731. NAGUMALILA MASONGA MU NDULU.

Imbuki ya lusumo lunulo, ingilile kubhulingi bho ng’wa munhu uyo olemaga ugugamalila masonga gakwe mu ndimu ndoo guti ndulu. Ubhumaji bho masonga mu ndulu, uwene hubhuli bho jiliwa ijo jigapinihyaga nda sagala mpaga uni ojo uduma ugulya ijilwa ijisoga ijakuwinga.

Olihoyi munhu uyo oliajile kuwinga. Agabhasanga bhanhu bhalilya bhung’wila, “egelaga dulye jiliwa.”  Uweyi agashosha, “nagumalila masonga mu ndugu.” Ijinaguyomba chiniko igolecha giki olemaga ugulya.

Hunalubhiza lusumo lo gutumila ulu munhu ajile gujulya jiliwa jinonu, ulu ukalibhushiwa gulya jiliwa umunzila, agushosha, “nagumalila masonga mu ndugu.” Ukwene huguhaya giki, umunhu ulu ajile kuwinga, adulya umunzila, kunguno ulu ulya aguipinihya inda ya gujulila jiliwa jinonu ukuwinga bhunubho.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agakoyakoyaga bho gutumama milimo yakwe kugiki adule gupangika jikolo jawiza kukila ijo alinajo. Umunhu ng’wunuyo, agilechaga mingi iyo idulile guntindika gukwabha sabho ningi aha shigu jahabhutongi. Uweyi agipunaga dilu oja gujutumama milimo yakwe mpaga oimala chiza iyo igang’winhaga matwajo mingi, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agagakejaga amaonga gakwe bho gwilemeja gwita mihayo mingi kugiki adule gupandika jikolo ijo jilijawiza kukila ijo alinajo. Uweyi agabhalangaga na bhanhu bhakwe inzila ja gwichobhela jikolo bho gwigulambija gutumama milimo yabho chiza. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “nagumalila masonga mu ndugu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo iyo idulile gubhenhela matwajo mingi, umukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika jiliwa ja gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Ijinagongeja ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwilemeja gwita ya bhubhi kugiki, bhadule gunkaribhusha Yesu, umuwikaji bhobho. UYesu adulile gubhinha jiliwa jawiza abhanhu bhenabho, kukila ijo bhalinajo.

Yohana 2:1-10.

Mathayo 22:3-4.

KISWAHILI: NITAMALIZIA MISHALE KWENYE PUNDAMILIA.

Chanzo cha methali hiyo, chatokea kwa mwindaji aliyekataa kumalizia mishale yake kwenye wanyama wadogo kama pundamiliya, wakati wale wakubwa walikuwa wanakuja katika siku za mbeleni. Umalizaji wa mishale kwenye pumbamilia ni ulaji wa chakula kisichokuwa kitamu wakati vile ambavyo ni vitamu vinakuja. Vyakula hivyo humaliza nafasi katika tumbo lake, ambayo ni ya kuwekea vyakula vitakavyo kuja kwenye sherehe anayoiendea.

Alikuwepo mtu aliye alikwa kwenye harusi. Mtu huyo alipoanza safari yake, aliwakuta watu wanakula, ambao walimwambia “sogea tule chakula.” Yeye akajibu, “nitamalizia mishale kwenye pundamilia.”

Hiyo ndiyo ikawa methali ya kutumia kwa mtu anayeenda harusini akikaribishwa chakula njiani. Yeye hujibu kwamba, “nitamalizia mishale kwenye pundamilia.”

