Ulusumo lunulo lwingine kuli munhu uyo agalingaga ndimu bho gutumila bhuta na masonga. Ubhuta bhunuyo guli nti uyo gugagondagwa bho gutungilwa luge lo ndimu, ulo agaludutaga unasi bho gutumila lisonga naolasa.
Ubhuta bhunubho, bhudulile gubhinzika kunguno ya gubhugonda bho gutumila luge. Ulubhubhinzika unasi agupandika bhungi kunguno uluge osagaga nalo. Hunagwene agayombaga giki, “bhuta bhinzika undekele luge lwane.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ochilagwa na ng’wana okwe. Umunhu ng’uwunuyo agapinihalaga noyi kunguno ya kuzumalikilwa na ng’wana okwe ng’wunuyo. Abhanhu bhaganungujaga bho gung’wila giki, agubyala ng’wana ungi kunguno nuweyi alihoyi.
Ung’wana ng’wunuyo, agikolaga nu bhuta ubho bhugabhinzikaga, kunguno nu ng’wana ozumalikaga. Ulu luge, lugikolaga nu nina ong’wana, kunguno nuweyi iki osagaga adulile gubyala ng’wana ungi. Hunagwene abhanhu bhagayomgaga giki, “bhuta bhinzika undekele luge lwane.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilija bho guchola nzila ja guginja amakoye ayo bhalinago, umukikalile kabho, na gubhalunguja bhichabho abho bhatali mumakoye, kugiki bhadule guyega kihamo, umuwikaji bhobho.
Mwanzo 2:18-23.
Marko 10:7.
KISWAHILI: UPINDE VUNJIKA UNIACHIE UGE(KAMBA YA MSHIPA WA MNYAMA) WANGU.
Methali hiyo ilianzia kwa mtu aliyekuwa akiwinda wanyama kwa kutumia upinde. Upinde huo ni mti ambao hukunjwa kwa kufungwa uge au mshipa wa mnyama, ambao huvutwa na mwindaji kwa kutumia mshale ndipo ana urusha mshale wake anapoachia.
Upinde huo unaweza kuvunjika kwa sababu ya kukunjwa na uge au kamba ya mshipa wakati wa kuurusha mshale huo. Upinde huo ukivunjika mwindaji hupata mwingine kwa sababu amebaki na ile kamba ya mshipa. Ndiyo maana husema, “upinde vunjika uniachie uge au kamba yangu.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye amefiwa na mtoto wake. Mtu huyo, huhudhunika sana, kwa sababu ya kuachwa na mtoto wake huyo wa pekee kwake. Watu humfariki kwa kumwambia kwamba, atazaa mtoto mwingine kwa sababu yeye yupo.
Mtoto huyo hufanana na upinde ambao huvunjika, kwa sababu naye mtoto amefariki. Uge au kamba hiyo ya mshipa hufanana na mama mzazi wa mtoto, kwa sababu naye amebaki kwa hiyo, anaweza kuzaa mtoto mwingine. Ndiyo maana watu husema kwamba, “upinde vunjika uniachie uge au kamba yangu.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilifu wanapopatwa na matatizo, na kuwafariji wenzao, ambao bado wako kwenye matatizo ili waweze kuishi kwa furaha, maishani mwao.
Mwanzo 2:18-23. “BWANA Mungu akasema, ‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wakumfaa.’’ Basi BWANA Mungu alikuwa amefanyiza kutoka katika ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lo lote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani na wanyama wote wa porini. Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake akapafunika mahali pale kwa nyama. Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume. Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.’’”
Marko 10:7. “Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’”
ENGLISH: BOW BREAK; LEAVE FOR ME MY STRING.
This saying originated from a man who was hunting animals by using a bow. The bow is made of a curved piece of wood joined at both ends by a taut string or a fibrous material extracted and dried from a dead animal skin, which is used as a bow string which the hunter pulls after attaching to it an arrow that he releases after extending the string to the maximum.
The bow can be broken as a result of being pulled by the hunter when he shoots the arrow. If the bow breaks, the hunter will find another one because he is left with the string. That is why he says, “bow break; but leave for me my string.”
This saying is compared with a person who loses a child in death. Such person becomes unhappy because he has lost the only child one had. However, people comfort such a person by telling her that she will give birth to another child because she is there.
In this context, the child who dies is like a bow that is broken. The string is similar to the baby’s mother, because she too has survived so she can give birth to another baby. That is why people say, “bow break; but leave for me my strinf.”
This sayinf teaches people on how to be patient when they are in trouble, and to comfort others, who are still in trouble, so that they can live happily.
Genesis 2: 18-23. Mark 10: 7.