Ikalagu yiniyo, ifumilile kubhanhu abho bhiganilaga hikanza lya gulya mandege madoto. Amandege genayo, gagikolanijiyagwa na ng’hala, kunguno ya ya guzujiwa amadutu gago, huna adule ugugalya umunhu, guti numo abhanhu bhagingijaga amakolele aga ng’halanga, huna bhajilya.
Giko lulu, umubhuyegi bho gubisha mandege genayo, uumo aganganila ung’wiye kugiki ajibadije ijigano, bho guyomba giki, ‘igashaga aha nu nene aha, dunzuje ng’hala myenda.’
Ung’wiye ng’wunyo, nang’hwe uyo olinabho ubhuyegi bhunubho, ubho gubisha na gulya mandege madoto genayo, agajibadija ijigano jinijo bho guyomba, ‘Mandege.’ Aho ujibadija ijigano jinijo, pye abhose bhagaseka, na gwandya gugalya amandege genayo.
Hunagwene abhanhu bhagandya huiganila giki, ‘igashaga aha nu nene aha, dunzuje ng’hala myenda:- Mandege.’ Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 29. Abhanhu ulu bhagakubhula amandege genayo, nulu ulu bhajitondola ing’halanga, igolechaga giki, bhalinzuja ng’hala myenda.
Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalandya wikaji bhupya bho gubhuzuula uwikaji ubho kale. Uwikaji bhunubho, ubho kale bhuli wikaji bho umushibhi.
Umunhu uyo obhatijiwa ung’wene obyalwa bhupya, kunguno ya gwingijiwa ishibhi jakwe, na gwandya wikaji bhupya, ubho nema ya bhutakaso. Inema yiniyo, ni jizwalo, nulu ng’wenda uyo duging’hiyagwa ulu dabhatijiwa.
Aliyo lulu, ushetani agaduzujaga ung’wenda gunuyo, bho gudulembalemba gwita shibhi. Giko, ulu duzunya dugulenganijiwa nu ng’hana uyo alizunya guzujiwa ng’wenda, guti numo ligazugijiyagwa ilindege linilo. Hunagwene ushetani na bhahemba bhakwe, bhagayombaga giki, ‘igashaga aha nu nene aha, dunzuje ng’hala myenda:- Mandege.’
Ikalagu yiniyo, yalanga bhabhu higulya ya kulema kuzujiwa nema ya bhutakaso bho guzunya mihayo ya gwita shibhi, kugiki bhadule guwikalana ubhulagani bhobho ubho bhatizimu, bho gugikalana amalagilo ga ng’wa Mulungu mpaga bhinghile umubhupanga ubho bhudashilaga.
Ayise bhahemba bha ng’wa Yesu Kristo ulu dang’winha wasa ushetani na bhahemba bhakwe, ubho guduzuja ing’wenda iyape iya bhubhatizo, tugabhizaga guti na mandege umo abhanhu agagakubhulaga na gugalya.
Ushetani, adadulile uguduhadikija gwita shibhi. Uweyi agadinhaga miganiko gabhubhi na yise dagabokela na dugazunilija, na hanuma yahoo, gwita shibhi. Igeleliwe dugalemeje amiganiko genayo, umu mioyo yise, bho gujitumila ijilanga ija gufumila kuli Mulungu. Gashinga yilichiza dusalile pye amakanza, kunguno ulu diyibha, ushetani agamanaga wiyungula na gulundula guti Shimba iyo igucholaga gulya munhu.
Olihoyi nsumba umo, uyo alina ng’wenda gope, uyo onondejaga Yesu, agading’wa aliyo, ubhipuluka na gupela uguleka ng’wenda gokwe ugope gunuyo. Nayise ushetani, agaduzujaga ung’wenda gunuyo, ugope, ulu dagazunilija amiganiko agabhubhi, umumioyo yise.
Marko 14:50-52.
Dimilagi higiki umugunya gwise, bho gugapeja amiganiko agabhubhi umumioyo yise, kugiki dukije ugung’inha wasa nulu bhudoo ushetani. Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 29-30.
1Petro 5:8.
Waefeso 6:11-13.
Mathayo 22:12-13.
KITENDAWILI:- TEGA.
KETI HAPA NA MIMI HAPA, TUMVUE MJINGA NGUO:- MAHINDI.
Kitendawili hicho, kinatokea kwa watu waliokuwa wanahadithiana wakati wa kula mahindi mabichi ya mwanzo wa mwaka. Mahindi hayo, hufananishwa na mjinga kwa sababu ya kuvuliwa maganda ndipo mtu aweze kuyala, kama wanavyoondoa maganda ya kalanga ndipo wanazila.
Hivyo basi, wakiwa na furaha ya kupata mahindi hayo mabichi ya mwaka, mmoja alimtegea mwenzake ili ategue kitendawili, akisema, ‘keti hapa na mimi hapa, tumvue mjinga nguo.’ Mwenzake huyo, naye akiwa na furaha ya kuyala mahindi hayo mabichi, alitegue kitendawili hicho kwa kusema, “Mahindi.” Baada ya kukipatia kitenawili hicho, wote wawili walicheka na kuanza kuyala mahindi hayo.
