675. KUPYANJA ITI KULUMANGA.

Ulusumo lunulo, lyungilile kubhanhu abho bhali na jiliwa aliyo ilikubhi bhali bhadinalyo. Abhanhu bhenabho, bhalyaga bhugali bho likoye linilo ilya gugayiwa makubhi.

Lushigu lumo, unzugi agabhatengela bhugali bho makubhi magehu, ubhakaribhusha aliyomba, ‘makaribhu ijiliwa.’ Umo obho abhakaribhushiwa ubhuja, ‘ni bhuli amakubhi gali magehu giko?”

Unzugi ushosha, ‘Mgumana ng’wupyanja mizuji migehu, kunguno ilihambohambo ugupyanja kukila ugulumanga.’ Aho bhigwa giko, abhakaribhushiwa bha jiliwa bhenabho, bhagandya gulya, bho gumana bhupyanja hado hado, mpaga nose bhiguta. Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba, ulu bhalilyinja ikoyi ilebhe giki, ‘kupyanja iti kulumanga.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalitimbya mholo ahikanza ilya kugukoyiwa na makoye umu Si. Ninga iki umunhu analina makoye, giki, alilya bhugali na misuji migehu, ili hambohambo kukila umunhu uyo alilumanga bhugali, ukurasa 25 bho jitabho ja Kueneza Injili kwa Methali.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji, Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Abhakengeji bhenabho, bhagabhulucha giki, abhanhu abho bhali na nzila ya gugingija amakoye gabho, nulu igabhiza giki, inzila yiniyo yilindoo, bhali hambohambo gukila abho bhadinayo nulu inzila indoo yiniyo iyagugingija amakoye gabho genayo.

Abhanhu bhenabho, bhagabhalanjaga na bhichabho ahigulya ya kuchola nzila ja gugamalila amakoye gabho, kukila ugusaga nago duhu.  Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagabhawilaga abhichabho giki, ‘kupyanja iti kulumanga.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwitimbya mholo na gwiyumilija nulu bhalimubhuluhi. Ilikoye na bhuluhi ubho ha Welelo, jidulile gulinganijiwa kuwikaji bho gucha na guhimbuka kihamo na Yesu.

UYesu Kristo, adayombile igiki, abhahemba bhakwe bhadupandika bhuluhi umu Si iyi, ubhuluhi ubhutale gulebha pye amaluho, ili kulekana na Mulungu. Guti umo agandikila Ntakatifu Paulo uku Bharumi 8:35. “Alinani uyo adulile gudulekanya nu bhutogwa bho ng’wa Kristo? Hamo, maluho, nulu makoye, nulu nzala, nulu bhugayiwa bho myenda, nulu mayanga nulu gubhulagwa?”

Nduhu jisumva jose jose ijagudula gudulekanya na bhutogwa bho Ng’wa Mulungu wise, kunzila ya ng’wa Kristo Sebha wise.” Ishibhi bhung’wene hijo jidulile ugudulekanya na Mulungu. Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa25-26.

KISWAHILI: KUCHOVYA UGALI KATIKA MCHUZI KIDOGO NI AFADHALI KULIKO KULA UGALI BILA MCHUZI.

Methali hiyo, yatokea kwa watu waliokuwa na chakula, lakini wakasosa mboga. Watu hao, walikuwa wanakula ugali kwa shida hiyo ya kukosa mboga. Siku moja, mpishi aliwapekelea ugali wenye mboga kidogo, akawakaribisha akisema, ‘karibuni mle chakula.’ Mmoja wa wale waliokaribishwa akauliza, ‘mbona mboga ni kidogo hivyo?’

Mpishi akajibu, ‘Mtakuwa mnachovya kwenye mchuzi kidogo, kwa sababu ni afadhali kula ugali wenye mchuzi kidogo kuliko kula ugali huo bila mboga kabisa.’

