Joe Healey

677. KALAGU – KIZE. IGASHAGA AHA NU NENE AHA, DUNZUJE NG’HALA MYENDA:- MANDEGE.

Ikalagu yiniyo, ifumilile kubhanhu abho bhiganilaga hikanza lya gulya mandege madoto. Amandege genayo, gagikolanijiyagwa na ng’hala, kunguno ya ya guzujiwa amadutu gago, huna adule ugugalya umunhu, guti numo abhanhu bhagingijaga amakolele aga ng’halanga, huna bhajilya.

Giko lulu, umubhuyegi bho gubisha mandege genayo, uumo aganganila ung’wiye kugiki ajibadije ijigano, bho guyomba giki, ‘igashaga aha nu nene aha, dunzuje ng’hala myenda.’

Ung’wiye ng’wunyo, nang’hwe uyo olinabho ubhuyegi bhunubho, ubho gubisha na gulya mandege madoto genayo, agajibadija ijigano jinijo bho guyomba, ‘Mandege.’ Aho ujibadija ijigano jinijo, pye abhose bhagaseka, na gwandya gugalya amandege genayo.

Hunagwene abhanhu bhagandya huiganila giki, ‘igashaga aha nu nene aha, dunzuje ng’hala myenda:- Mandege.’ Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 29. Abhanhu ulu bhagakubhula amandege genayo, nulu ulu bhajitondola ing’halanga, igolechaga giki, bhalinzuja ng’hala myenda.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalandya wikaji bhupya bho gubhuzuula uwikaji ubho kale. Uwikaji bhunubho, ubho kale bhuli wikaji bho umushibhi.

Umunhu uyo obhatijiwa ung’wene obyalwa bhupya, kunguno ya gwingijiwa ishibhi jakwe, na gwandya wikaji bhupya, ubho nema ya bhutakaso. Inema yiniyo, ni jizwalo, nulu ng’wenda uyo duging’hiyagwa ulu dabhatijiwa.

Aliyo lulu, ushetani agaduzujaga ung’wenda gunuyo, bho gudulembalemba gwita shibhi. Giko, ulu duzunya dugulenganijiwa nu ng’hana uyo alizunya guzujiwa ng’wenda, guti numo ligazugijiyagwa ilindege linilo. Hunagwene ushetani na bhahemba bhakwe, bhagayombaga giki, ‘igashaga aha nu nene aha, dunzuje ng’hala myenda:- Mandege.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhabhu higulya ya kulema kuzujiwa nema ya bhutakaso bho guzunya mihayo ya gwita shibhi, kugiki bhadule guwikalana ubhulagani bhobho ubho bhatizimu, bho gugikalana amalagilo ga ng’wa Mulungu mpaga bhinghile umubhupanga ubho bhudashilaga.

Ayise bhahemba bha ng’wa Yesu Kristo ulu dang’winha wasa ushetani na bhahemba bhakwe, ubho guduzuja ing’wenda iyape iya bhubhatizo, tugabhizaga guti na mandege umo abhanhu agagakubhulaga na gugalya.

Ushetani, adadulile uguduhadikija gwita shibhi. Uweyi agadinhaga miganiko gabhubhi na yise dagabokela na dugazunilija, na hanuma yahoo, gwita shibhi. Igeleliwe dugalemeje amiganiko genayo, umu mioyo yise, bho gujitumila ijilanga ija gufumila kuli Mulungu. Gashinga yilichiza dusalile pye amakanza, kunguno ulu diyibha, ushetani agamanaga wiyungula na gulundula guti Shimba iyo igucholaga gulya munhu.

Olihoyi nsumba umo, uyo alina ng’wenda gope, uyo onondejaga Yesu, agading’wa aliyo, ubhipuluka na gupela uguleka ng’wenda gokwe ugope gunuyo. Nayise ushetani, agaduzujaga ung’wenda gunuyo, ugope, ulu dagazunilija amiganiko agabhubhi, umumioyo yise.

Marko 14:50-52.

Dimilagi higiki umugunya gwise, bho gugapeja amiganiko agabhubhi umumioyo yise, kugiki dukije ugung’inha wasa nulu bhudoo ushetani. Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 29-30.

1Petro 5:8.

Waefeso 6:11-13.

Mathayo 22:12-13.

KITENDAWILI:- TEGA.

KETI HAPA NA MIMI HAPA, TUMVUE MJINGA NGUO:- MAHINDI.

