737. BHIMBA NTWE MASANGU GOKALE.

Ulusumo lunulo, lulolile bhubhimbi bho ntwe go ng’wa munhu nhebhe na masangu ayo gagokalaga umu ntwe gokwe gunuyo. Olihoyi munhu uyo agantuma ng’wiye gujutumama nimo nhebhe, aliyomba, “jaga ugatumame nimo ubhujiku welaga.” Uweyi agalema aliyomba, “unene nalemaga nadujaga ugujutumama unimo gunuyo.” Ung’wiye agashosha, “bhimba ntwe masangu gokale.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu nambu uyo agapandikaga makoye, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, adigwaga ya guwilwa na bhiye, kunguno ya gubhadalaha abho agikalaga nabho. Uweyi agisangaga opandikaga makoye, kunguno ya bhulambu bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu bhubhinbi bho ntwe uyo gugokalaga masangu. Amasangu genayo agikolanijiyagwa na makoye ayo gagenhelejiyagwa na bhulambu bhokwe, kunguno nuweyi agapandikaga makoye ga gwenhwa na bhulambu bhunubho, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “bhimba ntwe masangu gokale.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka bhulanbu, bho gulema gutung’wa na bhichabho umukikalile kabho, kugiki bhadule gwigulambija gutumama milimo ya gubhapandikila matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Yeremia 49:16.

Mathayo 23:33.

Ezekieli 7:24.

Yeremia 50:32.

KISWAHILI: VIMBA KICHWA MAKANDE YAJAE.

Methali hiyo, huangalia uvimbaji wa kichwa cha mtu fulani na makande ambayo hujaa kwenye kichwa chake hicho. Alikuwepo mtu mmoja ambaye alimtuma mwenzake kwenda kufanya kazi fulani, akisema, “nenda ukafanye kazi kumekucha.” Yeye alikataa akisema, “mimi nimekataa siendi kufanya kazi hiyo.” Mwenzake akajibu, “vimba kichwa makande yajae.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu mwenye kiburi ambaye hupata matatizo maishani mwake. Mtu huyo, huwa hasikii ya kuambiwa na wenzake, kwa sababu ya kuwadharau wenzake hao anaoishi nao. Yeye hujikuta amepata matatizo makubwa kwa sababu ya kiburi chake hicho.

Mtu huyo, hulinganishwa na uvimbaji wa kichwa ambacho hujaa makande. Makande hayo hufananishwa na matatizo yaletwayo na kiburi chake hicho, kwa sababu naye hupata matatizo yasababishwayo na kiburi chake hicho. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “vimba kichwa makande yajae.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kiburi, cha kukataa kutung’wa na wenzao, ili waweze kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yale yawapatiayo mafanikiyo mengi, maishani mwao.

Yeremia 49:16. “Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako vimekudanganya, wewe unayeishi katika majabali ya miamba, wewe unayemiliki katika miinuko ya kilima. Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai, kutoka huko nitakushusha chini,’’ asema BWANA.”

Mathayo 23:33. “Ninyi nyoka, ninyi uzao wa nyoka wenye sumu! Mtaiepukaje hukumu ya jehanam?”

Ezekieli 7:24. “Nitaleta taifa ovu kuliko yote ili kumiliki nyumba zao, nitakomesha kiburi cha wenye nguvu na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi.”

Yeremia 50:32. “Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka wala hakuna ye yote atakayemuinua, nitawasha moto katika miji yake, utakaowateketeza wote wanaomzunguka.””

head

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.