730. NAB´IKAGA NDA YA KUBHUGENI.

Imbuki ya lusumo lunulo, ingilile kubhub’iki bho nda ya ng’wa munhu uyo ohayaga gugeniha hanhu. Ubhub’iki bho nda bhunubho, bhuli bhutuji bho wasa ubho bhulatumilwe aha shigu ijaha bhutongi. Ugub’ika nda mumho gulekela wasa bho gutulile jiliwa ijo alatengelwe ukubhugeni bhokwe umunhu ng’wunuyo, kunguno ungeni agatengelagwa jiliwa jawiza, guti jaha winga.

Olihoyi munhu uyo ahayaga gugeniha. Abho obhalekaga ahaya bhagankalibhusha gulya jiliwa bhaliyomba, “nzugu dulye jatengagwa ijiliwa.” Umunhu ng’wunuyo agashosha giki, “nab’ikaga nda ya kubhugeni.”

Hunakubhiza kahayile ulu munhu ajile bhugeni nulu uyo ajile kuwinga, ulu ukalibhushiwa jiliwa umunzila, agayombaga chene giki, “nab’ikaga nda ya kubhugeni.” Ukwene huguhaya giki, umunhu ulu ajile kuwinga, nulu bhugeni, adulya ijiliwa, kunguno ulu ulya uguipinihya inda ya gujulila jiliwa jisoga uko ajile.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agakoyakoyaga bho gutumama imilimo yake kugiki adule gupangika jikolo jawiza kukila ijo alinajo. Umunhu ng’wunuyo, agilechaga mingi iyo idulile guntindika gukwabha sabho ningi aha shigu jahabhutongi. Uweyi agipunaga dilu oja gujutumama milimo yakwe mpaga uimala chiza iyo igang’winhaga matwajo mingi, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agab’ika nda ya kubhugeni, kunguno nu weyi agilechaga gwita mihayo mingi kugiki adule gupandika jikolo ijo jilijawiza kukila ijo alinajo. Uweyi agabhalangaga na bhanhu bhakwe inzila ja gwichobhela jikolo bho gwigulambija gutumama milimo yabho chiza. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “nab’ikaga nda ya kubhugeni.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo iyo idulile gubhenhela matwajo mingi, umukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika jiliwa ja gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Ijinagongeja ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwilemeja gwita ya bhubhi kugiki bhadule gunkaribhusha Yesu, umuwikaji bhobho. UYesu adulile gubhinha jiliwa jawiza abhanhu bhenabho, kukila ijo bhalinajo.

Yohana 2:1-10.

Mathayo 22:3-4.

KISWAHILI: NIMEHIFADHI TUMBO LA UGENINI.

Chanzo cha methali hiyo, chatokea kwenye uhifadhi wa nafasi tumboni mwa mtu anayetaka kwenda harusini au ugenini. Uhifadhi huo ni wa kutunza nafasi itakayo tumika kuwekea chakula kwenye siku za mbeleni. Hivyo kuhifadhi tumbo maana yake ni kuacha nafasi ya kuwekea chakula atakachokula mtu anayeenda kwenye harusi au ugenini, kwa sababu ataletewa chakula kizuri kuliko kile anachopewa nyumbani kwake.

Alikuwepo mtu ambaye alitaka kwenda ugenini ambako kulikuwepo na harusi. Watu wa nyumbani kwake, walimkaribisha chakula wakisema, “njoo tule chakula kimeletwa mezani.” Mtu huyo akajibu, “nimehifadhi tumbo la ugenini.”