Kitendawili hicho, kinatokea kwa watu waliokuwa wanahadithiana wakati wa kula mahindi mabichi ya mwanzo wa mwaka. Mahindi hayo, hufananishwa na mjinga kwa sababu ya kuvuliwa maganda ndipo mtu aweze kuyala, kama wanavyoondoa maganda ya kalanga ndipo wanazila.

Hivyo basi, wakiwa na furaha ya kupata mahindi hayo mabichi ya mwaka, mmoja alimtegea mwenzake ili ategue kitendawili, akisema, ‘keti hapa na mimi hapa, tumvue mjinga nguo.’ Mwenzake huyo, naye akiwa na furaha ya kuyala mahindi hayo mabichi, alitegue kitendawili hicho kwa kusema, “Mahindi.”  Baada ya kukipatia kitenawili hicho, wote wawili walicheka na kuanza kuyala mahindi hayo.

Ndiyo maana watu wakaanza kuhadithiana wakisema, ‘keti hapa na mimi hapa, tumvue mjinga nguo:- Mahindi.’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 29. Watu wanapotoa maganda ya mahindi au ya karanga humaanisha kwamba, wanamvua mjinga nguo.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Kitendawili hicho, hulinganiswa na watu walioanza maisha mapya baada ya kuyavua yale ya zamani. Maisha hayo ya zamani ni maisha ya dhambi. Mtu aliyebatizwa amezaliwa upya kwa maana ya kuondolea dhambi zake na kuanza maisha ya mapya akipewa neema ya utakaso. Neema hiyo, ni vazi au nguo tunayovaa baada ya kubatizwa.

Lakini shetani hutuvua nguo hiyo kwa kutushawishi kutenda dhambi. Hivyo, tukikubali kutenda dhambi tutafananishwa na mjinga anayekubali kuvuliwa nguo, kama yanavyovuliwa mahindi. Ndiyo maana shetani na wafuasi wake husema kwamba, ‘keti hapa na mimi hapa, tumvue mjinga nguo:- Mahindi.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kukataa kuvuliwa neema ya utakaso kwa kukubali kushawishiwa kutenda dhambi, ili waweze kuziishi ahadi zao za ubatizo wao kwa kuziishi amri za Mungu, mpaga waweze kuingia kwenye uzima wa milele.

Kama vile watu hutoa maganda ya mahindi na kula, sisi wafuasi wa Yesu Kristo tunampa shetani na wenzake nafasi ya kutuvulia nguo nyeupe ya ubatizo.

Shetani hawezi kutulazimisha kutenda dhambi. Bali hutupa mawazo mabaya na sisi tunayapokea na kuyakubali na baadaye kutenda dhambi.

Marko 14:50-52. “Hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia. Kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa anamfuata Yesu akiwa amevaa shuka. Nao wakajaribu kumkamata. Lakini yeye akaponyoka, akaiachilia ile shuka akakimbia uchi.”

Kijana yule aliyekuwa akimfuata Yesu amevaa nguo nyeupe, lakini alipojaribiwa akaiahilla ile shuka, akamvua Yesu na kukimbia uchi. Sisi wakati wa kujaribiwa tunashindwa kuvumilia, tunamwacha Yesu Kristo na kumkubalia shetani kuvua nguo ya ubatizo wetu.

Basi, tusimame imara tusimpe nafasi shetani hata kidogo. Tuyafukuze mawazo yetu maovu mara yanapoingia ndani yetu. Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 29-30.

1Petro 5:8. “Muwe macho, kesheni! Maana adui yenu, shetani, huzunguzunguka kama Simba aungurumaye akitafuta mtu ammeze.”

Waefeso 6:11-13. “Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za shetani, maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui, na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti. Basi, simameni imara.”

Mathayo 22:12-13. “Mfalme akamwuliza: “Rafiki, umeingiaje hapa bila mavazi ya arusi?” Lakini yeye akakaa kimya. Hapo Mfalme akawaambia watumishi: Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani, huko atalia na kusaga meno.”

mandege

mandege1

mandege2

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

SIT HERE AND I SIT THERE TO UNDRESS THE FOOL – MAIZE.

This riddle came from people who were talking to each other while eating cooked maize. As they were eating, they began riddling. One paused a riddle that ‘sit here and I sit there to undress the fool’ and the respondent answered it as maize and both of them burst out laughing. In this riddle, a mazie is considered to be a fool creature that can be stripped naked without any complain (Refer to Kueneza Injili kwa Methali, which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 29) written by Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

This riddle can be compared to people who started a new life after leaving aside their old type of life style that is full of sins. A baptized person is born again in the sense of taking away his/her sins and beginning a new life with the grace of sanctification. Grace is the garment or dress we wear after being baptized. But, Satan tends to take off the robe by inducing us to sin. So if we admit to sin, we will be compared to a fool who lets himself/herself be stripped of his/her clothes in the same way we see in maize. Satan and his followers will say, ‘Sit here and I sit there to undress the fool – Maize’ to mean the way human beings fall into the world of sin.