Hivyo ndiyo kusema kwamba, mtu akialikwa kwenda kwenye harusi, hatakula nyumbani atokako au njiani, kwa sababu akila atapunguza nafasi ya tumbo lake aliyoiweka kwa ajili ya kwenda kula chakula kizuri kwenye sherehe hiyo.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huhangaika kufanya kazi zake ili aweze kupata vitu vizuri zaidi kupita vile alivyo navyo. Mtu huyo, hujinyima mengi yawezayo kumchelewesha kupata mali nyingi kwenye siku za mbeleni. Yeye hujilawa asubuhi kwenda kuyatekeleza majukumu ya kazi zake mpaka anayamaliza vizuri, ambayo humpatia mafanikio mengi, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekataa kutumia mishale yake kwenye pundamilia, yaani kula chakula kisichokuwa kitamu njiani akienda kwenye harusi, kwa sababu naye hujinyima kufanya mambo mengi ili aweze kupata vitu vilivyo vizuri zaidi kupita vile alivyo navyo. Yeye huwafundisha pia watu wake njia za kujitafutia vitu vizuri kwa kujibidisha kufanya kazi zao vizuri. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “nitamalizia mishale kwenye pundamilia.”

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi ziwezazo kuwaletea mafanikio mengi, katika maisha yao, ili waweze kupata chakula cha kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Zaidi ya hayo, methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujizuia kutenda maovu ili waweze kumkaribisha Yesu maishani yao. Yesu aweza kuwapatia chakula kizuri zaidi kupita kile walicho nacho.

Yohana 2:1-10. “Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Yesu alikuwako huko. Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, “Wameishiwa na divai.” Yesu akamwambia, ‘‘Mwanamke, nina nini nawe? Saa Yangu haijawadia.’’ Mama Yake akawaambia wale watumishi, ‘‘Lo lote atakalowaambia, fanyeni.’’ Basi ilikuwapo huko mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi, kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu. Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.’’ Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu. Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.’’ Hivyo wakachota, wakampelekea. Yule mkuu wa meza akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilika kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji wao walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando akamwambia, “Watu wote hutoa kwanza divai nzuri, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa vya kutosha, lakini wewe umeiweka ile nzuri kupita zote mpaka sasa.””

Mathayo 22:3-4. “Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja. ‘‘Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba karamu iko tayari kwa ajili yenu, nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono. Karibuni |akaenda shambani mwake, mwingine akaenda kwenye biashara yake.”

zebra

woman

ENGLISH: I DO NOT WANT TO FINISH MY ARROWS SHOOTING AT ZEBRAS.

The basis of the above proverb comes from a hunter who refused to shoot his arrows at small animals like zebras, while the bigger ones would be coming in future. Finishing one’s arrows by shooting zebras is to take unpleasant food to the full when the ones that are palatable are coming. These unpalatable foods take up the space in the eater’s stomach, which is to store food that he will eat at the party he is going to attend.

There was a man who was invited to the wedding. When the man started his journey, he found people eating. They told him “come and eat.” But he replied, ” If do so, I will finish my arrows shooting at only zebras.”

This is a proverb that relates to a man who is going to a wedding and is invited to a meal on the way. To decline the offer, he answers, “If I do so I will finish my arrows shooting at zebras.”

That is to say, if a person is invited to a wedding, he will not eat at home or on the way, because eating on the way will reduce the stomach space he has set aside for going to a good meal at the ceremony.

The proverb is likened with a man who is anxious to get his own way so that he may have better things than he has. Such a person deprives himself of much that can delay him in obtaining more wealth in the future. He spends the rest of his life in the morning doing his job until he finishes it well, which gives him a lot of success, in his life.

Such man is like the one who refused to use his arrows to shoot at zebras, that is, to eat unhealthy food on the way to a wedding, meaning refusing to do things that are not good so that he can get better things than what he has. He also teaches his people how to get good things by striving to do their work well. That is why he tells the people, “I do not want to finish my arrows shooting at zebras.”

This proverb teaches people on how to work hard enough to make them succed in their lives, including having enough food to sustain their families.

Moreover, this proverb teaches people about abstaining from evil so that they can welcome Jesus into their lives. Jesus can give them better food than what they have.

John 2: 1-10, Matthew 22: 3-4.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.