750. UBHIPE B´EB`E NTOJI, NTOLWA ATI NA MHAYO.

Ulusumo lunulo lwingine kuli munhu uyo ocholaga nhola. Uweyi omanaga uja agubhuja kubhanhu kugiki bhang’olekeja unkima uyo ali owiza. Umunhu ng’wunuyo abhabhujaga bhanhu, “ali ng’wanani unkima uyo aliowiza nagantole umuchalo jiniji?” Munhu umo aganshokeja, “alihoyi akaya iyaho.” Uweyi agabhuja hangi, “unkima ng’wunuyo alina nhungwa jawiza ahene?” Abhiye bhung’wila, “ubhipe b’eb’e ntoji, ntolwa ati na mihayo.”

Ulusumo lunulo, lugelenganijiyagwa kuli munhu uyo agapandikaga ginhu jawiza ojikenagula, nulu uyo agapandikaga bhanhu bhawiza, aliyo uweyi adamanile ugubhalangaha abhanhu bhakwe bhenabho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agajikenagulaga sagala ijikolo ijawiza kunguno ya nhungwa jakwe ijo jidijawiza. Uweyi hangi agabhasalambanyaga abhanhu abho agikalaga nabho, kunguno ya gubhitila ibhengwe umukikalile kakwe.

 Abhanhu bhagang’wikolanijaga nuyo ocholaga kutola umpandika unkima uowiza, bhusaga ubhubhi gwigela kuliweyi duhu, kunguno nuweyi agapandika bhanhu abho bhalibhawiza, obhasambaja kubhitila ku nhungwa jakwe ijo jili jabhubhi. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ubhipe b’eb’e ntoji ntolwa ati na mhayo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gub’iza na nhungwa ja bhutogwa bho gubhambilija gwikala chiza na bhanhu, umukaya jabho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhanhu bhabho. Igeleliwa bhilange ugwikala chiza, bho gujilang’hana ijo bhali najo.

Mathayo 19:12.

KISWAHILI: UWE MBAYA WEWE MWOAJI, MWOLEWA HANA NENO.

Methali hiyo ilianzia kwa mtu yule ambaye alikuwa akitafuta mwanamke wa kuoa. Mtu huyo, katika kutafuta kwake alikuwa akiuliza watu ili wamuoneshe aliko mwanamke ambaye ni mzuri. Aliuza watu, “yuko kwa nani mwanamke ambaye ni mzuri nimuoe kwenye kijiji hiki?” Mwenyeji mmoja akamjibu, “yuko kwenye familia yile.” Yeye akazidi kuuliza, “mwanamke yule anatabia njema?” Watu wakamjibu, “uwe mbaya wewe mwoaji, mwolewa hana neno.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hupata vitu vizuri, lakini hushindwa kuvitunza, au hupata watu wema lakini hushindwa kuishi nao kwa sababu ya tabia yake mbaya, katika maisha yake.

Mtu huyo, hushindwa kuvitunza vitu vyake, kutokanam na mwenendo wake wa kuviharibu kwenye matumizi yasiyofaa. Yeye pia, huwasambalatisha watu anaoishi nao kwa sababu ya tabia yake ya kuwadharau wale anaoishi nao.

Watu humfananisha na mtu yule aliyekuwa akitatufa mwanamke mzuri wa kuoa, ambaye ubhaya ulibakia kwake tu, kwa sababu naye huwapata watu wenye tabia njema, lakini huwasambaza kwa kushindwa kuishi nao vizuri. Ndio maana watu humwambia, kwamba, “uwe mbaya wewe mwoaji, mwolewa hana neno.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia zenye upendo wa kuishi na watu kwa amani, kwenye familia zao, ili waweze kusaidiana vizuri maishani mwao. Wanatakiwa kujifunza namna ya kuishi na watu wao, kwa kuvitunza vile walivyo navyo.

Mathayo 19:12. “Kwa maana wengine ni matoashi kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine wamefanywa matoashi na wanadamu na wengine wamejifanya matoashi kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni. Yeye awezaye kulipokea neno hili na alipokee.”

samburu-wedding

africa wedding

traditional-wedding

ENGLISH: THE WOMAN WHO WANTS TO MARRY YOU IS READY MAY BE YOU YOURSELF ARE NOT READY.

This proverb began with the man who was looking for a woman to marry. Such man, in his search, was asking people to show him where the best woman was. He sold his idea to the people, “Who is the best woman to marry in this village?” One host replied, “She is in that family.” He kept asking, “Is that a good woman?” The people answered him, “The woman who wants to marry you is ready may be you yourself are not ready.”

 This proverb is compared with a person who finds good things, but fails to take care of them, or finds good people but fails to live with them because of his bad behaviour in his life.

Such person, in turn, fails to take care of his or her belongings, due to his or her tendency to ruin them for improper use. He, too, stigmatizes the people he lives with because of his contempt for those around him.

People liken him with a man who wanted to marry a beautiful woman, but had a bad behaviour because he could find women of good character and fail to live with them well. That’s why people say to him, that, “The woman who wants to marry you is ready may be you yourself are not ready.”

This proverb teaches people to have habits of living peacefully with people in their families, so that they can help each other in their lives. They need to learn how to live with their people, by taking care of them as they are.

Matthew 19:12.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.