This riddle teaches people about refusing to be deprived of the grace of sanctification by accepting the temptation to sin. People need to live up to their promises of baptism by living the commandments of God so that they can enter into eternal life.

Just as people remove corn husks and eat, we followers of Jesus Christ give satan and his followers an opportunity to strip off our white robes of baptism.

Satan cannot force us to sin but he gives us wrong ideas and we accept, admit it and then fall into sin.

Mark 14: 50-52: “Then all the disciples forsook him, and fled. A young man was following Jesus. And they tried to seize him. But he escaped, and let go the sheaf, and fled naked.”

The young man who was following Jesus was dressed in white, but when he was tempted, he slipped off the cloth, forsook Jesus and fled naked. When we are tempted, we fail to persevere, leaving Jesus Christ and allowing the devil to take off the rob of our baptism.

So, let us stand firm and not give the devil a chance. We have to get rid of our evil thoughts once they get into us (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 29-30).

1Peter 5:8. Ephesians 6:11-13. Matthew 22:12-13.

Father Zakaria Kashinje is consolidating all the Sukuma proverbs, sayings, riddles, stories and songs in his running list on our Sukuma Legacy Project Website https://sukumalegacy.org.

Father Zakaria Kashinje is consolidating all the Sukuma proverbs, sayings, riddles, stories and songs in his running list on our Sukuma Legacy Project Website https://sukumalegacy.org.

This website promotes the history, culture, Oral Literature — Stories, Proverbs, Sayings, Riddles and Songs — and visual representations of the Sukuma People in Tanzania in East Africa. Presently he is drawing from: Sybertz, Donald and Joseph Healey. Kueneza Injili Kwa Methali: Hekima ya Kisukuma na Lugha Mbalimbali juu ya Chakula — Kitabu cha Kwanza, Peramiho: Benedictine Publications Ndanda — Peramiho, 1984.

The English translation is Proclaiming the Gospel Through Proverbs: The Wisdom of Sukuma and Different Languages on Food – Book I. Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, Kugundua Mbegu za Injili: Hekima ya Kisukuma na Lugha Mbalimbali juu ya Familia na Ndoa — Kitabu cha Pili, Peramiho: Benedictine Publications Ndanda — Peramiho, 1993.

The English translation is Discovering Seeds of the Gospel: The Wisdom of Sukuma and Different Languages on Family and Marriage – Book II.

676. LELO WA KUTULILA MVA IGOKOLA.

Ikale abhasuguma bhajigabhanhaga inyama mumakono ahi kanza lya gulya, kigiki bhadizikeneja inyama jinijo, na bhuli munhu apandika iyakwe. Uluyigela mva bhadumaga ugwitula ubho makono ayo galikokala nyama na bhugali. Hunabhatumilaga igokola lya nkono. Idi guti haha, kunguno ishigu jiniji bhagasolaga nyama mujiseme jimo duhu. Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba giki, ‘Lelo wa kutulila mva igokola.’ Munho giki, ulunulo luli lushigu lo bhugali bho nyama. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali ukurasa 27.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji, Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa ku likanza lya sherehe iyo igitagwa na libhilinga lya bhanhu, kugiki bhadule gubhayeja ha nimo gunuyo, nulu umhayo nhebhe guti jigukulu ja winga, aho bhuli munhu agabhizaga na nyama ningi umumakono, bhalilomela abhakengeji bhenabho.

Abhanhu bhenabho, bhalina wizang’holo bho kubhabhilinga chiza aha jigukulu jinijo, kugiki bhuli ng’wene adule gupandika wasa bho guyega kihamo  na bhiye. Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagayombaga giki, ‘Lelo wa kutulila mva igokola.’

Usulumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhabhilinga abhichabho, umujigukulu jabho, kugiki abhanhu bhabho bhenabho, bhadule gulya nabho na gwiguta umujigikulu jabho ijitale ijo bhalinajo jinijo.

Guti abhayahudi umobhayegelaga na gubhusherehekea ubhupiji bho gufuma kubhusese umu si ya Misri, UYesu Kristo, giko agasherehekea na kuyega kihamo na bhahemba bhakwe, unimo uyo gulidupija, ugo gucha na kuhimbuka gokwe. Lolaga Kueneza Injili Kwa Methali bhakurasa bho 27.

