747. DUGULIMA HANGI LILALE LIDACHILE.

Ulusumo lunulo lwingilile kuli munhu uyo agalimaga jiliwa umutumami bhokwe oduma ugupandika. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga na wisaguzu bho gupandika jiliwa bhuli ng’waka.

Uweyi miaka yingi agakelaga bho gupandika jiliwa jigehu, nulu onoga ogayiwa gete nulu jigehu. Ulu ogayiwa, nulu abisha jiliwa jamalwa majilili, adagwaga ng’holo ugulima ulu goshiga hangi ung’waka kunguno atali nalyo ililale. Hunagwene agayombaga giki, “dugulima hangi lilale lidachile.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa ku bhanhu abho bhagapandika makoye ayo galikihamo na guchilwa na bhana bhobho, nulu gutajiwa jikolo jabho na masambo, umuwikaji bhobho. Abhanhu bhenabho bhagiyumilija bho gutumama milimo yabho chiza, kunguno bhalina wisagizu bho gupandika hangi. Abhoyi bhadagwaga ng’holo ugubhutumila ubhupanga bhobho ubho bhali nabho, iki bhadingijiwe.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga nu nimi uyo agagayiwaga ijiliwa ulu olima, aliyo agikomeja gulima hangi umusi iyo alinayo, kunguno nabhoyi, bhadagwaga ng’holo ulu bhapandika makoye umuwikaji bhobho. Hunagwene bhagabhawilaga abhichabho giki, “dugulima hangi lilale lidachile.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilija bho guchola nzila ja guginja amakoye ayo bhalinago, umukikalile kabho, na gubhalunguja abhichabho abho bhatali mumakoye, kugiki bhadule guyega kihamo, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 2:18-23.

Marko 10:7.

KISWAHILI: TUTALIMA TENA ENEO {ARITHI} HAIJAFA.

  Methali hiyo, ilianzia kwa mtu yule aliyekuwa akilima mazao mbalimbali katika utendaji wake wa kazi. Mtu huyo, alikuwa na matumaini ya kupata mazao mengi kila mwaka anapolima.

 Lakini miaka mingine alipata chakula kidogo na pengine alikosa kabisa. Yeye alipokosa au alipopata mazao yakaliwa na wadudu, alikuwa havunjiki moyo wa kuendelea kulima kwa sababu eneo la kulima bado analo. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “tutalima tena ardhi bado haijafa.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wale ambao hupata matatizo katika maisha yao, yakiwemo yale ya kukosa chakula au kufiwa na watoto wao. Watu hao, huvumilia matatizo yao kwa kuendelea kufanya kazi kwa sababu nguvu bado wanazo. Wao huwafundisha pia wenzao namna na kutokukata tamaa katika utendaji wao wa kazi hata kama watapata matatizo makubwa kiasi gani.

Watu hao, hufanana na mkuliwa yule aliyekosa chakula, lakini akaendelea kulima kwa vile ardhi alikuwa nayo bado, kwa sababu nao wanauvumilivu wa kuendelea kuutumia uhai wao katika kuyateleza vizuri majukumu yao. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “tutalima tena ardhi bado haijafa.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilifu wanapopatwa na matatizo, na kuwafariji pia wenzao, ambao bado wako kwenye matatizo ili waweze kuyamaliza na kuishi kwa furaha, maishani mwao.

Mwanzo 2:18-23. “BWANA Mungu akasema, ‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wakumfaa.’’ Basi BWANA Mungu alikuwa amefanyiza kutoka katika ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lo lote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani na wanyama wote wa porini. Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake akapafunika mahali pale kwa nyama. Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume. Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.’’”

Marko 10:7. “Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’”

farmer african-girl

woman-farming

farmer1

ENGLISH: WE WILL CULTIVATE AGAIN, THE FIELD IS NOT DEAD.

 The above proverb began with the man who was cultivating various crops in his field hoping to reap bountifully each year.

 But it was not happening so always, because in some years he got little yield or got nothing at all. Despite the fact that he got little or never got anything at all, or his crops were infested with pests, he was not discouraged from cultivating his field because he still had the field to cultivate again. That is why he would tell people, “we will cultivate again, the field is not dead.”

This proverb is likened with those who suffer from poor health, including malnutrition or are depressed because of the death of their children. These people endure their problems by continuing to work because they still have the strengths. They also teach their colleagues how to be consistent and not give up in their work, no matter how difficult the challenges may be.

These people are like the man who was harvesting less or who would not harvest anything but continued to cultivate because he still had the field. These peole are like him because they also have the patience that makes them fulfil their responsibilities. That is why such people are not discouraged in what they are doing, rather they tell the people, “we will cultivate again, the field is not dead.”

This proverb teaches people on how to be patient when they are in trouble, and also to comfort others, who are still in trouble so that they can go through such troubles with hope that they will one day end thus live happily in their lives.

Genesis 2: 18-23. Mark 10: 7.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.