734. NAMILA WAPI.

Olihoyi munhu uyo wiyityaga giki ali mfumu kunguno ya kuchola hela. Umunhu ng’wunuyo, obhatemaga salago abhanhu na gubhab’ila makala bhalihaya bhugota wapi abho bhali bhadina ndebha chiza. Abhanhu bhenabho bhahaga alibhatulila bhugota bhopi, gashinaga gali makala iki nago galigapi. Abhoyi bhang’winhaga ng’ombe ya gubhab’ilila wapi bhunubho, ulu wela ubhujiku. Hunagwene umunhu ng’wunuyo, abhawilaga abhiye giki, “namilaga wapi.” Gashinaga ugumila wapi, munho gung’wila mtu mihayo ya bhulomolomo mpaga ufuma sabho.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali na bhushilimu bho gubhalemba abhanhu mpaka bhang’winha jikolo. Umunhu ng’wunuyo, agapandikaga sabho bho gubhalembagula abho bhadandebhile igiki, alinomolomo, umukikalile kakwe. Uweyi agatumilaga pye nzila ijo ajimanile, mpaga ojipandika isabho ja gufumila kubhanhu abho bhadaitilaga bhukengeji, imihayo yakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu mfumu uyo abhab’ilaga makala abhanhu bhahaya giki obhab’ilaga bhugota wapi kugiki pandike hela, kunguno nuweyi agitaga bhulishilimu bho gubhalembagula abhanhu kugiki adule gupandika sabho. Hunagwene ulu omala gujipandika isabho jinijo, agayombaga giki, “namila wapi.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwita bhukengeji bho gubhambilija gubhabadija abho bhalihaya gubhasoja isabho jabho, gubhitilia bhushilimu bho gulembagula, kugiki bhadule gujilang’hana chiza isabho jinijo, umuwikaji bhobho.

Ayubu 13:9.

Zaburi 78:36.

Mithali 14:25.

Luka 8:42ª-44.

Mathayo 24:4-5.

NIMEMPAKA NYEUSI.

Alikuwepo mtu mmoja aliyejifanya mganga kwa lengo la kutaka kupata pesa. Mtu huyo, alikuwa akiwachanja chale na kuwapata mkaa uliosagwa, wale ambao walikuwa hawajaulewa ujanza wake. Wao walidhani kwamba anawapaka dawa nyeusi mpaka wakampatia ng’ombe siku iliyofuata, kwa sababu hawakugundua kuwa ni mkaa. Ndiyo maana mtu huyo, alipopokea ng’ombe, aliwaambia watu wake kwamba, “nimempaka nyeusi.” Kumbe kumpaka nyeusi maana yake ni kumdanganya mtu mpaka akatoa mali.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana ujanja wa kuwadanganya watu mpaka wakampatia mali. Mtu huyo, hupata mali kwa kuwadanganya wale ambao hawajamfahamu, kwamba ni muongo, katika maisha yake. Yeye hutumia kila njia anazozifahamu, mpaka anafaulu kupata mali za kutoka kwa wale wasioyafanyia utafiti maneno yake.

Mtu huyo, hufanana na yule mganga aliyepaka watu mkaa wakadhani kwamba, amewapaka dawa nyeusi, mpaka wakampatia ng’ombe, kwa sababu naye hutumia ujanja wa kuwadanganya watu ili aweze kupata mali. Ndiyo maana anapomaliza kuzipata mali hizo, husema kwamba, “nimempaka nyeusi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kufanya utafiti wa kuwawezesha kuwagundua wale wanaotaka kuwachuliwa mali zao, kwa njia za udanganyifu, ili waweze kuzilinda vizuri mali zao, maishani mwao.

Ayubu 13:9. “Je, ingekuwa vema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?”

Zaburi 78:36. “mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.”

Mithali 14:25. “Shahidi wa kweli huokoa maisha, bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu.”

Luka 8:42ª-44. “kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa. Yesu alipokuwa akienda, umati wa watu ukamsonga sana. Katika umati huo alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, tena alikuwa amegharimia yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya matibabu wala hakuna ye yote aliyeweza kumponya. Huyo mwanamke akaja kwa nyuma na kugusa upindo wa vazi la Yesu, mara kutokwa damu kwake kukakoma.”

Mathayo 24:4-5. “Yesu akawajibu, “Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo, nao watawadanganya wengi.”

south-africa2

south-africa1

wet-

ENGLISH: I HAVE RUBBED HIM/HER WITH PULVERIZED CHARCOAL.

There was one person who pretended to be a healer for the purpose of making money. This person, was incise  his clients with razors  then rubbing them with  pulverized charcoal claiming that it was medicine to heal or protect them from witches. They came to him thinking that he was rubbing them with black medicine for which they would each of them give him a cow the next day as a fee for the service. They did so because they had not found out that he was rubbing their incision with mere pulverized charcoal instead of the black powdery local medicine he was supposed to. That is why the man, whenever he received the cow as payment for his deceitful service, he would say to his people, “I have rubbed him/her with pulverized charcoal.” To rub a person with pulverized charcoal means to deceive such a person until he gives someone a valuable thing.

This proverb is likened with a man who is cunning and deceitful. That person acquires wealth by deceiving those who do not know him, that he is a liar. He uses every means at his disposal, until he manages to obtain wealth from unsuspecting ones.

That man is like the one who rubs people with pulverized charcoal deceiving them that he has given them black medicine, for which they give him cows.

This proverb teaches people to be careful in their dealings with people so that they identify those who want to take their properties through fraud.

Job 13: 9. Psalm 78:36.

Proverbs 14:25.

Luke 8: 42-44.

Matthew 24: 4-5.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.