IPasaka ya Bhaisraeli yolecha Pasaka ya bhakristo, iyo yili bhupiji ubho bhugeng’hwa na Kristo: Ng’wana o Ng’holo o ng’wa Mulungu wifunyaga munsalabha. Uweyi agifunya guti jiliwa umu Jigukulu ja Ng’wisho umu nyuma ya Pasaka ya Bhaisraeli.

UKristo oyenhelaga IDunia yose bhupiji bho jigukulu jakwe na nsalabha gokwe. Umo guli uguzunya go bhakristo, ijito jinijo ija jigukulu nu nsalabha jilendelejiwa nu Kristo umu Misa, iyo ilijigukulu na jitambo jene ijo jilijang’wa Kristo.

Bhuli ikanza ilo dulisherehekea iMisa unimo go bhupiji wise gulitiwa, lushugu lo lelo, na hikanza linili. Aise dubhuyegele na gubhusherehekea ubhupiji ahikanza lya Misa, bho sala na mimbo ga bhuyegi.

Kuyiniyo, yiligelelwa ise bhakristo duwikumbwe ubhupiji ahikanza lya Misa bho sala na mimbo ga bhuyegi. Dubhuyegele ubhupiji wise kukila ijigukulu ijingi. Dunumbilije uMulungu umu gudupija bho nzila ya ng’wa Sebha wise Yesu Kristo, na difunye gete kihamo nu Yesu Kristo na mugati yakwe kuli Mulungu Bhabha.

Dushiriki ijiliwa ija Ng’wa Sebha ijojilidulunganija nu Yesu no no, ijojigadulumanyaga ise na ise, na gudambilija ugwitogwa guti umo Umulungu odutogelwa. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukuraka 27-28.

Luka 22:15-16.

Luka 13:29.

Ufunuo 19:9

Luka 15:11-32.

Mathayo 22:1-14.

KISWAHILI: LEO NI UGALI WA KUMPIGIA MBWA KIWIKO CHA MKONO.

Zamani wasukuma walikuwa wanagawana nyama mikononi wakati wa kula kama kinga, ili wasigombanie nyama hizo, na kila mtu apate haki yake. Akitokea mbwa walishindwa kumpiga kwa mikono iliyojaa nyama na ugali. Badala yake walitumia kiwiko cha mkono kumpigia mbwa huyo. Si kama siku za sasa, kwa sababu siku hizi watu hao wanakuchukua nyama kwenye chombo kimoja tu. Ndiyo maana watu wakaanza kusema kwamba, ‘Leo ni ugali wa kumpigia mbwa kiwiko cha mkono.’ Hiyo ilimaanisha kwamba siku hiyo ina ugali wa nyama. Kueneza Ijili kwa Methali ukurasa 27.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti, Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hulinganishwa kwenye wakati wa sherehe inayofanywa na mkusanyiko wa watu ili kufurahia tukio au jambo fulani kama sikukuu ya arusi, ambapo kila mtu huwa na nyama nyingi mikononi, wanaeleza watafiti hao.

Watu hao huwa wana ukarimu wa kualikana vizuri kwenye sherehe hiyo, ili kila mmoja aweze kupata nafasi ya kufurahi pamoja na wenzake. Ndiyo maana watu hao husema, ‘Leo ni ugali wa kumpigia mbwa kiwiko cha mkono.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwashirikisha wenzao kwenye sherehe zao, ili watu wao waweze kula na kushipa kwenye sikukuu za furaha kubwa walizo nazo.

Kama wayahudi walivyojurahia na kuadhimisha wakovu kutoka utumwani katika nchi ya Misri, Yesu Kristo vile vile aliadhimisha na kufurahi pamoja na wafuasi wake, kazi inayotuokoa, yaani kufa na kufufuka kwake. Rejea kueneza Injili kwa Methali ukurasa 27.

Pasaka ya Waisraeli yadokeza Pasaka ya wakristo, yaani wokovu ulioletwa na Kristo: Mwana Kondoo wa Mungu ambaye amejitolea msalabani. Yeye alijitoa kama chakula katika Karamu ya Mwisho katika Juma la Pasaka ya Wasraeli.

Kristo ameiletea Dunia yote wokovu kwa karamu yake na msalaba wake. Kadiri ya imani ya kikristo, tendo lile lile, la karamu na msalaba, linaendelezwa na Kristo katika Misa iliyo karamu na sadaka ile ile ya Kristo.

