736. NG´ASHA IGUB´ILILAGA.

736. NG´ASHA IGUB´ILILAGA.

Ulusumo lunulo, lwingilile kubhazugi bha walwa abho bhalobhekaga ing´asha. Ing’asha yiniyo, bhuli wandijo wa guzuga walwa. Iyoyi ulu yub´ilila aha lushigu lo gubhuzuga uwalwa, jigab´izaga jimanyikijo ja giki, uwalwa bhunubho bhugupya. Umo agamuja ung’wiye, “ginehe ing’asha yab’ililaga koyi?” Ung’wiye agashosha, “Ing´asha igub’ililaga.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agapelanilaga gwita ginhu jilebhe, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunyo, agamanyikaga ukubhiye ikigi apenile umugati ya moyo gokwe.

Uweyi ulu ubhiza giki apelanilile gwita ginhu jawiza, guti gutumama nimo nhebhe, agugutumama unimo gunuyo bho bhukamu bhutale mpaga gushila. Aliyo lulu, ulu apelanilile gwita jito jabhubhi, guti gwibhonela bhanhu, abhiye bhagundebha wangu, bhandya gung’wiliga, kunguno adulile gulemaja bhanhu, umubhupelanu bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ng’washa iyo igapyaga yayubhilila, golecha giki uwalwa bhunubho bhugupya, kunguno nuweyi agabhililaga, umugati ya moyo gokwe, golebha giki adulile gwita jito jilebhe, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga kigi, “ing’asha igub’ililaga.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhupelanu bho gutumama milimo yabho bho bhugulambija bhutale, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho. Igelelilwe bhilemeje ugwikala na bhupelanu bho gwita jito ja bhubhi, umukikalile kabho.

Mathayo 13:33.

Luka 13:20-21.

Mathayo 16:12.

KISWAHILI: CHACHU INACHEMKA.

Methali hiyo ilianzia kwa wapika pombe walioandaa chachu. Chachu hiyo, ni kianzio cha kupika pombe. Hivyo yenyewe ikichemka siku ya kupika pombe, ni ishara kwamba pombe hiyo itaiva au itakuwa kali. Mmoja alimuuliza mwenzake, “vipi chachu imechemka huko?” Mwenzake alijibu, “chachu inachemka.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule akasilikiaye kufanya kitu fulani, maishani mwake. Mtu huyo, hujulikana kwa wenzake kwamba amekasilika moyoni mwake.

Hivyo, ikiwa kwamba, yeye amekasilikia kutekeleza kitu chema, kama vile kufanya kazi, ataitekeleza kazi hiyo kwa bidii mpaka mwisho. Lakini, ikiwa mtu huyo, amekasilikia kutekeleza kitendo kiovu, kama vile kuonea watu, wenzake watamgundua mapema na kuanza kumkwepa, kwa sababu aweza kujeruhi watu katika hasira yake hiyo.

Mtu huyo, hufanana na chachu ile ambayo huiva ikawa inachemka, kuonesha kwamba pombe hiyo itaiva, kwa sababu naye huchemka ndani ya moyo wake, kuonesha kwamba, aweza kutekelea kitendo fulani, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita kwamba, “chachu inachemka.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na hasira ya kuzitekeleza kazi zao kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao. Inafaa wajizuie kukaa na hasira ya kutekeleza kitendo kiovu, katika maisha yao.

Mathayo 13:33. “Akawaambia mfano mwingine, ‘‘Ufalme wa Mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika vipimo vitatu vya unga mpaka wote ukaumuka.’’”

Luka 13:20-21. “Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha Ufalme wa Mungu na nini? Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua na kuichanganya kwenye vipimo vitatu vya unga hadi wote ukawa umeumuka.””

Mathayo 16:12. “Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi juu ya chachu ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.”

tradition-

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.