA SIMBA KELELE KIJIJINI.

Chanzo cha msemo huu chaangalia simba. Simba ni mnyamapori ambaye ni mkali sana maishani mwake. Yeye akiingia kwenye zizi kujitafutia chakula, husababisha kelele kubwa kwenye kijiji hicho, kwa sababu ya hali yake hiyo ya kutisha. Mnyama huyo hurukia hata zizini na kuchukua ng’ombe. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘safari ya simba kelele kijijini.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni jambazi katika maisha yake. Mtu huyo huvunja milango ya watu na kuingia kuiba mali zao, maishani mwake.

Yeye akiiba vitu vya watu, husababisha kelele kijijini, kama simba aletavyo kelele anapochukua ng’ombe kijijini. Ndiyo maana watu husema, ‘safari ya simba kelele kijijini.’

Msemo huu hufundisha watu kuacha mwenendo wa wizi, katika maisha yao, ili wasisababishe kelele katika vijiji vyao, maishani mwao.

(Matendo ya Mitume 9:19-25; Mithali 4:10-18).

shimba

ENGLISH: A LION’S TRIP IS A COMMOTION IN THE VILLAGE.

The origin of this saying is a lion. The lion is the most fierce animal in its life. When it goes to hunt, it causes a lot of commotion in the village, because of its scary condition. The animal even jumps into barns and takes livestock. That is why people say, ‘a lion’s trip is a commotion in the village.’

The saying is used comparatively to refer to any who is a gangster in his/her life. The person breaks into people’s properties and steal belongings. When he/she steals people’s belongings, they cause a commotion in the village, just as when the lion visits a village a takeslivestock. That is why people say, ‘a lion’s trip is a commotion in the village.’

The saying teaches people refrain from the practice of robbery, so as not to cause commotion in their villages.

(Acts 9: 19-25; Proverbs 4: 10-18).

541. ULU ULI DIDI IYO ULAIPANDIKE UGWIMALA BHEBHE NG’WINIKILI.

Imbuki ya kahayile kenako yilolile mafumilo ga ng’wa didi. Udidi jilijisumva ijo jili na nhinda ya gulema gwigwa mihayo ya wiza iyo jigawilagwa na bhichajo. Ijoyi jigacholaga ndebho bho gubhikolosha abhangi umukikajile kajo. Uwikolosha bhunubho bhugajenhelejaga guminyiwa nabho jigabhikoloshaga. Hunagwene abhanhu bhagajiwilaga giki ‘ulu uli didi iyo ulaipandike ugwimala bhebhe ng’winikili.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinchoji o ndebho uumukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agabhikobyaga abhiye bho gubhitila mihayo ya bhubhi.  Uweyi agikalaga upandika mamihayo ng’hangala nyingi, kunguno ya bhudidi bhokwe ubho bhugabhenhelejaga na bhiye gupandika makoye umuwikaji bhobho.

Umunhu ng’wunuyo agabhizaga alemile uguhang’wa na bhiye. Abhanhu abho bhagang’hamaga olema ugubhazunilija bhaganekaga wibhegeje weyi ulu opandikaga makoye, kunguno obhanoja. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagang’wilaga giki, ‘ulu uli didi iyo ulaipandike ugwimala bhebhe ng’winikili.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu guleka bhuchoji bho ndebho, nulu wikomya ukubhichabho, kugiki bhadule gwikala bho gujilanija chiza na bhichabho umuwikaji bhobho.

(Yoshua Bin Sira 27:25-27; Yoshua Bin Sira 32:18-19; Zaburi 7:16-17).

KISWAHILI: UKIWA MTUKUTU YATAKAYOKUPATA UTAYAMALIZA MWENYEWE.

Chanzo cha msemo huu chaangalia matokeo ya asiyesikia. Asiyesikia ni kiumbe chenye kiburi cha kukataa kusikia maneno yaliyo mema yatokayo kwa wenzake. Kiumbe hicho ni kitukutu kwa kuwa hutafuta uchokozi kwa wenzake kinapoishi. Uchokozi huo hukisababishia kuumizwa na wale kinaowachokoza. Ndiyo maana watu hukiambia kwamba, ‘ukiwa mtukutu yatakayokupata utayamaliza wewe mwenyewe.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutafuta uchokozi katika maisha yake. Mtu huyo huwachokoza wenzake kwa kuwatendea maovu. Yeye hupata matatizo mara nyingi, kwa sababu ya kiburi chake ambacho pia huwasababishia wenzake kuingia kwenye matatizo. Mtu huyo huwa hataki kuonywa na wenzake. Watu wanaomuonya na kuwakatalia, humuacha ajitatulie mwenyewe matatizo aliojiletea, kwa sababu ya yeye kuwachosha watu hao. Ndiyo maana wao humwambia kwamba, ‘ukiwa mtukutu yatakayokupata utayamaliza wewe mwenyewe.’