Kila tunapoadhimisha Misa, kazi ya wokovu wetu inatendeke, siku ya leo na wakati huu. Sisi tuufurahie na kuuadhimisha wokovu huu kwa shangwe.

Kwa hiyo, yatupasa sisi wakristo kutamani wokovu wakati wa Misa kwa sala na nyimbo za shangwe. Tuufurahie wokovu wetu zaidi ya sherehe zingine. Tumshukuru Mungu kwa kutuokoa kwa njia ya Bwana Wetu Yesu Kristo, na tujitoe kabisa pamoja na Yesu Kristo na ndani yake kwa Mungu Baba.

Tushiriki chakula cha Bwana kinachotuunganisha na Yesu zaidi na zaidi, na kinachotuunganisha sisi kwa sisi, na kutuwezesha kupendana kama Mungu anavyotupenda. Rejea Kueneza Injili kwa Methali ukurasa 27-28.

Kutoka 12:14. “Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, ninyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mfaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kama amri ya milele.”

Luka 22:15-16. “Nimetamani kwa hamu kubwa kuila karamu hii ya Pasaka pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. Maana, nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika Utawala wa Mungu.”

Luka 13:29. “Watu watakuja kutoka mashariki na maghaibi, kutoka kaskazini na kusini, watakuja na kukaa kwenye karamu katika Utawala wa Mungu.”

Ufunuo 19:9. “Kisha malaika akaniambia, ‘Andika haya: heri wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-kondoo!”

Luka 15:11-32. Mfano wa Mwana Mpotevu.

Mathayo 22:1-14. Mfano wa Arusi.

dog3

dog5

 

ENGLISH: TODAY IS UGALI FOR BEATING A DOG WITH AN ELBOW JOINT.

In the past the sukuma people used to eat meat while each one of them holds his/her meat in order to avoid competition. This approach to eating ensured equality. Since their hands were occupied with eating (holding ugali and meat at the same) when dogs came nearby, they chased them using an elbow joint of hand instead of hands. This is why people could describe this scenario using the saying that ‘today is ugali for beating a dog with an elbow joint’ to mean ugali with meat. However, this approach changed later on and all people could pick meat from the same container (see Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 27, written by Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., published by Benedictine Publications Ndanda, – Peramiho, 1984.

This saying can be likened to an occasion held by a group of people to enjoy an event or something like a wedding feast. In this occasion, everyone is expected to have a lot of meat in their hands, explain the researchers. In such occasions, people can mean to be generous enough to invite members to join in celebrating for a certain feast.

The proverb teaches people to be able to join others whanever there are gatherings that need cooperation.

Just as the Jews rejoiced and celebrated after being redeemed from slavery in the land of Egypt, Jesus Christ also celebrated and rejoiced with his followers, the work that saved us; His death and resurrection (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 27).

The sacrifice of Israelites meant the sacrifice of Christians, which also is the salvation Christ brought: the Lamb of God who has given himself on the cross. He presented himself as a meal at the Last Supper in Israel during Easter Week.

Christ has brought salvation to the whole world through his feast and his cross. According to the Christian faith, the same act; banquet and cross, is perpetuated by Christ in the Mass with the same sacrifice of Christ.

Every time we celebrate Mass, the work of our salvation is done, both today and in this time. We should rejoice and celebrate this salvation with joy.

Therefore, we Christians aspire to seek salvation during Mass with prayers and songs of joy. May we rejoice in our salvation more than any other festival. We thank God for saving us through our Lord Jesus Christ, and give ourselves completely to Jesus Christ and into Him for God the Father.

We share the Lord’s food that unites us more and more with Jesus, and that unites us with one another, enabling us to love one another as God loves us (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 27-28). 

Luke 22:15-16. Luke 13:29. Revelation 19:9. Luke 15:11-32. Metthew 22:1-14.

675. KUPYANJA ITI KULUMANGA.

Ulusumo lunulo, lyungilile kubhanhu abho bhali na jiliwa aliyo ilikubhi bhali bhadinalyo. Abhanhu bhenabho, bhalyaga bhugali bho likoye linilo ilya gugayiwa makubhi.

Lushigu lumo, unzugi agabhatengela bhugali bho makubhi magehu, ubhakaribhusha aliyomba, ‘makaribhu ijiliwa.’ Umo obho abhakaribhushiwa ubhuja, ‘ni bhuli amakubhi gali magehu giko?”

