754. GUB´ISA MOTO UKUBHULWA LYOCHI.

Alihoyi munhu umo uyo agaja gujulomba moto habhuzenganwa aliyomba, “nalilomba moto nagazuge.” Unzenganwa ng’wiye agashosha, “nadina moto unene.” Aliyo lulu, aho lyakula ilikanza, lyuyufuma lyochi aha numba yiniyo aho wandya uguzuga ijiliwa, mpaka nose abhanhu bhudebha igiki alina moto. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagang’wila giki, “gub’isa moto ukubhulwa lyochi.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu ming´holo uyo adahayile gufunya jikolo jakwe gubhangi, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhimhaga abhiye ulu bhanomba ijikolo jakwe, kunguno ya wimimholo bhokwe. Uweyi agikalaga wimanile weyi duhu.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu uyo agang’wima moto unzenganwa okwe, kunguno nuweyi alimimholo ukubhiye, umukikalile kakwe. Giko lulu nuweyi agab´isaga ginhu ijo jidikomile ugub´iswa guti moto. Aliyo ilyochi hi ng´hanila yakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “gub’isa moto ukubhulwa lyochi.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleka nhungwa ja wiminholo, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwiyambilija chiza ijinaguitumama imilimo yabho. Igelelilwe bhabhize na witogwi bho gwidilila chiza, umuwikaji bhobho.

Yohana 3:20.

Warumi 2:16.

Mithali 28:13.

Zaburi 44:21.

KISWAHILI: KUFICHA MOTO UTAFICHULIWA MOSHI.

Alikuwemo mtu mmoja ambaye alienda kuomba moto kwa jirani yake akisema, “naomba moto nikapike.” Jirani yake alijibu, “mimi sina moto.” Lakini baada ya kupita muda, moshi ukaanza kutoka kwenye nyumba hiyo walipoonza kupika, mpaka watu wakaelewa kwamba, mwenye nyumba hiyo ana moto. Ndiyo maana wakaanza kumwambia kwamba, “kuficha moto utafichuliwa moshi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mchoyo, katika maisha yake. Mtu huyo hataki kutoa mali zake kwa wengine. Yeye huwakatalia wale wanaomuomba msaada kwa sababu ya uchoyo wake huo, wa kujijali yeye mwenyewe tu katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyemnyima moto jirani yake, kwa sababu naye huwanyima wale wanaoomba msaada wake. Hivyo basi, naye huficha hata kile kisichofichika kwa watu kama moto, kwa sababu ya uchoyo wake ambao hufichuliwa na moshi. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kuficha moto utafichuliwa moshi.”

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuachana na tabia ya uchoyo katika maisha yao, ili waweze kusaidiana vizuri katika kuyatekeleza majukumu yao. Wanatakiwa kuwa na upendo wa kuwajali wenzao vizuri katika maisha yao.

Yohana 3:20. “Kwa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe.”

Warumi 2:16. “Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za mioyo ya wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama isemavyo Injili yangu.”

Mithali 28:13. “Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali ye yote aziungamaye na kuziacha hupata rehema.”

Zaburi 44:21. “je,Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo?”

cooking

chungu na moto

bhakima bha ethiopia

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.