735. OWILAGWA YAPI.

Olihoyi munhu uyo agawilwa na ng’wiye giki agwambilijiwa gugutumama nimo gokwe go gulimila ngese mpaka gushile. Umunhu ng’winuyo, agaduka ulindilaga giki agwiza munhu ang’wambilije, nose insese yakwe yukula.

Abhanhu bhumuja, “nibhuli udulimilaga ingese yako?” Uweyi agashosha, “nanindilaga munhu uyo uniwila giki agwiza anambilije ugulimila mpaga ishile ingese yiniyo.” Ung’wila giki, “owilagwa yapi.”

Hashinaga uguwilwa yapi munho guwilwa mihayo ya bhulomolomo. Aho wigwa chele umunhu ng’wunuyo, agandya uguilimila ingese yakwe mpaga uimala. Huna lubhiza lusumo lo gubhahugula abhanhu abho bhalembagulagwa na bhichabho.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agawilagwa mihayo ya bhulomolomo oyizunya, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhizaga ndimu noyi aguidebha wangu imihayo ya bhulomolomo iyo agawilagwa na bhanhu.

Umunhu ng’wunuyo, agalenganijiyagwa nu munhu uyo agalembwa giki agwambilijiwa uguilimila insese yakwe, hunaulindila mpaka wize ung’wambilija okwe, naandye uguilimila ingese yiniyo, kunguno nuweyi, agawilagwa mihayo ya bhulomolomo uyizunya. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “owilagwa yapi.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guidebha wangu imihayo iya bhulomolomo iyo bhagawilagwa na wichabho, kugiki bhadule guitumama milimo yabho chiza bho nduhu ugutindikwa na mihayo ya bhulomolomo, umuwikaji bhobho.

Mathayo 24:4.

Warumi 16:18.

Waefeso 5:6.

KISWAHILI: UMEAMBIWA MEUSI.

Alikuwepo mtu mmoja ambaye aliambiwa kuwa atasaidiwa kufanya kazi ya kupalilia shamba lake mpaka liishe. Mtu huyo, alibaki akisubiri bila kumuona mtu anayekuja kumsaidia, mwishowe palizi ikawa kubwa.

Watu wakamuuliza, “mbona hupalilii palizi yako?” Yeye akajibu, “namsubilia mtu aliyeniambia kwamba atakuja kunisaidia kulipalilia shamba hilo mpaka liishe.” Mwenzake akamwambia, “umeambiwa meusi.”

Kumbe kuambiwa meusi maana yake ni kuambiwa maneno ya uongo. Aliposikia hivyo, mtu huyo, alianza kulipalilia shamba lake mpaka, akalimaliza lote. Hiyo ndiyo ikawa methali ya kuwashitua watu wanaodanganywa na wenzao katika maisha yao.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huambiwa maneno ya uongo na kuyakubali, maishani mwake. Mtu huyo, huchelewa sana kuugundua uongo anaoambiwa na wenzake. Yeye hujikuta anayaamini maneno hata yale yaliyo ya uongo na kuanza kuyafanyia kazi.

Mtu huyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye alidanganywa kwamba atasaidiwa kufanya kazi ya kulipalilia shamba lake, akasubiri mpaka palizi ikawa kubwa, kwa sababu naye huyakubali maneno ya uongo anayoambiwa na wenzake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “umeambiwa meusi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyagundua mapema maneno ya uongo wanayoambiwa na wenzao, katika maisha yao, ili waweze kuzitekeleza vizuri kazi zao, bila kucheleweshwa na maneyo hayo, maishani mwao.

Mathayo 24:4. “Yesu akawajibu, “Angalieni, mtu asiwadanganye.”

Warumi 16:18. “Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe.”

Waefeso 5:6. “Mtu ye yote na asiwadanganye kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juuya wale wasiomtii.”

fantasy1

angolan1

simu

ENGLISH: YOU HAVE BEEN RUBBED WITH SOMETHING BLACK.

There was one man who was told that he would be helped to weed his farm until it was finished. The man remained waiting without seeing anyone coming to help him. The weeds in the farm kept on growing, choking his plants.

People asked him, “Why don’t you weed your farm?” He replied, “I am waiting for someone who told me that he would come and help me weed it.” A colleague said to him, “You have been rubbed with something black.”

Being rubbed with something black means being told false words. When he heard this, the man began to weed his farm until he finished it. That became an idiom that is used to refer to people who have been deceived by their peers.

This idiom is compared with a person who is told false words and accepts them. Because he believes the lie he has been told, it takes very long for such a person to discover that he has been told lies. He believes these false words and begins to act on them.

Such man is like the one who was deceived into believing that he would be helped to weed his farm but who waited until the weeds grew tall, choking his plants. When making reference to such a person, people would say to him, “you have rubbed with something black.”

This idiom teaches people to recognize in advance any lies they are told by their peers. When they do this, they do their duties effectively, therefore succeeding in life.

Matthew 24: 4.

Romans 16:18.

Ephesians 5: 6.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.