Unzugi ushosha, ‘Mgumana ng’wupyanja mizuji migehu, kunguno ilihambohambo ugupyanja kukila ugulumanga.’ Aho bhigwa giko, abhakaribhushiwa bha jiliwa bhenabho, bhagandya gulya, bho gumana bhupyanja hado hado, mpaga nose bhiguta. Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba, ulu bhalilyinja ikoyi ilebhe giki, ‘kupyanja iti kulumanga.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalitimbya mholo ahikanza ilya kugukoyiwa na makoye umu Si. Ninga iki umunhu analina makoye, giki, alilya bhugali na misuji migehu, ili hambohambo kukila umunhu uyo alilumanga bhugali, ukurasa 25 bho jitabho ja Kueneza Injili kwa Methali.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji, Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Abhakengeji bhenabho, bhagabhulucha giki, abhanhu abho bhali na nzila ya gugingija amakoye gabho, nulu igabhiza giki, inzila yiniyo yilindoo, bhali hambohambo gukila abho bhadinayo nulu inzila indoo yiniyo iyagugingija amakoye gabho genayo.

Abhanhu bhenabho, bhagabhalanjaga na bhichabho ahigulya ya kuchola nzila ja gugamalila amakoye gabho, kukila ugusaga nago duhu.  Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagabhawilaga abhichabho giki, ‘kupyanja iti kulumanga.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwitimbya mholo na gwiyumilija nulu bhalimubhuluhi. Ilikoye na bhuluhi ubho ha Welelo, jidulile gulinganijiwa kuwikaji bho gucha na guhimbuka kihamo na Yesu.

UYesu Kristo, adayombile igiki, abhahemba bhakwe bhadupandika bhuluhi umu Si iyi, ubhuluhi ubhutale gulebha pye amaluho, ili kulekana na Mulungu. Guti umo agandikila Ntakatifu Paulo uku Bharumi 8:35. “Alinani uyo adulile gudulekanya nu bhutogwa bho ng’wa Kristo? Hamo, maluho, nulu makoye, nulu nzala, nulu bhugayiwa bho myenda, nulu mayanga nulu gubhulagwa?”

Nduhu jisumva jose jose ijagudula gudulekanya na bhutogwa bho Ng’wa Mulungu wise, kunzila ya ng’wa Kristo Sebha wise.” Ishibhi bhung’wene hijo jidulile ugudulekanya na Mulungu. Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa25-26.

KISWAHILI: KUCHOVYA UGALI KATIKA MCHUZI KIDOGO NI AFADHALI KULIKO KULA UGALI BILA MCHUZI.

Methali hiyo, yatokea kwa watu waliokuwa na chakula, lakini wakasosa mboga. Watu hao, walikuwa wanakula ugali kwa shida hiyo ya kukosa mboga. Siku moja, mpishi aliwapekelea ugali wenye mboga kidogo, akawakaribisha akisema, ‘karibuni mle chakula.’ Mmoja wa wale waliokaribishwa akauliza, ‘mbona mboga ni kidogo hivyo?’

Mpishi akajibu, ‘Mtakuwa mnachovya kwenye mchuzi kidogo, kwa sababu ni afadhali kula ugali wenye mchuzi kidogo kuliko kula ugali huo bila mboga kabisa.’

Baada kusikia hivyo, wale waliokaribishwa chakula hicho, walianza kula kwa kuchovya kidogo kidogo, mpaga mwishowe wakashipa. Ndiyo maana watu wakaanza kusema kama namna ya kutatua tatizo, kwamba, ‘kuchovya ugali katika mchuzi kidogo ni afadhali kuliko kula ugali bila mchuzi.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wanaopeana moyo wakati wa kusumbuliwa na shida hapa duniani. Ingawa mtu ana shida, yaani anakula ugali na mchuzi kidogo, ni afadhali kuliko mtu yule anayekula ugali bila mboga hata kidogo, ukurasa wa 25 wa kitabu cha Kueneza Injili kwa Methali.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti, Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Watafiti hao, waligundua kwamba, watu waliopata njia ya kutatua tatizo hata kama njia hiyo ni ndogo, wana unafuu kuliko wale ambao hawana njia ya kuwatatulia tatizo lao.

Watu hao, huwafundisha pia wenzao juu ya kutafuta njia za kuwawezesha kutatua matatizo yao, badala ya kubaki nayo tu. Ndiyo maana watu hao, huwaambia wenzao kwamba, ‘kuchovya ugali katika mchuzi kidogo ni afadhali kuliko kula ugali bila mchuzi.’

