749. WELELO IDANAMHALAGA.

Ulusumo lunulo, lwingile kumahoya ga bhanhu higulya ng’wa Welelo. Umumahoya gabho genayo, munhu umo agayomba, “Welelo alina nguzu ijo jidashilaga makanza gose, kunguno agabhalang’hanaga bhose, bhanigini na bhakuji.” Ung’wiye agashosha, “inguzu ja ng’wa Welelo jidashilaga kunguno Uweyi adanamhalaga guti bhanhu abho bhagamalaga inguzu jabho ulu bhakula.” Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “Welelo idanamhalaga.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo abhumanile ubhudula bho ng’wa Welelo ubho gujilabhila chiza pye ijisumva jakwe. Umunhu ng’wunuyo, ang’wisanije Welelo umubhutumami bhokwe bhose, ubho bhugang’wenhelaga mafumilo mingi, umukikalile kakwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu inzila ja gunsendamila Welelo umubhutumami bhobho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi shiju jose.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhanhu abho bhahoyelaga higulya ya nguzu ja ng’wa Welelo ijo jidashilaga, kunguno nuweyi, ang’winsanije Welelo umubhutumami bhokwe bhose. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “Welelo idanamhalaga.”

 Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gunzunya Welelo bho gung’wisanya weyi umubhutumami bhobho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umumilimo yabho, shiku jose.

KISWAHILI: MUNGU HAZEEKI.

Methali hiyo, ilitokea kwenye maongezi ya watu waliokuwa wakiongelea juu ya Mungu. Mmoja wao, katika maongezi hayo, alisema, “Mungu ana nguvu ambazo haziishi wakati wote, kwa sababu Yeye huwalinda watu wote watoto na wazee.” Mwenzake alijibu, “nguvu za Mungu haziishi kwa sababu Yeye hazeeki kama wanadamu walivyo, ambao nguvu zao hupungua wanapozeeka.” Ndiyo maana watu husema kwamba, “Mungu hazeeki.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anauelewa uwezo wa Mungu ambao huvilinda viumbe vyakwe vyote. Mtu huyo, humtegemea Mungu katika utekelezaji wa majukumu yake yote, ambaye humpatia mafanikio mengi, maishani mwake. Yeye huwafundisha pia wenzake namna ya kumtegemea Mungu katika kazi zao, ili waweze kupata mafanikio mengi, siku zote.

Mtu huyo, hufanana na wale watu waliokuwa wakiongelea juu ya uwezo wa Mungu ambao hauishi, kwa sababu naye, humtegemea Mungu katika utendaji wa kazi zake zote. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “Mungu hazeeki.”

Methali hiyo, huwafundisha watu juu ya kumwamini Mungu kwa kumtegemea Yeye katika utekelezaji wa majukumu yao yote, ili waweze kupata mafanikio mengi katika kazi zao, maishani mwao.

Mwanzo 6:11-12. “Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na jeuri machoni pa Mungu. Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao.”

Mathayo 23:37-39. “Ee Yerusalemu, mnaowaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hukutaka! Tazama nyumba yako imeachwa tupu na ukiwa. Kwa maana nawaambia, hamtaniona tena mpaka siku ile mtakaposema, ‘Amebarikiwa Yeye ajaye kwa Jina la Bwana.´”

Luka 13:34-35. “Ewe Yerusalemu, Yerusalemu, weweuwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hamkutaka! Tazama nyumba yenu inaachwa ukiwa, ninawaambia hamtaniona tena mpaka wakati ule mtakaposema, “Amebarikiwa Yeye ajaye katika Jina la Bwana.’””

bhabhini bha benini

berber older

musicians-older

ENGLISH: GOD DOES NOT GROW OLD.

This saying came from the conversation of people who talked about God. In the conversation one of them said, “God has power that does not last forever, because He protects all people, young and old.” His companion replied, “The power of God exists because He does not grow old like the human race, whose vigour decreases with age.” That is why people say, “God does not grow old.”

This saying is likened with a man who understands the power of God that protects all his creatures. That person depends on God in discharging all of his responsibilities, he also teaches his fellow human beings on how to rely on God in what they are doing so that they can always be more successful.

That person is like those people who were talking about the inexhaustible power of God in whatever a human being does. That is why he tells people, “God does not grow old.”

This saying teaches people to trust in God by relying on Him in the discharge of all their responsibilities. By doing so, they are always more successful in what they are doing than those who do not.

Genesis 6: 11-12. Matthew 23: 37-39 Luke 13: 34-35.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.