742. UGUB´INAGA WISAGILILE ULU UKABHONILE UDUKALEKA.

Ulusumo lunulo, lulolile nguno ya ng’wa munhu uyo agub’inaga mbina. Inguno yakwe yiniyo igang’winhaga wisagizu bho gujipandika ijo ajihayile jinijo umubhutumami bhokwe.

Olihoyi munhu uyo ob’inaga mbina kunguno ya kuchola nyiye bhitole. Umunhu ng’wunuyo, agikomeja noyi ub’ina mbina yiniyo, mpaga nose umpandika ung’wiye bhitola, naoya lulu ugub’ina. Hungwene abhanhu bhang’wilaga giki, “ugub’inaga wisagilile ulu ukabhonile udukaleka.”

Ulusumo lununo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe na wisagizu bhutale bho gupandika matwajo mingi, umubhutumami bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agikomeja noyi uguitumama imilimo yakwe na bho bhukamu bhutale, kunguno amanile igiki agupandika ijo alijichola.

Uweyi agabhalanjaga na bhanhu bhakwe inzila ja gwikomeja uguitumama imilimo yabho na wisagizu bho gupandika matwajo mingi. Kunzila yiniyo, agapandika amatwajo mingi noyi, umuwikaji bhokwe, ayo gagenhagwa na uwisagizu bhokwe bhunubho, ubho bhugang’winaga nguzu ja gwikomeja kutumama milimo yakwe mpaka ojipandika ijo alijichola.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu mini ombina uyo ob’inaga na wisagizu bhutale bho gupandika ng’wiye ogwitola nang’hwe mpaka nose umpandika, kunguno nuweyi agatumamaga milimo yakwe na wisagizu bhutale mpaka opandika matwajo mingi umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki,  “ugub’inaga wisagilile ulu ukabhonile udukaleka.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gutumama milimo yabho na wisagizu bho gupandika matwajo mingi, umubhutumami bhobho, kugiki bhadule guitumama imilimo yabho na bhukamu bhutale mpaka bhapandika matwajo gagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 13:45-46.

Mathayo 10:10.

Mithali 6:23.

1 Wakorintho 9:23-27.

1 Yohana 3:2-3.

Luka 18:28-29.

Sala ya gwisagila

Mathayo 19:27-29.

KISWAHILI: UNACHEZA KWA MATUMAINI KAMA UMEKAONA HUTAKAACHA.

Methali hiyo, huangalia lengo la mtu anayecheza ngoma. Lengo hilo, humpatia matumaini ya kukipata kile anachokitaka, katika utendaji wake wa kazi. Alikuwepo mtu mmoja ambaye alikuwa anacheza ngoma kwa lengo la kumpata mwenzake wa kuoana naye.

Mtu huyo, alijibidisha kucheza ngoma hiyo, mpaka mwishowe akafanikiwa kumpata mwenzi huyo wa maisha, wakaoana, ndipo alipoacha kucheza ngoma hizo. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “unacheza kwa matumaini kama umekaona hutakaacha.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi zake kwa matumaini makubwa ya kupata mafanikio mengi, katika utendaji wake. Mtu huyo, hujibidisha kuzitelekeza vizuri kazi zake hizo, na kwa bidii kubwa kwa sababu anayo matumaini makubwa ya kufanikiwa.

Yeye huwafundisha pia wenzake njia za kujibidisha katika utekelezaji wa majukumu yao, wakiwa na matumaini ya kufanikiwa zaidi. Kupitia njia hizo, yeye pia hupata mafanikio mengi katika maisha yake, yatokanayo na kuwa na matumaini makubwa ambayo humpatia nguvu za kuyatekeleza vizuri majukumu yakwe.

Mtu huyo, hufanana na mcheza ngoma aliyekuwa aliyecheza huku akiwa na matumaini makubwa ya kumpata mwenzi wake wa maisha mpaka akampata, kwa sababu naye huyatekeleza majukumu yake kwa matumaini makubwa ya kufanikiwa kuyafikia malengo yake, maishani mwake. Ndiyo maana watu, humwambia kwamba, “unacheza kwa matumaini kama umekaona hutakaacha.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyatekeleza majukumu yao wakiwa na matumaini makubwa ya kufanikiwa katika utendaji wao, ili waweze kuongeza bidii ya kuwapatia mafanikio ya kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Mathayo 13:45-46. ‘‘Tena, Ufalme wa Mbinguni unafanana na mfanya biashara aliyekuwa akitafuta lulu safi. Alipoipata lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza vyote alivyokuwa navyo akainunua.”

Mathayo 10:10. “Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtenda kazi anastahili posho yake.”

Mithali 6:23. “Kwa maana maagizo haya ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,”

1Wakorintho 9:23-27. “Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nipate kushiriki baraka zake. Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo. Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji isiyodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji idumuyo milele. Kwa hiyo mimi sikimbii kama mtu akimbiaye bila lengo, sipigani kama mtu anayepiga hewa, la, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha ili nikishawahubiria wengine, mimi nisiwe mtu wa kukataliwa.”

1 Yohana 3:2-3. “Wapenzi, sasa tu watoto wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba, Yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. Kila mmoja mwenye matumaini haya katika Yeye hujitakasa, kama vile Yeye alivyo mtakatifu.”

Luka 18:28-29. “Ndipo Petro akasema, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwanavyo tukakufuata!” Yesu akajibu, “Amin nawaambia, hakuna hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu”

Sala ya matumaini

Mathayo 19:27-29. “Ndipo Petro akamjibu, ‘‘Tazama, sisi tumeacha kila kitu na kukufuata, tutapata nini basi?’’ Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia , wakati wa kufanywa upya vitu vyote, wakati mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake cha utukufu cha enzi, ninyi mliomfuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli. Kila mmoja aliyeacha nyumba au ndugu zake wa kiume au wa kike au baba au mama au watoto au mashamba kwa ajili Yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo na ataurithi uzima wa milele.”

man dance botswana

dancers

people-

ENGLISH: YOU DANCE WITH A GOAL TO ACHIEVE.

This proverb focuses on the goal of the dancer. The goal that gives him some hope of achieving what he wants, in his career. There was one man who was dancing with the intention of finding a mate to marry him.

He danced until he finally managed to find the life partner. They got married, and then he stopped dancing. Of such a person, people woud “You dance with a goal to achieve, unless you realise it, you will not stop.”

This proverb is likened with a man who performs his duties with high hopes of achieving great success. Such person never loses hope because he expects to achieve something great.

He also teaches his colleagues how to work hard when discharging their duties. Through these means, he realises many successes in life, because he has high anticipations something that gives him strength to carry out his responsibilities effectively.

The above man is like the dancer who played with high expectations of finding his life partner until he found her. He succeeded because he fulfilled his responsibilities with the great hope of achieving his goal. That’s why, when people people make reference to people like that they would say, “You dance with a goal to achieve, unless you realise it, you will not stop.”

This proverb teaches people on how to fulfill their responsibilities with high anticipations of succeeding

Matthew 13: 45-46 Matthew 10:10 Proverbs 6:23. 1 Corinthians 9: 23-27 1 John 3: 2-3. Luke 18: 28-29 Prayer of hope, Matthew 19: 27-29.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.