Methali hiyo, huwafundisha watu juu ya kupeana moyo wa kuvumilia hata kama wamo taabuni. Taabu na shida za hapa duniani zaweza kurahishwa kwa kuyaishi Maisha ya kufa na kufufuka pamoja na Yesu.

Yesu Kristo hakusema kwamba, wafuasi wake hawatapata taabu katika dunia hii, bali aliwahimiza kuchukua msalaba wao kila siku na kumfuata Yeye. Kwa maana hiyo, dhiki kubwa kuliko dhiki zote ni kutenganishwa na Mungu. Kama anavyosema Mtakatifu Paulo kwa Warumi 8:35. “Ni nani awezaye kututenga na mapendo ya Kristo? Je, ni dhiki, au mateso, au njaa, au ukosefu wa nguo, au hatari, au kuuawa?”

Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na mapendo ya Mungu wetu kwa njia ya Kristo Bwana wetu.” Dhambi peke yake inaweza kututenganisha na Mungu. Kueneza Injili kwa Methali ukurasa 25-26.

Zaburi 84:10. “Hakika siku moja katika njia zako ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani kwa Mungu wangu kuliko kukaa katika hema za uovu.”

Habakuki 3:17-18. “Ikiwa mtini hautachanua maua, wala mizabibu hamtakuwa na matunda; taabu ya mizeituni itakuwa bure na mashamba hayatoi chakula, zizini hamtakuwa na kundi, wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe walakini nitamfurahia Bwana, nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.”

Waebrania 12:1-11. “Msife moyo, wala msikate tamaa, maana katika kupambana na dhambi, ninyi hamjapigana mpaka kiasi cha kumwaga damu yenu.”

Marko 9:43-48. “Na jicho lako likikukosesha, ling’oe! Afadhali kuingia katika utawala wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yote mawili na kutupwa motoni.”

bhugali4

cooking

child eating food

 

ENGLISH: DIPPING UGALI IN A LITTLE SAUCE IS BETTER THAN EATING IT WITHOUT SAUCE.

The proverb comes from people who had ugali but lacked sauce. Those people kept on eating ugali without sauce because it was not easy to get it (sauce). One day the cook gave them little sauce to eat with ugali but one of the eaters asked as to why the sauce is too little. The response he/she got from the cook is ‘ dipping ugali in a little sauce is better than eating it without sauce.’

This proverb can be compared to people who give encouragement to one another in times of distress in this world. Although a person has a problem, it is better to simplify it so that one can see it as something that can be easily handled. See also Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 25 for more clarification on this proverb.

This book was written by researchers, Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and was published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984. In this book, researchers found that people can use even small items they have to solve their immediate problems. These problem solvers teach others about ways to solve their problems. They can use the limited resources they have to solve their own problems.

This proverb teaches people to encourage one another during distress times. As holy scriptures say, Jesus Christ did not say that His followers would not suffer in this world, but He encouraged them to take up their cross daily and follow Him. In that sense, the greatest tribulation is separation from God. As St. Paul states in Romans 8:35, “Who can separate us from the love of Christ? Shall it be tribulation, or distress, or famine, or nakedness, or peril, or death?

No creature can separate us from the love of our God through Christ our Lord. Sin alone can separate us from God (Refer Kueneza Injili kwa Methali) which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 25-26.

674. IGEMBE LIDALEMBAGA.

Bhalihoyi bhalimi abho bhilomelaga umugufumila mulilima lyabho. Uumo agang’wila ung’wiye, ‘dujage dugalime kunguno ilikanza lya gulima lyashigaga.’ Ung’wiye ushosha, ‘igelelilwe dugandye gulima ng’hana, kugiki nulu dugakela dugupandika nulu jigehu, kunguno iligembe lidalomalomaga.’ Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Igembe lidalembaga.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kulikanza ilo abhanhu bhagatumamaga milimo bho gutumila Igembe mpaga bhapandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho, bhadebhile igiki ilegembe luli lumeng’ho lutale lo gutumama milimo umu wikaji bhobho, pye nu mu Africa ngima. Kueneza Injili kwa Methali ukurasa 13.

 ‘Kueneza Injili kwa methali’ jili jitabho ijo jigandikwa na Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey, M.M., ijojigachapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Abhalimi bhenabho, bhagalitumilaga iligembe linilo, bho bhukamu bhutale, mpaga bhapandika matwajo mingi, umukikalile kabho. Amatwajo gabho genayo, gagabhambilijaga abhanhu bhenabho ugujibheja chiza ikaya jabho, kunguno ya gulitumila chiza ilimbe linilo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Igembe lidalembaga.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kudebha igiki, imilimo yose iyo bhagaitumamaga ibhize midoo nulu mitale, ili na solobho ya ying’wene ukubhutumami bhobho, nuku miso ga ng’wa Mulungu. Gitumo umo iligembe lidalembelaga, uguzunya go kuli Mulungu, nago gulalembaga.