Msemo huu hufundisha watu kuacha kutafuta uchokozi kwa wenzao, ili waweze kuishi kwa kuelewana vizuri na watu wengine maishani.

(Yoshua Bin Sira 27:25-27; Yoshua Bin Sira 32:18-19; Zaburi 7:16-17).

ligusha na nzoka

pingu

 

ENGLISH: IF YOU ARE NAUGHTY, YOU WILL DEAL WITH WHATEVER BEFALLS YOU.

The origin of this saying is a person that is never told. Such a person refuses to listen to good advice from others. The person seeks out aggression from others by provoking them. The aggression, in turn, hurts the him/her and his/her company. That is why people tell him/her, ‘if you are naughty, you will deal with whatever befalls you.’

The saying is used comparatively to refer to a provocative person. The person annoys others by by provoking them and when they harm him they also do so to his/her companions. Such an individual often gets into trouble, because of his/her pride, which also causes his colleagues to get into troubles.

That person doesn’t want to be warned by his/her colleagues. Therefore they leave him alone to deal with whatever problem arising from his/her provocation to others. That is why they tell him/her, ‘if you are naughty, you will deal with whatever befalls you.’

This saying teaches people to refrain from aggression, so that they can live in harmony with other people in their lives.

(Joshua Bin Sira 27: 25-27; Joshua Bin Sira 32: 18-19; Psalm 7: 16-17.

540. LYAMOLOLO.

Imbuki ya kahayile kenaka yingilile kujisumva ijo jili na mololo umumili gojo. Amololo genayo gali malonda gapilile, ayo jagapandika ijisumva jinijo, kunguno ya nguzu jajo, ijo jidahebhagwa na oseose. Ijoyi jidulile gutumama milimo mingi bho nguzu mpaga guyimala. Hunagwene abhanhu bhagajitanaga giki, ‘lwamololo.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali na nguzu ja gutumama milimo yakwe chiza, mpaga guyimala. Umunhu ng’wunuyo, agigulyambijaga uguyitumama imilimo yiniyo, bho wangu wangu, na guyimala chiza aha kaya yakwe.

Uweyi agikolanijiyagwa ni lyamololo, kunguno nang’hwe ali na nguzu ja gudula gung’wenhela bhupandiki wingi umuwikaji bhokwe. Uwikaji bhokwe bhunubho, bhugabhambilijaga abhiye ugongeja bhukamu bho kutumama milimo yabho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, ‘lwamololo.’

Akahahile kenako kalanga bhanhu gongeja nguzu ja guitumama bho bhukama bhutale imilimo yabho, kugiki bhadule ugujibheja chiza ikaya jabho umuwikaji bhobho.

(Kutoka 2:11-15; Waamuzi 15:11-16; 1Wafalme 11: 15-16).

KISWAHILI: LENYE MAKOVU.

Chanzo cha msemo huu chaangalia kiumbe chenye makovu mwilini mwake. Makovu hayo ni madonda yaliyopona ambayo yalitokana na kiumbe hicho kuwa na nguvu za kutoshindwa na chochote. Kiumbe hicho kinaweza kufanya kazi nyingi mpaka kuzimaliza. Ndiyo maana watu hukiita ‘lenye makovu.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye nguvu za kufanya kazi vizuri mpaka kuzimaliza. Mtu huyo hujibidisha kuzitekeleza kazi zake hizo kwa haraka hadi kuzikamilisha. Yeye hufanana na dude lenye makovu, kwa sababu naye ana nguvu za kumwezesha kujiletea mafanikio mengi katika maisha yake. Maisha yake hayo huwasaidia pia wenzake katika kuongeza bidii za kuyatekeleza vizuri majukumu yao. Ndiyo maana watu humwita kwamba yeye ni ‘lenye makovu.’

Msemo huo hufundisha watu kuongeza nguvu za kuyatekeleza kwa bidii kubwa na vizuri majukumu yao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

(Kutoka 2:11-15; Waamuzi 15:11-16; 1Wafalme 11: 15-16).

mozambique-milimo

king-arthur-

 

ENGLISH: HE WHO IS FULL OF SCARS.

The origin of this saying is a creature with scars on his body. These scars are the healing wounds that resulted from the creature having the power to be invincible. The creature can do many tasks to complete it. That is why people call it ‘the one with scars.’

The saying is used comparatively to refer to any person who has the power to do jobs well and complete it on time. The person undertakes to carry out and complete his/her tasks quickly. He/she is like a creature full of scars, because he also has the power to work bring about notable successes in his life. His own life also helps other to work harder  in fulfilling their roles. That is why people call him ‘he who is full of scars.’

The saying teaches people to maximize effort to carry out their hard work and responsibilities, so that they can better support their families.

(Exodus 2: 11-15; Judges 15: 11-16; 1Kings 11: 15-16).