Baada kusikia hivyo, wale waliokaribishwa chakula hicho, walianza kula kwa kuchovya kidogo kidogo, mpaga mwishowe wakashipa. Ndiyo maana watu wakaanza kusema kama namna ya kutatua tatizo, kwamba, ‘kuchovya ugali katika mchuzi kidogo ni afadhali kuliko kula ugali bila mchuzi.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wanaopeana moyo wakati wa kusumbuliwa na shida hapa duniani. Ingawa mtu ana shida, yaani anakula ugali na mchuzi kidogo, ni afadhali kuliko mtu yule anayekula ugali bila mboga hata kidogo, ukurasa wa 25 wa kitabu cha Kueneza Injili kwa Methali.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti, Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Watafiti hao, waligundua kwamba, watu waliopata njia ya kutatua tatizo hata kama njia hiyo ni ndogo, wana unafuu kuliko wale ambao hawana njia ya kuwatatulia tatizo lao.

Watu hao, huwafundisha pia wenzao juu ya kutafuta njia za kuwawezesha kutatua matatizo yao, badala ya kubaki nayo tu. Ndiyo maana watu hao, huwaambia wenzao kwamba, ‘kuchovya ugali katika mchuzi kidogo ni afadhali kuliko kula ugali bila mchuzi.’

Methali hiyo, huwafundisha watu juu ya kupeana moyo wa kuvumilia hata kama wamo taabuni. Taabu na shida za hapa duniani zaweza kurahishwa kwa kuyaishi Maisha ya kufa na kufufuka pamoja na Yesu.

Yesu Kristo hakusema kwamba, wafuasi wake hawatapata taabu katika dunia hii, bali aliwahimiza kuchukua msalaba wao kila siku na kumfuata Yeye. Kwa maana hiyo, dhiki kubwa kuliko dhiki zote ni kutenganishwa na Mungu. Kama anavyosema Mtakatifu Paulo kwa Warumi 8:35. “Ni nani awezaye kututenga na mapendo ya Kristo? Je, ni dhiki, au mateso, au njaa, au ukosefu wa nguo, au hatari, au kuuawa?”

Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na mapendo ya Mungu wetu kwa njia ya Kristo Bwana wetu.” Dhambi peke yake inaweza kututenganisha na Mungu. Kueneza Injili kwa Methali ukurasa 25-26.

Zaburi 84:10. “Hakika siku moja katika njia zako ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani kwa Mungu wangu kuliko kukaa katika hema za uovu.”

Habakuki 3:17-18. “Ikiwa mtini hautachanua maua, wala mizabibu hamtakuwa na matunda; taabu ya mizeituni itakuwa bure na mashamba hayatoi chakula, zizini hamtakuwa na kundi, wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe walakini nitamfurahia Bwana, nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.”

Waebrania 12:1-11. “Msife moyo, wala msikate tamaa, maana katika kupambana na dhambi, ninyi hamjapigana mpaka kiasi cha kumwaga damu yenu.”

Marko 9:43-48. “Na jicho lako likikukosesha, ling’oe! Afadhali kuingia katika utawala wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yote mawili na kutupwa motoni.”

bhugali4

cooking

child eating food

 

ENGLISH: DIPPING UGALI IN A LITTLE SAUCE IS BETTER THAN EATING IT WITHOUT SAUCE.

The proverb comes from people who had ugali but lacked sauce. Those people kept on eating ugali without sauce because it was not easy to get it (sauce). One day the cook gave them little sauce to eat with ugali but one of the eaters asked as to why the sauce is too little. The response he/she got from the cook is ‘ dipping ugali in a little sauce is better than eating it without sauce.’

This proverb can be compared to people who give encouragement to one another in times of distress in this world. Although a person has a problem, it is better to simplify it so that one can see it as something that can be easily handled. See also Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 25 for more clarification on this proverb.

This book was written by researchers, Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and was published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984. In this book, researchers found that people can use even small items they have to solve their immediate problems. These problem solvers teach others about ways to solve their problems. They can use the limited resources they have to solve their own problems.

This proverb teaches people to encourage one another during distress times. As holy scriptures say, Jesus Christ did not say that His followers would not suffer in this world, but He encouraged them to take up their cross daily and follow Him. In that sense, the greatest tribulation is separation from God. As St. Paul states in Romans 8:35, “Who can separate us from the love of Christ? Shall it be tribulation, or distress, or famine, or nakedness, or peril, or death?

No creature can separate us from the love of our God through Christ our Lord. Sin alone can separate us from God (Refer Kueneza Injili kwa Methali) which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 25-26.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.