Ulu dunzunya Weyi dugupandika matwajo, ayo galigawiza ijinagunzunya Yesu na kumsumbila Weyi umumioyo ise. Giko lulu, dugupandika mhela ya bhupanga ubho bhudashilaga.

Mwanzo 3:17.

Wagalia 6:7.

Yohane 6:29.

KISWAHILI: JEMBE HALIDANGANYI.

Walikuwepo wakulima waliokuwa wakiongea juu ya kazi yao ya kulima. Mmoja alimwambia mwenzake, ‘twende tukalime kwa sababu wakati wa kulima umefika.’ Mwenzake alijibu, ‘inafaa kweli tukalime, kwa vile hata tukikosa mazao mengi, tupata walau kidogo, kwa sababu Jembe halisemi uongo.’ Ndiyo maana watu wakaanza kusema kwamba, ‘Jembe halidanganyi.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwenye wakati ule ambao watu hufanya kazi za kilimo kwa kutumia Jembe, mpaka wanafanikiwa kupata mazao mengi zaidi maishani mwao.

Watu hao, wanafahamu kwamba Jembe ni alama maalum ya kazi kwao na kwa Africa nzima, kama walivyoandika watafiti Padre Donald Sybertz, M.M., na Padre Joseph Healey M.M., kwenye kitabu cha ‘Kueneza Injili kwa methali’, ukurasa 13. Kitabu hicho kilichapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Wakulima hao, hulifanyia kazi Jembe hilo kwa bidii kubwa mpaka wanafanikiwa kupata mapato mengi, katika maisha yao. Mafanikio yao hayo, huwasaidia watu hao, katika kuziendeleza vizuri familia zao, kwa sababu ya wao kulitumia vizuri Jembe hilo. Ndiyo maana watu husema kwmba, ‘Jembe halidanganyi.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuelewa kwamba, kazi yoyote wanayoifanya iwe ndogo au kubwa, ina faida ya pekee katika utekelezaji wa majukumu yao, na machoni pa Mungu. Kama vile Jembe lisivyodaganya, imani kwa Mungu, nayo haidanganyi.

Kwa maana hiyo, tukimwamini, tutapata mafanikio ambayo ni mazuri katika kumwamini Yesu na kumpokea Yeye mioyoni mwetu. Hivyo basi, tutapata thawabhu ya uzima wa milele.

Mwanzo 3:17. “Kwa uchungu utakula mazao yako siku zote za maisha yako.”

Mithali 14:23. ‘Katika kila kazi mna faida, bali maneno ya midomo huleta hasara tu.”

Wagalia 6:7. “Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.”

Yohane 6:29. “Hii ndiyo kazi anayotaka Mungu umuifanye: kumwamini yule aliyenituma.”

plow ethiopian

plow

maize

ENGLISH: THE HOE DOES NOT LIE.

The source of this proverb is a hoe and two farmers. Two farmers were in conversation, one of them said, we need to go farm because it is the farming season and the second one agreed by saying that yes, we have to go because we can get something from the farm because ‘the hoe does not lie.’

This proverb can be comparable to people who engage in seasoned activities. These people, for example, farmers, know when and how to plant their crops. In Africa, for example, agriculture being the backbone of the economy, people need to spend their farming season accordingly in order to make sure that they have enough food to feed their families. The awareness of Africans in farming activities is also shown in research works by Fr. Donald Sybertz, MM, and Fr. Joseph Healey MM, in the book Kueneza Injili kwa Methali ‘Spreading the Gospel in Proverbs’, page 13. The book was published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

The farmers work hard using their hoes in order to earn living and their success helps to improve their families’ welfare.

This proverb teaches people to understand that whatever work they do, however small it might be, has a benefit in future. It will help them achieve something better in life. Just as the hoe does not lie, faith in God too does not lie people. If people believe in Him, they will succeed in life.

Genesis 3:17 “ Through painful toil you will eat food from it all the days of your life”

 Proverbs 14:23: “All hard work brings a profit, but mere talk leads only to poverty”

Galatians 6: 7: “A man reaps what he sows”

John 6:29: “ The work of God is this: to believe in the one he has sent”