743. OBHUKIJAGA MULI PUNDUKILE.

Olihoyi munhu uyo oliabhuchije jiliwa ja guchala hanhu. Aliyo lulu, ijiliwa jinijo jamanaga jugeha duhu, umu lugendo lokwe. Nose uibhuja bhung’wene, “ni bhuli unigo gone guli geha chiniki?”  Munhu umo uyo alihanuma yakwe ujibhona ijiliwa ijo jidikaga umunzila, ung’wila, “obhukikaja mulipundukile.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga nimo uyo gudina na solobho yose yose, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’winuyo agajimijaga makanza gakwe bho nduhu solobho, ukunhu alijimala sagala ni nguzu jakwe. Uweyi agamalaga nguzu jakwe bho nduhu gupandika solobho yose yose.

Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga nimo uyo gudikilile nu munhu uyo obhukijaga jiliwa jakwe muli ginhu ilo lipundukile, kunguno nuweyi agatumamaga nimo uyo gudina solobho, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga umunhu ng’wunuyo giki, “obhukikaja mulipundukile.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka gutumama milimo iyo idina solobho yose yose, kunguno munho bhagujimija makanza gabho sagala. Gashinaga lulu, igelelilwe bhaisolanye imilimo iyo idulile gubhenhela solobho ningi, hunabhayitumame lulu iyiniyo, umuwikaji bhobho.

Hagai 1:6.

Mhubiri 2:11.

Isaya 49:4.

Yeremia 12:13.

Luka 17:10.

1 Wathesalonike 3:5.

Tito 3:9.

Luka 10:38-42.

Luka 16:16-20.

KISWAHILI: UMEBEBEA KWENYE CHOMBO KILICHOTOBOKA.

Alikuwepo mtu aliyebeba chakula akikipeleka sehemu fulani. Lakini, chakula hicho kilikuwa kikizidi kupungua tu katika safari yake hiyo. Mwishowe akaanza kujiuliza mwenyewe, “kwa nini mzigo wangu unazidi kupungua?” Mtu mmoja aliyekuwepo nyuma yake akakiona chakula hicho kilichokuwa kikimwagika, akamwambia, “umebebea kwenye chombo kilichotoboka.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi isiyo na faida yoyote, katika maisha yake. Mtu huyo, hupoteza wakati wake bure, huku akizimaliza hovyo nguvu zake hizo. Yeye huzimaliza nguvu zake hizo kwa kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu na bila faida yoyote.

Mtu huyo, hufananishwa na yule aliyebebea chakula chake kwenye chombo kilichotoboka, kwa sababu naye hufanya kazi isiyo na faida, katika utendaji wake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “umebebea kwenye chombo kilichotoboka.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kupoteza muda wao katika kufanya kazi isiyo na faida yoyote, maishani mwao. Kumbe basi, wanatakiwa kuzifanyia utafiti kazi zao, ili waweze kuzichagua na kuzitekeleza zile zinazowaletea faida katika kuziendeleza familia zao, maishani mwao.

Hagai 1:6. “Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotoboka toboka.”

Mhubiri 2:11. “Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayo mikono yangu ilikuwa imefanya na yale niliyotaabika kukamilisha, kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbizaupepo, hapakuwa na faida yo yote chini ya jua.”

Isaya 49:4. “Lakini nilisema, “Nimetumika bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida. Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa BWANA, nayo ijara yangu iko kwa Mungu wangu.””

Yeremia 12:13. “Watapanda ngano lakini watavuna miiba, watajitaabisha lakini hawatafaidi cho chote Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako kwa sababu ya hasira kali ya BWANA Mungu.’’”

Luka 17:10. “Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili, tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.”

1 Wathesalonike 3:5. “Kwa sababu hii nilipokuwa siwezi kuvumilia zaidi, nilimtuma mtu ili nipate habari za imani yenu. Niliogopa kwamba kwa njia fulani yule mjaribu asiwe amewajaribu, nasi tukawa tumejitaabisha bure.”

Tito 3:9. “Lakini jiepushe na maswali ya kipuzi, mambo ya koo, mabishano na ugomvi kuhusu sheria, kwa sababu haya hayana faida tena ni ubatili.”

Luka 10:38-42. “Ikawa Yesu na wanafunzi Wake walipokuwa wakienda Yerusalemu, akaingia kwenye kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha nyumbani kwake. Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Maria, ambaye yeye aliketi chini miguuni mwa Yesu akisikiliza yale aliyokuwa akisema. Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike. Martha akaja kwa Yesu na kumwuliza, “Bwana, hujali kwamba ndugu yangu ameniachia kazi zote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie.” Lakini Bwana akamjibu, “Martha,Martha, mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.””

Luka 16:16-20. ‘‘Torati na manabii vilitumiwa mpaka kuja kwa Yohana Mbatizaji. Tangu wakati huo habari njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu. Lakini ni rahisi zaidi mbingu na nchi kupita kuliko hata herufi moja kuondoka katika Sheria. “Mtu ye yote ampaye mkewe talaka na kumwoa mwanamke mwingine azini, naye mwanaume amwoaye mwanamke aliyetalikiwa azini.  ‘‘Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, ambaye aliishi kwa anasa, kila siku. Hapo penye mlango wake aliishi maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima.”

water carrying africa

water carrying africa1

bhakima bha madagascar

ENGLISH: YOU HAVE CARRIED IT IN A LEAKY CONTAINER.

There was a man carrying food to a certain place. However, the food he was carrying went on diminishing as he was going. He began wondering by asking himself, “Why is my load becoming lighter?” A man behind him saw the spilled food and said, “You have carried it in a leaky container.”

This proverb is likened with a man who works in vain. Such man wastes his time, as well as his energy. He completes his task by working for a long time and to no avail.

Such person is likened with a person who carries his food in a leaky container. That is why, when making reference to such a person, people say to him, “You have carried it in a leaky container.”

This proverb teaches people how to stop wasting their time doing useless work. Therefore in order to succeed, they need to scrutinise what they are doing so that they can choose and implement those activities that can benefit them for the development of their families, in their lives.

Haggai 1: 6 Ecclesiastes 2:11. Isaiah 49: 4 Jeremiah 12:13. Luke 17:10. 1 Thessalonians 3: 5 Titus 3: 9. Luke 10: 38-42 Luke 16: 16-20.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.