745. DUMOGAGI JUZWA.

Ulusumo lunulo, lwingine kubhanhu abho bhimogaga nzwili jabho. Inzwili ja abhanhu bhenabho, jamanaga juzwa ulubhajimoga, golecha giki bhuli ng’wene atali na bhulamu ubho gwikala ukuwelelo. Aho bhadebha chene, bhuyilombela gubhiza na mbango ja bhulamu bhuli ng’wene kugiki bhamane bhibhona na gwilomela kihamo umukikalile kabho. Hunagwene bhagayiwila giki, “dumogaji juzwa.”

 Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhalombelaga mbango ja gwikala mhola, abhanhu abho agikalaga nabho, umubhulamu bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, adebhile ugwikala bho bhutogwa na bhiye. Uweyi ali na bhidohya bho gulomba bhulamu gwingila kuli Ng’winikili bhupanga, Uwelelo, kunguno adebhile igiki imbango jigafumilaga kuli Weyi.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhanhu abho bhimogaga na gwilombela mbango ja gwikala na bhuyeji, kunguno nuweyi agabhalombelaga mbango ja gwingila kuli Mulungu abhiye, umuwikaji bhokwe.

Uweyi hangi agabhalangaga abhanhu bhakwe higulya ya gwikala na witogwi bho gwilombela mbango kugiki bhikale mhola, umubhulamu bhobho. Hunagwene agabhawilaga abhiye giki, “dumogaji juzwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutogwa bho kubhalombela mbango ja gwikala chiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gwendelea gutumama milimo yabho na bhuyegi, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 45:28.

Waamuzi 19:3.

2 Wakorintho 2:13.

KISWAHILI: TUNYOENI ZIKIOTA.

Methali hiyo, ilianzia kwa watu waliokuwa wakinyoana nywele zao. Nywele za watu hao, zilikuwa zikiota wanapozinyoa, kuonesha kwamba kila mmoja bado ana uhai wa kuishi hapa duniani.

Walipoelewa hivyo, walianza kuombeana baraka za kuishi maisha marefu, ili waendelee kuonana na kuongea pamoja katika maisha yao. Ndiyo maana waliambiana kwamba, ‘tunyoeni zikiota.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwaombea baraka za kuishi salama watu anaoishi nao, katika uhai wake. Mtu huyo, anaelewa kuishi kwa upendo na wenzake.

Yeye ana upendo wa kuwaombea wenzake baraka za kutoka kwa Mungu, kwa sababu ya uelewa wake, kwamba, Mungu ndiye mwenye baraka hizo, ili waendelee kuishi kwa amani, maishani mwao.

Mtu huyo, hufanana na watu wale waliokuwa wakinyoana na kuombeana baraka za kuishi kwa furaha, ili waendelee kuwa na amani maishani mwao, kwa sababu naye huwaombea wenzake anaoishi nao, baraka za kutoka kwa Mungu, maishani mwake.

Yeye huwafundisha pia watu wake juu ya kuwa na upendo wa kuombeana baraka za kutoka kwa mwenyezi Mungu, ili waendelee kuishi kwa amani. Ndiyo maana huwaambia wenzake kwamba, “tunyoeni zikiota.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na upendo wa kuombeana baraka za kutoka kwa Mungu, ili waweze kuendelea kuonana na kuyatekeleza vizuri majukumu yao, maishani mwao.

Mwanzo 45:28. “Ndipo Israeli akasema, “Nimesadiki! Mwanangu Yosefu bado yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa.’’”

Waamuzi 19:3. “mume wake akaenda kumsihi ili arudi. Alikwenda na mtumishi wake na punda wawili. Yule mwanamke akamkaribisha nyumbani mwa baba yake, baba yake alipomwona akamkaribisha kwa furaha.”

2 Wakorintho 2:13. “bado nilikuwa sina utulivu akilini mwangu kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao nikaenda Makedonia.”

africa lady2

african-lady

africa lady

ENGLISH: LET US SHAVE OUR HAIR IT WILL GROW.

This saying began with people who were cutting their hairs. The hairs of these people were growing whenever they had been shaved, showing that every one of them was still alive on this earth.

When they understood this, they began to pray for each other for blessings so that they live longer enough to enable them to continue to see eath other and talk together in their lives. That is why they said to one another, “Let us shave our hair it will grow.”

This saying is likened with a man who prays for the blessings to live safely with the people he lives with. He loves to pray for his fellows for blessings from God, because of his understanding, that God is the one who has those blessings. He does so that they may continue to live peacefully in their lives.

This person is like those people who used to shave and pray for the blessings of living happily, so that they could continue to have peace in their lives. This is because he also prays for his companions who live with him, so that they can get God’s blessings in their lives.

He also teaches his people to love one another and to pray for one another’s blessings from God, so that they may live in peace. That is why he tells his companions: “let us shave our hair it will grow.”

This saying teaches people how to love one another and pray for one another for blessings from God, so that they can continue to see each other and fulfill their responsibilities in their lives.

Genesis 45:28. Judges 19:3. 2 Corinthians 2:13.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.