Ndiyo maana watu wakaanza kuhadithiana wakisema, ‘keti hapa na mimi hapa, tumvue mjinga nguo:- Mahindi.’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 29. Watu wanapotoa maganda ya mahindi au ya karanga humaanisha kwamba, wanamvua mjinga nguo.
Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Kitendawili hicho, hulinganiswa na watu walioanza maisha mapya baada ya kuyavua yale ya zamani. Maisha hayo ya zamani ni maisha ya dhambi. Mtu aliyebatizwa amezaliwa upya kwa maana ya kuondolea dhambi zake na kuanza maisha ya mapya akipewa neema ya utakaso. Neema hiyo, ni vazi au nguo tunayovaa baada ya kubatizwa.
Lakini shetani hutuvua nguo hiyo kwa kutushawishi kutenda dhambi. Hivyo, tukikubali kutenda dhambi tutafananishwa na mjinga anayekubali kuvuliwa nguo, kama yanavyovuliwa mahindi. Ndiyo maana shetani na wafuasi wake husema kwamba, ‘keti hapa na mimi hapa, tumvue mjinga nguo:- Mahindi.’
Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kukataa kuvuliwa neema ya utakaso kwa kukubali kushawishiwa kutenda dhambi, ili waweze kuziishi ahadi zao za ubatizo wao kwa kuziishi amri za Mungu, mpaga waweze kuingia kwenye uzima wa milele.
Kama vile watu hutoa maganda ya mahindi na kula, sisi wafuasi wa Yesu Kristo tunampa shetani na wenzake nafasi ya kutuvulia nguo nyeupe ya ubatizo.
Shetani hawezi kutulazimisha kutenda dhambi. Bali hutupa mawazo mabaya na sisi tunayapokea na kuyakubali na baadaye kutenda dhambi.
Marko 14:50-52. “Hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia. Kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa anamfuata Yesu akiwa amevaa shuka. Nao wakajaribu kumkamata. Lakini yeye akaponyoka, akaiachilia ile shuka akakimbia uchi.”
Kijana yule aliyekuwa akimfuata Yesu amevaa nguo nyeupe, lakini alipojaribiwa akaiahilla ile shuka, akamvua Yesu na kukimbia uchi. Sisi wakati wa kujaribiwa tunashindwa kuvumilia, tunamwacha Yesu Kristo na kumkubalia shetani kuvua nguo ya ubatizo wetu.
Basi, tusimame imara tusimpe nafasi shetani hata kidogo. Tuyafukuze mawazo yetu maovu mara yanapoingia ndani yetu. Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 29-30.
1Petro 5:8. “Muwe macho, kesheni! Maana adui yenu, shetani, huzunguzunguka kama Simba aungurumaye akitafuta mtu ammeze.”
Waefeso 6:11-13. “Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za shetani, maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui, na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti. Basi, simameni imara.”
Mathayo 22:12-13. “Mfalme akamwuliza: “Rafiki, umeingiaje hapa bila mavazi ya arusi?” Lakini yeye akakaa kimya. Hapo Mfalme akawaambia watumishi: Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani, huko atalia na kusaga meno.”
ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.
SIT HERE AND I SIT THERE TO UNDRESS THE FOOL – MAIZE.
This riddle came from people who were talking to each other while eating cooked maize. As they were eating, they began riddling. One paused a riddle that ‘sit here and I sit there to undress the fool’ and the respondent answered it as maize and both of them burst out laughing. In this riddle, a mazie is considered to be a fool creature that can be stripped naked without any complain (Refer to Kueneza Injili kwa Methali, which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 29) written by Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.
This riddle can be compared to people who started a new life after leaving aside their old type of life style that is full of sins. A baptized person is born again in the sense of taking away his/her sins and beginning a new life with the grace of sanctification. Grace is the garment or dress we wear after being baptized. But, Satan tends to take off the robe by inducing us to sin. So if we admit to sin, we will be compared to a fool who lets himself/herself be stripped of his/her clothes in the same way we see in maize. Satan and his followers will say, ‘Sit here and I sit there to undress the fool – Maize’ to mean the way human beings fall into the world of sin.
This riddle teaches people about refusing to be deprived of the grace of sanctification by accepting the temptation to sin. People need to live up to their promises of baptism by living the commandments of God so that they can enter into eternal life.
Just as people remove corn husks and eat, we followers of Jesus Christ give satan and his followers an opportunity to strip off our white robes of baptism.
Satan cannot force us to sin but he gives us wrong ideas and we accept, admit it and then fall into sin.
Mark 14: 50-52: “Then all the disciples forsook him, and fled. A young man was following Jesus. And they tried to seize him. But he escaped, and let go the sheaf, and fled naked.”
The young man who was following Jesus was dressed in white, but when he was tempted, he slipped off the cloth, forsook Jesus and fled naked. When we are tempted, we fail to persevere, leaving Jesus Christ and allowing the devil to take off the rob of our baptism.
So, let us stand firm and not give the devil a chance. We have to get rid of our evil thoughts once they get into us (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 29-30).
1Peter 5:8. Ephesians 6:11-13. Matthew 22:12-13.