Huo ndiyo ukawa msemo kwa mtu anayeenda harusini au ugenini, akikaribishwa chakula, hujibu hivyo kwamba, “nimehifadhi tumbo la ugenini.” Hivyo ndiyo kusema kwamba, mtu akialikwa kwenda ugenini au kwenye harusi, hatakula nyumbani atokako, kwa sababu akila atapunguza nafasi ya tumbo lake aliyoiweka kwa ajili ya kwenda kula chakula kizuri ugenini.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huhangaika kufanya kazi zake ili aweze kupata vitu vizuri zaidi kupita vile alivyo navyo. Mtu huyo, hujinyima mengi yawezayo kumchelewesha kupata mali nyingi kwenye siku za mbeleni. Yeye hujilawa asubuhi kwenda kuyatekeleza majukumu ya kazi zake mpaka anayamaliza vizuri ambayo humpatia mafanikio mengi, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyehifadhi tumbo la ugenini, kwa sababu naye hujinyima kufanya mambo mengi ili aweze kupata vitu vilivyo vizuri zaidi kupita vile alivyo navyo kwa sasa. Yeye huwafundisha pia watu wake njia za kujitafutia vitu kwa kujibidisha kufanya kazi zao vizuri. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “nimehifadhi tumbo la ugenini.”

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi ambazo zaweza kuwaletea mafanikio mengi, katika maisha yao, ili waweze kupata chakula cha kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Zaidi ya hayo, methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujizuia kutenda maovu ili waweze kumkaribisha Yesu maishani yao. Yesu aweza kuwapatia chakula kizuri zaidi kupita kile walicho nacho.

Yohana 2:1-10. “Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Yesu alikuwako huko. Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, “Wameishiwa na divai.” Yesu akamwambia, ‘‘Mwanamke, nina nini nawe? Saa Yangu haijawadia.’’ Mama Yake akawaambia wale watumishi, ‘‘Lo lote atakalowaambia, fanyeni.’’ Basi ilikuwapo huko mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi, kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu. Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.’’ Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu. Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.’’ Hivyo wakachota, wakampelekea. Yule mkuu wa meza akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilika kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji wao walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando akamwambia, “Watu wote hutoa kwanza divai nzuri, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa vya kutosha, lakini wewe umeiweka ile nzuri kupita zote mpaka sasa.””

Mathayo 22:3-4. “Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja. ‘‘Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba karamu iko tayari kwa ajili yenu, nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono. Karibuni |akaenda shambani mwake, mwingine akaenda kwenye biashara yake.”

king1

cooking

eating smoothie

ENGLISH: I HAVE KEPT MY STOMACH FOR A VISIT.

The origin of the above proverb came through the person who wanted to go for a visit or a wedding and who for that, did not want to eat his usual food at home claiming that he had kept his stomach for a visit which he wanted to make or wedding that one would attend. He claimed so with the argument that if he ate food at home or along the way before getting where he had planned to, there would not be  enough  room in his stomach to store the  nice or palatable food he  would eat  in his host’s house after he had made or at the wedding after he had attended one.

 When the people of his family invited him to the meal saying, “Come and eat, the food has been brought to the table.” The man replied, “I have kept my stomach for a visit.”

That is what a man who goes to a wedding or a visitor does. When invited to a meal, he responds by saying, “I have kept my stomach for a visit.”That is to say, if a person is invited to go for a visit or a wedding, he will not eat at home, because eating at home will reduce the amount of stomach space he has set aside for going to eat the good food he is expecting to eat at the home of one’s host or at the wedding.

The proverb is likened with a man who is anxious to get his own way so that he may have better things than he has. Such a person deprives himself much of what can delay him in obtaining more wealth in the future. He gets up early in the morning, works very hard in order to fulfill his responsibilities which gives him a lot of success, in his life.

This person is like the one who refused to eat his usual food at home claiming that he had kept his stomach for for a visit. This is because; this person also keeps from doing many things which affect his goal. Instead, he focuses on what one is doing so that he can get better things than those he has now. He also teaches his people how to make a living by working hard. That’s why people say, “I have kept my stomach for a visit.”

This proverb teaches people about working hard something that can bring them great success in their lives, because they can have food to sustain their families.

Moreover, this proverb teaches people about abstaining from evil so that they can welcome Jesus into their lives. Jesus can give them better food than what they have.

John 2: 1-10, Matthew 22: 3-4.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.