Ulusumo lunulo, lulolile Si na bhubhipi bhoyo. Isi iyoyi igikalaga numo ili duhu, kunguno idagaluka ilihanga lyayo gitumo bhagalukilaga abhanhu bho gwingila mu bhusoga mpaga mu ilihanga lya bhubhi. Hunagwene abhanhu bhagayomgaga giki, “Si idabhipaga.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile akakulile ka bhanhu, umuwikaji bhokwe. Abhanhu bhagingilaga mubhunigini ulu bhabyalwa. Ahikanza linilo bhagabhiza ni hanga lyawiza kunguno bhatali bhaniki nulu bhayanda. Aliyo lulu, ili hanga lyabho ligajaga lyubhipa ulu bhandya ugunamhala abhayanda, nulu ugugiguluha abhanike.
Gashinaga lulu, akakulile ka bhanhu kagingila kubhuyanda nulu kuwaniki, kaja mpaga kubhunamhala, nulu kubhugikulu, uko bhagabhipile abhanhu abho bhali bhasoga aho bhatali bhadoo.
Abhanhu bhanebho bhagamanaga bhuphipa hado hado nose mpaga bhazumalika, bhajikwa musi, iyo bhagaiyeka mumo ili duhu. Ukubhunamhala nulu ikubhugikulu ili kwihanga lyabhub’i. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “Si idab’ipaga.’
Ulusumo lunulo, lolanga abhanhu higulya ya gubhiza na bhutogwa bho bhugwikala na bhanhu bhose, umukikalile kabho kunguno bhuli ng’wene alab’ipa duhu ulu unamhala, nulu ulu ugiguluha, kugiki bhadule gwiyambilija chiza, umuwikaji bhobho.
Mwanzo 6:11-12.
Mathayo 23:37-39.
Luka 13:34-35.
KISWAHILI: ARDHI HAIHARIBIKI.
Methali hiyo, huangalia ardhi na uhalibikaji wake. Ardhi hiyo, huwa kama ilivyo siku zote kwa sababu yenyewe haibadiliki kama walivyo wanadamu. Uso wa ardhi haikui kama wanavyokuwa watu ambao huwa na sura nzuri wakati wakiwa kwenye rika la ujana wao ambao huharibika, na kuwa na muonekano mbaya wanapofikia kwenye rika lao la uzeeni. Ndiyo maana watu husema kwamba, “ardhi haiharibiki.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anaelewa ukuaji wa watu katika maisha yake. Watu hao hutokea kwenye hali ya rika la uzuri ambalo ni la ujana, hadi kwenye rika lenye muoneno mbaya ambalo ni la uzeeni. Hivyo sura za watu huendelea kuwa mbaya kwa kadiri wanavyozidi kuzeeka, maishani mwao.
Kumbe basi, ukuaji wa watu huanzia kwenye kuzaliwa, kuelekea ujanani, hadi kwenye uzee kule ambako sura zao hubadilika na kuwa mbaya. Watu hao huendelea kuwa na sura mbaya, mpaka mwishoni hufariki dunia na kuzika ndani ya arbhi ambayo hupaki kama ilivyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘ardhi haiharibiki.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na upendo wa kuishi na watu wote vizuri, katika maisha yao, kwa sababu kila mmoja ataonekana kuwa mbaya akifika kwenye rika la uzeeni, ili waweze kuishi kwa uelewano, maishani mwao.
Mwanzo 6:11-12. “Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na jeuri machoni pa Mungu. Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao.”
Mathayo 23:37-39. “Ee Yerusalemu, mnaowaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hukutaka! Tazama nyumba yako imeachwa tupu na ukiwa. Kwa maana nawaambia, hamtaniona tena mpaka siku ile mtakaposema, ‘Amebarikiwa Yeye ajaye kwa Jina la Bwana.´”
Luka 13:34-35. “Ewe Yerusalemu, Yerusalemu, weweuwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hamkutaka! Tazama nyumba yenu inaachwa ukiwa, ninawaambia hamtaniona tena mpaka wakati ule mtakaposema, “Amebarikiwa Yeye ajaye katika Jina la Bwana.’””
ENGLISH: THE EARTH DOES NOT ROT.
This saying looks at the Earth and its incorruptibility. This is because it is always the same; it does not change as humans do. The surface of the Earth does not grow old as do people who are in good shape when they are in their youth, but have a bad appearance when they get old. That is why people say that “the Earth does not rot.”
This saying is compared with a person who understands how times change when it comes to human beings’ life. People may be young, beautiful or handsome today, but they get old in course of time. So the appearance of people is not like that of the Earth which is more or less permanent as it continues to deteriorate as they get older.
The human beings’ life extends from birth, through adolescence, into adulthood where their physical appearance changes. Over time, these people changes as they become old and therefore lose their good appearance. They keep on changing appearance wise until at last they die and are buried in the Earth which remains as it is. That is why people say, “The Earth does not rot.”
This saying teaches people how to live peacefully with all people because everyone will look bad when they reach old age. So no one is better than the other.
Genesis 6: 11-12. Matthew 23: 37-39 Luke 13: 34-35.